MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI-22






MREMBO WA WA KIJIJI


       SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI-22

"Bibi Pili bibi Pili.." Moja ya wachawi waliofika nyumbani  kwa bibi Pili alipasa sauti kumuita bibi huyo. Bibi Pili sauti ile hakuweza kuisikia kwa sababu hirizi ambayo ingemfanya ajue kinacho endelea kwanye ulimwngu wa giza hakuwa nayo iliungua na moto. Hivyo sauti iliendelea kupaza mpaka pale mkuu wao alipomwambia akae kimya "Wananzengo hapa tayari hili jambo limeshakuwa tata, kwa sababu kwa dalili hizi ni wazi mwanachama mmoja tumempoteza naye si mwingine ni bibi Pili.." Alisema mkuu wa kikosi hicho cha wachawi akiwaasa watu wake. Baada kusema hayo akakaa kimya kidogo kisha akaendelea kusema "Nafikiri kila mmoja kuna harufu anaisikia " Mkuu huyo aliposema hivyo mara ghafla wale wachawi wakaanza kuzifanyisha kazi pua zao kwa kunusa huku na kule. Zoezi hilo lilichukuwa takribani dakika tano, na baada ya hapo mchawi mmoja akasema " Ndio mkuu harufu ipo.. "

"Je, harufu gani hiyo" Alihoji mkuu huyo wa kichwani kwa upande wa kundi la kinabibi Pili. Hapo akamnyooshea mkono mchawi mwingine tofaut ina yule aliyemthibitishia mkuu wake uwepo wa harufu.

Yule aliyenyoisha kidole alisimamishwa ili ataje, naye akataja kitendo ambacho kilizua tafarani katika mji wa bibi Pili kila mmoja alionekana kutoamini kama kweli bibi Pili angechoma hirizi yake ya muhimu hali ya kuwa wanamtihani mzito mbele yao, hata wasijue kuwa kuna maombi yalifanyika yaliyopelekea hirizi ya bibi Pili iliyokuwa juu kwenye kichanja kudondokea kwenye moto ulikokuwa ukiwaka jikoni.

"Mkuu kwahiyo hatua gani itachukuliwa?.." Alihoji mchawi mmoja. Kabla mchawi huyo hajajibiwa mchawi wa pili akadakia kwa kusema "Mkuu nafikiri utulize jazba kwanza ili kesho asubuhi mmoja wetu aje azungumze na bibi Pili ili tujue kimemkuta nini hasa mpaka ikampelekea kuchukuwa hii" Hoja hiyo ya mchawi wa pili aliyetoa kwa niaba ya kumtetea bibi Pili iliweza kuungwa mkono na wachawi karibia wote. Na hapo ndipo mkuu wao alipoamuwa kukubaliana na ushauri huo. Hilo suala likiwa limekwisha, punde si punde wakaanza kumjadili yule tamtalaamu.

Mkuu wao akasema "Huu sasa ni wakati wa kuzungumzia yule mtalamu ukiachilia mbali adui mwingine aliyeongezeka. Yeye anatumia Biblia, habari zake nafikiri manazipata maana kajizolea umaarufu mkubwa tangu aingie hapa kijijini..." Alisema mkuu huyo akiwaambia watu wake.

"Ndio mkuu " Walijtikia wachawi hao, na hapo ndipo mkuu huyo alipo teua makundi matatu tofauti. Kundi moja liliteuliwa kwa niaba ya kula sahani moja na mtaalamu aliyeletwa kwa niaba ya kuwaumbua wachawi wa kijiji ilihali kundi la pili nalo liliteuliwa kwa niaba ya kula sahani moja na mtumishi wa Mungu ambaye yupo kijijini kwa niaba ya kukibadilisha kijiji kimgeukie Mungu. Huku kundi la tatu nalo, liliteuliwa kwa niaba ya kufika nyumbani kwa bibi Pili ili kumuuliza kwa ufanisi kipi kisa na mkasa kilicho mpelekea kukiuka utaratibu wa chama chao.

"Natumaini nyinyi niliowachagua hamtoniangusha, kila mmoja kati yenu naelewa umahiri wake wa kufanya kazi. Na nyinyi mliobakia ni kutoa ushirikiano mara moja pindi utakapo takiwa.." Aliongeza kusema hayo mkuu wao wa wachawi mara baada kukamilisha zoezi la kugawa makundi ambayo yatashughulika na masuala yale aliyoyaagiza. Kila kundi lilikuwa na watu watatu.

Baada ya hapo ndelemo na vificho vikafuatia, wachawi hao waliimba na kucheza ngoma za asiri. Na mwisho wa ndelemo hizo kila mmoja alipotea mpaka pale alipobakia mkuu peke yake ambapo naye hakuchukuwa muda mrefu kusalia mahala hapo, punde si punde akapotea, vumbi ikatimka na Miele ya radi.

   Usiku huo huo upande wa pili alionekana mzee Nhomo akiwa kilingeni kwa mara nyingine baada kupotea kwa kipindi kirefu tangu aombe nguvu za kukabiliana na mzee J, ikimbukwe mzee J na mzee Nhomo ni maadui wa muda mrefu na yote shauri ya watoto wa mzee J wakuitwa Chitemo anamtaka mtoto wa mzee Nhomo ambaye ni Chaudele ilihali jambo hilo Nhomo halitaki hali ya kuwa tayari kishika uchumba cha mwanae  ameshakula huku hataki kumtoa mtoto wake. Kitendo ambacho kinazaa tafarani kijijini Ndaulaike. Vita hiyo ya wahenga inajikuta ikiambatana na bibi Pili mara baada mtoto wa mzee J yule yule Chitemo kuamua kumbwaga mjukuu wa bibi Pili hali ya kuwa amemchezea kwa kipindi kirefu mno na kuwekeana ahadi kuwa wataoana. Lakini mwisho wa siku Chitemo anamtosa Pili kwa matusi na dharau kubwa, habari hiyo Pili ikamfikishia bibi yake na hapo ndipo uhasama unapoanzia baina ya mzee J na bibi Pili. Lakini wakati yote hayo yanajili kijijini Ndaulaike, mara ghafla wageni wawili kwa nyakati tofauti wanaingia. Mtumishi wa Mungu na mtaalamu wa mambo ya giza, wote nia yao ikiwa ni moja tu nayo ni kukibadilisha kijiji cha Ndaulaike kiepukane na kutegemea ushirikina.

  Hivyo basi mzee Nhomo akiwa katika mavazi ya kichawi aliomba uwezo mara mbili kama alivyoambiwa kuwa anatakiwa kuongeza nguvu za kuweza kufua DAFU kwa mzee J. Ajabu siku hiyo alichokitegemea mzee Nhomo hakuweza kutokea na mwishowe aliondoka mikono nyuma kichwa chini huku akiwa na hofu kubwa moyoni "Nitarudi kesho" Alijisemea mzee Nhomo baada kutoka kapa.
   Kesho yake asubuhi palipo kucha, nyumba kwa mzee J asubuhi na mapema mzee huyo aliamka kwa kujikongoja. Alipofika nje ghafla alipigwa na butwaa baada kukuta majivu kando kidogo ya nyumba yake,J alichechemea kuyakaribia majivu hayo alipoyakaribia akabaini mazaga zaga yake yote yameteketezwa kwa moto.  Alikasirika sana hima akarudia ndani kusema na mkewe lakini kabla hajaingia ndani akakutana naye mlangoni akiwa na furushi lililojaa nguo.

 "Khe unaenda wapi na ni nani kachoma mazaga zaga yangu?.." Alihoji mzee J kwa sauti kali. Mama Chitemo akamtazama kwa jicho ngebe kisha akajibu "Waliokuleta jana ukiwa umepoteza fahamj, lakini pia nataka nikuulize wewe baba nilini utacha ushirikina? Faida gani unayo ipata?. Sasa ngoja nikwambie ukweli, nimechoka kukuvumilia narudi kijijini kwetu ebo.." Mzee J akashtuka kusikia maneno hayo ya mkewe, na kabla hajasema jambo lolote ghafla akatokea yule mtumishi wa Mungu na akisema" Naam Mungu mkubwa, na sasa umefika ule wakati wa kumrejesha zizini kondoo aliyekuwa amepotea "

"wewe kijana wewe unamaana gani kusema hivyo?.." Mzee J Aliuliza kwa jazba, mtumishi wa Mungu Steven akacheka kidogo kisha akajibu "Namaanisha leo lazima wewe na mkeo muokoke, kwani nyie ni kama kondoo mliokuwa mmepotea kwa maana hiyo nawarudidha zizini, mmh bwana yesu asiwe sana"

J alionekana bado kutomuelewa Steven, na ndipo kwa hasira akaongeza kusema "Utakuwa kichaa na kama sio kichaa basi umetumwa uje kunitukana. Uanamanisha ubongo wangu ni wadudu na ndio maana ukaamua kuniita kondoo si ndio? Sasa nasema hivi mimi sio kondoo wala punda, kuokoka siokoki na kipigo cha mbwa koko utakipata leo mshenzi wewe" Maneno hayo mzee J aliyaongea kwa msisitizo mkubwa, laikin mtumishi wa Mungu  Steven hakuogopa mkwala huo, kwa kujiamini akajibu "Mzee kipigo hicho hakipo na kuokoka utaokoka tu " Alipokwisha kusema hayo ghafla mzee Bidobido akatokea akiwa na dhana za kichawi.

"Ahahaha hahaha, safi sana umeona kijiji hiki ni kama pombe ya ngomani" Alisema mzee Bidobido akitanguliza cheko kubwa lililo pelekea upepo mkali kuvuma sambamba na wingu jeusi kutanda kwa muda mfupi, radi ikamulika, Ngurumo nzito nayo iliyo pelekea kuzua hofu Ndaulaike ikapaza..
Biblia aliyoshika mtumishi wa Mungu mkononi ikamponyoka..
   BALAA
 

Itaendelea..
    NI KIPI KILIJILI HAPO?.. Mbona kama Bidobido ni moto kuliko brother wake? 😂Biblia chini..
  SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA.



No comments: