BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA KUMI NA MOJA






ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI: mbona akuna kilicho tokea leo" hapo mzee Haule na mke wake wakashangaa, Malaika alitumia akili nyingi sana, kucheza na akili zao, asa huyu shangazi yake, kwa maneno hayo ya Malaka wote wakatazamana kwa mshangao "una uakika Malaika, kuwa akuna lolote?" mama alimwuliza mwanae ambae toka amefika alionekana mwenye uso wafuraha kuliko siku zote, kwa siku za hivi karibuni toka atangaziwe ndoa na Martin, na yeye mama Malaika alikuwa anatabasamu, maana alisha gundua mchezo wa Malaika, kwa shangazi yake "ndiyo mama, kwani kama kuna jambo lolote, si’ninge kuambia?" aliuliza Malaika kwasauti ambayo mtu yoyote mle ndani ange amini kuwa anachoongea Malaika ni chakweli kabisa, ENDELEA ......
"nikweli jamani, maana ata uso wake unaonekana wenye furaha kuliko siku zote,” alioongea baba Malaika akianza kuamini kuwa apakuwa na tatizo lolote zaidi ni matatizo yasiyo isha ya dada yake, “kumetokea nini mwanangu, mbona leo umechelewa kurudi nyumbani, tena naona umekuja na zawadi za kutoka shamba" alimaliza kuongea baba Malaika huku akitabasamu, "nilipitia kwarafiki yangu, tena nimekuja na zawadi nyingi tu!, nyingine zinashushwa kwenye gari" shangazi muda wote alikuwa ameduwaa, huku ahibu kwa mbali ilimshika, ukweli Malaika hakuonyesha tofauti au dalili ya kugombana na Martin, "he! mwanangu kwarafiki yako ndo mpaka madoa ya nyanya kwenye shati?, Inaonyesha ulikula pilipili nyingi maana hayo macho mekunduuuuuu, kama umetoka kulala au kulia" aliongea mama Malaika, huku akigusa pale kifuani kwenye doa la nyanya, lililo mndokea mchana nyumbani kwa Edgar "yani mama nimefaidi sana leo" aliongea Malaika, kwauchangamfu mkubwa, huku akikwepesha macho yake, yasi tazamane na macho ya mama yeke, wakati huo shangazi yake Malaika alikuwa anatunga sharia, "ok! ndio maana unaonyesha unafuraha sana, vipi ulipoenda kwa Martin ulimkuta?, maana mama yako amesema ulimwambia utaenda huko" lilikuwa swali la mtego, toka kwa baba yake, hapo shangazi ambae alikuwa anajuwa kisa kamili cha Malaika na Martin, akatabasamu, akijuwa Malaika amesha banwa, lazima aongee ukweli, ilimpango wake ukamilike "yes! nilimkuta alikuwa na mteja ofisini, nikaona ngoja nirudi ofisini kwangu, nika malizie shuguli zangu, hapo nikakutana na rafiki yangu, tukaenda kwao seed farm" hapo shangazi akapata nafasi ya kuingiza mtego mwingine "hapo ulipo mkuta ofisini kilitokea nini?, Ebu! ongea bila kunificha, siunajuwa madhara ya kuficha vitu" aliongea shangazi akimkazia macho Malaika, maana anafahamu kuwa Malaika toka akiwa mdogo uwa ana mwogopa sana, "kwani shangazi wewe umeambiwa kimetokea nini, sidhani kama kuficha ukweli ni kitu kizuri" aliongea Malaika huku akitabasamu ila safari hii alijitaidi kumazia macho shangazi yake, ambae alijikuta akitazama chini kwa ahibu, "kwa hiyo hakuna ugomvi wowote na Martin?" alidakia mama yake Malaika, baada ya kuona wifi yake akuwa na lakujibu, huku wote wakionyesha kushangazwa na mambo jinsi yanavyo kwenda "mama hakuna lolote, labda Martin mwenyewe ndio anajuwa" shangazi akaona na anachokitaka kina karibia kuwa "hapo Malaika, unatukosea adabu, kwahiyo uwezi kutumbia wewe mwenywe unatufanya sisi wajinga?" sasa Malaika alisha badilika sura, ikaingia sura ya uoga kutokana na shangazi yake kuongea kiukali "wifi haitakiwi ukali, ebu tumsikilize mtoto anachosema, eti! mwanangu kilitokea nini?" amam Malaika aliongea kwa sauti yaupole sana, "mama mimi naomba uniamini, akuna lolote baya, nivyema shangazi angetusimulia alichoelezwa na mama yake Martin, mimi sijuwi lolote, ila shangazi atakuwa na ukweli wote ambao mimi siujuwi" aliongea Malaika kisha akainuka na kukimbilia chumbani kwake, akimwacha shangazi yake Sonia, amechomwa na yale maneno, japo shangazi alijifanya kutostushwa na maneno yale, "unaona wifi hukimwendekeza huyu binti, atakuwa aolewi, sijuwi atakaa hapa nyumbani mpaka lini?" aliongea shangazi kwa hasira, "dada kwani tatizo lipo wapi? maana ata mtoto mwenyewe anaoyesha akuna tatizo kwenye swala hilo, ila nahisi wewe kunajambo unalijuwa lakini unalificha?" aliogea baba Malaika kwa sauti y achini yenye usuluhishi, kisha mama Malaika akamalizia "ila wifi akuna mtoto kati yetu, sisi ni watu wazima, tunafumba macho kama hatujaona, lakini kuna kitu kilichopo nyumaya panzia" shangazi hakuwa najibu, baada yamaongezi machache shangazi akaaga mama Malaika akamsindikiza kwa gari mpaka barabara kuu, alipo pandaa daladala kisha yeye akageuza, ile kurudi tu! akapitiliza moja kwa moja chumbani kwa mwanae Malaika, ambae alimkuta anatoka kuoga, “niambie mwanangu, naona leo umefurahi sana” aliongea mama malaika huku akikaakwenye kitanda cha mwanae, “yani sana mama, leo nimefurahi sana” alijibu Malaika akiwa amejifunga taulo kifuwani amesimama mbele ya kioo chake kikubwa, “hivi mwanangu huu mchezo umeanza lini?,” ilikuwa sauti ya upole ya mama yake Malaika, iliyo ustua moyo wa Malaika, nakumfanya astuke na kutetemeka, “He! mama mchezogani tena jamani” aliongea Mlaika kwa mstuko huku akijikaguawa kwenye nguo pengine kuna damu inatoka, “mbona umestuka sana mwanangu, ni uomchezo wa kushindwa kunijulisha kuwa umeenda kwa rafiki yako, maana tumezowea kama unaenda sehemu lazima unatujulisha” aliongea mama yake Malaika huku akicheka kwa jinsi mwanae alivyo stuka, “ok! mama sito rudia tena,” alisema malaika huku akishusha pumzi, nzito, hapo wa kaagana huku mama yake akitoka nje ya chumba cha Malaika, Malaika naye akamaliza shuguli zake na kupanda kitani akiinyuwa simu yake ya mezani iliyopo mle chumbani, na kuisogeza kitani alipo jilaza, akachukuwa namba aliyo andikiwa na Edgar akaboyeza kwa uiandika kwenye simu kisha akaipiga na kutegesha mkonga wake sikioni kwake, simu ikaanza kuita, simu iliita mda mrefu mpaka ikakatika, pasipo kupokelewa, “bado hajafika” **** Edgar alifungua mlango wa nyumbani kwake kwa pupa, kuiwai simu iliyokuwa ikihita ndani, lakini ikakatika kabla haja ifikia , alikuwa ndio anafika toka kumsindikiza Malaika, akawasha jiko la mkaa, moto ulipoanza kukolea akabandika yama ya kuku, hisiyo ungwa ile waliyoibakiza mchana, maana awakuiunga yote, wakati anasubiri ichemke, mawazo mengi ya matukio ya mchana yalimpitia kichwani, akakumbuka jinsi Sophia alipo kuja ijiweni kwake na kumwambia asi mfwate fwate, akakumbuka jinsi Martin alivyo mkosa kosa mala mbili kumgonga na gari, alimkumbuka yule mama alie mwagia maji machafu, asubuhi, mwisho aka mkumbuka Malaika, akivuta picha ya tkio zima la toka wakutane mapaka walipo achana usiku huu, huku maswali mengi yasiyo na majibu yakikisumbua kichwa chake, iweje Malaika aje adondokee kwake, au ndio kweli kila kitu kina tokea kwa sababu, maana leo ameachana na Sophia na anampata Malaika, tena yeye akiwa ndie mwanaume wake wakwanza, **** mama Malaika alitoka chumbani kwa mwanae Malaika akaelekea sebleni na kukaa kwenye moja yakochi kubwa, wakati huo mume wake alikuwa chumbani, mama huyu alikuwa anajaribu kutafakari vitu viwili ambavyo alviona kwa mwanae wakati anaingia toka kwa huyo alie msema kuwa rafki yake, kwanza kabisa kwajinsi makalio yake yalivyo kuwa yakicheza, ilionyesha kabisa Malaika akuwa amevaa chupi, na pia kilicho mstua zaidi nikule kuchechemea,  “isije kuwa wamekutana na Martin akamshawishi wafanye mapenzi” aliwaza mama huyu huku akishikwa na kiholo, akaona bola arudi chumbani kwa mwanae akamwulize vizuri, maana mala ya kwanza alishindwa, kutokana na mwanae kustuka sana alipo taka kumwuliza, swala hilo,  **** wakati Edgar anawaza na kutafakari juu ya mambo yaliyo mtokea siku hiyo, huku nako,  Malaika naye alikuwa hivyo hivyo, baada yakuona simu aipokelewi akatoka kitandani na kusimama kwenye kioo, akiwa ajavaa nguo ata moja, alijiangalia kwa muda mrefu, huku matukio ya mchana ya kimjia kichwani, alianza kukumbuka juu ya Martin, licha ya kusimuliwa mambo machafu anayo yafanya kila siku mitaani, lakini jana na leo ameshuhudia kwa macho yake akiwa na mwanamke, tena ofisini, isitoshe wana shirikiana na mama yake kutengeneza mbinu, ili yeye Malaika ndie anaonekane, anatengeneza mbinu ya kukataa kuolewa na Martin, mawazo ya Malaika ya namezwa na kumbukumbu ya jinsi walivyokutana na Edgar, jinsi walivyo cheza na kufurahi pamoja, na ata waliyoanza kale kamchezo kaliko mfanya azidi kumpenda Edgar, na kumchukia Martin mala dufu "siolewi na Martin" alijisemea Malaika, huku akirudi kitandani ,  moja kwamoja alichukuwa simu akajilaza kitandani, akijifunika shuka, akabofya sehemu moja yenyekupiga namba yamwisho kutumika, mkonga ukiwa sikioni simu ikaanza kuita ..., nikwamba nyumba yao ilikuwa na line mbili za simu, moja ya familia na nyingine nia ya Malaika kwajili ya shuguli zake za ofisi, simu hii iliwekwa chumbani kwake, safari hii haikuita sana ikapokelewa, akasikia sauti ya Edgar "hallo Edgar hapa, naongea nani mwenzangu?" hapo Malaika akona ngoja kwanza amjaribu Edgar, aone kama anamwanamke mwingine,  **** "mimi ni yule mchumba wako wa matogoro" Edgar alisikia sauti ya mwanamke, "umekosea namba" Edgar aliongea nakukata simu kwa hasira, maana alitegemea simu kutoka kwa Malaika, mala simu ikaita tena akapokea, akakutana na sauti ya kike tena, lakini tofauti kidogo na ile ya mwanzo "Edgar kweli unanikatia simu" sasa Edgar alitambua anaongea na nani “mh! Kumbe wewe mambo vipi?” aliongea Edgar akijuwa anaongea na Malaika, "umenikumbuka mimi mchumba wako wa matogoro?" Malaika alijaribu kubadirisha sauti "hapana wewe mchumba wangu wa mahenge" wote wakacheka kicheko cha kivivu kilicholegea kimahaba, "kumbe unaijuwa sauti ya mchumba wako?" aliuliza malaika "siwezi kuisahau sauti yako tamu" aliongea Edgar huku akitafuta bakuri, kwenye kabati huku ameikumbatia simu kubwa ya mezani yenyewaya mrefu, "mmh! tamu kama kama nini?" aliuliza Malaika huku akiceka cheka,  "kwani utamu unaelezeka?" aliluza Edgar akuendelea kutafuta bakuri na kijiko, "ndiyo si useme nitamu kamaaa…, lada unataja kitu kitamuuuu" alielekeza Malaika, "si’uniambie nitaje nini" alliuliza Edgar akmtega Malaika aone kama aatakuwa na uwezo wa kusema chochote mbele yake, "si utaje tu! ata vitu tulivyo kula mchana, henheee nimekumbuka unibakizie supu ya kuku, usisaau kuipasha moto" aliongea Malaka kwa sauti iliyo jaa furaha, "tena kama ulikuwepo ndio naichemsha, yani sili mpaka tuje tule wote" aliongea Edgar akiwa na bakuri pamoja na kijko mkononi, akilifwata sufuria la supu jikoni "aya ni subiri, na mimi kuanzia sasa sili chochote, mpaka kesho tukiwa pamoja" aliongea Malaika bila kujuwa kuwa mama yake alikuwa njiani anakuja chumbani kwake, "mh! utakufa na njaa shauri yako" alisema Edgar “ayaniambie sautiyangu tamu kamanini?” alikumbusha Edgar, “haa! Nawewe ujasaau tu!, tamu kama wewe mwenyewe” alisema  "hahahaha! hilooo lione kwanza, alafu mimi ni meshaingia kitandani kwani wewe hupo nanani hapo" aliuliza Malaika akionyesha wivu kidogo "nipo peke yangu kwani vipi?" Edgar alijibu huku anaendelea kupasha mboga moto "mh kama hupo peke yako kweli ni busu" Malaika alianzakushikwa na wivu aswaaaa "mmmwaaaa" Edgar alimchumu Malaika "asanteee, aya!, sasa niambie kama unanipenda kweli kweli" alisema tena Malaika "nakupenda sana, yani nakupenda kuliko unavyozani na kupenda kama Jack na Rose wa titanic" alitaja jina la filamu moja, iliyokuwa imetoka miaka michache nyuma "mhhh! nitaje jina bwana" Malaika aliongea kwasauti ya kudeka "nakupenda sana Malaika, najiona mwenye bahati, Kamani meokota embe dodo chini ya mti wa mwarobaini" alongea Edgar kwa hisia kali sana, "kweli Edgar?, yani unanifanya nizidi kuku penda" aliongea Malaika "asante sana Malaika, nahaidi kuku penda na kukulinda kwenye hatari yoyote ya mwili na moyo" aliongea Edgar huku mama Malaika akiwa amesha fika mlangoni kwa chumban kwa Malaika, "mhh! wewe! mbona unaonja paja la kuku kuku?" Malaika aalimstua Edgar, ambaye kweli alikuwa amesha pakuwa kipapatio cha kuku, anataka kuanza kukitafuna, wote wanacheka "kumbe kweli umedokoa hen?" aliuliza Malaika "nani tena anadokoa mboga?" sauti ya mama Malaika ilisikika vyema masikioni kwa Edgar kupitia kwenye simu,"nani tena anadokoa mboga?" sauti ya mama Malaika ilisikika vyema masikioni kwa Edgar kupitia kwenye simu, Edgar akatulia kusikilizia Malaika na mama yake, wanaongea nini, huku nako, mstuko mkubwa ulimpata Malaika, kwani akujuwa mama yake aliingia saa ngapi mle chumbani, na huku Malaika akiwa bado ajakatasimu alijishika kifuani, akipooza mpigo ya moyo "vipi mwanangu nimekustua sana?" mama Malaika alimuliza mwanae, ambae alionyesha mstuko wawazi "sana mama umeingia saa ngapi?" Edgar alisikia wakiendelea kuongea "sasa hivi tu!” alijibu mama yake,"ok! nilikuwa naongea na rafiki yangu, niliekuwa naye mchana" aliongea Malaika, huku hali yake yakawaida ikirudi "ho! kumbe mlichinja kuku, ndio maana umeshaingia kulala mapema, bila kula" "ndiyo mama, yani nimeshiba sana" simu ikiwa bado hewani, Edgar alisikia maongezi ya mama na mwanae, kisha akasikia Malaika ana mwita "hallo Ed ngoja niongee na mama, nitakupigia usilale" aliongea Malaika "poa msalimie mama" alijibu Edgar "aya nitamsalimia tena yupo hapa anakusikia" **** mama Malaika alisikiliza maongezi hayo pasipo kutilia shaka, kikubwa alianza kupunguza isia kuwa Malaika mchana waleo alikuwa na Martin, maana alimtambua vyema mwanae, kuwa hakuwai kujiusisha na mapenzi, amepanga kufanya hivyo, na mume wake baada ya ndoa "ndiyo mama, naona umerudi tena kuna tatizo?" aliuliza Malaika, baada yakukata simu, huku akijiweka sawa nakujifunika vizuri shuka lake,  "ebu nimbie mwanangu, ulipoenda kwa Martin kilitokea nini?" aliongea mama yake Malaika, huku akikaa kwenye kitanda kikubwa cha mwanae, kama aliyo kaa mwanzo, Malaika alimsimulia mama yake kila kilicho tokea ofisini kwa Martin, mama naye akamsimulia jinsi Martin alivyopigia simu, na jinsi alivyosikia akitukana, mwisho mama alimwambia Malaika kuwa wayaache kama yalivyo, maana wataonekana wabaya, pengine akisha kuwa naye ndani kama mume wake, anaweza kubadirika nakuwa mume mwema kwake, mwisho mama alitoka na kumwacha Malaika akimpigia simu Edgar, baada ya dakika chache walikuwa wakiendelea na maongezi yao yakimahaba, adi walipo legezwa na usigizi nakuagana wakikubaliana kuonana kesho saa tano asubui  **** Shangazi yake Malaika alipo shuka gari(daladala) akapitia kwa mama Martin kabla hajaenda kwake, alikutana na mama Martin, akamsimulia yaliyo tokea nyumbani kwakina Malaika, huku akimficha bahadhi, kikubwa alimhakikishia kuwa ndoa hipo pale pale, hakuna atakaye pinga, walicheka na kugongeana mikono kwa pongezi, wakaagana na shangazi akaelekea kwake***** Wakati huo Martin alikuwa bado yupo bar na yule mshana wabenk, wakiwa wamelewa sana ,wakijiandaa kuingia kwenye chumba walicho kikodi kwa shughuli ya usiku waleo ***** asubuhi siku yapili, wakwanza kuamka alikuwa mschana wa benk, ambaye alijiandaa na kumwamsha Martin, “tayari kumekucha,” katika hali ya ulevi Martin alifumbua macho na kutazama dirishani, kweli kulianza kuwa kweupe, akavuta suruali yake, kaingiza mkono mfukoni, akatoa kibunda cha fedha akampatia yule dada "nitafute baadae wacha nilale kidogo" aliongea Martin huku akivuta shuka nakujifunika gubi gubi, yule binti akaondoka zake kuwai kazini, **** Saa moja kasolo, Malaika akiwa mwenye uso uliojaa tabasamu la matumaini, alikuwa amesha amka, nasasa alikuwa anajiandaa kuondoka akiwa amevalia gauni lefu la blue lilio gusa viatu vyake vilefu vya blue pia nywele zake alizo zichana vizuri, akapiga simu kwa Edgar, simu iliita kwa sekunde chache, kisha ikapokelewa na sauti nzito yenye kulewa kwa usingizi "hallo" "wewe mwanamme bado umelala" aliongea Malaika kwa sauti ya chini yakuvutia, "ha! Malaika umeshaamka, kwani sahizi saa ngapi?" aliuliza Edgar kwa sauti ya kivivu,  "saa moja na nusu, amka bwana uwai kazini " alisema Malaika kwa sauti ya kubembeleza, "poa nimesha amka mke wangu, ngoja nijiandae, baadae nitakupitia" ile kuitwa mke ilimsisimua sana Malaika, akakatasimu, kisha akarukaruka kwa furaha mlechumbani, kabala haja chukua mkoba wake wa blue na funguo zagari na ofisi, kama kawaida alipotoka nyumbani, alianza kuzunguka kwenye maduka mawili, kisha kwenye kiwanda cha kushona, alipo lizika yako poa, akaanza kuelekea kwenye duka languo, ambako kuna ofisi yake, sasa basi wakati anapita sehemu moja, akaliona gari la Martin likiwa limepaki nje ya lodge ya Nyumbani Peace, akatazama saa yake ya mkononi, ilikuwa ni saa mbili na robo, “mh! huyu anafanyanini mapema hii, hapa guest, lazima atakuwa amelala hapa hapa” aliwa za Malaika huku akikata kona kkuingia Nyumbani peace lodge, na kusimamisha gari lake kwenye maegesho ya Hotel hii, “leo wata juwa kuwa mimi nina akili kuliko wao HAYA SASA TUONANE KESHO ILIKUJUWA, MALAIKA ALIFANYA NINI HAPO HOTELINI, PIA TUONE KILICHO ENDELEA KATI YA WAWILI AWA, like page yetu Hadithi ZA MBOGO EDGAR



No comments: