BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA NNE





IPOISHIA SEHEMU YA TATU : “Tena muwai kabla hajaenda kumfanyia fujo Mart, maana anaonekana anapigana yuleee”
Jane alimsisitiza Sophia, kwa kujuwa kuwa, Martin ana pesa nyingi kuliko Edgar, hivyo angewasaidia sana, na wangeishi maisha mazuri zaidi kuliko mwanzo, akisahau Edgar alikowatoa, walikuwa wakizurura na sahani za vyakula, huku wakitaniwa na pengine kuzalilishwa na wateja wachache wapuuzi, “Wewe ndo maana yake yani namchukia Edgar mpaka najilaumu kwanini nilikuwa nae" 
MARTINI NA EDGAR
baada ya kutembea kwa mda mrefu, sasa Edgar alikuwa amekaribia kwenye eneo lake la biashara ya kuuza viatu vya mitumba, eneo la soko kuu la Songea, sasa basi wakati akiwa anamaliza kukatiza eneo la bank ya biashara, tawi la chabruma, mara akakoswa koswa na gari moja, aina ya rand cruizer jeusi, lililokata kona ya ghafla mbele yake, hapo Edgar anaruka pembeni lulikwepa lile gari, nusura aingie mtaroni, lile gari linapita na kuingia pale bank, Edgar analiona lile gari likisimama, kisha anashuka Mart Jons, akiwa na briefcase mkononi, hapo Edgar anashikwa na hasira ya ajabu, aijawai tokea, anatamani amfwate lakini anawaona polisi maeneo yale, ni polisi wanaolinda benk wakiwa na bundukiza mapegani, akaona itakuwashida kwake, tena moja kwa moja ataonekana amevamia kwa nia ya kuiba fedha, hivyo akaamua kuondoka zake, na kujisogeza eneo lake la biashara, akimwacha Martin akiingia ndani ya jengo la bank, ambapo Moja kwa moja Martin alielekea kwenye dirisha moja, lililokuwa na mdada mmoja mrembo, lakini siyo kama Malaika ,yule dada alimpokea kwa tabasamu na bashasha “hooo karibu shemeji naona leo umechelewa, saa nne sasa” aliongea yule dada akimaanisha kumfahamu Martin, kuwa ni mteja wao wakilasiku, “acha tu shemeji, yani jana nimechelewa sana kulala, nilikunywa sana pombe, yani mpaka sasa najihisi bado nimelewa, vipi Eliza yupo wapi?” aliuliza Mart, huku anafungua brifcase na kutoa mabulungutu ya fedha, na kuyapanga juu ya dirisha, huyo Eliza ni mpenzi wake mwingine ambaye ni mfanya kazi wa hapa bank, alimfahamia hapa hapa kutokana nakuja mara kwa mara kuleta fedha “Leo yupo ndani,  kwani mimi siwezi kukuhudumia shemeji?” alijibu Yule binti huku akijichekesha chekesha, wakati huo alikuwa ana chukua bulungutu moja baada ya jingine na kulifugua, kisha anaweka kwenye mashine ya kuhesabia fedha “Kwanini usiweze, tena unaonekana utanifaha zaidi kunihudumia” alisema Martin huku akiilamba midomo yake na macho yake amemkazia yule mdada,
“Mhhh! mwone kwanza, yani utaniwi, tena usisahau kuniletea kadi yako ya mwaliko wa harusi” alisema yu;e mdada huku akiendelea kijichekesha, macho yake yapo kweny kihesabio ha fedha, ambacho lilikuwa kina endelea kuhesabu fedha, “Husikonde kadi umepata, sasa nikupitie saa ngapi?” aliuliza ,artin akionyesha kuwa alikuwa atanii, “Unipite vipi tena jamani Mart?, ujuwe namwogopa da Eliza, akijuwa je, unazani itakuwaje?” aliongea yule mdada kwa sauti ya siki na taka, “Unamwogopaje Eliza, wakati unajuwa na yeye ni mwizi pia?” maongezi na kazi mpaka wakamaliza kuhifadhi fedha, na wao wakawa wamesha kubaliana, kuwa Martin ampitie Yule binti saa 12 jioni, waende kujichana Nyumbani Peace, hapo wakaagana Mart Jons akaondoka zake,
MALAIKA NA MAMA YAKE
“ina maana hata lift amekataa, au amekasirika ulivyo mmwagia maji?” aliuliza Malaika kwa mshangao
nibaada ya mama yake kumsimulia tukio la kummwagia maji yule kijana, “hapana, mbona alikuwa anaongea kawaida tu! sema yule ni kijana mstaarabu sana, yani sijawahi kuona, tofauti na mwonekano wa mavazi yake” Malaika na mama yake walikuwa kwenye ofisi ya Malaika iliyopo pembeni ya moja ya duka lake kubwa la nguo, wakiongea mawili matatu, huku wakicheka na kufurahi pamoja, ghafla Malaika akabadirika na kuongea kwa sauti ya chini na ya upole sana,  “Mama naona harusi inakaribia, sina budi kuikabili, maana nyie ndo mmesha hamua hiwe hivyo,” aliongea Malaika huku mama yake akimtazama kwa umakini na roho ikimsuta, “leo naenda kwa Martin kuongea nae juu ya tabia yake, yani kila siku nasikia habari mbaya za usaliti juu yake, tena jana nimeshuhudia kwa macho yangu, nilimwekea zwawadi ya suit, leo nampelekea, nimeona nifanye hivyo labda atabadilika, sina namna tena, najuwa nikimwambia baba matendo ya Martin, atonisikiliza kama kawaida yake" maneno hayo yalimchoma sana mama yake Malaika, “sawa mwanangu, lakini jitahidi kusimamia ule msimamo wako, usimvulie nguo mpaka siku ya harusi" mama yake Malaika aliongea, huku akionyesha hisia za wazi za uchungu, kwa mwanae “Yani mama unaposema hivyo, unanitonesha kidonda, yani hapa nawaza sijui siku hiyo kama nitaweza kufanya nae, yani ata kama tutakuwa tumefunga ndoa” alionongea Malaika kwa sauti yenye uchungu mwingi sana, “mh! usinichekeshe Malaika, yani ulale na Martin kitanda kimoja, mpaka asubuhi, usiweze kufanya chochote, thubutuuuu! lakini mwanangu nakusifu sana kwa kujitunza mpaka umri huo” aliongea mama Malaika huku akimfanyia utani mwanae, “halafu naenda kumkabidhi mwili wangu kijana mhuni kama nini“ aliongea Malaika kwa uchungu sana, huku anakwenda pale alipokaa mama yake na kumkumbatia kwa mgongoni, mama yake pia anamshika mkono uliopita kifuani kwake kutokea mgongoni, “pole mwanangu atuna la kufanya, baba yako na rafiki yake tokea walivyoKazania swala la wewe kuoana na Mrtin, japo mimi sijafurahi, maana Yule kijana namfahamu sana” aliongea mama huyu akiupapasa mkono wa Malaika, "na shangazi pia, sijui wamempa nini?, halafu mama unajuwa nimesahau diary yangu sijui nyumbani, maana nimeitafuta kila sehemu hapa ofisini, lakini sijaiona, alafu ina mambo yangu mengisana ya ofisini" Malaika alikuwa amekumbuka kuhusu diary yake, na sasa alishaanza kuingiwa na wasiwasi maana ndani ya ile diary kulikuwa kuna kumbukumbu nyingi sana za ofisini, pamoja na majina ya madeni ya zaidi ya shiringi million ishirini ya wateja wao, "mh! kwakweli sijaiona, tena niliingia chumbani kwako kupiga simu, lakini sijaona hiyo diary, hebu kumbuka vizuri"aliongea mama Malaika ambae alikuwa anaujuwa umuhimu wa hiyo diary, "mama, yani nimetafuta kote, nimejitahidi kukumbuka weeeee! lakini sikumbuki nilipoiacha, yani mle kuna kila kitu" Malaika na mama yake, waliongea sana, kisha mama Malaika akaaga na kuondoka zake, huku akimsisitiza mwanae akaongee na Martin, *****
MZEE KOMBA MABASI NA MZEE HAULE.
Wazee hawa wawili walikuwa ndani ya hotel moja kubwa sana hapa mjini Songea, ijulikanayo kwa jina la Chabluma Hotel, ni kawaida yao kukutana hapa mida ya mapumziko, kupata chai na hata mchana pia ucheza darts, huku wakipata vinywaji, lakini leo walikuwa wanazungumzia juu ya harusi ya watoto wao, ambayo ilikuwa imebakiza siku chache kufanyika, “jana nimewasiliana na watu wa mikoani, wakasema wanahitaji usafiri, hivyo nitawapelekea mabasi ya kuwaleta na kuwarudisha, vipi mziki uliongea na ile bend ya safari music?” aliongea mzee Komba mabasi kwa majisifu, huku mzee Haule akimsikiliza kwa umakini, huku akiendelea kunywa chai taratibu, “hayo yote nimesha kamilisha, pia ata nguo na viatu vya maharusi na wapambe wao, pamoja na za watoto wa kubeba maua, na pete za dhahabu zimeshaingia nchini jana, kutoka uingereza, nadhani mpaka keshokutwa zitakuwa hapa” aliongea mzee Haule huku wote wakionyesha nyuso za furaha, waliongea mengi sana, na mipango yao ya baadae juu ya watoto wao, ikiwa pamoja na kuwafungulia kampuni kubwa sana, na kuwakabidhi jumba moja kubwa la kifahari, lililopo mtaa wa Mateka, nje kidogo ya mji wa Songea, ni mtaa uliotulia sana, pia unaokaliwa na watu wenye maisha ya juu, japo sio sana, wakati wote wakipanga hayo, Marafiki awa wawili, mzee Haule akuwa anaujuwa ujanja wa mwenzie mzee Komba mabasi, ambae licha ya kushawishiwa na mwanae Martini kuwa akaongee na mzee Haule yeye amwoe Malaika, binti aliemtamani miaka mingi sana huku malaika akijifanya mgumu kumkubalia, pia mzee huyu alona, mwanae aki mwoa binti wa mzee Haule ata pata faida kubwa sana, maana Malaika alikuwa mtoto wa pekee wa mzee Haule, na kwa biashara anayo ifanya mzee Huyu katika kampuni yake ya nguo na viatu, akiwa ameshika tenda zote za kiserikari na binafsi mkoa mzima wa Ruvuma, lazima Malaika ndie mlithi pekee wa mzee huyu, na kwakuwa atakuwa ameolewa na mwanae, itakuwa lahisi kwake yeye kujichotea mali za rafiki yake huyu wa miaka mingi,  ****** saa tano, Edgar alikuwa ametulia kwenye benchi, ndani ya kibanda kilicho zungukwa na nguo za mitumba, zilizo kuwa zinauzwa, tokea alipofika pale kijiweni, Edgar akiwa amechelewa, alimsalimia rafiki yake Justin, ambaye ni msaidizi wake ktk biashara, na leo ndiye aliefungua mapema, baada ya hapo Edgar aliingia ndani ya kile kibanda, bila kuangalia viatu vilivyokuwa juu ya meza, akatulia zake huku akikumbuka tukio la jana yake, la kumkuta mpenzi wake Sophia, akinyonya dudu, Justin akutaka kumsemesha Edgar, maana alishajuwa kilichomtokea rafiki yake huyo, sababu wakati Edgar akipewa ile taarifa, na rafikiyao mmoja ambae nae ni mfanya biashara kama wao pale soko kuu, na yeye Jastin alikuwepo, japo akwenda nae huko Nyumbani Peace, Jastin alimwacha Edgar bila kumsumbua, akuona kama itakuwa vyema, iwapo atamsemesha Edgar, maana anajuwa jinsi alivyokuwa anampenda na kumgharamia Sophia, hivyo yeye akaendelea kuuza biashara, na Edgar akiwa amekaa ndani ya banda, huku matukio ya jana Nyumbani peace ya kijirudia kichwani mwake, ilimjia picha ya mkono wa Martin ukitafuta kitu kule chini kabisa ya utamu wa Sophia, nambaya zaidi alivyo mshuhudia Sophia akiwa ame ingiza dudu ya Martini mdomoni mwake, wakati yeye ajawai kunyonywa dudu ata siku moja, hapo Edgar alijikuta akiuma meno kwa uchungu, kama mtu anayetolewa kipande cha mwiba kwenye mguu, akimalizia na kujikuna kwanguvu nywele zake, akakumbuka ahadi walizokuwa wakipeana na Sophia, akajikuta akisema "kweli nimeamini, kila mtu na kifo chake, ata mwanao ufinae”
Eneo la soko kuu la mjini Songea, watu walikuwa wengi sana, kila mmoja akiendelea na pilika zake, kelele za watu na magari vilisikika kwa pamoja, kwasasa vilikuwa ni kelo tupu kwa Edgar, ambae alikuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo, mala Edgar anastuliwa na Justin, “hoya Sophia namwona kama anakuja, kwako hivi“ Edgar akainuka na kuchungulia kule alikooneshwa na Justin, ni kweli, Edgar anamwona Sophia akija kwa kasi sana, upande ilipo biashara yao, akiwa amevalia ki skert kifupi sana, juu kilichoishia juu magoti na kiblauzi kilichombana kifuani, na kufanya maziwa yake makubwa kuonekana yakitikisika kila anapopiga hatua, moyo ukamlipuka Edgar, na kunza kumwenda kasi, yakipiga kwa mwendo wa Frasi, akupenda kumwona tena Sophia, uchungu ukaongezeka maradufu, akarudi akaa kwenye benchi kama alivyokuwa mwanzo “anakuja kufanya nini?” Akanong’ona Edgar akimwambia Jastin, ambae bado alikuwa pembeni yake “vipi nika mzuwie?” aliuliza Jastin kwa bashasha, “Hapana, mwache tuone anacho fwata” Naam sasa wanamwona Sophia akiuliza jambo, kwa kijana mmoja mfanya biashara mwenzao, naye anaonyesha kwenye kile kibanda, alicho kaa Edgar, kwakuwa anajuwa Sophia ni shemeji yao, wakamwelekeza moja kwa moja alipo Edgar, sasa Sophia anaelekea kwenye kibanda walipo Edgar na Jastin, hapo jastin anatoka nje, wanapishana na Sophia, bila kusalimiana, ni kama wasio fahamiana, Edgar alikuwa bado ametulia kwenye bench, kama mwanzo, akimtazama Sophia anavyoingia, Sophia alipofika pale, bila atasalamu akaanza kuongea, huku ameshika kiuno, nakujitikisa tikisa, "Edgar naomba usinifwate fwate, ujanioa wala barua ujatoa, na kwetu awakujuwi wala awakutambui, yani usinijuwe kabisaaaaaaa!, usije ukaniaribia maisha yangu, tena ukae ukijuwa kuwa, mapenzi ayalazimishwi, kama mtu akutaki, ndio akutaki, usimfwate fwate, umenielewa lakini?” Hapo Edgar akainua uso wenye upole na utulivu, na kumtazama Sophia, kiukweli japo Edgaralionekana kuwa mpole na mtulivu, lakini moyoni mwake alikuwa na hasira kali sana, akajitahidi kwasauti ya upole akamjibu Sophia, “Sophia, nilikufwata sababu ulionyesha kunipenda, na mimi nikakupenda, tukawa wapenzi, kwasasa sina sababu ya kukufwata, kwa sababu unipendi, unampenda mtu mwingine, nimesha ushinda moyo wangu, siku pendi tena, nakuomba usiongee neno jingine, pengine litakuletea matatizo, tafadhari nakuomba ondoka mala moja” Hapo Sophia akatoa msonyo marefu, kisha akondoka zake, akipiga kibega Jastini, kumbe Jastin akuwa mbali, alikuwa akifwatilia kinacho endelea, wakamwona Sophia alipotelea mtaa wapili, akielekea mtaa ilipo ofisi ya Martin Johnson  *****
Malaika baada yakumsindikiza mama yake, anaingia upande wadukani, ndani kuna wateja wengi sana kiasi kwamba, mhudumu mmoja kati ya wanane waliopomle ndanni ya duka, anazungukwa na wateja  tisa mapaka kumi, Malaika ile anaingia tu! dukani, akadakwa na muhudumu mmoja alie simama na mama mmoja wa makamo “Eti dada ile suit uliyosema tukuwekee tuiuze?” aliuliza yule muhudumu wakike, “Weeeee usithubutu kuiuza hiyo suit, hiyo nizawadi maalumu kwa shemeji yako” alisema Malaika huku akiwasogela karibu, pale walipo simama yule mama mteja wao na mhudumu “Mwanangu weeee! naomba niuzie, nitaipata wapi tena kama hii? kwabei kama hiii” aliongea yule mama kwa namna ya kubembeleza, huku akionyesha sura ya ucheshi, “mama, kwani ulikuwa unataka kumchukulia baba yetu” alitania Malaika huku akitabasamu “siyo baba yako, ni kijana mwenzio, ni mwanangu wa kwanza, yani ni muhimu sana, naomba unisaidie mwanangu, najuwa kuja tena suit kama hizi, kwa bei ndogo kama hii siyo leo”alisema mfululizo yule mama, huku malaika akitamani kucheka kwanjisi yule mama anavyoongea kwa ucheshi “Hoooo! mama, ni muhimu sana, kwani vipi mwanao anafunga ndoa?” Safari hii Malaika alipunguza sauti, akawa kama ananong’ona hivi “ndoa wapi mwanagu, kwani ata huyo mchumba mwenyewe anae?, hakuna cha ndoa wala nini,” hapo Malaika akaangua tena kicheko, wakati yule mama akendelea kuongea “ujuwe huyu mwenzio ata simwelewi, kila siku anasema bado ajampata mchumba, eti anamtafuta atakae mfaa, sasa utampataje anaefaa, na mtu mwenyewe unavaa kiuni?” alimalizia yule mama  kwasaurti ya chini, nakumfanya Malaika sasa azibe mdomo ili wateja wengine wasi sikie kicheko chake, “Mh! sasa hiyo suit yanini mama?” aliuliza Malaika baada ya kuacha kucheka, japo watu wote mle dukani walikuwa wanamtazama, asakutokana na uzuri wake, na jinsi anvyoongea na kila mtu, “Labda akivaa suit atapata mke bola, anaemtafuta miaka yote, namimi nataka yeye ampate mke  anaemtaka yeye,  maana najuwa akaishi kwa amani” Malaika alicheka tena kidogo, kabla ya kutulia na kumwuliza yule mama “inaonyesha mama unampenda sana mwanao” hapo yule mama akatabasamu kwamla ya kwanza, kisha akamtazama Malaika usoni “Familia yetu wote tunapendana, binti Haule, ngoja nikuambie kitu” aliongea yule mama kwa sauti ya upole sana, tofauti na mwanzo, hapo Malaika akamsikiliza kwa umakini, “mwanangu siku zote, ninapo mpa furaha mpendwa wangu, namimi na jiwekea nafasi ya kuwa na amani na furaha, moyoni mwangu” Malaika alivutiwa na maneno ya yule mama, akaingiwa ma moyo flani hivi wa Imani, akaona bora asipeleke zawadi kwa mchumba wake Martin, amwuzie yule mama, Malaika akamgeukia yule mhudumu wa dukani kwake, ambae bado alikuwa amesimama pembeni yao, “sarah mfungie hile suit, huyu mama” aliongea Malaika, ambae aliona bola kumwuzia yule mama ile suit kuliko mtu anaye huumiza moyo wake kila siku “Asante sana mwanangu mungu akubariki”  alishukuru yule mama huku akifungua pochi yake ndogo, tayari kutoa fedha za kulipia suit, “Sasa mwanao akipata mchumba, unialike kwenye harusi” aliongea Malaika, wakati huo yule muuzaji akiangaika kuifunga vizuri ile suit “wala usijari mwanangu, atakama ikiwa  ndoa ya mkeka, nitakualika, japo wewe ujanialika kwenye harusi yako, ila nitakuja kushuudia japo kanisani” Malaika akacheka kidogo, japo kicheko chake kilisikika duka zima, kiasi cha watu wote mle ndani, kumgeukia na kimtazama “Hahahaha wemama una maneno, ebu ngoja nikakuchukulie card, tena ya watu wawili, uje na baba ukumbini” Malaika aliogea huku  akielekea ofisini kwake, akimwacha yule mama akipekuwa pochi yake kutafuta frdha ya kulipia suit, Malaika akiwa ndani ya ofisi yake, akafungua droo ndogo, iliyopo chini ya meza, akatoa card, akaifunua na kuitazama, alipo lizika kuwa ni ya watu wawili, akaiweka kwenye bahasha kisha akaanza kurudi dukani, huku moyoni akimuwaza yule mama, asa maneno yake, ni yautani lakini yana maana sana kwake, “ninapo mpa furaha mpedwa wangu, namimi najipa nafasi ya kuwa na amani na furaha moyoni mwangu” Malaika aliyarudia maneno ya yule mama mcheshi, “Mh! pengine Martin akabadilika na mimi nikamfurahia” alijiwazia Malaika huku akipishana na wateja wanao ingia na kutoka, lakini wakati akiingia dukani, mala anadakwa na Sarah Yule muhudu, alie mwambia amfungie suit Yule mama mcheshi, “dada ebu ona, eti anatoa shilingi elfu mbili miatano” alisema Sarah huku akimwonyesha mkononi mwa yule mama, “Haaaa! elfu mbili na mia tano?” Malaika akaduwaa, kabla ajaanza kucheka, kisha huku bado anacheka, Malaika aka muuliza yule mama “eti mama kwani hukujuwa bei yake?”hapo kwa sauti ya unyonge na upole sana yule mama akasema, “mwangu samahani kwa usumbufu, nazani sikusoma vizuri bei yake, mimi nilijuwa nishilingi elfu mbili miatano, kumbe elfu ishirini na tano, basi mama, naona Mwangu hana bahati” tofauti na mwanzo sasa huyu mama aliongea kwa sauti yakukata tamaha, huyu siyo mwingine, ni mama yake Edgar, HAYA SASA, VIPI MAMA EDGAR NDIO AMEIKOSA ILE SUIT?, HUKU NAKO SOPHIA ANAELEKEA KWA MPENZI WAKE MPYA, WAKATI HUO MARTIN AMESHA WEKA MIADI NA MWANAMKE WABENK, PIA MALAIKA NAE ANAITAJI KUONANA NA MARTINI, UNAONA ITAWEZEKANA,  nichukuwe nafasi hii kuwatakia maisha mapya wafungwa wote waliopewa msamaha na rais wetu, akiwemo babu NGUZA VIKING, na PAPII KOCHA, mkajiunge na watanzania wenzenu katika kulijenda taifa, na mkaishi mahisha mema na bola mkiwa huru, ENDELEA KUWA NASI KILA SIKU,



No comments: