LEYLA..! (Binti bikra) ~Sehemu ya9~
LEYLA..!
(Binti bikra)
~Sehemu ya9~
Ilipoishia..
Mara ghafla nikasikia mlango wa chumba kile ukigongwa..
Endelea..
Kwanza kabisa nilijikuta nikimfunika yule mwanaume kwa mashuka mashuka na kuzificha sehemu zenye damu zisionekane.
Kisha ndio nikaenda kufungua mlango.
"Kuna dada mmoja ameacha hii simu pamoja na funguo za gari yako pale mapokezi, amesema jana ulikua umelewa sana hivyo asingeweza kukupa kitu chochote..!" Alisema dada huyo ambae aliyekuwa akifanya usafi wa vyumbani.
"Yeye ameelekea wapi..?" Niliuliza kwa shauku ya kutaka kujua ni wapi alipoelekea mama lishe ili nijue ni nini cha kufanya na ile maiti iliyokua ndani.
"Amesema anawahi kazini kwake na wewe unapajua, hivyo ukiamka uende ukapate supu..!" Alisema mdada huyo huku akiendelea na usafi.
Niliufunga ule mlango na kurudi ndani, nilivaa nguo zangu harakaharaka na kutoka nje hadi kwenye gari langu, niliwasha gari na kuondoka maeneo hayo.
Huku nyuma niliacha kelele za watu tu..
Jioni ya siku hiyo nilikua mpweke na mwenye uchovu sana nikiwa nimekaa sebuleni kuangalia taarifa ya habari.
Looh.. nilishtuka sana baada ya kumuona yule kijana aliyekufa kule gest akitangazwa, mwandishi aliyekua akiitangaza habari ile alisema kuwa kifo cha mtu yule kilifana na kifo cha juzi yake tu kilichotokea kule baharini, hivyo inaonyesha wazi kuwa mtendaji wa matukio haya ni mtu mmoja..
Kiukweli moyo wangu ulienda mbio sana, ghafla nilimuona yule binti aliyenipa funguo za gari yangu akiwa anahojiwa.
"Nikimuona huyo dada mwenyewe ninamjua kwa sura..!" Alisema binti yule.
Hee.. mwenzangu, yaani kumbe msako uliokuwa ukifanywa uliwakumba watu wengi jamani, niliweza kumshuhudia mama lishe wangu akiwa amepigwa pingu pamoja na yule mwanaume mmoja miongoni mwa tuluokuwepo ile jana pale bar.
Laa haulaa.. kumbe nilisahau kuwa ile jana yule mama lishe alinipiga picha kupitia ile simu yake, basi yule mtangazaji aliiweka picha yangu kwenye televisheni na kunitangaza kuwa mimi ndio muuwaji..
Kwa hakika niliogopa sana na sikujua nitafanya nini sasa ili kuyakomboa maisha yangu.
Kwa jinsi nilivyokua nimechoshwa na zile habari, nilijikuta napitiwa na usingizi hadi asubuhi.
Katika usingizi ule, niliota eti tupo kwenye duka la nguo la mavazi ya harusi tunachagua nguo kwa ajili ya harusi yetu mimi na mwarabu huku tukipigana mabusu tele.
Tukatoka katika duka hilo na kuingia katika gari, lakini kabla hatujaondoka walikuja askari na kulisimamisha gari lile, wakatuangalia huku wakiangalia picha waliokuwanayo mkononi na kunifananisha mimi, huku nikiwa natetemeka ambapo nilimsikia mwarabu wangu akisema eti nisihofu chochote.
Wale askari waliondoka na kuturuhusu..
Hee.. kumbe ilikua ni ndoto tu jamani..
Nilikuja kushtuka baada ya kusikia kelele za mlango ukigongwa.
Moyo wangu ulifanya paa.. hofu ilinitawala na kushindwa hata kusimama ili nikafungue mlango.
Basi nilijikaza na kwenda hadi mlangoni na kuufungua mlango ule..
Hee.. sikuweza kuamini macho yangu kwa nilichokiona, kumbe alikua ni mwarabu wangu amerudi kutoka Oman.
Unaambiwa nilimkumbatia kwa furaha na kuona sasa nipo katika mikono salama.
Sijui ni kwa sababu ya ile ndoto au nini, lakini kitendo cha kumuona tu kwangu ilikua kama ni ushindi.
Tulishinda wote ndani kutwa nzima, huku akinipa stori za kwao Oman jinsi walivyokua wakini subiri kwa hamu.
"LEYLA.. nataka tufunge ndoa na tukaishi kwetu Oman..!" Alijaribu kushawishi mwarabu huyo akijua bado nitaendelea kukataa.
Moyo wangu uliripuka, furaha tele ilinishika na kuona huyu mwarabu ni kama mkombozi, kiukweli sikuweza kukataa, ukizingatia na taifa langu likini tafuta kuwa mimi ni muuaji, basi sikuona sababu ya kuendelea kuishi katika nchi hii, hivyo nilimkubalia.
Siku iliyofuata tuliingia kwenye gari na kuelekea mlimani city katika maduka ya mwarabu huyo, tuliingia katika duka lake moja lenye vifaa vyote vya maharusi na kuanza kuchaguachagua na kupata tulichokihitaji, ghafla ikanijia ile ndoto ya usiku wake, nikakumbuka tukio hili mbona kama nilishawahi kulifanya katika ndoto.
Basi tulitoka hadi nje na kuingia hadi ndani ya gari, lakini kabla hatujaondoka walifika pale askari wanne wakiwa na silaha zao mkononi na kutuamuru tushuke, hii kidogo ilikua tofauti na ile ndoto niliyoiota, ghafla nikamsikia yule mwarabu wangu akisema usijali.
Tuliposhuka wale askari wakanifunga pingu na kuniingiza katika gari yao na kuondoka na mimi ambapo hata sikujua napelekwa wapi, nilimuacha mwarabu akipata tabu ya kulifuatilia gari lile kwa nyuma..
Tulipita njia ya chuo cha ardhi kupandishia njia ya chuo cha UDSM, ambapo tulipofika mbele sehemu yenye ukimya na utulivu wale askari walisimamisha gari lao na kupaki pembeni.
Mara na yule mwarabu wangu naye alikuja kupaki pembeni na kuanza kuongeanao, nilimshuhudia akitoa kitita cha pesa kwa askari wale, baadae niliachiwa na kuondoka na mwarabu wangu.
Tulipofika nyumbani, yule mwarabu aliniuliza kwanini nilikua muuaji, ambapo nilimwambia wamenifananisha tu lakini muuaji sio mimi.
Alinielewa japo sio sana.
Basi usiku ulipofika ndio mwarabu wangu akadai chenji yake, alinishika mkono hadi chumbani.
"LEYLA..! mimi mwenzio leo nimeshikwa, japo nilikuahidi sitokugusa hadi nikuoe lakini leo unipe tu..! Alisema maneno hayo yule mwarabu huku akianza kunivua nguo na kubaki kama nilivyozaliwa.
"Kiukweli mimi mwenzako ni bikra.. na nilimuahidi marehemu mama yangu mpaka nikiolewa ndio nitampatia mtu atakaekuwa ni mume wangu..!" Nilijaribu kujitetea huku nikijifanya kulia kwa unafki.
"Hee.. kumbe wewe ni bikra..! Sasa mbona hukuniambia mapema.. lakini mbona unaonekana mtundu sana kitandani..!" Aliuliza maswali hayo mwarabu kumaanisha alikua kama hajaniamini bado, lakini baada ya kunichunguza kwa muda aliridhika na kukubali kuniachia, hivyo tulipanga kufunga ndoa baada ya wiki moja, hapo ikiwa bado wiki mbili tu nifikishe miaka21 ambapo niliamini nitakuwa huru.
Itaendelea...
Unadhani LEYLA atakuwa huru..!
Je.. vipi kuhusu hatma ya mwarabu baada ya ndoa..
Majibu yako yapo katika sehemu ya10..
No comments: