SIMULIZI:RAHMA SEHEMU YA MWISHO
Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher
SEHEMU YA MWISHO
Tunaendelea .......
Fatuma alifumba macho Rahma alivua cheni yake akampatia Fatuma kisha akamwambia afumbue macho, Fatuma baada ya kufumbua macho alitazama zawadi aliyopewa alistuka sana mapigo ya moyo yalikwenda haraka haraka akamwangalia Rahma kisha akaitazama tena cheni alivyopewa na Rahma kwa muda mrefu. Kitendo hicho kilimpatia simanzi Rahma akasema :-
"" Mama kwanini unaitazama sana hiyo cheni au kwakua ni cheni ya zamani huenda hujaipenda lakini ungejua Thamani ya hiyo cheni katika maisha yangu ungeipokea kwa mikono miwili kwa sababu katika Dunia hii hakuna kitu chenye thamani kwangu kama hiyo cheni mama .
"" Unaweza kuniambia hii cheni umeitoa wapi binti yangu ?
"" Ni Stori ndefu mama lakini kifupi hii cheni inahusiana na maisha yangu kwa sababu mama yangu mlezi ambaye nilidhani ni mama yangu mzazi kabla hajapoteza maisha aliniambia ukweli kwamba yeye sio mama yangu mzazi aliniambia aliniokota nilipokuwa mdogo pamoja na cheni hiyo sasa sijui kuna nini katika hiyo cheni huenda inamaana kubwa katika maisha yangu.
Moyo wa Rehema ulizidi kudunda kwa kasi zaidi akamuuliza Rahma tena wakati huo Suleyman na Othuman walishindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea :-
"" Sabrina unaweza kuniambia huyo mama yako mlezi alikuwa anaishi wapi binti yangu ?
"" Tulikuwa tunaishi kijijini #BITALE
"" Haaaah 😭 RAHMA mwanangu !!
Moyo wa Rahma ulistuka na kuanza kwenda mbio, Muda huo huo Fatuma alianza kulia, Fatuma alilia zaidi. Suleyman alishindwa kumuelewa mke wake halikadhalika Rahma na Othuman walishikwa na butwaa. Fatuma aliendelea kulia hadi akakaa chini mume wake ( Suleyman ) na Othuman walimsogelea Fatuma wakamtuliza Suleyman ikabidi amuuliza mke wake :-
"" Kuna tatizo gani mke wangu ?
"" Mume wangu huyu Sabrina ni mtoto wangu niliyemuacha Porini kijijini bitale baada ya kupata matatizo niliyokueleza na hii cheni ni cheni yangu nilimvisha pia siku niliyomvisha cheni nilimpatia na jina anaitwa RAHMA sio SABRINA, nisamehe binti yangu mimi ni mama yako mzazi nifanyaje Mimi jamani.
"" Unasemaje mama !! inamaana Sabrina ni Dada yangu ?
"" Ndio Othuman mwanangu huyo ni Dada yako anaitwa Rahma ndio jina nililompa nisamehe mtoto wangu Rahma Mimi ndio mwenye makosa, Aibu gani hii jaman angalia leo hii umeshiriki kitendo kibaya na kaka yako nisameheni watoto wangu.
Rahma baada ya kusikia maneno yale aliondoka akiwa amechanganyikiwa, Othuman aliishiwa nguvu akajikuta amechoka mwili mzima, Rahma alirudi nyumbani, alipofika Nyumbani alimkuta Baba Martin na wengine wamekaa nje alipiliza hadi chumbani kwake akiwa analia sana. Hussein alimwita Rahma lakini Rahma hakuitika aliingia ndani kwake akafunga mlango. Baba Martin pamoja na Hussein walijaribu kumwita na kugonga mlango lakini Rahma hakufungua mlango, Rahma alipokuwa ndani alijuta sana kwa kitendo alichofanya alishika tumbo lake akiwa anatokwa na machozi akachukua kalamu na karatasi akaanza kuandika .
Fatuma alipata wasiwasi mkubwa akamwambia Othuman ampeleke anapoishi Rahma. Haraka haraka walichukua gari wakaondoka walipofika waliwakuta Hussein na baba martin wakimuita Rahma. Hussein alishangaa kumuona Othuman amekuja na Fatuma, Hussein alimuuliza Othuman :-
"" Kuna nini Othuman ulikuwa pamoja na Sabrina au kwa maana hatuelewi kuna kipi kinachoendelea hapa ?
Fatuma alimuangalia Hussein kwa hasira akamshika shati kisha akasema :-
"" Unauliza kitu gani wakati wewe ndio chanzo mshenzi mkubwa wewe unaona sasa kitendo ulichonifanyia kule kijijini Bitale nilipata ujauzito na nikamzaa Mtoto wa kike kwa kuogopa aibu na hali ya maisha niliamua kumtupa Mtoto wako na kama ulikuwa hujui Rahma ndiye mtoto wako ninaemzungumzia hapa.
""Rahma ndio nani mbona sikuelewi?
"" Hunielewi eee sawa sasa nisikilize unielewe vizuri Sabrina unaemjua wewe ambaye unataja jina lake hapa ndiye mtoto wako na haitwi SABRINA jina lake ni RAHMA nililompatia mimi
""Nini inamaana Sabrina ni mtoto wangu mungu wangu kwanini ulimtupa mtoto wangu hata kama nilikukosea vipi unawezaje kumtupa Mtoto wako tena wa kumzaa mwenyewe umemkosea sana mungu
Fatuma na Hussein walishikana mashati na kuanza kugombana kila mmoja alimuona mwenzake ndio mkosaji, Baba martin aliwaamua akawaeleza wamalize la aliye ndani kwanza. Hussein alijitahidi akavunja mlango walipoingia ndani wote walishangaa, hawakuamini walichokiona. Walimkuta Rahma amejinyonga kwa kutumia shuka alilofunga kwenye feni , Hussein alimfungua Rahma alipomkagua aligundua Rahma ameshakufa, Juu ya Kitanda waliona Barua Othuman akaisoma kwa sauti 📖📖📖
💌 Othuman najua utaumia sana kwa maamuzi haya, lakini sina budi kufanya hivi kwa sababu nitaiweka wapi sura yangu nimefanya mapenzi na kaka yangu na nina Ujauzito hivi Mtoto nitaemzaa siku akitambua ukweli atanitafsiri vipi Mimi mama yake Pia Jamii kwa ujumla nitaeleza nini Mimi 😢 Hapana siwezi kuishi naomba mwambie baba yangu Hussein anisamehe sana nampenda sana baba yangu, Pia wambie wazazi wangu kwamba nimefanya hivi ili kufuta aibu katika familia yangu.
Fatuma alipogungua Rahma ameshafariki alisimama akakimbia nje akiwa anasema:-
"" Hapana huwezi kufa binti yangu huwezi ngoja nifuate vifaa hospital nije nikusaidia Rahma wangu .
Othuman aligundua mama yake amechanganyikiwa alianza kumkimbiza ili amziwie alimkimbiza hadi barabarani wakati Fatuma anavuka Othuman aliona gari linakuja kwa kasi sana, Othuman alifika akamsukuma mama yake nje ya barabara lile gari lilikuwa karibu sana lilifika likamgonga Othuman na kumrusha nje ya barabara. Othuman alipoteza maisha papo hapo, Fatuma alimsogelea Othuman akaanza kumwita :-
"" Othuman mtoto wangu amka baba usilale, Mama yako nipo hapa si ulisema huwezi kulala kabla mama yako sijalala amka mwanangu usilale
Fatuma aliita sana akaanza kuomba msaada Ghafla wananchi walikusanyika na kumchunguza Othuman walipogundua Othuman ameshakufa walimwambia Fatuma kwamba mtoto wako ameshafariki Fatuma alikataa alisema haiwezekani akazidisha kulia wakati analia alianza kucheka sana, Fatuma akacheka zaidi watu wakashangaa kuona hilo. Wakamchukua Fatuma pamoja na mwili wa Othuman wakawapeleka hospital, suleyman alipewa taarifa akawahi hospital alipofika Daktari alimwambia FATUMA amepata uchizi .
Suleyman akishirikiana na familia ya baba martin walifanya maziko ya watu wawili kwa siku moja. Baada ya maziko suleyman alimchukua Fatuma japo alikuwa chini akaenda nae nyumbani. Baada ya miaka mitatu fatuma nae alipoteza maisha.
____________________________________
#CHA__KUJIFUNZA
Wewe mwanamke / Msichana unaesema unakwenda na wakati kuwa makini katika suala la kutoa mimba au kutupa watoto kwa sababu hujui kesho yako itakuaje. Unaweza kuiangamiza familia yako kama yaliyotokea kwa Fatuma.
Tambua kosa la baba si kosa la mtoto kumbuka mungu anakuona, Pia Wewe msichana unaetoa ujauzito kwa siri na kujiona bado ni Msichana unajidanganya kuwa wewe bado ni msichana lakini ukweli wewe si msichana ni mama wa marehemu.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: