BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA






ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI : Huku nako Malaika alipata wazo, lakini iliwazo lake litimie lazima aongee na Edgar, swali likabaki, je? ataongea naye vipi, maana chumba kile akikuwa na simu, na pia nguo na vitu vyote ambavyo alitakiwa kuvitumia kesho vilisha letwa pale chumbani, akuwa nakisingizio, atafanyaje akaona bora atumie akili za ziadi, aliwaza hayo Malaika akiwa amelala katikati ya shangazi na mama mdogo Semeni, ambao walikuwa wamesha pitiwa na usingizi, yeye alikuwa amesha tengenezwa nywele, na amepakwa rangi za kucha, pia alikuwa amechorwa kwa ina kama wafanyavyo watu wa pwani ya mashariki, tayari kwa kuingia kanisani kesho mapema, endelea.........
 Malaika litumia muda mrefu kuwaza jinsi ya kufanikisha mpango wake huo, alio uwaza, mpaka alipopitiwa na usingizi saa tano, leo alilala mapema kidogo tofauti na sikumbili zilizopita, **** Saa tano usiku ilisikika Sauti ya music, ilikuwa ni sauti kubwa sana ndani kwa Edgar, ni reggae ya bob marley ilikuwa inalindima, bandika bandua, ukiisha wimbo huu unaingia mwingine, lakini msikilizaji wa music huo alikuwa amesha pitiwa na usingizi, ni baada ya Edgar kumaliza chupa moja kubwa ya pombe kari, kati ya zile mbili alizokuja nazo nyumbani, alikuwa amelala fofo akikoroma juu ya kochi, ***** Ilikuwa juma mosi saa kumi na mbili kasolo, ndipo Malaika alipoamshwa ilikuanza kujiandaa kwenda kanisani, kula kihapo cha ndoa, awe mke alali wa Martin Johnson Komba, mapigo ya moyo yalimwenda kasi Malaika, alikuwa anawaza namna yakuepuka hii ndoa, japo aliona uwezekano ni mdogo sana, naam maandalizi yalianza, wapambaji walianza kazi ya kumuandaa bibi harusi, Malaika alipambwa akapendeza mala mbili ya uzuri wake wa kawaida, mwisho wakamalizia kwa kumvesha gauni jeupe maalumu kwa ajili ya harusi (shera), kwa kweli Malaika alipendeza sana, akuna mfano wake kwa maandishi,
Wapambaji walimtoa kule chumba cha nje, na kumpeleka sebuleni nyumba kubwa, tayari kwenda kanisani, hapo sebuleni alikaa sambamba na msimamizi wake wa kike, ambae alimkuta yupo pale tayari kwenda kanisani, walikuwa wawili tu!, hakiri ya Malaika ikafanya kazi mala mbili, akaiangalia simu juu ya meza ndogo kwenye kona ya sebule yao, lakini akakumbuka namba zipo chumbani kwake, hakuwa amezishika kichwani, na muda unazidi kusonga, ilishatimia saa moja na nusu, saa mbili kamili muda wakuingia kanisani, “lazima nitumie muda huu” alijisemea Malaika, ***** wakati huo huo, pale nyumbani peace kwenye chumba kimoja, binti mrembo toka dar alikuwa amesimama akimalizia kuvaa vizuri, tayari kwenda kanisani kushuhudia watu wakila viapo vya ndoa, akaweka vizuri mabulungutu ya pesa aliyo pewa na bwana wake, ambae alikuwa nae usiku kucha, na sasa alikuwa bado amelala mle chumbani, kutokana na kuzidiwa na pombe za jana usiku, alipomaliza kuweka vizuri pesa zake, aka mwamsha mtu wake kwa ajili ya kumuaga, iliyeye aende kanisani, alimstua kwa muda mrefu adi jamaa alipo kurupuka toka usingizini “mungu wangu nimechelewa” alikurupuka Martin akitaka kutoka bila kuvaa nguo, lakini yule binti alimuwai mlangoni akamzuwia, Martin akagundua kwamba kweli hakuvaa nguo, akarudi na kuvaa nguo na kutoka mbio, akimwacha yule binti akimshangaa huyu mtu asielewe kilicho msibu mpenzi wake huyo, dakika kumi mbele Martin alikuwa akisimamisha gari nyumbani kwao, watu walisha msubiri kiasi cha kukata tamaha, sasa wanamwona Martin akiingia mbio mbio, huku akinuka pombe vibaya mno, zilibaki dakika ishilini ili misa (ibada) ianze, msimamizi wake wakiume anmbae alikuwepo tayari pale nyumbani, akaanza kumsaidia kujiandaa, kwanza Martin aliingia bafuni kuoga, alitumia dakika tano, akaanza kujiandaa kwa kuvaa, baada ya dakika kumi alikuwa amesha maliza kujiandaa, watu wote walikuwa wakimzungumzia vibaya, kwa tabia aliyo ionyesha, tena siku yake ya harusi mbele ya wageni walio kuja kushuhudia harusi yake, ****akiwa pale sebuleni Malaika akiwa na msimamizi wake wakike, alichezesha akili mpaka akapata jibu, akasoma ramani ya mchezo, akawaona watu wapo bize na pilika pilika za harusi, mama yake alikuwa chumbani pamoja na baba yake Malaka, “ngoja kwanza niende chooni, maana nikiingia kanisani, sitopata nafasi ya kwenda chooni” Malaiaka akamuaga msimamizi wake wakike kuwa anaenda chooni kujisaidia, akainuka na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake, alipoingia tu! akuzubaa moja kwa moja akaelekea kwenye simu, kitendo cha haraka akainua simu, na kuchukua kikaratasi chenye namba, akainua mkonga na kubonyeza namba haraka haraka, kisha akaitega sikioni kusikilizia, simu iliita kwa muda mrefu, “pokea! pokea! pokea simu Edgar baba” Malaika aliomba simu ipokelewe haraka, **** mlio wasimu ulimstua Edgar toka usingizini pale juu ya kochi, mwanzo alizani ni mawenge ya usingizi, lakini akagundua ni kweli simu ilikuwa inaita, baada ya kukaa kimya siku tatu bila kuita, Edgar akainuka haraka na kwenda kuipokea, huku mapigo ya moyo ya kienda kasi “Hallo…..hallo” Upande wapili ulikuwa kimya, zaidi alisikia sauti ya pumzi ya mtu anaye pumua, huku akivuta mafua ku jizuwia kulia, alikuwa Malaika akijizuwia kulia, ni kilio cha gafla baada ya kusikia sauti ya Edgar, kisha kwa sauti ya chini yenye kujizuwia kilio cha uchungu na hasira “Edgar ni kweli una nipenda?” moyo wa edgar ulilipuka kwa furaha, baada ya kuisikia sauti ya Malaika, japo ilikuwa iemeambatana na kilio cha kwikwi, lakini ile kupigiwa simu, ilionyesha ni kiasi gani Malaika alitambua uwepo wake, ukizingatia kwamba leo hii ana funga ndoa “Malaika na kupenda kuliko unavyoweza kuzani, siwezi kueleza jinsi navyo kupenda, yani sidhani kama kuna mtu alisha wai kupenda kama ninavyo kupenda” Malaika alitambua kuwa, jibu la Edgar lilitokea ndani kabisa ya moyo wake “Edgar unakumbuka uliniambia kuwa, hupo tayari kunipigania kwa hali yoyote?” aliuliza Malaika huku akiachia kicheko cha chini, kilicho changanyika na kilio “Malaika nipo tayari kwa uwezo wangu wote, lakini Malaika nasikia unaolewa leo nikweli?” Swali hilo alikujibiwa, zaidi Malaika aliongea kwa msisitizo “Edgar usiniache niondoke mume wangu, njoo unichukue, fanya haraka, nazani pikipiki yako inamafuta, njoo nichukue kanisani matogoro, fanya haraka” Kauli hiyo ilimchanganya Edgar, maana akuelewa Malaika anamaanisha nini, alipotaka kumwuliza akasikia Malaika akiitika “abee mama nakuja” kwa maana kuna mtu alikuwa akimwita, ni mama yake, alipo mkosa sebuleni aliambiwa yupo chumbani kwake ameenda kujisaidia kwenye choo cha huko, akamfwata huku akimuita, kweli Malaika alitika na mama yake alipoingia chumbani, alimkuta amesimama karibu na kioo chake kikubwa, pembeni kuna simu ambayo ilikuwa imekaa vibaya, baada ya mtumiaji kuiweka pembeni ya sehemu yake, baada ya kuitumia, pia Malaika alionekana kama alietoka kulia muda mfupi uliopita, “mwanangu leo utaniliza sana, ebu! jikaze kidogo, twende unasubiriwa nje” Malaika alikuwa wakwanza kutoka nje ya chumba, mama yake aliinua mkonga wasimu na kuweka sikioni, akagundua kuwa ilikuwa hewani, bado aija katwa, “hallow.. .......hallow” akaita kwa lengo la kumjuwa aliekuwa akiongea na mwanae, akizani kuwa ndie ambae alikuwa akiongeanae mala kwa mala, lakini akujibiwa zaidi simu ikakatwa, naye akaiweka mahali pake, kisha aka tabasamu, huku akitikisa kichwa, “mh! sijuwi nini kinaendelea” ***** Baada ya kukata simu Edgar alikaa kwenye kochi akitafakari juu ya maagizo ya Malaika hakujuwa anamaanisha nini, baada ya nusu saa mbele akazinduka toka mawazoni akaingia bafuni akaoga, alipomaliza akaona kwakuwa anaenda kanisani bora avae suit aliyo letewa na mama yake, na shati jeupe kwa ndani, akavaa pamoja na viatu vyeusi, alivifuta vikang’aa, sana akapanda juu ya pikipiki yake, alipiga sana kiki mpaka ikakubari kuwaka, akaondoka zake kuwai kanisani Matogoro, kushuhudia Malaika akiolewa, **** Ndani ya kanisa la matogoro watu walikuwa wengi sana, Misa ilichelewa kuanza sababu bwana harusi alichelewa kuingia pale kanisani, Malaika alikuwa ndani ya gari akaingaza macho huku na huku, pengine ange mwona Edgar, lakini hakumwona, waiendelea kumsubiri bwana Harusi, huku kila mmoja akisema la kwake, wapo waliosema walimwona bar mpaka usiku sana, wapo walio sema kijana alikujwa na dharau sana,
 baada ya kumsubiri sana bwana harusi, atimae Martine akawasili, bwana Harusi alipoingia tu, awakuchelewa, wakashikana mikono na bibi harusi, huku wasimamizi wao wakiwa nyuma yao wakaingia kanisani nakwenda kukaa mbele kabisa, nyuma yao wakifwatia wasimamizi na nyuma tena wazazi wa pande zote mbili, Malaika aliweza kuisikia vyema harufu mbaya ya pombe toka mdomoni kwa mume wake mtarajiwa, kila alipo pumua, ikionyesha jamaa amekesha kwenye pombe, na pengine akupata ata nafasi ya kupiga mswaki asubuhi ya leo, Malaika alikeleka sana, aliwaza matukio machache ya kumfumania, akiwa na wanawake bar, alijikuta akidondosha machozi, maana alivuta picha kuwa hizo pombe hakuwa amekunywa peke yake, “Edgar baba njoo unichukuwe” aliwaza Malaika, ambae
muda wote alikuwa akipambana na arufu kari ya pombe, yenye kukela toka kwenye midomo ya Martin, huku macho yake ya kiangaza huku na huko, kutazama kama Edgar alikuwepo ndani ya kanisa, lakini akumwona, kitendo cha Malaika kuangalia huku na huko japo kilikuwa ni cha umakini sana, kiasi watu wengine kuto kujuwa, lakini mama yake alisha kiona, maana alikuwa makini sana huku moo wake ukimtuma kuna kitu mwanae anakwaza, mama Malaika akajaribu kufwatatilia, ili ajuwe mwanae ana angalia nini? ****ndani ya kanisa Mzee mbogo na mwanae mdogo Prosper, walikuwa wamekaa pamoja upande wa wanaume, mama Edgar alikuwa upande wa wakina mama, karib kabisa na mume wake na mwanae, wakitenganishwa na uwazi katikati ya kanisa, unaotumika kama njia ya kupita waumini, na kuwafanya wawe karibu kiasi cha kuonana kwa ukaribu sana, pengine wengeweza atakunong’ona,
Pia karibu na mama Edgar, mtu wa tatu toka kwake alikuwa ni mschana matata Veronica, binti huyu licha yakujivunia laki tano toka kwa bwana harusi mtarajiwa, lakini alishikwa nafadhaa baada yakumwona Martin ndie wana harusi, na sasa yupo mbele ya kanisa akifunga ndoa, alifadhaika siyo kwa sababu amefanya naemapenzi kwa siku hizi mbili, lakini alimwonea huruma bibi harusi mtarajiwa, maana Martin ameamkia guest kifanya uzinzi, na sasa yupo kanisani anafunga ndoa na mwanamke huyu, akamsikitikia sana bibi harusi, kisi cha mwenzie aliekuwanae pembeni kumwuliza, “vipi mwenzetu, mbona hivyo?” ilikuwa ni sauti ya chini tka kwa dada mmoja alietoka nae Dar, “mwenzangu sijuwi nisemeje, siuna kumbuka nilikusimulie kuhusu yule jmaa nilie kuwa nae guest” alisema Veronika kwa sauti ya chini pia, mama Edgar alikuwa akiwaskia pia, “ndiyo nakumbuka siume nisimulia leo hii, tukiwa nje yakaisa” alijibu yule mwenzie akianza kuonyesha ahadhari, “uwezi amini, ndio huo bwana harusi” siyo yule dada peke yale, ata mama Edgar akapigwa na butwaa, huku nako  Misa iliendelea, vipengele vilipita, taratibu zilifanyika, sasa ukawadia ule wakati ambao kilamtu alikuwa akiusubiri, ni wakati wakula kiapo cha ndoa, nakuvalishana pete, padre alianza kwa Martin huku akitumia kipaza sauti “utanifwata ninavyo sema, … mimi Martin Komba “ “Mimi martin komba” Martin alifwatisha maneno ya padre, huku tabasamu la ushindi likiwa limechanua usoni mwake “nimekubari kumuoa Malaika Haule” adi hapo Malaika alionyesha kukata tamaha, wasi wasi ulimzidi, mama yake aliweza kumwona wazi binti yake akianza kuonyesha uso wauzuni, wakati huo Martin alikuwa akiendelea na kiapo, Baada ya kumaliza upande wa Martin shangwe na vigelegele vikasikika toka kwa mashuhuda, sasa ikaja zamu ya Malaika, watu walikuwa kimya, kama vile mle kanisani akukuwa na watu zaidi ya padre na Malaika, naye akaambiwa “utanifwata kama ninavyo sema,…….. mimi Malaika Haule” “mimi …………..” hapo Malaika alisita kidogo, hali ya utulivu ikiwa imetawala ndani ya kanisa Malaika na waumini wengine wakisikiliza mlio mkubwa wa pikipiki, ambao ulisikika kanisa zima, kwa mala ya kwanza, mama Malaika aliweza kushuhudia tabasamu pana la matumaini mapya usoni kwa mwanae, misiri ya juwa linalo chomoza baada ya mvua kari ya upepo “…. Malaika Haule” Malaika alimalizia sentesi yake baada ya muungurumo wa pikipiki kuzimwa, na padre akapata nafasi yakuendelea, “nimekubali kuolewa na Martin Komba” hapo Malaika aliinua usowake akamtazama Martin ambaye alikuwa ametoa tabasamu la ushindi, lililomkela sana Malaika, kisha akageuza uso wake kutazama mlango mkubwa wakuingilia mle kanisani, mama Malaika alimfwatilia mwanae akigeuza shingo kutazama aliko tazama mwanae,  akamwona mwanae akizidisha tabasamu ambalo watu wengi walilishuhudia, wakizani nifuraha aliyonayo binti huyu, nikwaajili ya kufunga ndoa na mwanamume anaye mpenda, lakini kwa mama yake Malaika akiri ikamcheza haraka akatazama zaidi mlango mkubwa wakuingilia mle ndani ya kanisa, ambako mwanae alikuwa ametazama, naam sasa mama Malaika alimshuhudia kijana anaye mfahamu akiwa anaingia kwa mwendo wa taratibu huku macho yake akiyaelekeza mbel kabisa ya kanisa, mama Malaika aliweza kumtambua kijana huyu, ambae leo alionekana kuwa smati sana, akipendeza ka suti aliyo ivaa, japo hakumfahamu kwa, jina lakini anamjuwa, tofauti na alivyo zowea kumwona yule kijana, uwa ana avaa tishert na jinsi, leo alipendeza sana, baba Malaika naye pasipo kujuwa kilicho mtuma, akageuza kichwa kuangalia alipo angalia mke wake, ni kawaida unapoona mwenzio anaangalia kitu na wewe lazima utageuka, mzee Haule anamwona kijana mmoja ambae si mgeni sana machoni mwake, pasipo kujiuliza mala mbili, akapuuza na kutazama mbele, mwingine alie gundua uwepo wa kijana huyu, ni Prosper ambae alimstua baba yake kwa kumnong’oneza “baba mwone kaka alivyo pendeza” mzee Mbogo akugeuka peke yake, mke wake mama Edgar nae aligeuka wote kwa pamoja wakamtazama Edgar akiwa amesimama atuwa chache toka walipo kaa wao, kama aliekuwa anatafuta pakukaa, huku macho yake kaya elekeza kwa bibi Harusi, mzee Mbogo alistahajabishwa na jinsi mwanae alivyopendeza, alizowea kumwona akiwa amevaa jinsi na tishert, kiasi kwamba mzee huyo alisha shikwa na kicheko, akajizuwia kucheka,  lakini wakati huo huo, walizinduliwa na sauti ya bibi Harusi kule mbele, ambae alikuwa anakula kiapo “hapana sipo tayari kuolewa na Martine, yeye mwenyewe na wazazi wake wanajuwa sababu” Watu wote mlendani walistuka sana, sauti za fadhaa zilitawala, miguno ya ghafla kama sauti za kundi la nyuki linapita eneo hilo ilisikika, Martine na wazazi wake walistuka sana, nyuso za fadhaa na aibu zikiwashika, mama Martin hakuwai kuwaza kama kinaweza kutokea kitendo kama hicho, alizani kuwa Malaika atakufa kikondoo, ghafla mama Martin aliona mwili ukimlegea, na macho yake ya kijawa na giza, kisha akapoteza fahamu, huku akianguka chini, mama Malaika alitabasamu kidogo, ni tabasamu la matumaini mapya, huku mume wake akishangaa kwa kitendo kile cha mwanae kukataa ndoa kanisani, kisha akamshuhudia mwanae kiinama chini, akavua viatu vyake vilefu akavishika mkononi, kisha akakunja gauni lake na kulishika kwa mkono mwingine, alafu akaanza kutembea akipita katikati ya watu, kuufwata mlango mkubwa wa kuingilia, macho yote usoni kwa Edgar akijaribu kumpa ishara fulani, unzani Martin atakubari bibi Harusi atoke kanisani, itaendelea......... kwastory zaidi like page yetu Hadithi ZA MBOGO EDGAR Devotha Salufu HII HAPA



No comments: