MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA YA ISHIRINI NA MOJA-21
MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA YA ISHIRINI NA MOJA-21
Steven akageuka akakutana na uso wa mzee J akiwa ndani ya mavazi yake ya kichawi. "Hahahahahah habari zako nimezipata tangu uingie hapa kijiji, hivi wewe kijana ni Mungu yupi unayemzungumzia wewe ambaye anaweza kubadilisha mwenendo wa maisha yetu?.." Alihoji mzee J akianza kwa kuangua kicheko. Mtumishi Steven alipoyasikia maneno hayo naye akacheka kidogo halafu akajibu "Ni mwamba kati ya miamba, ndiye aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote uvionapo katika uso wa dunia. Wewe ni mwanadamu katu huwezi kushindana na roho mtakatifu aliye ndani ya mwili wangu. Kukuaminisha hivyo ngoja nikuonyeshe ili kuanzia leo utubu na uokoke katika Jina la yesu.. "
" Unasemaje? Mimi kabisa mzee J, kingunge hapa kijijini eti niokoke? Hapana labda sio mimi " Aliongeza kusema mzee J na kisha akapiga mrunzi uliowaita watu wake ambapo walitokea moja baada ya mwingine. Vijana wale walioambatana na Steven waliogopa lakini Steve akawatoa was wasi kwa kusema " Msiogope vijana, hawa ni kondoo waliomkimbia zizi, mimi kama mtumishi ama mchungaji wa kondoo hawa jukukumu langu ni kuwarudisha zizini.. " Maneno hayo ya mtumishi wa Mungu Steve yaliwatoa hofu wale vijana iliahli muda huo kila baada ya sekunde mchawi mmoja baada ya mwingine walizidi kuongezeka na mwishowe timu nzima ya mzee J ikatimia.
" Hahahahahah " Mzee J alicheka kwa mara nyingine, na mara baada ya kukatisha kicheko chake akawaambia watu wake "Wananzengo mnamuona huyu mtu?.. " wafuasi wake wote kwa pamoja wakaitikia
" Ndio mkuu.. " J akatikisa kichwa kama ishara ya kukubali jambo fulani, akaguna kidogo kisha akaongeza kusema " Basi tunaanza na huyu mtu kisha tutamaliza na yule anayejiita mtalamu ili kazi iwe imekwisha. Baada ya hapo tuendelee na michakato wetu wa kumtaka Chaudele, haiwezekani Nhomo anifanyie unyama.. Haya mara moja wote motooo" Ghafla kikosi hicho cha wachawi kilichokuwa kikiongozwa na mzee J kikaanza kumtupia makombora mtumishi wa Mungu bwana Steve. Kwa kutumia biblia aliyokuwa nayo Steve aliweza kuyamudu yale makombora huku akikemea kwa Jina la yesu. Vurumai la hatari lilizuka maeneo hayo, mzee J na kundi lake hawakukubali kushindwa bado walizidi kuungana kwa pamoja na kisha kupigana na mtumishi wa Mungu, baadaye kundi hilo la wachawi lilijikuta likiishiwa nguvu baada mtushi Steve kujibu mashambulizi kwa kuomba moto kutoka kwa angani uweze kuwadabisha wachawi hao ili mioyo yao iliyomigumu kama jiwe ilainike iwe mfano wa mkate na waamini kuwa Mungu pekee ndio kila kitu hapa duniani,vile vile kila amtumainiye katu hawezi kupata tabu. Moto huo wa ajabu, moto mwembamba ufananao rangi ya blue. Moto ambao mkali kama moto wa gesi ulitua kifuani kwa mzee J kutoka kwenye ile Biblia aliyoshika mtumishi Steve.
Mzee J akaanguka chini na kupoteza fahamu. Kitendo kile kiliwaogopesha wale wengi waliobakia, na hapo wakakubalina wapotee mahali hapo kabla mambo hayajawaharibikia zaidi. Muda huo wanajadili upande wa pili mtumishi wa Mungu Steve alikuwa akipiga maombi.
"Taondoke tumuache mkuu?.." Aliuliza moja ya wachawi waliokuwepo mahala hapo.
"Msogelee mguse ili tuondoke naye" Amri ilitoka kwa mchawi mwingine. Punde si punde yule mchawi wa awali aliyeuliza uwezekano wa kuondoka na mkuu wao alimsogelea mzee J kwa dhumuni ya kumgusa ili atoweke naye. Lakini alipomgusa ghafla alitoa mkono wake na kisha kuhaha kana kwamba aligusa kaa la moto. "Mbona unatoa mkono kwani kuna nini?.." Aliuliza yule mchawi aliyetoa amri kwa mwenzake kwamba amguse mzee J.
"Moto, mwili wake wote unamtoto" Alijibu yule mchawi. Jambo hilo liiwashangaza wale wachawi wakati huo mtumishi wa Mungu alikuwa akiendelea kuomba kwa imani ya hari ya juu, na mwisho wa maombi akasema "Baba wa mbinguni shusha moto wako, shushaa Mungu wangu ili wakujue kuwa wewe ni Mungu kati ya miungu" Maombi hayo ya yaliyafanya kazi, kwa mara nyingine tena moto wa ajabu kama ule wa awali ulivuma kuelekea mahala pale walipo wachawi ambao walikuwa wakijaji na kustaajabu kitendo cha mwili wa mkuuu wao ambao ulikuwa moto mithili ya chuma kilichotoka kufuliwa na muhunzi. Moto ule kabla haujawafikia ghafla wakapotea ikabaki vumbi tu, lakini kitendo hicho bado hakikumfanya mtumishi wa Mungu kukatisha maombi yake. Bado aliendelea kuomba kwa imani kubwa huku akikiombea pia na kijiji kizima cha Ndaulaike, maombi hayo yaliweza kusababisha balaa upande wa pili nyumbani kwa bibi Pili kwani wakati bibi huyo akiwa nje akichambua mboga za majani ili apike chakula, mara ghafla alisikia kitu fulani kikilia ndani mfano wa puto lilopasuka.
Haraka sana akasitisha zoezi lake akakimbilia ndani kwenda kuangalia kipi kilicho tokea. "Mmmh ndaheze" Alijisemea bibi Pili akiwa na maana kuwa amekwisha, na hiyo yote ni kwa sababu alikuta kibuyu alichokuwa amekining'iniza juu ya kichanja kilicho juu ya mafiga kilikatika na kakadondokea kwenye moto ambao tayari ulikuwa umekolea ukingojea sufuria. Hirizi mbali mbali za bibi Pili zilianza kufungua, na hapo ndipo akaanza kuhaha kwa kuziokoa alifanikiwa ingawa kuna baadhi ziliteketea kwa moto.
"Mmmmh Nitasema nini kwa mkuu sasa? Na hii iliyoungua ndio ya muhimu kuliko zote" Alirudia kujisemea bibi Pili safari hiyo akiwa ameshika kiuno chake, mwili na akili yake vyote kwa pamoja vikiwa vimechoka.
Jioni ilipo wadia kijiji cha Ndaulaike kilionekana kupooza, hali hiyo iliweza kuwashtua watu wengi sana. Katika nyumba ya mzee J simanzi nzito ilitanda, kwa sauti ya unyonge J akasikika akimwambia mkewe mama Chitemo "Mke wangu, balaa nililokumbana nalo kiukweli sijawahi kulishuhudia katika maisha yangu"
Mama Chitemo alipoyasikia maneno hayo ya mumewe akamgeukia kisha akamuuliza "Balaa gani tena hilo mume wangu? Halafu istoshe watu waliokuleta hapa nyumbani wawili nawafahamU ila mmoja simfahamu" Mzee alishtuka baada kusikia maneno ya mkewe.
"Unataka kuniambia walikuwa watu watatu? Vijana wa wawili mtu mzima fulani hivi wa makamo?.." Alihoji mzee J kwa taharuki kubwa. Mama Chitemo akajibu "Ndio, istoshe mmoja alikuwa ni mchungaji bila shaka kwa sababu walipokufikisha tu wakanisalimia kwa ukarimu na upole, nikawauliza wamekutoa wapi? Hawakunijibu. Ammh vile vile yule mtu ambaye ni mchungaji alikuombea na akanihakikishia kuwa utapona na utakuwa Sawa.. " Maneno hayo ya mama Chitemo bado yalimshangaza mzee J, ndani ya moyo wake akajisemea "Hivi maombi hayo yatakuwa yameayaacha salama matunguli yangu?.. " Kabla hajapata jibu, mara ghafla mkewe akamuuliza "Baba Chitemo, unampango gani wa kuachana na haya masuala ya uchawi? " Swali hilo lilizidi kumuweka mzee J katika hali ya sintofahamu kuhusu matunguli yake kwani hata mara moja haijawahi kutokea mama Chitemo kumuuliza swali hilo.
"Sina mpango wa kuacha labda mpaka nitimize azma yangu niliyopanga, na hata hivyo sifikirii kuacha. Na kwanini umeniuliza swali hilo..."
Ghafla mama Chitemo akawa mnyonge akashindwa aseme nini, mwishowe akashusha pumzi ndefu akatabasamu kidogo kisha akasema "Usijali nitakwambia kesho "
"Kesho? Namkwambia hivi ole wako nisikute matunguli yangu ndio utanijua kuwa mimi ni nani?" Aliongeza kusema J kwa jazba kubwa huku akijinyanyua kwa tabu kutoka kwenye kilago alichokuwa amelalia akiota moto jioni, alizipiga hatua za pole pole kuingia chumbani kulala kwani siku hiyo hakuwa na hata hamu ya kula kabisa.
Usiku ulipo ingia, usiku wa balaa, kundi la wachawi lilitua nyumbani kwa bibi Pili kwa niaba ya Kujadili mambo mawili tofauti. Jambo la kwanza ni kuhusu mtaalamu, na jambo la pili ni kumuhusu matumishi wa Mungu aliyeingia kijijini kwa nia ya kuleta mapinduzi. Lakini kikao hicho cha dharura ghafla kiliingia dosari baada kugundua kuwa bibi Pili kuna jambo tata kalifanya na kwa kanuni zao kufanya jambo hilo ni kinyume na sheria yao kwani utakuwa umevunja mashart ya kuwa mwanachama na adhabu yako ni kifo ili usivujishe siri..
JE, NI JAMBO GANI HILO? NA VIPI UPANDE WA MAMA Chitemo, mtumishi kafanya jambo gani baada kufika nyumbani kwa mzee J?
Usikose Sehemu ijayo siku ya JUMA TATU.. lakini kama utataka kulijua jambo hilo leo leo... SHEA MARA kisha njoo Inbox..
MAMBO NI MOTO DADEKI ISIWE MTU KACHOMOLEWA BETRI 😂😂🙈

No comments: