BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA PILI




TULIPO ANZIA: Kijana Edgar Mbogo anamfumania, mchezaji wa mpila wa kikapu na muuza viatu vya mtumba, anamfumania mpenzi wake Sophia, akiwa na kijana tajiri sana mwenye fedha nyingi Martin Johnson, ambae kwa sasa ni bwana Harusi mtarajiwa, akijiandaaa kufunga ndoa siku chache zijazo, wakati huo huo kijana Edgar anaokota diary ya mschana mmoja mrembo sana, nakuiifadhi akiaidi kumkabidhi siku akikutana naye.

ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA: dah! adharani kabisa,” aliendelea kuwaza Edgar, kijana alie jengeka mwili kimazoezi, kwakuwwa maili katika mchezo wa mpila wa kikapu (basket ball) anao upenda sana, “dah! kama ningekuwa nimemtambulisha kwa mzee Mbogo sijuwi ninge iweka wapi sura yangu?” aliwaza sana Edgar pale juu ya kitanda chake,  baada wakuwaza kwa muda kidogo, Edgar anainua uso wake nakuangalia saa kubwa ya ukutani. “saa moja na nusu nimesha chelewa” ENDELEA.......
Edgar alipiga kelele huku akiinuka haraka toka kitandani, na kuanza pilika zake za anazo zofanyaga kila siku, anaonekana Edgar anaenda sebuleni akiwa amevalia bukata bila tishert, anabadirisha tape kwenye redio anaweka kanda (tape record) nyingine ya hip hop halafu anaenda sehemu ya kulia chakula anafanya mazoezi mengi mchanganyiko akifwata mapigo ya mziki wa hip hop alio ueka kwenye redio cassata, mwisho anamalizia kwa kupiga push up ishirini, baada ya kumaliza, sasa anaanza maandalizi ya kuandaa kifungua kinywa, ni baada ya kupiga mswaki na kunawa uso, alitoka nje akazunguka nyuma ya nyumba kubwa kiasi, akiyapita mabanda mabali mbali mbali ya mifugo, kama kuku sungura, pimbi (simblisi) nawengine kibao, kama kanga bata N.K, kisha akaingia kwenye shamba kubwa sana, lililotawaliwa na miti ya matunda ya aina mbalimbali machenza, mananasi, matopetope, machungwa, mapeasi na farafaraji pia mazao kama karanga, viazi vitamu, mahindi pia mboga za majani kila aina pamoja na nyanya, hivyo vyote viliwekwa kwa mtindo wa bustani, na hutumia mto uliokatiza hapo kwao kumwagilia mazao haya, pia bwawa kubwa la samaki wakufugwa, lilikuwepo mwishini kabisa mwa eneo upande wa mtoni
Baada ya kuingia shambani, Edgar akaibuka na viazi vitamu viwili kisha akapitia kwenye banda la kuku wa kienyeji, akachukua mayai manne, akaelekea jikoni, na ndani ya muda mfupi alikuwa ameshatengeneza chips ya viazi vitamu, na mayai ya kukaanga pembeni na chai ikiwa imejaa kwenye kikombe,  akiwa anaanza kula kijana huyu, akakumbuka tena tukio la jana pale Nyumbani Peace Logde, hamu ya chakula ika isha kabisa, japo Edgar alitumia kama dakika tano, kujaribu kusahau tukio lile la kumkuta mpenzi wake Sophia Mapunda mwenye umri wa miaka ishirini na saba,  na yule kijana wa kitajiri Martin Johnson, wakifanya uchafu wao adharani, lakini hakuweza na hamu ya kula ikazidi kupotea kabisa.
Hapo akaifadhi chakula kwenye bakuli moja kubwa yenye mfuniko, kipindi hicho hot pot ilikuwa adimu sana,  na kuifunika vizuri kisha akaiacha pale pale juu ya meza akachukua begi dogo la blue lenye vifaa vyake vya mazoezi, akatoa ile diary na kuiweka kwenye meza kubwa pembeni ya TV kubwa ya inchi 24, kisha akaweka mpira ndani ya begi kama kawaida yake, maana siku zote uwa akimaliza shughuli zake za biashara, jioni lazima apitie mazoezini, wkati anataka kutka, kaiona ile diary ya yule dada mrembo sana aliyekutana nae jana pale Nyumbani Peace, akaichukuwa pale juu yameza, aliwaza kidogo huku ile diary ikiwa mkononi, kisha akairudisha mezani, Edgar kwa kuwa alikuwa amechelewa, akaona si vibaya akitumia pikipiki yake kubwa, aliyopewa na baba yake baada yaa kununua land rover one ten, nipiki piki kubwa sana, ambayo alikuwa ajaitumia ya pata wiki mbili zilizopita, akaiendea kule inakokaa, ni kwenye sehemu iliyo jengwa kwaajili ya maegesho ya gari, akafungua kifuniko cha mafuta akachungulia ndani, akaona patupu, akajaribu kuitikisa kidogo, labsa ange sikia mafuta yakitikisika, lakini kulikuwa hakuna kitu, hapo Edgar akiwa mevalia rubber zake nyeupe, suruali ya jinsi ya blue mpauko na t-shirt ya kijivu, iliyomkaa vyema mwilini akaamua atembee kwa miguu, awahi kwenye shughuli zake za kila siku, maana kule kwao hapakuwa na daladala. kwa kipindi hicho *****
Malaika Willson Haule, ni mshana mrembo wa miaka ishilini na sita, mida hii alikuwa amesha jindaa, tayari kwenda kazini, akiwa amevalia suti yake ya rangi ya kijivu ya suruwali ndefu iliyo mkaa vyema sana na kuruhusu kuonekana jinsi alivyo jaliwa umbo zuri lenye mapaja manene na makalio makubwa ya wastani, huku juu akiwa ame valia kikoti kifupi cha kijivu kilicho achia wazi kifua chake, na kuruhusu shati lake jeupe alilovalia, kuonekana likiwa lime ficha maziwa makubwa ya wastani yaliyo simama vyema kukiwa hakuna dalili ya kuvaiwa sidilia, chini kabisa alikuwa amevalia viatu yake vyeusi, vya visigino virefu, na mikanda ya njano, kichwani malaika alikuwa ame zichana vyema nywele zake fupi alizo zinyoa kwamtindo wa kupendeza, Malaika alikuwa amesimama mbele ya kioo chake kikubwa kwenye meza yake ya vipodozi, Malaika alijitazama sana kuamziajuu mpaka chini, huku akiwaza tukio alilo lishuhudia jana pale Nyumbani Logde, lilimjia kichwani tukio la kukumkuta mchumba wake, yani mumewake tarajiwa, ambae wamebakiza siku chache tu wafunge ndoa, akifanya uchafu ule nadani ya ukumbi wa bar, “inamaana watu wengi sana wamesha washuhudia, sinitakuwa nazaraaulika sana “ aliwaza Malaika,juu ya mume wake mtarajiwa, ambae kuikweli aliuwa anafahamu toka utotoni, sababu wazazi wao ni marafki wakubwa sana, kipindi wakiwa wame maliza kidato cha nne, kabla yeye ajaenda kusoma kidato cha tano, aliweza kumshuhudia Martin akiwa anabadirisha wanawake, kila kukicha huku wengine wakipigana kwaajili yake, kipindi hicho akufikilia kama angekuja kuchumbiwa na kijana huyu, “nilimwambia mama Martin anifai, lakin hakuna aliee nisikiliza, aliwaza Malaika pale mbele ya kioo, machozi yakimlenga lenga asa anapo kumbuka jinsi alivyojitunza toka akiwa binti mdogo, akikwepa wanaume walio kuwa walkimsumbua kila kukicha, toka kidato cha kwanza mpaka chuo kikuu, “alafu leo nije nimkabidhi uschana wangu huyu mshenzi” aliwaza Malaika, huku machozi yakimtillika, kimya kimya, “vipi mwanangu mbona kama unalia” Malaika alistuliwa sa sauti ya mama yake ambae akujuwa kuwa ameingia saangapi mle ndani ya chumba chake, “hapana mama, ni mambo yangu mwenyewe” alisema Malaika huku akichukuwa kitambaa chake na kujifuta machozi, “sikia Malaika, najuwa una waza kuhusu kuolewa na Martin, naimani kabisa mkisha oana atatulia, pia unaweza kumweka karibu na kumnyima nafasi ya kufanya ujinga” alisema mama Malaika ambae analijuwa tatizo la Martin, kupenda sana pombne na wanawake, “kwani ni lazima niolewe na Martin?” aliuliza Malaika huku akijizuwia kulia, “sasa tuta fanya nini na wakati baba yako na rafiki yake wamesha amua” aliongea mama Malaika, na wakati huo huo simu ya mezani ya chumbani kwa Malaika ikaita, “akaipokea Malaka Willson, nikusaidie tafadhari” aiongea Malaka huku akilekebisha sati yake isionekane kama alikuwa analia, “mkurugenzi wa Songea girls secondary school, tunaitaji kukupatia tenda ya mavazi ya wanafunzi na wafanyakazi,” ilisikika sati ya kiume upande wapili, “ok! sawa nitapitia hapo nusu saa ijayo” alisema Malaika, kisha akakata simu na kuanza kuanza kutafuta Diary yake ambayo utumia kuandikia kumbukumbu zake, hakukiona kabisa akapekua sehemu zote alizo hisi kuwa ile diary hipo lakini hakuiona, “mwanangu najuwa utanichukia na mimi, usifanye hivyo, nitakuja baadeae ofisini ili tuongee kidogo” aliongea mama Malaika ambae mda wote alikuwa mle chumbani akimtazama mwanae, ambae alimwona wazi kabisa kuwa wanamwingiza kwenye maisha ya tabu kwa kuolewa na na kijana Martin, mtoto wa shemeji yake, yani rafiki wa mume wake, ukizingatia alikuwa anafahamu fika kuwa binti yake akuwai kuingiziwa dudu na mwanamume yoyote, “sawa mama” baada ya makubariano hayo Malaika akatka nje na kuingia kwenye gari lake, nako alitafuta kile kijitabu chake bila mafanikio, “sijuwi nime kiweka wapi jamani? au nilikiacha ofisini” aliwaza Malaika, huku anawasha gari lake aina ya Mercides benzi jeusi, na kuondoka zake, wakatu huo mama yake Malaika alikuwa ame simama mlangoni akimtazama mwanae wakati anaondoka, kiukweli kama mama roho ilikuwa ina muuma sana, kwa mwanae kuolewa na kijana kama Martin, ambae ukiachilia nidhamu binafsi, pia kijana huyu alikosa ustaalabu na kuendekeza pombe na tabia ambayo, amekuwa nayo toka utotoni ya kupenda kila mwanamke, mama malaika aliisha mweleza sana mume wake juu ya tabia mbaya za yule kijana wanae mwozesha binti yao, lakini bwana Haule mzee anae miliki maduka makubwa sana hapa mjini, ambae alisha kukuwa mahari ya miilioni, toka kwa rafiki yake bwana Komba mabasi, hakutaka kusikia juu ya kuvunja uchumba huo walio upanga yeye na bwana komba, juu ya watoto wao, na alisha sema atakae sababisha uchumba huo kuvunjika lahana itamwangukia, Wakati huo malaika alikuwa ana elekea shule ya sekondali ya wanawake Songea, kuchukuwa tenda ya kupeleka mavazi, **** wakati huo kijana Edgar alikuwa amesiama nje ya nyumba moja kubwa sana akitazama pembeni yake, ambako aliliona gari aina ya land rover 110, ambalo liliashilia uwepo wa baba yake, kuwa yupo ndani, kiukweli akutegemea kabisa kumkuta baba yake mzee Mbogo ambae kipindi hicho alikuwa ni mwanajeshi wa jeshi la wananchi, maana mda huu anakuwa amesha enda kazini,  “mh! nikiingia hapa huyu mzee ataanza kuleta zake” aliwaza Edgarakiofia masimango ya baba yake, ambae kila siku alikuwa anamsisitiza kuoa, wakati Edgar akitaka kugeukailiaondoke, mala mlango ukafunguliwa, akatokea baba yake, na saasa alikuwa amevalia sale za jeshi, akiwa na cheo cha afisa mteule, mkononi mwake sehemu ya kuvalia saa,  “ hahahahaha mama Eddy njoo umwone kapela” aliongea mzee Mbogo huku akiachia kicheko cha mwaka, mpaka akapaliwa, maana Edgar aliduwaa na kushindwa la kufanya, “yupo wapi” alisema mama Edgar huku akitoka nje, “haaaa jamani baba Edgar, mbona unamnyima laha mtoto?” alisema Edgar akmtazma Edgar ambae alionekana kabisa kuwa leo hakuwa sawa, “sasa kamasiyo kapela tumwite nani, mtu ataki kuoa basi tafuta mwanamke umjaze mimba, niletee mjukuu” alisema mzee Mbogo baada yakuwa amekaa sawa, akiwa amemaliza kupaliwa, “laini baba Eddy, mtoto simpaka ajiweke sawa kwanza” aliongea mama yake Edgar, “haaaaa! wapi wewe, nime mpatia nyumba mtaji wa biashara, tena nikamwongezea pikipiki, ya kupigia misele, ajiandae na nini tena?” aliongea mzee huyu mwnye watoto wawili tu! Edgar na  mdogo wake waliopishana miaka kumi saba, anaitwa Prosper Mbogo, mida hii alikuwa ameenda shuleni, alikuwa darasa la nne, “kwahiyo wewe unataka mtoto aokote tu ata mwanamke mwenye tabia chafu?” aliongea mama Edgar huku amtazama mume wake ambae ana shuka ngazi kulifwata gari lake, “sasa je, abebe tu wataelewana wakikaa pamoja, hahahaahahahha” aliongea baba Edgar akimalizia kwa kicheko, akaingia kwenye gari lake akaliwasha, “hoyaa! twende zetu! nika kuache mbele hapo” mzee Mbogo alimwambia Edgar,ambae alikataa kwa kutikisa kichwa, kisha mmzee huyu mkolofi akaondoa gari kwa fujo, “usi msikilize baba yako mwanagu, tuliza akili utapata mwanamze zuriiii, tena kuna nguo nimeziona naenda kukununulia baadae” alisema mama yake Edgar, pasipo kujuwa kilicho mtokea mtoto wake huyo, jana jioni kuhusu wanawake, kiukweli Edgar hakuweza kukaa zaidi akaaga, ilikuwai kijiweni japo alijuwa kuwa rafiki yake Jastin kiguru angekuwa amesha fungua bihashara, ***** wakati huo Malaika alikuwa amesha maliza kuchukuwa oda ya mavazi waliyoitaji wateja wake kisha akaelekea mjini ambako maduka yao matatu makubwa yapo, ikiwa ni ratiba yake ya kila siku kuzungukia maduka yote matatu, kisha kutulia kwenye ofisi yake iliyopo pembeni ya duka lao kubwa karibu na mtaa wa zanzaibar, “wacha nijaribu kumbadirisa tabia huyu mwaname, pengine atakuwa mume bola” alijipa moyo Malaika, akiwaza kukutana na mchumba wake huyo mida ya chakula cha mchana, pia akampatie zwadi aliyo mtunzia kwa mda mrefu, lakini wakati anakatiza kwenye Hotel ya Nyumbani peace akaliona gari la Marti likiwa bado lipo pale pale kama alivyo liacha jana jioni, alipo mkuta yupo na mwanamke akimnyonya chuluchulu, “mh! jamani huyu mwanamume ataniauwa, lakini wacha kwanza niongeenae, pengine atabadirika” aliwaza Malaika akipanga kto kumwambia kuwa alimwona jana jioni, ukweli nikwamba Malaika alijaribu kupuuzia huku roho ikimuuma, lakini hakuwa na la kufanya sababu ndoa ni maamuzi ya wazazi wake, asa baba mzee Haule alie shawishiwa na rafiki yake mzee Komba, lakini kwa lililotokea jana jioni, na ili la kushuhudia gari la mchumba wake lipo pale pale Hotelini, lilimfanya Malaika apange kwenda kuongea na Martin, mida ya chakula cha mchana, pamoja na kupatia zwadi alio mtunzia kwa mda mrefu, nia ikiwa ni kwamba, amsisitize aache tabia ya ufuska kama ile ya jana, japo Martin mwenyewe akujuwa kuwa ameshabainika ...... haya mdau bibi harusi mtarajiwa anataka kuogea na bwana harusi mtarajiwa, akipanga kumpatia zawadi, je nizwadi gani hiyo, ambayo inaweza kumbadirisha Martin? vipi bwana Edgar atapata mchumba mwingine, baada ya kusalitiwa na Sophia?, bado tupo mwanzo kabisa wa mkasa wetu wa bibi harusi mtarajiwa, endelea kuifwatilia kila siku, hapahap kwa Hadithi Za Mbogo Edgar



No comments: