MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA MWISHO






Usiku huo huo kundi lile la kwanza lililopania kumfanya bibi Pili kitoweo lilitua nyumbani kwake kwa niaba ya kumchukua, lakini walijikuta wakipata tabu baada kukutana na na maajabu nyumbani kwa bibi Pili. Ulionekana moto mkubwa ukiwa umeuzunguka nyumba hiyo wakati huo mbele ya moto walionekana watu sita wamevaa nguo nyeupe huku mikononi wakiwa wameshika mapanga.

Mkuu wa kundi hilo baada kuona ile hali aliogopa sana, ila hakutaka kunyesha woga wake mbele ya watumishi wake na ndipo alipozidi kufanya makeke ya kumvuta bibi Pili nje. Lakini bado mambo yalikuwa magumu sana, alishindwa. Nguvu ya ajabu ilimrinda bibi Pili. Mkuu huyo ndipo akawageuki wenzake ambao walikuwa nyuma yake kisha akawaambia "Jamani hapa tayari mipango inakwenda tofauti, ila sitaki kusema kuwa tumeshindwa hapana bali kinachotakiwa tuungane nguvu moja ili tuweze kufanikiwa jambo hili. Sawa sawa?.."

"Sawa mkuuuu.."waliitikia wachawi hao, punde wakakutanisha viganja vyao ili kupata nguvu kubwa ya kumchomo bibi Pili ndani ya nyumba yake sababu kuingia ndani wasingeweza shauri ya moto mkali uliozunguka nyumba lakini pia sababu nyingine ni wale watu walioshika mapanga.  Zoezi hilo la kuunganisha nguvu za giza kwa pamoja kabla halijazaa matunda ghafla moto ulishuka katikati yao, haraka sana wakasambalatika mfano wa punje za njegere kavu. Walistaajabu na kuanza kuinua nyuso zao kutazama juu ulikotokea moto, ajabu waliona miale zaidi ya kumi ya moto ikiwashukia. Mkuu aliona ni hatari kwao  alitoa amri kwa watu wake wapotee mahali hapo haraka sana iwezekanavyo. Hima walipotea.  Dhamira yao ikaota mbawa.

        Upande wa pili nako, kundi lile lililokua likiongozwa na mzee J lilionekana angani wakiwa ndani ya nyungo  tayari kwa kutua nyumbani kwa mzee J ili kumuadabisha kutokana na kuvunja katiba ya kundi lao. Ila sasa kabla wachawi hao hawajatua kwenye ardhi ya mzee J, mara ghafla nyungo zao ziliweweseka na punde si punde mmoja baada ya mwingine alidondoka mfano wa maembe yadondokapo kutoka kwenye mti wake. Ajabu walipotaka kuondoka walishindwa, walijaribu zaidi ya mara tatu lakini bado walishindwa  hatimaye  palipambazuka wakiwa bado hawajatoweka.

 Mzee J alipotoka nje alishangaa kukuta waliokuwa watu wake wapo nyumbani kwake wakiwa na mavazi ya kichawi, J aliwatazama kisha akarudi ndani kumpasaha mkewe habari hizo huku akimuasa kutowasemesha wachawi hao kwani endapo akiwasemesha basi ndio kigezo kitakacho wafanya mmoja baada ya mwingine kutoweka.

"Sawa nimekuelewa.." alijibu mama Chitemo wakati huo mzee J alikwenda upesi nyumbani anakoishi mtumishi  wa Mungu alipofika alimueleza namna hali ilivyo nyumbani kwake, haraka sana mtumishi akamaambatana na Mzee J kwa niaba ya kuwaokoa kondoo walipotea, si wengine bali ni wale wachawi waliodondoka nyumbani kwa mzee J.
   Zoezi hilo lilikamilika kwa haraka sana, hatimaye timu nzima ya mzee J ikawa imemjua Mungu ipasavyo na kuachana na masuala ya giza. Ingawa haikuwa kazi rahisi.

            BAADA YA WIKI TATU..

Hali ya Saidon iliimarika, sasa aliruhusiwa kurudi nyumbani amalize dozi akiwa nyumbani kwao. likuwa ni furaha isiyo kifani kwa mzee Mligo na majirani zake achilia mbali wanakijiji waliofahamu unafuu wa Saidon. Mmoja baada ya mwingine alifika nyumbani kwa mzee Mligo kumpa pole Saidon, kijana Maige hakuwa nyuma lakini pia mrembo wa kijiji wa kuitwa Chaudele naye alifika pia.

Siku zilisonga,  Chitemo mwishowe alijikuta akijutia kitendo alicho mfanyia Saidon alitamani akamuombe msamaha ila aliona kama atakuwa amejishusha sana, "Hapana siwezi labda nimtume mtu.." siku moja Chitemo alijisemea  wakati huo akiwa nje ya nyumba yao akifikiria mambo mbali mbali yanayo mkabili.

 Kwingeneko alioneakana mama Chaudele na mumewe wakirudi nyumbani kutoka shamba, wakiwa njiani mzee Nhomo alimuasa mkewe wapite kwa mzee Mligo kumjulia hali Saidon. Hapo ndipo mama Chaudele alipokumbuka jambo, kwa sauti ya upole akasema "Baba Chaudele hivi unahabari kuwa mwanao Kapata mchumba?.."

"Mchumba? Basi ni jambo la heri kama na yeye mwenyewe Chaudele atakuwa ameridhiaa, yuko wapi huyo mchumba wake? Asiwe Chitemo"

"Kwa mzee Mligo.." alijibu Mama Chaudele.

"Mmh kwahiyo wataka kuniambia ni Saidon?.."

"Ndio huyo huyo.."

"Lah basi hilo jambo la heri, kwa kijana yule wala sina matatizo naye. Ngoja tukamuone.." alisema mzee Nhomo.

Huo ndio ukawa mwanzo wa wazazi wa Chaudele Wakafahamu juu ya uchumba wa mtoto wao na mjukuu wa mzee Mligo. Mzee Mligo nae alijua fika kuwa mjukuu wake anatoka kimahusiano na binti Nhomo. Na siku moja wazee hao walikutana ili kufahamu mstakabali wa vijana wao.

"Ni vyema kama vijana wamependana, kina chotakiwa ni kufuata taratibu tu.."  mzee Mligo alipoyasikia maneno hayo ya mzee Nhomo alitikisa kichwa ishara ya kukubali kile alichokisema mzee mwenzake,  alishusha pumzi kwanza kisha akajibu "Ni kweli mzee mwenzangu ila nikwambie kitu ambacho ulikuwa hukijui.."

"Kipi hicho?.." Aliuliza mzee Nhomo.

Mzee Mligo akajibu "Saidon bado anasoma sijui itakuaje sasa."

"Hapo itatakiwa tuwaite vijana wetu kisha tuwaulize ili tufahamu wamekubaliana vipi, sababu ni ngumu sana kuvunja uchumba wao.." aliongeza kusema mzee Nhomo. 

Wazee hao walilidhia,  baada ya siku kadhaa kupita, hali ya Saidon ikiwa tayari imeimalika. Jioni moja babu yake akamuuliza swali la kizushi, siku hiyo ilikuwa jioni sana." Saidon, hivi ni kweli unampenda sana Chaudele?.. "

" Ahahahah ndio babu kuliko kawaida.." alijibu Saidon akianza kwa kicheko.

"Na vipi kuhusu chuo?"

"Chuo? Kwangu sio tatizo babu, kwanza  tarehe za kurudi shule kumalizia mwaka wa pili wa kozi yangu umewadia, kwahiyo nikisha hitimu nakuja kuchukuwa mchumba wangu.." Alisema Saidon. Maneno hayo yake yalimfanya babu yake kuangua kicheko kisha akasema "Safi sana wewe ni kidume, basi kama ni hivyo, mimi nitaenda kuzungumza na wazazi wa yule binti kwa mara nyingine kisha mengine yatafuata.."

"Sawa babu.."  alikata kauli Saidon.

   Mzee Mligo hakufanya kosa alimuuliza mzee mwenzake kila kitu, mzee Nhomo hakutia shaka wakati huo huo Saidon alimueleza Chaudele hali harisi  ya kwamba yeye ni msomi na anahitaji kurudi chuo baada muda wake wa kuishi kijijini kumalizika. Chaudele alifarahi sana kusikia habari hiyo, akiwa na haibu usoni mwake akajibu "Sawa kila laheri mpenzi wangu, muhimu usinisahau tu. Na uaminifu ndio kila kitu mpenzi wangu" Saidon akacheka kisha akasema "Usijali nakupenda sana Chaudele. Ondoa shaka, nipo pamoja na wewe"

      Hatimaye siku ya safari iliwadia, hakika huzuni ilitanda kwa wanakijiji waliomzoea kijana Saidon kipenzi chao, umati mkubwa ulimsindikiza.

 Siku ile ya safari alibahatika kukutana na Chitemo, haibu ilimkamata  lakini Saidon alionyesha kutojali jambo hilo, zaidi alisema "Chitemo, mimi naondoka mshkaji wangu. Ila nitarudi na ningependa nikuulize kipi nikuletee kama zawadi pele wa Ndaulaike" Maneno hayo Saidon aliyaongea huku akitabasamu wakati huo Chaudele  akiwa amemlalia begani. Chitemo hakusema neno lolote kwanza,  alishusha pumzi  kisha akasema "Saidon naomba unisamehe sana, lakini pia Chaudele naomba unisamehe pia. Nimejifunza mpenzi hayalazimishwi hakika najutia sana makosa yangu"

"Wala usiwe na hofu mzee baba, nilisha kusamehe kitambo sana. Acha nikasome ila nitarudi Ndaulaike. Lakini kaa ukijua nitakuletea zawadi nzuri sana " aliongeza kusema Saidon kisha akapeana mikono ya amani na kijana Chitemo ambapo kwa pamoja waliambatana kwenda kijiji cha pili kupanda gari ya kuelekea jijini Dar es salaam huku nyuma Ndaulaike akimuacha Chitemo akiwa na taharuki juu ya moyo aliojaliwa bishoo huyo wa jiji la Bandari.

     Baada ya kuhitimu masomo yake, alirejea kijijini Ndaulaike kutimiza azma yake, furaha isiyo kifani ilitawala kwa Saidon na wazazi wake ikiwemo na babu yake pia marafiki zake. Chereko na ndelemo zilitamaraki kijiji cha Ndaulaike, zilizidi maradufu baada Chitemo kumrudia Pili ambapo nao walioana ipo haja ya kusamehana mambo yaliyopita.

"Mke wangu tulitabiri mwanetu aolewe mjini na hatimaye imewezekana, hakika Mungu mkubwa, na kwa maana hiyo hakuna haja ya kuendelea kuutumikia uchawi. Kesho namuita yule mtumishi aje kutuombea ili na sisi tuwe kama Familia ya mzee J na bibi Pili..." alisikika akisema mzee Nhomo akimwambia mkewe, na kabla mama Chaudele hajaunga mkono hoja ya mumewe ghafla mzee Mligo akatokea akasema "Hilo suala hata mimi naliunga mkono, uchawi hauna faida mzee mwenzangu. Huu ni wakati wa kumrudia Mungu wetu sasa ili kijiji chetu cha Ndaulaike kibarikiwe. Ahahahah Hahaha Ndaulaike oyeee ee"

" Oyeeeee mzee mwenzangu" Aliitikia mzee Nhomo.
              ********
Sasa kijiji cha Ndaulaike nguvu ya Mungu ikawa imetaraki kila kona, makanisa na misikiti ilijengwa kwa kasi na watu kujua ukuu wa Mungu ipasavyo. Saidon naye alimchukuwa mkewe akaondoka naye kuishi mjini, wakati huo huo Chitemo akibaki na Pili wake kijijini. Upande a mtumishi Steven, tayari kazi yake ilikuwa imekwisha na hivyo jioni moja alichukuwa kilicho chake akaondoka na kukiacha kijiji cha Ndaulaike kikiwa na amani tele kwani hata wale wachawi wengine nao waliokuwa wakiongozwa na mwenyekiti walijiengua moja baada ya mwangine mpaka kundi hilo likafa moja kwa moja. ha
Huo ndio ukawa mwisho wa uchawi katika kijiji cha Ndaulaike, maendeleo yakazuka kwa kasi, kijiji kikapendeza kwa kujengwa nyumba za kisasa. .. NDAULAIKE NGUVU YA MUNGU ILITANDA JUU YAKE..
       ➡️➡️MWISHO⬅️⬅️🇹🇿






No comments: