UTAMU WA BINAMU 63





SEH.63  Nilinyoosha mikono juu nikamwambia nipo tayari kufa lakini sio kufanyiwa mchezo huo mchafu na wenye uzalishaji mkubwa hasa kwa mwanume rijali kama.Basi jomba hakuwa na jinsi ingine zaidi ya kukoki bastola yake akafunga macho na kuanza kuhesabu moja….mbili…ile taatuuuuu na mimi nilishituka usingizini.
Nilikuwa nahema sana na sikujua ndoto hiyo ilikuwa na maana gani.Jasho jembamba hofu na mashaka vilikuwa ni sehemu ya usiku huo.Nilikuwa na wakati mgumu sana maana nilihisi ile ndoto ilikuwa na ukweli na ndio maana mjomba alirudi ghafla kutoka hiyo safari yake aliyoenda.Nilitamani pakuche haraka ili niweze kuondoka na kurudi zangu kijijini.Niliamka na kuwasha Tv iliyokuwa kwenye chumba hicho na kuanza kujifariji kwa kunagalia filamu za kusisimua.Niliamua kuangalia filamu za mapenzi nia ikiwa ni kujisaulisha ndoto hiyo.Usiku huo nilimtumia sms dada binamu na kumuambia nimeshindwa kuendelea kuishi hapo kwao nahitaji kurudi nyumbani kwetu nikaishi maisha ya dhiki lakini yenye uhuru na amani kuliko hayo ya raha lakini yenye hofu na vifungo vya ushirikina.
Dada binamu alinipigia na tukaongea kirefu sana akanambia nivumilie tu wiki ijayo anakuja na atanipa zile hela hili tuanze mikakati mingine ya biashara na maisha.Ingawa nilimuitikia lakini ukweli roho yangu iikuwa ikinituma niondoke kwa mjomba na kurudi kwa mama yangu mzazi.Asubuhi ilifika na kujikuta nikiwa bado nipo kwenye Tv nikiangania movie.Nikaamua kujikaza hivyo hivyo na kutoka nje na kufanya shuguli za usafi banadani na mazingira kwa ujumla.Nilifanya kazi kwa nguvu huku nikiendelea kutathimiini uamuzi wangu huo wa kuondoka na kurudi Kijijini.
****ITAENDELEA***


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: