MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA-29
MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA-29
Heka heka hiyo ilidumu kwa takribani masaa mawili, wachawi hao wakipishana huku na kule. Punde si punde wakapotea angani, ndipo kwenye mto mkubwa kijijini Ndaulaike walionekana wachawi wasio pungua ishirini wakiwa wamejikusanya kando kando ya mto ilihali wakiwa wamezungukwa na moto kila kona. "Habari zenu.." alisema mkuu wa kundi hilo la kichawi, wale wachawi wote kwa pamoja wakainamisha nyuso zao na kisha kuziinua kuashiria kuitikia salamu ya mkuu wao.
Mkuu akatikisa kichwa kama ishara fulani ya kukubali jambo fulani, baada ya kufanya hivyo akakohoa kidogo halafu akasema "Hofu dhofu lihali tayari imetanda katika kijiji hiki, lakini kabla sijaenda mbali sana kulielezea jambo hili naomba kwanza mawasilisho kutoka kwa watu wale nilio watuma" alisema mkuu kisha akakaa kimya kidogo halafu akaendelea kusema "Nafikiri niliteua makundi matatu, kila kundi nililipa majukumu yake kwahiyo kundi moja baada ya jingine naombeni nyaraka zenu haraka sana iwezekanavyo.." kwisha kusema hivyo mkuu huyo alitulia.
Punde kundi namba moja lilisimama, walikuwa wachawi watatu. Mmoja kati ya hao watatu alizipiga hatua kumsogelea mkuu wake, alipomfikia alimkabidhi mazaga mbali mbali aliyokuwa akitumia yule mtaalamu aliyeletwa kijijini kwa niaba ya kuwaumbua wachawi wa kijiji. Mkuu alifurahi sana, akatabasamu kisha akasema "Safi sana vijana, kazi nzuri.. Haya kundi lingine!.."
Kundi la pili lilisimama, hili ni kundi ambalo lilipewa jukumu la kuchukua vitu mbali mbali vya kichawi kwa bibi Pili kwani tayari bibi huyo alioneakana kuzua sintofahamu baada kupoteza nguvu za giza. Hivyo kama ilivyo ada,mmoja alijitokeza akamsogelea mkuu wake na kisha akamkabidhi vitu hivyo alivyokuwa navyo bibi Pili. Jambo hilo lilimpendeza sana mkuu wao, hakusita kutoa pongezi kwa watumishi wake. Na kundi lililofuata ni kundi la tatu, kundi ambalo lilitumwa kwenda kumalizana na mtumishi wa Mungu.
Kundi hilo lilishindwa kifua dafu kwa mtumishi Steve. Kundi hilo lilisimama, ghafla wakajikuta wakishindwa cha kuongea mbele ya mkuu wao jambo ambalo liliweza kuzua tafarani kwa mkuu na wachawi wengine waliokuwepo ndani ya kikao hicho, lakini mwishowe mmoja wao kati ya wale watatu alisema kwa sauti ya upole iliyojaa woga.l "Mkuu tumemshindwa mtumishi.."
"Eti nini?.." Alihoji mkuu wao kwa taharuki kubwa huku wachawi wengine nao wakipigwa na butwaa.
"Mimi na timu yangu hatujawahi kushindwa, iweje wenzenu waweze halafu nyie mshindwe? Hawa wana nini na nyinyi mna nini! Sitaki kusikia upuuzi huo, msinichezee akili yangu. Naomba mnipe sababu ipi hasa iliyowafanya mumshindwe yule mtu. Na ndio maana ngome ilikuwa unayumba kumbe kuna ujinga umeufanya?.. "aliongea kwa kufoka mkuu huyo, wakati huo wachawi wote walikuwa kimya kila mmoja akiwa ameinamisha chini uso wake huku wakiyasikiliza maneno ya mkuu wao aliyokuwa akiyaongea kwa hasira.
"Nipeni sababu haraka sana.. " aliongeza kusema mkuu hayo. Ndipo mchawi mmoja alipojibu "Mkuu yule mtu ananguvu sana, anatumia biblia. Ndio sababu pekee iliyotufanya kushindwa kutekeleza hitaji lako"
"Biblia?.." Alihoji mkuu kwa msisitizo, wachawi wale watatu kwa pamoja wakajibu "Ndio mkuuuu..".
Alishtuka sana mkuu huyo baada kusikia biblia, neno hilo halikuwa geni masikioni mwake. Na licha ya hivyo lakini pia naye katika harakati za kiuchawi aliwahi kukutana na hatari hiyo ya kupigana na mtu anayetumia neno la Mungu, ni zamani saaaana enzi ya ujana.. Hapo mkuu huyo akakumbuka kisa hicho.
*********
Usiku mmoja akiwa chumbani amelala alishtuka baada kusikia ngoma zikipigwa nje ya nyumba ya bibi yake, haraka sana akanyanyuka kutoka kitandani akapapasa juu ya ndoo kutafuta kibiriti. Alipokipata aliwasha kibatali kisha akasogea kwenye dirisha la chumba alichokuwa amelala ili apate kutazama nje aone jambo gani linalo endelea huko. Pole pole alifunua pazia la kitambaa kilichokuwa kimetundikwa kwenye dirisha, akashtuka kuona wachawi wakiimba na kucheza ngoma wakiwa uchi. Na katika wachawi wale alikuwemo na bibi yake.
"Laah! Bibi kumbe naye mchawi?.." alijiuliza huku akiendelea kutazama ngoma zile za kichawi. Kesho yake asubuhi aliamka akachukuwa kilicho chake tayaru kwa niaba ya kuondoka nyumbani hapo kwa bibi yake aliogopa sana. "Sule mbona mapema? Na je huko utaishi na nani?.." Aliuliza bibi huyo.
Sule ndio yule mzee mwenyekiti wa kijiji aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha baada kutaka kuumbuliwa na mtaalamu. "Naondaoka bibi ukweli mimi siwezi kuishi na mchawi.." alijibu Sule.
"Mchawi? Mshenzi mkubwa wewe. Kwahiyo Unamanisha mimi ni mchawi?.." alihamaki bibi huyo na kisha kunena maneno hayo kwa jazba. Sule akajibu "Ndio kwani uongo?.."
"Mjukuu wangu naona tayari umekua, unasikiliza maneno ya watu si ndio?. Eeh kweli hiki kijiji sio kabisa.." aliongeza kusema bibi huyi wakati huo Sule akiambaa na njia kurudi kijijini kwao Ndaulaike.
Lakini kabla hajafika mbali, bibi yake akamuita. Sule akageuka ghafla bibi yule aliasama mdomo wake, ukatokea mfuke mzito mweusi katika kinywa.. Mfuke huo ulipomfikia Sule alidondoka chini alipozinduka alijikuta yupo pembezoni mwa mto asijue kafikaje mahala hapo ama ni kipi kikichomtokea. Ajabu aliona wachawi wakiimba na kucheza, katika wachawi wale hakumtambua hata mmoja ingawa baadaye kidogo alimuona bibi yake.
Alipagawa Sule baada kuona mambo yale, alitamani kukimbia lakini alishindwa sababu hakujua njia ipi iliyomfikisha pale alipo. Muda mchache baadaye shamla shamla zile na nderemo zilitulia, wachawi wote waliokuwepo pale walikaa kimya wakisikiliza kipi kinatarajia kujili siku hiyo. Baada ya utukivu ule bibi Sule alisimama kisha akasema "Jamani mnakumbuka kuwa niliwahi kuwaambia kwamba nitamleta mjukuu wangu kwenye himaya yetu? Basi muda na wasaa umewadia. Ni yule pale ndio atakaye rithi mikoba yangu.." alisema yule huku akimnyoishea kidole mjukuu wake.
"Aha hahahahaha" waliangua vicheko wale wachawi baada bibi Sule kumnyooshea kidole mjukuu wake. Ngoma zilipigwa kwa shamla za hapa na pale lakini punde ukimya ukarudia kutamalaki eneo hilo ambapo bibi Sule alimtaka Sule asimame, Sule kwa kuwa hakufurahishwa na mambo hayo aligoma kusimama wakati huo moyoni akijisemea "Siwezi kuwa mchawi hata siku moja.."
Alipokwisha kujisemea hayo ghafla mbele yake akatokea mtu ambaye alioneakana kuwa na uso mzito uliojaa alama kila kona, mtu huyo alimsogelea Sule kisha akamwambia "Kijana hebu tazama kiganja changu" Hima Sule japo alionyesha woga ila aliinua macho yake kukitazama kiganja cha mtu yule wa kutisha ambapo katika kiganja hicho lilionekana tukio la mauaji ya kinyama yaliyowakumba wazazi wa Sule, wazazi hao walichomwa moto na wanakijiji wa Ndaulaike baada kushutumiwa kuwa ni wachawi miaka kadhaa iliyopita.
Sule alipokiona kitendo hicho alisikitika sana, aliumia moyoni mwake ilihali muda huo huo yule mtu akakifumba kiganja chake kisha akasema "Je, upo tayaru kulipa kisasi juu watu hawa walio waua wazazi wako, ama haupo tayari? Na kama upo tayari basi itakulazimu kumpokea bibi yako majukumu ili upambane vilivyo na watu hawa ambao asilimia kubwa, wengi wao nao wananguvu za giza" Alisema mtu yule kwa sauti nzito.
Na hapo ndipo Sule alipozinduka kutoka usingizini, alihema kwa kasi huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio, yote ilikuwa ni ndoto, ndoto hiyo aliyoota ilimuweka roho juu. "Je, upo tayari kulipa kisasi juu watu hawa walio waua wazazi wako, ama haupo tayari? Na kama upo tayari basi itakulazimu kumpokea bibi yako majukumu ili upambane vilivyo na watu hawa ambao asilimia kubwa, wengi wao nao wananguvu za giza" maneno ya yule mtu yalijirudia kichwani mwake. Pumzi ndefu alishusha akiyatafakari maneno hayo aliyoyaota ndotoni.
Lakini wakati yupo kwenye hiyo hali mara ghafla alisikia sauti ya bibi yake ikimuita chumbani, haraka sana alitii wito ambapo alishtuka kumkuta bibi yake akitetemeka mwili mzima asiweze hata kuongea vizuri.
"Kulikoni bibi umeshikwa na nini?.." Aliuliza Sule lakini hakujibiwa, zaidi bibi yake alihenya kwa maumivu makali aliyokuwa akiyasikia mwili mwake. Baadaye kidogo bibi huyo alijikaza kisabuni kisha akamwambia Sule ainame kuingia uvunguni atoe jungu ambalo alihifadhia mazaga zaga yake. Sule akiwa na hofu dhofu lihali juu ya afya ya bibi yake alifanya hivyi, alichukuwa chungu hicho akamkabidhi bibi yake.
Bila kupoteza muda kabla hata jogoo hajawika Sule alijikuta akikabidhiwa na bibi yake uchawi, hapo ndipo alipoamini kuwa ile ndoto aliyoota haikuwa ndoto bali ni ukweli uliokuja kwa style ya ndoto. Lilikuwa jambo tata kwa Sule kupokea mikoba ile kutoka kwa marehemu bibi yake ila kwa kuwa alihitaji pia kulipa kisasi hakuwa na budi kukubali. Rasmi akawa mchawi mtiifu na makini wa kazi yake, jambo ambalo lilimfurahisha sana mkuu wake na hivyo baada kuutumikia ulimwengu huo wa giza kwa kipindi kirefu hatamaye aliyekuwa mkuu wake alitaka kumkabidhi madaraka.
Kabla hajatunukiwa cheo hicho alipewa mtihani kwanza, nao ni kwenda kuchukuwa damu ya mtumishi wa Mungu aliyekuwa kikwazo kwa upande wao. Huko ndiko Sule alipoijua ugumu wa kupigana na mtu anayetumia neno la Mungu ama Biblia, japo mtihani huo alishinda lakini cha moto alikipata.
Jaribu ndilo lililomfanya yule mtumishi kushindwa na Sule, ni pale mwanaye wa kike alipofukuzwa shule kwa madai kwamba ni mjamzito kitendo ambacho kilimpelekaea mtumishi yule wa Mungu kufoka na kujikuta akiteteleka kwenye Imani yake baada kuongea maneno ambayo hayakumpendeza Mungu, nafasi hiyo ya kushindwa jaribu Sule aliitumia vyema na kuibuka mshindi.
***********
"Mmh! Naam! Sawa nimewaelewa lakini hakuna tabu nitajua cha kufanya, ila kwa sasa ni kumshughulikia bibi Pili kama katiba yetu itupasavyo.." Alisema mkuu yule baada kukumbuka mambo kadhaa ya nyuma enzi ya ujana wake jinsi alivyokabiliana na mtumishi wa Mungu.
" Sawa sawa mkuu" waliitikia wachawi wale watatu walioshindwa kumuua mtumishi wa Mungu sasa wote kwa pamoja walikubaliana kumleta bibi Pili kwenye himaya yao ili wamgeuze kitoweo pasipo kujua tayari bibi Pili analindwa na nguvu ya Mungu.
Kwingeneko nako, mambo yalikuwa sio mambo kwenye lile kundi lililokuwa likiongozwa na mzee J. Watu wake walionekana kukerwa na uamuzi aliochukuwa huyo, kitendo ambacho kiliwapelekea wao kwa wao kujumuika pamoja kikao cha dharula kisha kaimu kiongozi wa kundi hilo akasema kwa sauti kuu iliyo jaa ukali wa aina yake.
Kaimu huyo ambaye alikuwa bibi KIZEE alisema "Jamani kama tunavyoona hali harisi iliyotokea, kiongozi wetu tayari katusaliti wakati ilani ya chama chetu inafahamika kuwa mwanachama awe kiongozi ama sio kiongozi, endapo kama atakisaliti chama halali yake ni kifooo. Kwahiyo basi kazi ni moja tu, Jaluo afe, damu yake iwe ngao ya ngome yetu. Sawa sawa? "
" Sawaaaaaa"
"Sawa Sawaaaaaa?" Alihoji tena kaimu yule.
"Sawa mkuuuuuuuuu" Nao kwa mara nyingine tena waliitikia kwa mbwembwe na hasira ya hali ya juu. Mara baada kukubaliana hayo walikutanisha viganja vyao kisha wakapotea #Shaaap ikasalia vumbi na sauti ya vilio vya paka, Ngurumo kubwa nayo ikapaza angani..
HATARI SANA ILA SALAMA TUKUTANE SEHEMU IJAYO..
Naona wameamuwa, hatimaye Mwenyekiti anajitosa kumkabili mtumishi mwingine baada awali kushinda, je, atashinda? Atampa jaribu gani? Na vipi hali ya MCHIZI wetu SAIDON? Na ni kweli mzee J anaimani au kaokoa kichwa kichwa tu.. Uhondo upo sehemu ijayo dadeki.. balaa kubwa NDAULAIKE #Kocha.
SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA.

No comments: