Faida ya kufikiri Kama tajiri hata Kama huna kitu mfukoni
Kuna wakati unakuwa unashangaa kwa nini watu wengine ni matajiri sana na wakati wengine ni maskini. Najua umekuwa na mawazo mengi juu ya hili na kufikiri pengine hawa ni watu wenye bahati sana, wamezaliwa kwenye familia tajiri au pengine watu hawa wana kazi nzuri na wamezaliwa kwenye nchi zenye mafanikio.
Ni ukweli, yote haya yanaweza kuwa majibu kwa namna fulani, lakini hata hivyo kipo kitu kimoja muhimu sana ambacho kinafanya watu wengine kuwa matajiri na wengine kuendelea kubaki kwenye umaskini. Kitu hiki ambacho kinaleta tofauti zote hizo si kingine bali ni mawazo yako.
Badala ya kuendelea kulalamika kwa nini upo kwenye hali ngumu, kwa nini maisha yako yako magumu, kwa nini hufanikishi malengo yako fulani ambayo unayatamani sana karibu kila siku, kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukiangalia, angalia sana mawazo yako hasa linapokuja suala la pesa.
Mawazo yetu mara nyingi sana yana nguvu ya kutupa kitu chocho ambacho tunakihitaji katika maisha yetu. Mawazo yetu yamepewa uwezo wa kuumba fursa na kila hali ambayo tunaitaka ijitokeze kwetu. Kinachotakiwa kufanyika ni kuamua kutumia mawazo haya kwa ufasaha hadi kuweza kutufanikisha.
Kwa hiyo mpaka hapo unaelewa kabisa faida kubwa ya kufikiri kama tajiri hata kama huna kitu mfukoni inakusaidaia wewe kuweza kupata kile unachokihitaji kwa hatua. Ni suala la kuujaza ubongo na akili yako taarifa za kitajiri, taarifa za mafanikio na hapo utatengeneza mazingira mazuri ya kufanikiwa.
Epuka sana kuwa na mawazo mgando, mawazo ambayo kila wakati yanalenga kukukwamisha. Ukiwa na mawazo hayo utateseka sana kwenye dimbwi la umaskini na hautaweza kutoka hapo. Kikubwa endelea kuwa chanya mpaka kuhakikisha ndoto zako zinatumia na kuwa kweli.
No comments: