MREMBO WA WA KIJIJI 19
MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA YA KUMI NA TISA-19
Ujio wa mgeni huyo aliyeonekana ndani ya suti huku akiwa amevalia viatu vyeusi na begi ndogo mgongoni ilihali mkononi akiwa ameshika Bibilia uliwashtua baadhi ya wanakijiji waliomuona. Maswali mengi walijiuliza huku wakitamani kujua dhamira mgeni huyo.
"Bwana Yesu asifiwe?.." Mgeni huyo aliwasalimu wamama wawili aliokutana nao njiani, wamama hao walikuwa wameshika mitungi wakielekea kisimani kuchota maji. Kwa taharuki walitazama baada kusikia salamu hiyo, wakaguna kisha wakarudisha nyuso zao kumtazama mgeni. Hakujali akaendelea kusema "Samahani sana, bila shaka hiki ndio kijiji cha Ndaulaike"
"Ndio kwani wewe ni nani na utaka nini?.." Aliuliza mama mmoja. Mgeni huyo akatabasamu kisha akajibu "Mimi jina langu naitwa Steven Nicholas, ni mtumishi wa Mungu" Akatabasamu tena mtumishi wa Mungu Steven (32)
"Umefuata nini kijijini kwetu?.." Mama wa pili aliuliza. Steven akacheka kwa madaha na kujibu "Swali nzuri sana hilo, na niliitaka kuja huko huko ila kwa kuwa umeniwahi basi ngoja nikujibu. Kilicho nilita hapa kijijini kwenu ni kazi maalumu, kijiji hiki kwa kipindi kirefu nakisikia kikisifika kwa ushirikina. Kwahiyo Mungu kanituma nije niokoe kondoo wake kwani wanateketea pasipo wao kujua"
"Sikilizeni nyie wakinamama, unajua Mungu huwa anamakusudi nanyi kwahiyo hataki kuona kijiji cha Ndaulaike kinaangamia, kijiji kina ardhi nzuri yenye rutba. Kijiji kina mito na visima vizuri, ujumla kijiji kimejaaa neema ambayo kaitunuku kwa upendeleo wa aina yake, kasoro jambo moja tu nalo ni wanakijiji kutokumjua Mungu. Hivyo kwa kuwa muda wa kuteketeza nguvu za giza umewadia? Hakika nina imani kwa nguvu ya Mungu wanakijiji wote wa Ndaulaike mtaokoka, wachawi wote watachoma matunguli yao. Oooh haleluya!.. " Aliongeza kusema Steven.
Kwa mara ya pili wale wakinamama walitazamana, mmoja akasonya kisha akasema "Tuondoke achana naye huyu atakuwa mwenda wa zimu "
Wamama hao waliondoka zao. Mtumishi wa Mungu Steven alipowaona wanaondoka alitikisa kichwa, ndani ya nafsi yake akajisemea "Kwa nguvu ya Mungu aliyejuu hakika mtanyooka tu mtake msitake kuokoka ni lazima "
Alipokwisha kusema hayo akaendelea na safari yake kuzama zaidi ndani ya kijiji huku kila mara akiwageukia wale wakinamama aliokutana nao.
Kisimani wamama wale walionekana kushangazwa na ujio wa mgeni yule, mazungumzo mawili matatu yalianza huku wakiendelea kuchota maji ndani ya kisima "Mwenzangu hivi yule mtu umemuelewa kweli?.."
"Mmh kuna zile habari watu huwa wanasema mjini kuna watu utawakuta barabarani wanasema oooh njoo uokoke sijui kuna hili na lile. Hawa watu ukiwatazama kwa umakini utagundua kuwa wamechanganywa na ugumu wa maisha, hakuna jipya, dunia ya leo kuna kuokoka?.. "
"Hapo sasa, ila nafikiri huyu mtu anachokitafuta atakipa labda hakifahamu hiki kijiji, atanyonyolewa mpaka asahau alichokifuata"
"Mwenzangu achana naye, malizia kujaza mtungi wangu tuaondoke"
"Kabisa kuliko kuzungumzia mtu aliyefeli maisha, kijana mdogo anadandia masuala yasiyo muhusu" Alikata kauli mama huyo ambapo mwisho wa yote walibeba mitungi yao yenye maji haraka sana wakaanza safari kurudi majumbani mwao.
Wakiwa njiani, ghafla akatokea mzee J. J akazipiga hatua kuwafuata. Alipowafikia akasema "Jamani jamani habari zenu" Wamama hao walipofika sauti hiyo nyuma yao wote kwa pamoja walishtuka wakati huo tayari mzee J alikuwa amewapita na kusimama mbele yao. "Mbona mnashtuka?.." Aliuliza mzee J huku akiachia tabasamu bashasha.
"Umetushtua, na vipi umepitia wapi..?.."
"Nimepita wapi? Hahahah mbona swali lako linachekesha! Mimi ni mwanaume kwahiyo nina uwezo wa kupitia popote bila kujali poli. Ama miguu yangu itapata pancha labda kama nitakanyaga mwiba?.." Aliuliza J. Lakini wamama hao ambao tayari kichwani mwao walikuwa wamebeba mitungi ya maji, hawakujibu walikaa kimya ingawa punde mmoja akavunja ukimya akasema "Enhee nini shida?maana tumechoka kusimama"
Mzee J akajibu " Shida yangu ni moja tu, nataka ujumbe wangu huu nitakao wambia mumfikushie mlengwa"
" Mlengwa gani?" Mama wa pili akarudia kuhoji. Mzee J akakunja uso wake kana kwamba emeghadhibika, kwisha kufanya hivyo akajibu "Ni Mligo. Mwambieni yule mzee sitaki tuharibiane siku. Chonde Chonde amkanye mjukuu wake akae mbali sana na Chaudele, tofauti na hivyo chamoto atakiona " Maneno hayo ya mzee J yaliwaudhi sana wakinamama wale mpaka ikapelekea mmoja kutua mtungi chini kisha akamjibu "We baba Chitemo, una nini mzee wewe? Kwani umekuwa nani hadi umtishe mwenzako namna hiyo? Yule kijana ni mzuri kijiji kizima hakuna kijana anayemfikia, kwahiyo kupendwa na Chaudele ni jambo la kawaida sana. Je, unataka ampende mwanao yule mwenye kichogo kama kiuno cha kinu? Ama unataka nini? Acha ujinga bwana, na nyinyi ndio wachawi moja wapo wa hiki kijiji msiopenda mafanikio ya wenzenu " Alifoka mama huyo.
"We mama unadiliki kumtusi mwanangu? " Mzee J akiwa amefura hasira akamuuliza mama huyo aliyekuwa akimjibu kwa ghadhabu kali.
"Ndio nakujibu kwani wewe umekuwa nani haswa mpaka nikuogope, mzee mwenye pua kama boga usiyena haya hata kidogo. Chaudele hamtaki mwanao ila mnalazimisha tu wajinga wakubwa nyinyi. Na kwa taarifa yako sisi sio wajumbe, ujumbe wako huo peleka mwenyewe mpumbavu wewe" Aliongeza kusema mama kwa kujiamini kabisa.
Maneno hayo yalizidi kumchefua mzee J. "Sasa hunijui nitakukomesha mjinga mkubwa wewe" Alisema mzee J na kisha kupotea mbele yao ikisalia vumbi tu. Ni kitendo cha ajabu ambacho kiliwaogopesha wakinamama hao upesi wakatelekeza mitungi yao na kisha kutimua mbio huku wakipiga mayowe. Walipofika mbali kidogo na eneo lile walilokuwa wakijibizana na mzee J wakasimama. Mama yule ambaye hakusema jambo akamwambia mwenzie "Unaona sasa? Yale yale yaliyotokea kwa mwenyekiti, na leo kwa mzee J yametokea. Na kama alivyokwambia utaona, kwahiyo mwenzangu kazi kwako"
"Lah kweli nimeamini jambo usilo lijua ni sawa na usiku wa giza, yamenikuta sasa. Sikujua kama yule mzee yuko vile. Lakini naomba unishauri nifanyeje mimi?.." Alihaha mama huyo aliyekuwa akijibizana na mzee J. Alikuwa tumbo joto kwani hakifahamu kama mzee J ni mtu ambaye angefanya kitendo kile, hivyo basi kupitia kitendo kile kilitosha kumuaminisha mama huyo kuwa mzee J sio mtu wa kawaida. Ni moto wa kuotea mbali.
Wakati mama huyo yupo katika hali ya sintofahamu, kwingineko mzee Mligo alimuweka kitako mjukuu wake huku wakichoma nyama ya sungura. Sababu siku hiyo mitego yake ilifanikiwa kumnsa sungura.
"Mjukuu wangu unajua sana kucheza soka tena sana ila kuna jambo moja napenda nikwambie"
"Jambo gani babu?.." Saidon aliuliza.
"Nataka uachane na binti mmoja anayeitwa Chaudele. Huyu ni binti ambaye yupo katika vita kali sana ya kichawi, hivyo basi nisingependa vita hii ihamie na kwako" Alijibu mzee Mligo. Jambo hilo ni kama lilimchanganya sana Saidon kwani alionyesha kupoa huku akishusha pumzi. Na kabla hajasema neno lolote, mzee Mligo akaongeza kusema "Sijui umenielewa?.."
"Ndio babu ila.."
"Ila nini Saidon? Naomba unielewe sitaki balaa mimi bwana" Alidakia mzee Mligo. Saidon akakaa kimya ilihali akilini mwake akiondoa kabisa wazo kabisa la kuachana na mrembo Chaudele kwani moyo wake ulimuhitaji vilivyo.
"Saidon mimi siwezi kumuacha mrembo kama yule kirahisi, istoshe sijamkwichi hata mara moja. Sasa siutakuwa ujinga kwa mjanja kama mimi?" Aliwaza Saidoni.
"Haya wewe endelea kuwaza ujinga ila unacho kitaka utakipata" Alisema mzee Mligo. Saidon akashtuak akajiuliza kusikia maneno hayo, akamtazama babu yake kwa taharuki kubwa samabamba na kujiuliza kuwa amejuaje kile akiwazacho? Kabla hajapata jibu la swali alilojiuliza, mara ghafla babu yake akageuka akawa mzee Bidobido kisha akaangua kicheko. Alicheka sana mzee Bidobido wakati huo huo Saidoni alishtuka upesi akanyanyuka akatimuwa mbio sanjari na kupiga kelele kuomba msaada. Ghafla akashtuka kutoka usingizini.
Ilikuwa ndoto, katu Saidoni hakuwa akiongea na babu yake pasipo yeye kujua mzee Bidobido alimtokea kwa njia ya ndoto pindi alipokuwa amelala chini ya mti mara baada vijana wa kijiji kuondoka. Vijana mbali mbali wa kijiji walikuja kumpa pongezi kwa kuonyesha kandanda Safi siku ya jana.
"Haya wewe endelea kuwaza ujinga ila unacho kitaka utakipata" Maneno hayo yalijirudia kichwani mwa Saidoni ambapo alijiuliza yule mzee ni nani? Na anamaana gani? Punde mara baada kujiuliza maswali hayo akasikia sauti ya Chaudele ikimuita. Saidon akageuka kutazama kule ilipotokea sauti, akamuona Chaudele akija mahali alipokaa. Alipomfikia akasema "Afadhali leo nimekukuta, nina habari njema kwako"
"Habari njema ipi hiyo?.." Alihoji Saidon huku akionyesha hofu moyoni mwake.
Chaudele akiwa na nyuso iliyojaa haibu akajibu "Nataka uwe mwanaume wa kwanza kunitoa bikira yangu, zoezi hili lifanyike upesi leo leo"
"Bikira?.." Alirudia kuhoji kijana Saidon. Chaudele kabla hajaongeza neno lolote mara ghafla ilisikika ikisema "Haya wewe endelea kuwaza ujinga ila unacho kitaka utakipata tu" Safari hiyo haikuwa ndoto ingawa hakujua wapi inapo tokea sauti hiyo, muda mfupi baadaye kicheko kizito kilisikika, cheko ambalo aliisikia yeye pake yake..
BIKIRA ITABANDULIWA KWELI? USIKOSE SEHEMU IJAYO.
SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA..

No comments: