SIMULIZI : RAHMA 06




Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

         
👉NAMBA 06

Tunaendelea ......

Fatuma alisimama akachukua kisu kilichokuwa juu ya meza akamsogelea suleyman akamwangalia kwa hasira sana akanyanyua kile kisu alipotaka kumchoma juma alishika alimziwia fatuma na kumsihi asifanye mauaji , Wakati huo suleyman alibaki analia na kujilaumu sana sana sana , Suleyman alimtazama sana Fatuma kisha akasema :-

"" Fatuma najua unanilaumu na unanichukia sana lakini hujui tu kilichotokea nilishindwa kukusaidia na ndio maana nilikimbia wakati nilipoona umeamka na kuniangalia. Nimejaribu kuficha siri hii muda mrefu sana lakini leo ngoja nikueleze ukweli mbele ya mdogo wangu juma. Fatuma ukweli mimi sijakubaka kama unavyosema na kwa jinsi nilivyokuwa nakupenda sana nawezaje kukubaka fatuma, lakini sikulaumu kwakua hujui chochote kilichotokea siku ile kwa sababu ulikuwa umelala , Usiku ule nilikuwa narudi nyumbani njiani nilikutana na mussa yule mtoto niliyekuwa nampatia barua akuletee. Nilimsimamisha nikamuuliza kwanini anakimbia akiwa analia, alinijibu kaka suleyman wale wahuni wa mtaani wanampiga dada fatuma nenda kamsaidie nilikuwa naenda kumwambia mama yake, Niliposikia vile nilirudi nae hadi sehemu uliyokuwepo nilipofika sikuwakuta nilikukuta umelala chini na mazingira niliyokukuta nayo nilitambua tayari umeshabakwa. Nilisikitika sana , roho iliniuma mno nikakuvalisha nguo kwa maana nilikukuta ukiwa umevuliwa nguo za ndani . Wakati nakuvalisha zile nguo ndipo ulipoamka ilibidi niondoke sehemu ile nikiwa na mussa nilijisikia aibu sana kwa tukio lile , Lakini pamoja na yote bado nilikupenda na nitaendelea kukupenda nisamehe kwa kushindwa kukusaidia fatuma 😢

Fatuma aliposikia maneno hayo aliishiwa nguvu akadondosha kisu chini hakuamini kama alibakwa na zaidi ya mtu mmoja na alijilaumu sana kwa sababu alikuwa anachuki sana na suleyman akijua kuwa yeye ndiye aliyefanya tukio lile na ndio baba mzazi wa rahma , kumbe sivyo na rahma sio mtoto wa suleyman "" Daaaah bora nife kuliko haya yalinikuta nimekukosea nini mungu wangu. """"" Hayo yote yalikuwa maneno ya fatuma akijiuliza kichwani mwake fatuma alimsukuma juma aliyekuwa amemshika alafu akaokota kile kisu akajichoma tumboni. Suleyman na juma walimchukua fatuma haraka haraka wakampeleka hospital.

Baada ya miezi mitatu hali ya fatuma ilikuwa nzuri na akaruhusiwa kwenda nyumbani,  juma akamchukua wakarudi nyumbani fatuma akiwa katika msongo mzito wa mawazo muda wote akilia , Suleyman alijaribu kumliwaza na kumuuliza habari ya huko nyumbani kwao ( kijijini ).

"" Suleyman nisamehe sana najua sina thamani tena mbele yako l na nikikuambia kilichotokea baada ya kubakwa nahisi huwezi kunipenda tena suleyman. Baada ya kutoka pale nilipata ujauzito nilijua ni ujauzito wako, kwakua nilijua umenibaka nilijaribu kutoa kwa dawa mbali mbali lakini haukutoka. Ujauzito ulipokuwa mama aliponiona nina ujauzito alipoteza maisha kwa presha nikabaki peke yangu. Niliuchukia sana ule ujauzito hata nilipozaa yule mtoto nilimtupa lakin baadae nilipomfuata nilimkuta ameliwa na mnyama masikini mwanangu "

Fatuma baada ya maneno yale aliwashukuru sana juma na suleyman kwa msaada waliompatia alafu akahitaji kuondoka , Suleyman alimsimamisha kisha akasema :-

"" Fatuma usiseme huna thamani , unanikosea sana moyo wangu bado unakuhitaji sana naomba kubali uwe mke wangu bado nakupenda sana.

Fatuma hakuamini aliposikia maneno yale alimkumbatia suleyman , Baada ya miezi kadhaa walifunga ndoa Fatuma na Suleyman wakaanza maisha ya ndoa , Ndoa yao ilikuwa na amani, furaha na upendo wa dhati fatuma alirudisha furaha yake aliyokuwa ameipoteza muda mrefu sana, Fatuma alisahau tabu na mateso yote kutokana na upendo wa juu zaidi alioupata toka kwa mume wake Suleyman.

Ilipita miaka saba #Rahma akiwa amekuwa binti kiasi alikuwa binti mrembo , mzuri , mwema na mwenye heshima sana hakika alipendwa na kila aliyemuona. Rahma hakujaliwa kwenda shule kwakua wazazi waliomlea hawakuwa na fedha na alikuwa na mama mlezi tu kwa sababu baba mlezi alipoteza maisha muda mrefu uliopita na wakati huo mama mlezi nae alikuwa mgonjwa sana , Rahma alikuwa anamhudumia mama yake (mlezi) ambaye yeye alijua ni mama yake mzazi.

Baada ya siku kadhaa Rahma akiwa anapika alisikia mama akimuita, rahma alikimbia hadi ndani alimkuta mama amezidiwa sana yule mama akamwambia rahma alete kitambaa kilichokuwa ndani chini ya kitanda, rahma alifuata kitambaa hicho na kurudi haraka yule mama  akamwambia afungue rahma alipofungua alikuta cheni nzuri sana, mama akasema :- 

"" Mwanangu Sabrina cheni hiyo inamaana kubwa kwako, Ukweli Mimi sio mama yako mzazi nilikuokota tu, ninaamini mama yako ndio mwenye cheni hiyo kwa sababu ilikuwepo sehemu niliyokukuta .

Yule mama baada ya maneno Yale alifariki, Rahma ( sabrina) jina alilopewa na baba mlezi alilia sana na hakujua afanye nini kwakua alikuwa bado binti mdogo , alikwenda kuwaita majirani , majirani Wema walipofika walimkuta mama yake Sabrina ( rahma ) kafariki walimfanyia maziko. Rahma ( Sabrina ) akiwa amebaki peke yake alijitokeza mwanaume mmoja akasema ataishi na binti yule kwakua alikuwa anaitambua vizuri familia hiyo, Wanakijiji walimkubalia alichotaka kwakua walikuwa wanamuamini. Usiku wakiwa wamelala yule kijana alirudi akiwa amelewa alipofika aliingia moja kwa moja hadi apikuwa amelala rahma ( Sabrina) akawa anahitaji kumbaka, Rahma alipiga kelele lakin kelele zile hazikusaidia kitu yule mwanaume alikuwa bado kamshika rahma. Rahma alishika ile chini aliyokuwa ameivaa kisha ......

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: