SIMULIZI:RAHMA 22
Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher
👉NAMBA 22
kwakua alikuwa anakimbia akiwa na wasiwasi alijikwaa na kudondoka chini kwa bahati mbaya aliangukia tumbo baada ya kuangukia tumbo Rahma alipata maumivu makali mno na kushindwa kuendelea kukimbia, wakati huo Mama Martin alikuwa anamfuata nyuma alipofika nje alistuka kumuona Rahma yupo chini akihangaika huku na huko akiwa ameshika tumbo, Mama Martin alirudi ndani akachukua gari akampeleka Rahma hospital, walipofika Rahma alipatiwa huduma ya kwanza, Madaktari walipomaliza kazi yao walimpatia Rahma kitanda ili atulie kwa ajili ya kurudisha afya yake. Mama Martini akiwa ndani ya Wodi aliyolazwa Rahma alisikia simu ya Rahma inaita ndani ya mfuko wa suruali aliyokuwa ameivaa, Mama martin alichukua simu ya Rahma :
📱 MY DARLING OCHU Calling...📲
Jina lililokuwa linapiga simu ya Rahma lilimtisha sana Mama martin ikapelekea kushindwa kupokea simu ya binti yake simu ilipopigwa zaidi ikabidi apokee :-
"" Hallow
"" Naam hallo habari samahani mwenye siku yupo wapi ?
"" Amelazwa anaumwa .
"" Amelazwa 😨 samahani amelazwa hospital gani nahitaji kuja hapo .
Mama Martin alimuelekeza Othuman sehemu walipo haikuchukua muda mrefu Othuman alifika katika hospital hiyo akamkuta Rahma amelala Mama martin alimuomba Othuman amuangalie Rahma yeye aliondoka na kurudi nyumbani. Baada ya saa moja kupita Rahma alipata fahamu na kufumbua macho hakuamini kumuona Othuman mbele ya macho yake Rahma alianza kulia:-
"" Sabrina unalia nini Usiniambie umetoa mimba yangu ?
"" Othuman kwanini wanifanyia hivi lakini kwanini Othuman kumbe ulikuwa hunipendi ulinidanganya daah siamini Mimi kama kweli ni wewe nakuchukia sana Othuman toka mbele ya macho yangu 😢.
"" Nisikilize Sabrina Mimi nilikutania tu na nilitaka kujua kitu toka kwako lakini kwa bahati mbaya baba alinituma nchini UINGEREZA yaani muda huu ndio nimetoka uwanja wa ndege sijaenda hata nyumbani nimekupigia simu akapokea mama yako ndio akanieleza upo hapa hebu niambie tatizo ni nini Sabrina ?
"" Ochu yote haya umesababisha wewe mama alitambua kuwa Mimi ni mjazito na Mimi sikuhitaji nyumbani wajue suala hili hususa baba laiti akijua anaweza kuniua ikabidi nitoroke nyumbani kwa bahati mbaya nilijikwaa na kudondoka chini niliangukia tumbo sasa sijui kama mtoto yupo salama .
"" Unasemaje wewe acha kunitania sasa Kwanini ulikimbia ngoja nimfuate Doctor usinitanie wewe mtoto wangu lazima awe hai hawezi kutoka nasema haiwezekani .
Othuman alipotaka kuondoka ghafla daktari aliingia kisha akamfanyia vipimo Rahma, Othuman alimuuliza Daktari :-
"" Doctor samahani naomba kujua hali ya mtoto aliye tumboni.
"" Kwanza wewe nani yake ?
"" Mimi ni mume wake .
"" Afadhali kwa sababu watu kama ninyi tunawatafuta sana .
Daktari aliondoka baada ya kuzungumza maneno hayo na kumuacha Othuman njia panda wakati Othuman anatafakari kauli ya Daktari alisikia mlango unafunguliwa yule Daktari alirudi akiwa na askari watatu, Askari walimshika Othuman wakamfunga pingu Othuman alishindwa kuelewa akasema :-
"" Nimefanyaje Daktari ?
"" Watu kama ninyi mnaowapiga wake zenu hadi kuhatarisha maisha ya mtoto lazima serikali iwapatie adhabu ili na wengine wajifunze.
Rahma alivyosikia hivyo alistuka na kumwambia Daktari :-
"" Hapana Daktari mume wangu hajanipiga nilidondoka chini nilipokuwa napiga mazoezi .
"" Sikia wewe binti usilete balaa hapa najua unamtetea mume wako sasa ipo hivi alikupiga au hajakupiga serikali itachunguza hilo askari mpelekeni kituoni huyo .
Othuman alijitahidi kujieleza sana mwisho askari walimuelewa wakamfungua pingu, Daktari aliwatoa wasiwasi kuhusu mtoto aliwambia mtoto yupo salama, Othuman alifurahi mno kusikia Mtoto yupo salama. Baada ya masaa mawili kupita Daktari alimpatia ruhusa Rahma akarudi nyumbani akiwa na Othuman walipofika nyumbani mlangoni walikutana na Mama martin akiwa na Familia yake, Hussein aliwasogelea akiwa amekasiria akamuuliza Othuman :-
"" Ujauzito uliopo tumboni kwa binti yangu ni wako au unaweza kuwa unamjua mwenye ujauzito huu ? Kwa sababu najua Sabrina hawezi kuniambia ukweli ndio maana nakuuliza wewe Kijana .
"" Ujauzito huu nimempatia mimi baba samahani kwa kitendo hiki lakini ukweli ninampenda sana Sabrina baba nipo tayari kumuoa .
"" Acha upumbafu wewe unajua ni kiasi gani nilivyosumbuka juu yake alafu leo unazungumza kirahisi kiasi hicho nahisi hunijui vizuri ee .
Hussein alichomoa bastola kisha akaweka kichwani kwa Othuman cha ajabu walimuona Othuman anacheka na kusema akiwa hana hofu :-
"" Piga risasi baba siwezi kuogopa kufa kwa ajili ya binti ninaempenda toka moyoni mwangu siogopi .
"" Et ee vizuri sana kijana nakuua .
Hussein alipotaka kufyatua Risasi Rahma alisogea mbele ya Othuman alafu .......
___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: