MREMBO WA KIJIJI. SEHEMU YA SABA-07





MREMBO WA KIJIJI.

     SEHEMU YA SABA-07

"Daah babu bwana na maneno yake,yani hata sielewi kamanisha nini. Ila  nisubiri akirudi nitamuuliza kamanisha nini kusema hivyo" Alijisemea Saidon wakati huo babu yake ameshaindoka zake kuelekea shambani. Na kabla hajarudi chumbani walau amalizie lepe la usingizi, alielekea kwanza jikoni akakuta sufulia mbili juu ya mafiga. Sufuria moja likiwa na mihogo ilihali sufuria lingine likiifunika mihogo hiyo. Saidon aliguna baada kufunua na kukutana mfuke. Kimoyomoyo akajisemea  "Kitu cha kuchemshwa hicho, nasikia iko poa kwa karanga za kukaangwa"

"Ahahahaha" Alimaliza kwa kicheko Saidoni.

  Uapande wa pili kunako mji wa mzee Nhomo yalisikika mazungumzo ya Nhomo na mkewe. Mzee Nhomo alianza kwa kusema "Unajua mke wangu  hiki kijiji hakinitambui vizuri"

"Kwanini mume wangu?.." Aliuliza mama Chaudelea.  Mzee Nhomo kabla hajamjibu mkewe alishusha pumzi ndefu halafu akasema

"Unafikiri huu ushenzi unaotaka kufanyika nisipokuwa makini sinitawakosa wote?.."

"Enhee" Aliongeza kuuuliza mama Chaudele akitaka kujua ni nini anachomanisha mumewe.

"Inamaana mama Chaudele hujui kama kuna vita ya chini kwa chini kati yangu na mzee J?.." Alihamaki mzee Nhomo. Mama Chaudelea  alipona mumewe kahamaki alijishusha na kisha kujibu "Haswaa nafahamu hilo mume wangu, Kwahiyo vipi umejiandaa kweli?.."

"Kabisa nipo nimejaa tele, na jana usiku nilipotoka  nilienda kuwaomba msaada wanachama wenzangu ili wanisaidie kuhusu suala hili. Maana kama unavyojua mimi kitambo nilistafu na kilichonisaidia ni kwa sababu enzi zangu nilikuwa mtiifu na mchapa kazi, kwahiyo kurejea kwangu haikuweza kuwafanya wanibinie"

"Looh!  Jambo la heri hilo mume wangu, waonyeshe kuwa wewe sio mtu wa kuchezewa hovyo " Alisema mkewe Nhomo. Mzee Nhomo aliangua kicheko kisha akaongeza kusema "Vipi leo nianzie wapi? Mtoni kukagua nyavu zangu ama nianzie porini kukagua mitego?.."

"Mmh mimi naona leo anza mtoni, tena uwahi kabla  wenzako wajafika" alijibu mama Chaudele.

"Hahahaha! Hahahah!  Hahah" Alicheka mzee Nhomo, alipokatisha  kicheko hicho alinyanyuka akatoka chumbani akiwa tayari na mavazi ya kwenda nayo kuzungukia mtoni na porini. Lakini kabla hajafika nje, ghafla Chaudele alitoka chumbani. Binti huyo alimsalimu baba yake na hapo ndipo mzee Nhomo alipopata nafasi ya kumuasa binti yake.

"Chaudele, nadhani unafahamu kuwa mzee J alileta posa ya mwanae akiwa na lengo la kukuoa.."

"Ndio baba nafahamu vizuri tu, tena kibaya zaidi mwanae ameshatangaza ubaya kwa vijana wa hapa kijijini. Yani kijana yoyote atakayenisimamisha akimuona tu balaa analo" Alisema Chaudele.

Baada kusema hayo, mzee wake aliendelea kusema "Enhee sasa basi, nakuomba popote pale utakapo muona Chitemo achana naye kaa naye mbali kabisa, na pia popote pale utakapokutana na mzee wake hata salamu usimpe wanalengo baya dhidi yetu"

"Sawa baba wala usijali kuhusu hilo, kwanza huyo Chitemo mwenyewe sitaki hata kumsikia" alijibu Chaudele.

"Sawa mimi ngoja nikaangalie mitego yangu"

"Anhaa sawa baba safari njema, na nakuombea upate ili leo tule kitoweo kizuri" Alisema hivyo Chaudele huku akiachia tabasamu. Nhomo aliondoka zake, wakati huo upande mwingine aliona kijana akiendesha baiskeli kwa kasi ya ajabu. Kijana huyo aliitwa Maige, kasi hiyo aliyokuwa akiindesha baiskeli yake alikuwa akielekea nyumbani kwa mzee Mligo. Alipofika alimkuta kijana Saidon ameshaamka, alikuwa amekaa nje akiota jua.  "Aaaah Swahiba, habari za tangu jana bwana" Alisema Maige akimsalimu Saidoni, Saidoni alimkumbuka Maige kwani kwa mara ya kwanza walikutana stendi na alimpokea begi  moja kwa moja akamfikisha mpaka kwa babu yake.

"Daah salama tu mambo vipi?.." Alijibu Saidon wakati akimpa mkono Maige.

"Nzuri pia, naona umetulia unaota jua"

"Ndio bwana maana kibaridi hiki sio mchezo"

"Ahahahaaa ni kweli, istoshe mmeshazoea maisha ya mjini. Ukiamka tu unakunywa chai kwahiyo baridi lote linaondoka"

"Kweli kabisa" Alijibu Saidon kisha akanyanyuka akazipiga hatua kuelekea ndani, punde si punde alitoka na vipande kadhaa vya mihogo pia na slesi kadhaa za mikate. "Karibu mihogo na mikate"  Alisema Saidon akimkaribisha chakula hicho Maige. Maige alipoona mihogo iliyochemshwa pamoja na mikate aliachia kicheko kidogo huku akikataa akidai kuwa ameshiba, ila Saidon alimbembeleza mwishowe Maige alikubali akala.  "Daah rafiki bwana? Haya ngoja nile.  Enhee mjini mnatunyima nini?.."

"Mjini kule safi tu, hivi unaitwa nani?.."

"Mimi. Mimi naitwa Maige, kijana mstarabu kijiji kizima." Alijibu Maige baada Saidon kumuuliza jina lake. Saidon alicheka kidogo kisha akasema ""Ni kweli wewe ni kijana mstaarabu, kwanza unaonekana hata machoni. Ujue jana uliponipokea begi nikajua kabisa jamaa huyu mkarimu na mstarabu pia.ammh mimi naitwa Saidon"

"Waooooh! Bonge la jina ndugu yangu. Saidon. Kijiji kizima hakuna jina kali kama jina lako, na kuaminisha hilo hata hawa warembo wa hapa watakushobokea" Alisema Maige. Saidon aliachia tabasamu baada kusikia maneno ya kijana Maige. Baada ya hapo alishusha pumzi na kisha akauliza "Kwahiyo bwana Maige hapa kijijini kuna madem wakali sana?.."

"Weweweeeeeh! Nakwambia sio mchezo, usifikiri mjini tu ndio kuna wanawake wazuri hata vijijini napo wazuri wamejaa. Moja ya vijiji iliyojaza mabinti wazuri ni hiki hapa kijiji cha Ndaulaike "

"Daah! Safi sana. Kwanza bwana Maige ukae ukijua asilimia kubwa madem wa mjini sio wasafi sana, yani utakuta akipanda daladala ananukia mafuta yenye harufu nzuuuri ila sasa akimuingiza chumbani tu akavua nguo ya juu na yandani. Anatoa halufu kali kama kama kafa panya ndani"

"Anhahahaaaa hahahaaa, wewe weeh Saidoni bwana acha utani wako. Kwahiyo unataka kuniambia kwamba madem wa mjini wananuka?.." Aliuliza Maige baada kukatisha kicheko chake. Saidon kabla hajamjibu alicheka kisha akajibu "Ndio maana yake ingawa sio wote" . Mara baada kujibu hivyo maongezi mengine yalifuatia. Waliongea kwa tabasamu na furaha pia, Maige alimtajia baadhi ya maisha ya kijijini hapo, kwa muda mfupi tu watu hao wakawa marafiki zaidi. Lakini baadae kidogo babu yake alirejea kutoka shamba, akajikuta akifurahi kumuona Maige yupo na mjukuu wake sababu alijua tabia njema aliyonayo kijana huyo inamfaa kuwa mwenyeji wa mjukuu wake ambaye ni Saidoni.

"Saidon.."

"Naam babu" Aliitika Saidon baada kuitwa na babu yake.

"Eeeh huyo ndio rafiki yako, anakufaa sana.  Na Maige huyu  ni mjukuu wangu, kaa naye bega bega sawa?.."

"Sawa babu wala usijali" Alijibu Maige. Baada ya hapo, mzee Mligo aliwataka vijana hao waelekea nyumbani kwa mzee Nhomo wakanunue nyama kwani alisikia mzee Nhomo amenasa swala. Saidon na Maige walikubali, waliambatana na  mzee Mligo mpaka nyumbani kwa mzee Nhomo kununua nyama. Walipofika walikaribishwa na mrembo Chaudele, Saidon alipomuona mrembo huyo alijikuta akishtuka, nafsi na moyo wake vikahisi kumuhitaji mrembo huyo.  Akimtazama pasipo kupepesa uso wake, wakati huo huo Chaudele naye alipo mtazama Saidoni akajikuta akuachia tabasamu na kutazama pembeni akimuona haibu.

"Naam! Ama kweli kijijini ndipo walipo warembo walio umbika, mjini yale makapi tu. Zana ninazo za kutosha, sasa nitaanza na huyu huyu"

  "Play Boy ameingia kazini. Ahahahaha hahahaha" Alijisema Saidoni ndani ya nafsi yake huku akimkodolea macho Chaudele. Wala asijue kuwa kuna vita ya kali  ya kichawi inachemka shauri ya mrembo huyo. Na kuna mwamba Chitemo mtoto wa mzee J anamfukuzia mrembo huyu huyo..

   HILI NI BALAA KUBWA, NAHISI HUWENDA HATA MZEE MLIGO babu yake SAIDON NI MEMBER.. ngoja tuone,  maana hata Chaudele kama kashaanza kushoboka. Asije mponza mwamba wetu.
    TUKUTANE SEHEMU IJAYO.
 



No comments: