BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA TATU







ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI : lakini hakuwa na la kufanya sababu ndoa ni maamuzi ya wazazi wake, asa baba mzee Haule alie shawishiwa na rafiki yake mzee Komba, lakini kwa lililotokea jana jioni, na ili la kushuhudia gari la mchumba wake lipo pale pale Hotelini, lilimfanya Malaika apange kwenda kuongea na Martin, mida ya chakula cha mchana, pamoja na kupatia zwadi alio mtunzia kwa mda mrefu, nia ikiwa ni kwamba, amsisitize aache tabia ya ufuska kama ile ya jana, japo Martin mwenyewe akujuwa kuwa ameshabainika ENDELEA.....
MAMA MALAIKA:
Mahenge D ni mtaa mdogo na tulivu, unaokaliwa na watu wenye fedha nyingi matajiri wa mji huu wa Songea, mtaa huo umepakana na ikulu ndogo ya mkoa wa Ruvuma pembezoni mwa barabara kuu iendayo mikoa ya Mbeya, Iringa, Morogoro, Pwani na Dar es salaam, katika njia moja ya mtaa huo isiyo na msongamano wa magari, wala uwingi wa watu, anaonekana mama yake Malaika, akiwa peke yake ndani ya gari lake dogo jeupe, aina ya Toyota corolla, akiendesha kwa mwendo wa taratibu sana, na kwa tahadhari ya mashimo na vidimbwi vya maji, huku akiwaza juu ya ndoa ya mwanae Malaika, maana ameona amekiona wazi kilio cha mwanae Malaika, juu ya huyu mchumba wake anae tarajia kufunganae ndoa siku chache zijazo, mama huyu huku anaendesha gari lake taratibu, aliendelea kuwaza mengi sana, ikiwa pamoja na tabia ya kijana Martin ya ulevi na uzinzi, huku akichukulia kuwa mwanae Malaika akuwai kujiusisha na mapenzi hata mara moja, mama huyu alitamani kughailisha harusi hii, lakini tatizo ni mumewake, ambae ni baba yake Malaika na wifi yake yani shangazi yake Malaika, dada wa mume wake, kung'ang'ania na kupigania ndoa hiyo ifungwe, wakati mama Malaika akiwaza hayo, mara ghafla akamwona kijana mmoja mbele yake, akiwa anamwonyesha ishara flani hivi, ishara ambayo mama Malaika alihisi kuwa yule kijana anaomba lifti, kutokana na tulivu wa njia ile na hadithi za watu kutoa lifti na kuibiwa mala kwa mala,  mama Malaika akajuwa kwamba, yule kijana aliebeba kibegi cha brue, ni mmoja kati ya vijana wezi aliowai kuwasikia, na kwa kuhofia kuibiwa vitu vyake pamoja na fedha zake, mama huyu akaongeza mwendo wa gari lake, ili ampite kijana huyu, pasipo kujari mashimo wala maji aliyo yakanyaga kwa fujo, kiasi cha maji hayo machafu kumrukia yule kijana, mama Malaika aliweza kushuhudia yule kijana kwakupitia side morror, akijirusha kwa pembeni, akijaribu kukwepa yale maji, japo machache yalimpata kwenye suruali yake ya jinsi sehemu za miguuni, Wakati mama Malaika akilishuhudia hilo, ghafla alianaaza kuona mabadiliko kwenye tairi moja la gari lake la upande wa kushoto, lilikuwa tupu alikuwa na hewa, hapo mama Malaika akuwa na ujanja tena, ikambidi asimame kiitaji kushuka na kuliangalia lile tairi la gari lililo ishiwa hewa, lakini kabla ya kushuka, kamwangalia yule kijana, akitumia side mirror (yaani kioo cha pembeni) alimwoana yule kijana, ambaye alikuwa amemwacha kwa umbali wa mita 50, sasa alimwona anaokota kitu kama kipisi cha ubao na kuanza kuulifwata gari lake akiongeza mwendo, hapo mama Malaika akajuwa anakuja kukiona cha mtemakuni, kwa kosa la kummwagia maji machafu yule kijana, mama Malaika akiwa anahisi ikijasho chembembe kiki churuzika kwenye uti wa mgongo mpaka kwenye msambwanda, akaanza kusali sala ambayo alihisi inge mkomboa, tokakwenye kipigo kibaya cha ule ubao, lakini wakati akiwa kwenye sala yake,  akasikia akisalimiwa “shikamoo mama” ni sauti ya kiume ya upole iliyojaawa na tulivu na nidhamu ya hali ya juu, ilipenya masikioni mwake, hapo mama Malaika akafumbua macho, akamtazama kijana huyu kwa mshangao wenye tahadhari na hofu kubwa “malahaba mwanangu“ aliitiikia mama Malaika kwa sauti ilyo jaa uoga,  maana alizingatia kuwa, licha ya kuhisi kuwa yule kijana ni mwizi, psasa alishammwagia maji machafu, taratibu mama malaika huku anashusha pumzi ya hofu, aliinua uso wake na kutazama ubao mkononi mwa yule kijana, mbaya zaidi aliona ubao hul ulikuwa una misumari kama miwili iliyo gogwa na kutokea upande wapili, mama malaika akainua usowake zaidi na kumtazama yule kijana kwamacho ya kuomba msamaha, lakini akakutana na sura ya pole sura ambayo ilionyesha dalili zote za kuwa, yule kijana ni mtu mwema “pole sana mama, nilikuwa nakuonyesha usimame ili niutoe huu ubao, maana niliuona una msumari, sasa bahati mbaya ukunielewa” aliongea tena yule kijana kwa sauti ile ile ya upole na taratibu, huk akimwonyesha ule ubao, mama Malaika aliduwaa asijuwe cha kujibu, akamtazama yule kijana usoni, kiukweli alikuwa ni kijana mzuri, mwenye umbo zuri la kiujana, aliyejengeka kimazoezi  “mama una tairi la akiba, nikubadilishie?” mama Malaika akagutuka kama anatoka usingizini, na kugundua kuwa kijana alikuwa mtu mwema sana kwake, “Ninalo baba yangu lipo kwenye buti” aliongea mama Malaika huku akivuta kidude cha kufungulia buti la gari lake, akamwona yule kijana akizunguka nyuma ya gari, akatoa begi lake dogo alilokuwa amebeba mgongoni, akaliweka pembeni kisha akafunua buti na kutoa tairi pamoja na jeki na wheel spana ya kufungulia tairi, akaanza kazi ya kupandisha jerck, sasa mama Malaika alikuwa ameshuka toka kwenye gari, amesimama pembeni anamtazama yule kijana, huku akijiwazia moyoni "ningekuwa bado binti mdogo, leo ningempata huyu kijana kwa gharama yoyote" mama huyu alimtazama vizuri kijana amba aliendelea kupiga jerck, huku akiwaza mengi sana juu ya kijana huyu ambae akuwa anamfahamu “eti kijana wewe ni fundi magari?, niwe naleta gari langu ofisini kwako” mwishowe mama huyu alivunja ukimya “Hapana mama, mimi ni muuza viatu vya mitumba” alijibu yule kijana huku, akiendelea na kazi, “Ok! sawa, labda nikuulize tena, hivi umeoa?” hapo kijana akujibu chochote, mama Malaika akadhani ladba kijana huyu akusikia alichomuuliza “eti mwanangu, una mke?” “Hapana” huyu kijana alijibu kwa sauti ya unyonge sana, kiasi kwamba mama mama Malaika, akahisi akupendezewa na swali kama lile, hapo kazi ikaendelea na maswali ya hapa na pale nayo yakaendelea,  baada ya dakika kama kumi na tatu yule kijana alikuwa amesha maliza kazi, na kumwekea vifaha vyake kama vilivyo kuwa mwanzo ,“naona tayari sasa una weza kwenda “ “Hooo asante sana mwanangu” alishukuru mama yake Malaika, huku akionyesha uso wa tabasamu, yani japo ni mama mtu mzima. lakini uzuri wake ulionekana wazi wazi, mama malaika aliingia ndani ya gari akatoka na noti za shilingi elfu moja moja tano, akiwa amezishika mkononi na kumpatia yule kijana  “hapana mama, nimekusaidia kama mama yangu sihitaji malipo” mama Malaika akashangaa kidogo  “hapana mwangu, sina maana ya malipo, ni asante yangu kwako, au hutaki siku nyingine nikipatwa na tatizo unisaidie” aliongea mama Malaika akionyesha tabasamu usoni kwake, “usijari mama yangu, basi naomba uniwekee pengine kuna siku nitapata tatizo ukaja kunisaidia" aliongea yule kijana huku anachukua begi lake, na kuanza kuondoka zake kuelekea mjini, hapo mama yake Malaika anaingia ndani ya gari, nakondoka zake,  kuelekea mjini, anafika usawa wa yule kijana, anasimamisha gari  “basi ingia nikusogeze, si unaelekea mjini” aliongea mama Malaka “Hapana mama, natembea kwa miguu sababu ya mazoezi” alongea yulee kijana akiachia tabasamu, “mmh! haya kwaheri baba “
aliongea mama yake Malaika huku anaondoka na gari lake,  anamtazama yule kijana kupitia vioo vya pembeni side mirror, anamwona kijana akiwa katika hali ya kawaida, kama hakuna kilichotokea muda mfupi uliopita, akajisemea mwenyewe “huyu kijana wa ajabu sana, mmh!“ hapo aliendelea na safari yake huku anajikumbusha tukio zima anajicheka sana akiwa peke yake ndani yagari *******
SOPHIA MAPUNDA “Ina maana alikukuta kabisaaaaaaa, upo na Martin, sasa akafanyaje?”  Jane rafiki yake Sophia, anaae kaa nae chumba kimoja wlicho pangishiwa na Edgar, aliuliza kwa shahuku  “atafanya nini, nikamtimua kama omba omba, tena sasa hivi kabla sijaenda kwa Mart, nampitia Ed pale kwenye maviatu yake, naenda kumwambia akome kabisa kunifwatilia, yani akome kabisa”
alionge Sophia kwa Nyodo na msisitizo, akiwa ameshikilia kioo kidogo mkononi anaendelea kujipodoa.
Huyu ni Sophia Mapunda ni binti aliyetokea kijiji cha Namabengo, mwaka mmoja uliopita, akimfwata dada yake aliyekuwa akiishi mjini Songea na mume wake, mwanzo maisha yalikuwa mazuri kidogo hadi dada yake na shemeji yake walipohamia mbinga kikazi, miezi saba iliyopita, nakushindwa kuhama na Sophia, kwasababu zilizo kuwa nje ya uwezo wao, hapo wakashauriana wamrudishe kijijini, lakini Sophia akukubali, aliona ni vyema akajiunga na Jane wafanye biashara ya kuuza chakula (mama ntilie) kwa kutumia nauli aliyopewa na dada, yake akachanga na Jane na kuanza biashara yao, huku wakikaa kwenye chumba kimoja mtaa wa majengo, na sehemu kubwa waliyokuwa wanauzia biashara hiyo, ni soko kuu, wateja wao wakubwa ni wafanya biashara wamaeneo hayo, ya soko kuu, mteja mmoja  wapo alikuwa ni Edgar, na ndipo mapenzi yao yalipoanzia, Sophia alionyesha kupendana sana na Edgar, na ndipo Edgar akaamua amuhudumie kwa kila kitu, ili aachane na biashara ya mama ntilie, kweli Sophia na Janeth wakaacha biashara ile, na Edgar alishajuwa kuwa amepata mchumba, na alikuwa anajiandaa kwenda kumtambulisha nyumbani kwa wazazi wake, ambao kila siku walikuwa wana mshauri kuoa,
“Tena muwai kabla hajaenda kumfanyia fujo Mart, maana anaonekana anapigana yuleee”
Jane alimsisitiza Sophia, kwa kujuwa kuwa, Martin ana pesa nyingi kuliko Edgar, hivyo angewasaidia sana, na wangeishi maisha mazuri zaidi kuliko mwanzo, akisahau Edgar alikowatoa, walikuwa wakizurura na sahani za vyakula, huku wakitaniwa na pengine kuzalilishwa na wateja wachache wapuuzi, “Wewe ndo maana yake yani namchukia Edgar mpaka najilaumu kwanini nilikuwa nae"   nitumie nafasi hii kutoa pole kwa makamnda wetu walio patwa na shambulizi huo mashariki ya congo pembeni kidogo ya mji wa Ben, katika kitongoji cha simlike, pole ni pia kwa familia zao,
STORY NDO KWANZA INAANZA, JE SOPHIA ATA ENDA KWA EDGAR NA NINI KITA TOKEA? JE AHADI YA MALAIKA KWENDA KWA MARTINI ITATIMIA?, NA VIPI AKIWPEWA ZAWADI  MARTIN ATABADILIKA? IAKUWAJE KATI YA MAMA MALAIKA NA EDGAR ENDELEA KU LIKE NA KUCOMMENT MAONI IN BOX



No comments: