MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA ISHIRINI-20






Saidon alimtazama Chaudele wakati huo Chaudele naye akiendelea kumtazama huku macho yake akiwa ameyalegeza, ukweli muda huo Chaudele alionyesha nia ya kutaka tendo kutoka kwa kijana Saidon. Lakini ugumu ukaja kwa mlengwa kwani tayari alishapewa onyo juu ya Chaudele.

 "Saidon inamaana hunielewi?.." Alihoji Chaudele. Saidon alishusha pumzi kisha akajibu kwa unyonye "Nimekuelewa sana Chaudele ila.."

"Ila nini?.." Alidakia Chaudele.

Saidon akasema "We husikii kitu chochote?.."

"Kitugani Saidon? Ama hunipendi?.." Kabla Saidon hajamjibu Chaudele mara ghafla Maige alifika. Kitendo hicho kilimkera sana Chaudele ambapo alisema "Unaona sasa? Tungewahi kuingia ndani Maige asingetukuta hapa. Kwaheri" Alipokwisha kusema hayo akaondoka zake huku akiwa amefura hasira moyoni mwake, hata Saidon jambo hilo aliligundua kuwa kamkera sana Chaudele. Lakini hakuwa na namna ya kufanya, kwa sababu aliogopa vitisho aliyokuwa akivisikia pasipo Chaudele kusikia "Lah sasa ule uchawi aliokuwa akiniambia rafiki yangu Maige sasa naanza kuuona bila chenga, leo hii nimeikosa bikira? Kitu adimu duniani? Daah ila subiri sikubali" Alisema Saidon ndani ya nafsi yake kisha akazipiga hatua kuingia ndani lakini kabla hajafika mlangoni akasikia sauti kutoka kwa Maige ikisema "Saidon hujaniona ama ndio hutaki mgeni kisa nimekukuta na mrembo wa kijiji?.."  Saidon aliposikia maneno hayo ya Maige akacheka kidogo kisha akajibu "Ah hapana naingia ndani kuchukuwa mapapai ili tule, wakati huo tukiongea mambo mbali mbali. Nina kitu nataka kukueleza rafiki yangu"

"Aanhaa basi sawa ngoja nikae kwanza kwenye kilago nikusubiri ili unambie hicho kitu"  Aliongeza kusema Maige.  Saidon akaingia ndani, muda wa dakika mbili akatoka na mapapai mawili pamoja na kisu.
"Kuna haja ya kuyaosha?.." Aliuliza Saidon.

Maige akaguna kisha akajibu "Mimi tena? Sijui wewe mtoto wa mjini ila kwangu mimi Safi tu yatajiosha tumboni"  Alitania Maige, Saidon akacheka kidogo.

"Basi hakuna tatizo ngoja tuendelee"  Alisema na kisha akapasua katika papai moja.

 "Enhee nambie, nimemuona Chaudele hapa lakini ajabu aliponiona akaondoka zake. Vipi nimewatibulia au?

"Maige rafiki yangu we acha tu, unajua hapo awali uliniambia habari kuhusu huyu binti na vita inayoendelea. Lakini mimi nikakujibu kuwa siku zote uchawi hauji kwa mentali, ila sasa kwa dalili ninazo ziona. NI dhahili huo uchawi utampata mentali tena kwa kasi ya ajabu " Alisema Saidon. Maige akacheka sana, na mara baada ya kukatisha kicheko chake akahoji" Kwanini sasa?.

"Muda mchache uliopita kuna ndoto nimeota imenitisha sana, na kiukweli jambo hili itabidi ni mwambie babu huwenda naye akanisaidia hata kunipeleka kwa mtalamu tofauti na hivyo Saidon sina maisha marefu kwa sababu nipigwa mkwala niachane na Chaudele wakati mimi  moyo wangu umeshamchagua yeye"

"Ndoto? Ndoto gani hiyo?.. " Alirudi kuhoji Maige wakati huo akionyesha utulivu wa hali ya juu ili kumsikiliza Saidon. Saidon akasimulia mwanzo mpaka mwisho namna ndoto ilivyokuwa, na cha ajabu zaidi kilicho mshangaza Maige ni pale Saidon aliposema kuwa sauti ile ya onyo juu ya Chaudele ilirudia kumkanya hata pindi alipokuwa yupo na Chaudele.

"Daaah pole sana, enhe Chaudele naye alifuata nini?.."

 "Alikuja kwa madai kwamba  nimtoe usichana wake" Alijibu Saidon, alishtuka Maige, akashusha pumzi kwa nguvu kisha akasema "Doh kumbe Chaudele pale alipo bado bikira? Enhe bahati hiyo ndugu yangu.."

"Sawa ni bahati ila bahati hiyo inaweza kughalimu maisha yangu, kwa sababu mimi mbishi sitokubali mpaka nimzindue Chaudele ndio nafsi yangu itatulia ngoja babu aje najua kama kijiji hiki kinawachawi basi waganga wa kienyeji hawakosekaniki" Alisema Saidon tena kwa msistizo.
        **********
Upande wa pili alionekana yule mtaalamu aliyeletwa kijiji kwa dhumuni la kuwaumbua wachawi. Mtaalamu huyo alikuwa akiandaa baadhi ya dawa ili kesho rasmi aanze kazi pasipo kuhofia jambo lolote. Lakini kipindi mtaalamu huyo yupo makini na kile anacho kifanya mara ghafla akatokewa na wachawi wawili vikongwe ambaye ni bibi Pili aliyembatana na mwenzake ambaye naye ni mchawi. Mtaalamu alijua tayari mahali alipo sio salama hivyo alisimama na kisha kuwatazama "We kama nani umekuja hapa kijijini kwetu, na kwanini dhamira yako ni kutaka kutuchefua? Unajua historia ya kijiji hiki?.." Alisema bibi Pili kwa sauti kali.

Mtalamu hakutishwa na sauti hiyo, aliangua kicheko  kisha akajibu "Huu sio mkutano wa kuuliza na kujibiwa maswali yako, nimekuja kufanya kazi na hakuna mchawi yoyote atakaye nitingisha mimi ni mwamba kati ya miamba hapa duniani kama mnabisha ngoja niwape dozi ili mjue kuwa aliyejitosa vitani huwa haogopi kifo" Papo hapo mtaalamu akafanya makeke, ghafla jua likatoweka na giza likatanda mchana wa jua kali.

Bibi Pili na mwenzake wakapigwa na butwaa wakatazamana kwa muda wa sekunde kadhaa kisha wakagongeana viganja, kwa nguvu ya pamoja wakamrushia mtalamu makombora. Makombora hayo ya kichawi yalimpata mtaalamu, ajabu punde si punde pale alipokuwa amesimama mtaalamu zilidondoka chini nguo alizovaa huku zikiwaka moto ilihali pasipo yeye kuonekana. Kitendo hicho kikawaacha mdomo wazi Bibi Pili na mwenzake, na hapo ndipo walipojua kuwa mtaalamu sio mtu wa kubeza hata kidogo.

 "Ahahah hahaha" Aliangua kicheko mtaalamu wakati huo yupo nyuma yao, baada ya kukatisha kicheko chake akasema "Kama ni mvua basi haya ni manyunyu, sasa subirini niwaletee mvua ya mawe"  Maneno hayo yaliwaogopesha hao wachawi kitendo kilicho pelekea kupotea eneo hilo. Punde si punde mtaalamu akarudisha ile hali ya kawaida, giza likatoweka zaidi akawacheka sana.

Muda mchache baadaye balozi wa nyumba kumi ambaye ndio aliyempokea na kumpa hifadhi mtaalamu alikuja akamkuta mtalamu yupo bize anatengeneza dawa "Naam habari za mida  hii tena" Alisema balozi.
"Ni salama karibu tutengeneze dawa" Alitania mtaalamu. Balozi akacheka sana kisha akajibu "Haya mambo yanawenyewe bwana"

"Ni kweli kabisa  hujakosea, na unajua siku hizi mbili tatu nilizokaa ndani ya kijiji hiki nimegundua kuwa tayari baadhi ya wale watu wasio wachawi wamelishwa vya kula vya kichawi pasipo wao kujijua, hivyo basi dawa hii ni mahususi ya kuwatapikisha wale wanakijiji waliokula vyakula hivyo vya kichawi "Aliongeza kusema mtaalamu, maneno hayo yalimshangaza sana Balozi, kwa hamaki kubwa akahoji " Kwahiyo unataka kusema mpaka mimi hapa nilipo nimelishwa hivyo vyakula?.. "

 "Ndiooo umekula sana tu, tena sio mara moja wala mara mbili. Na muhusika mkuu ni mwenyekiti wa kijiji"

"Lakhaula nimekwisha,.." Alitaharuki Balozi huku akiwa haamini kile akisikiacho kutoka kwa mtalamu.

     Upande wa pili mzee Nhomo alijikuta akiumiza kichwa kwa kuwaza namna ya kumlinda mwanaye ambaye anahitaji kwa vyovyote vile kuishk na mtoto wa mzee J jambo ambalo mzee huyo hakubaliani nalo licha ya kwamba ameshakula kushika uchumba alicholetewa kwa niaba ya binti ysje. Hivyo kitendo hicho kinapekelekea vita nzito ambayo inamtaka mzee Nhomo aongeze nguvu maradufu ili aweze kupigana kikamilifu "Lazima nirudi kwa wakuuu kama nilivyo ambiwa la sivyo nitajikuta na kosa vyote, heshima kijijini na mwanangu pia"  Alijisemea mzee Nhomo  baada kutafakari kwa muda mrefu.

 Kwingeneko alionekana  mtumishi wa Mungu akiambatana na vijana wawili huku  akiwa katika mavazi yale yale na begi lake ilihali mkono akiwa ameshika Biblia, safari hiyo ya mtumishi na hao vijana ilikuwa ni kuelekea nyumbani kwa mzee J baada kupata taarifa kuwa mzee huyo ndio nguli wa nguvu za giza.  kabla hawajafika kwa mzee J mara ghafla nyuma yao akatokea mzee J akiwa katika mavazi yake ya kazi, mboni za macho yake zilibadilika rangi na kuwa kijani kwani alikuwa na hasira sana baada kupata taarifa ya kuhusu mgeni huyo aliyejionyesha kuwa ni mtumishi wa Mungu . Vile vile aliijua dhamira yake..

KIPI KILIJILI HAPO? USIKOSE SEHEMU IJAYO..
   PIA SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA SEHEMU IJAYO..



No comments: