BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA SITA





ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO : , Mage naye alimtazama kwa jicho la chuki Sophi, kisha bila kumjibu chochote, akamwachia msonyo mkali  wazarau huku anaingia ndani, wakati huo akapishana na Martin alie kuwa anatoka haraka haraka haraka, nakuingia kwenye gari lake, nakuliondoa kwa speed, akijaribu kumfukuzia fukuzia Malaika, alijuwa lazima atakuwa ameenda nyumbani, kumsimulia mama yake kilichotokea, hivyo Martin alijitahidi kuuwai ilikumzuwia, ikiwezekana kumpigia magoti Malaika, Sophia nae baada ya kuona Martin ameondoka, akajiinua taratibu, huku akijifuta machozi, nakumalizia kwa kujifuta vumbi, kwenye nguo zake, kisha na yeye huyooo, akapotelea kwenye chocholo za mtaa wa Zanzibar. endelea...
Kumbe basi wakati Martin anaelekea barabara ya mahenge nyumbani kwa kina Malaika akawai kumzuwia, Malaika asiongee na mama yake, kumbe Malaika akwenda nyumbani, alipinda kushoto na kurudi ofisini kwake, alipo fika pale ofisini kwake, Malaika alishuka kwenye gari bila kuongea na mtu yoyote, akaingia ndani ya ofisi yake, akachukua kimkoba chake kidogo, kisha akafunga mlango kwa ufunguo, alafu akaingia kwenye gari na kuondoka zake, kuelekea nyumbani kwao Mahenge D, bila kujuwa kuwa, Martin naye amesha tangulia huko nyumbani kwao, kwa lengo la kwenda kuwai kusuluhisha, kabla yeye Malaika ajawaambia wazazi wake, juu ya tukio alilolikuta ofisini, wakati Martin akiwa speed kali sana, mbele kidogo ya njia panda, karibu na ikulu dogo ya mkoa, Martin alikata kona ya ghafla na kuiacha barabara kuu kuingia mtaa waMahenge D, hapo alijikuta akimkosa kosa kumgonga mtembea kwa miguu, kijana mmoja aliyekuwa akitembea taratibu kwenye barabara hiyo ndogo yavumbi, na kumfanya yule kijana aruke pembeni na kuingia kwenye mtalo, ambao bahati nzuri ulikuwa na nyasi nyingi sana, zilizo jaa vumbi, ambazo zili msaidia asiumie, na Martin bila kumwangalia yule kijana, kwamba alikuwa salama au vipi, yeye akatimua vumbi na kuendelea na safari yake, kwa mwendo ule ule wafujo, kijana huyu alikuwa ni Edgar ambae alihiona sikuile kuwa ni yamikosi sana, Edgar akiwa bado mtaloni, alitikisa kichwa kwa masikitiko, huku anacheka kwa uchungu “huyu jamaa kunakitu kitaokea katiyetu” Edgar alikuwa amesha mkumbuka Martin, kwani gari lake rand cruzer jeusi, ndio lilomkosa leo asubuhi, pale Bank, basi taratibu Edgar akajitoa pale mataloni, nakuokota begi lake, ambalo lilikuwa limeangukia pembeni wakati ule alipo ruka, basi Edgar akaanza kutembea taratibu kuendelea na safari yake, akatembea kidogo huku akiwaza ili na lile, asa jinsi mambo yanavyo enda siku ile, “Huyu jamaa sijuwi ananitafutia nini?, Yani dah!!!!” mwisho Edgar akajikuta anacheka mwenyewe, akuwa nalakufanya, akasimama nakuinama kidogo, kisha akaanza kujifuta vumbi ambazo alizipata kwenye zile nyasi, na takataka zilizokaa kwenye nguo zake, lakini wakati ana endelea kufanya hivyo, mala ghafla akasikia mhungurumo wa gari jingine likija upande wake, akaona bora aliwai kabla alija mfanyia vurugu, kama lilivyo fanya lile la Martin, lakini alikuwa amechelewa, sasa gari hilo lilikuwa limemkaribia kabisa sehemu alipo, kwani Edgar alikuwa katikati ya barabara hiyo ya vumbi, hapo Edgar akujiuliza, alijirusha tena pembeni ya barabara, na kutelezea mtaroni, akaanguka kama mwanzo, huku gari aina ya mersidice benzi nyeusi, likisota kwa breck za ghafla, nakutimua vumbi, huku likijitahidi kumkwepa Edgar, safari hii Edgar akabaki amekaa pale alipo angukia, kwa dakika kadhaa akiwa aamini mambo yanayomtokea, sikuile, tokea kume kucha mpaka sasa, “pole kaka, umeumia nikupeleke hospital?” Edgar alistuliwa na sauti tamu ya kike, sauti ambayo kwake ilikuwa kama sauti ya kinanda chenye kuliwaza, hapo Edgar akainua uso wake kumtazama mmiliki wa sauti ile, naam alikutana na sura moja matata ya mrembo Malaika, mrembo aliekutana nae jana,  pale Nyumbani Peace Lodge jana jioni, Edgar alimwona yule mrembo akishuka toka kwenye gari, na umfwata pale alipo dondokea, Edgar akajibu kwa sauti yake ya upole “Hapana dada sijaumia” hapo Malaika naye akajikuta akiduwaa “mh! kaka wewe sindie yule wa jana apale NYUMBANI LODGE?” aliongea Malaika, baada ya kumkumbuka huyu kijana, kuwa ndie alie mdaka jana, pale Nyumbani Peace, kama vile hakuwa amelisikia swali la yule dada Edgaralikuwaamekodoa macho, huku nayeye akimtazama huyu dada mrembo zaidi ya warembo, alio wai kuwaona kwa ukaribu, ni kweli Edgar alimkumbuka Malaika, kuwa alikutana nae jana, Malaika akaliangalia begi la yule kijana, ambalo lilikuwa pembeni yake, akapata uakika kuwa ndio mwenyewe mwisho wakajikuta wametzamana usni macho yao yakagongana, wakajikuta wame tabasamu,  “Samahani kaka yangu, yani nilikuwa mbali sana kimawazo, ebu inuka basi tuone kama umeumia” Malaika alijikuta akiongea kwa sauti yaupole iliyo zidisha utamu zaidi, tena aliongea kwa unyenyekevu mkubwa, mfano wa mama anae ongea namwanae, aliejikwaa au kujiumiza katika michezo, Edgar akuwa mbishi, aliinuka huku akitumia macho yake, kwa ujanja, ku ukagua mwili wa huyu binti mrembo mbele yake, kiukweli Malaika alikuwa ni mzuri sana, na Edgar akuwai kuwa karibu na binti mzuri alafu mrembo kama huyu, tena leo alimwona vizuri sana, yani zaidi ya jana alipo mdaka pale nyumbani peace “Hapana dada yangu sijaumia, pia siyo kosa lako we!nenda tu! ila ansante kwakunijari, pia nina diary yako sjijuwi nita kupataje, ilinikuletee” hapo Malaika aliruka furaha “sante sana jamani kumbe wewe ndio uliiokota?, asante sana kaka yangu” alisema Malaika huku akuruka karuka kisha akatulia na kumtazama yule kijana, ambae sasa alikuwa anajifuta vumbi kwenye nguo zake, na tabasamu likiwa lime tawala usoni mwake,  Malaika huku  akiendelea kumtazama kijana huyu, akagundua kitu kilichofichwa katika mwili wa huyu kijana, maana licha ya kuchafuka vumbi mda ule, lakini aliona wajihi wa yule kijana kuwa ni mwenye mwili wa kuvutia, ukweli Malaika akuwai kumchunguza mwanaume yoyote kabla ila huyu, lakini alimwona  kuwa ni wakipekee kabisa, kuanzia mwili, sura na tabia, “aina haja ya kuniletea, mida hii sina kazi twende nikupeleke nyumbani ukanipatie,” alisema Malaika akichukuwa kitambaa cha mkononi toka kwenye mfuko wa koti lake la suit, na kumpatia Edgar, kwamba atumie kujifutia vumbi, kitendo kile kilimshanagaza ata Malaika mwenyewe, ambae alijikuta akimthamini sana kijana huyu, japo bado tukio la Martin na yule mwanamke pale ofisini, lilikuwa kichwani mwake, “usijari dada yangu, usimalize mafuta yako bule, we nenda nyumbani, mimi nitakuletea ata ukitaka sasa hhivi, ila nimegundua jambo toka kwako” aliongea Edgar huku akimrudishia kitambaa chake Malaika, na kuendelea kujifuta vumbi kwakutumia mikono yake, malaika anaonyesha hamu ya kujuwa hicho alichokigundua huyu kijana, toka kwake, “ni kitugani umegungua toka kwangu?” aliuliza Malaika kwa sauti ya chini, na tuliu, huku uso wake ukionyesha tahadhari na macho yake yakiwa yamemtazama Edgar, nakumfanya azidi kuwa mzuri zaidi, hapo Edgar akatabasamu kidogo, “wewe ni mtu mwema sana, yani kwa kifupi na shindwa nikuambieje” aliongea Edgar kwa sauti tulivu sana, na kuishia kucheka cheka kidogo “ok! kaka yangu ingia basi kwenye gari, twende nyumbani kwenu,  kwani unakaa wapi?” aliongea Malaika, kwasautinyololozaidi ya kupembeleza, huku kwamala ya kwanza katika maisha yake akamshika mkono Edgar, akiwa ajawai kuushika mkono wa mwanaume yoyote namana hile, na kumvutia kwenye gari, “nakaa Seed farm,” alijibu Edgar huku akiongoza kwenye gari, nakuingia ndani yagari, hivi dada unakumbuka vizurijana?” Edgar alimwuliza Malaika,  "nakumbuka sana kaka yangu, tena nakushukuru sana, maana jana ulinisaidia sana sijuwi usowangu ungekuwaje?" alijibu Malaika na wote wakacheka kidogo, safari ya kuelekea seed Farm ikaanza, walitembea mwendo kidogo mrefu kidogo, wakiwa kimya, ndani ya gari nisauti yamusic wa reggae tu!, “Unakaa nani huku?” Malaika alivunja ukimya “nakaa peke yangu, wazee wanakaa hapo Mahenge A” alijibu Edgar ambae muda wote alikuwa anatafakari, uzuri wa huyu mscha aliekuwa nae ndani ya gari, “mbona unazungumzia wazee, vipi kuhusu mke, mchumba au rafiki?” aliuliza Malaika na kuachia tabasamu la kichokozi, lakini akastushwa nakicheko kidogo na kifupi sana, cha kama mtu alieguna, Malaika akamtazama Edgar, akamwona kama alie badilika kidogo, utoweza kuzani kama yeye ndie aliecheka “vipi kuna tatizo juu ya hilo?, mbona naona kama haupo sawa” Malaika aliuliza kwa sauti ya tahadhari, “Hapana dada yangu, hakuna tatizo, ujuwe kuna mambo ukiyakumbuka kila mala unajipanafasi yakuiumiza nafsi yako, nibora kuyatupilia mbali, nakugeukia upande mwingine” aliongea Edgar kwa sauti tulivu sana, “Unamaneno mazuri sana kaka, lakini tatizo lako ufafanui ok!, mimi naitwa Malaika Haule, je wewe unaitwanani?, maana tokea jana atukuwai kutambulishana majina?” aliongea Malaika huku akizidi kuwa mchangamfu mbele ya Edgar, japo siyo kawaida yake, asa kwa wanaume, maana wengi wao walihisia kumtamani na kumtaka kimapenzi "Yani bila kujitamburisha dada yangu, nilisha kutambua toka jana, sizani kama kuna mtu asiekujua Songea hii, mimi Naitwa Edgar Mbogo, nauza viatu vya mitumba pale soko kuu, karibu sana” alijibu Edgar wakati wakiendelea na safari yao, “Husijari nitakutembelea kesho” ni kama Malaika alimaanisha alichoongea, kiasi cha kumfanya Edgar ashangae, akijihisi kuwa yu pondotoni “mh! kutembelwa na mtoto kama huyu kijiweni?” **** Martin alifunguliwa geti na mlinzi, nyumbani kwa kina Malaika, aliingiza gari ndani, akashuka huku akiangaza macho huku na huko, asilione gari la Malaika, zaidi aliyaona magari mengine matatu, Martin akaelekea kwenye mlango wakuingilia ndani ya nyumba ya kina Malaika, akapokelewa na mschana wakazi, akasalimiananae, huku Martin akionyesha mwenye wasiwasi sana, akauliza kama Malaika yupo ndani, akajibiwa hakuna mtu mwingine pale nyumbani, zaidi ya mama yake Malaika, hapo Martin akachekecha akili, akaona endapo ataingia ndani, atamwambia nini yule mama, akapata wazo kuwa atoke hapo nyumbanni kwa kina Malaika, akakae mashujaa bar, iliyopo njiani, ni mtaa wapili tu! toka mtaa wa wakina Malaika, ili akimwona Malaika anapita, amuwai aongee naye, ikiwezekana ampigie magoti kabisa ili amsamehe, Basi Martin akatoka, na kuelekea Mashujaa bar, hapo akatege mingo yake
NAAM SAFARI IMEANZA KUELEKEA NYUMBANI KWA EDGAR, MARTIN NAYE AMETEGA NJIANI KUMSUBIRI MALAIKA, ILIKUJUWA KILICHO TOKEA ENDLEA KU LIKE KU COMMENT KAMA UNA CHOCHOTE KARIBU IN BOX



No comments: