MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE-28
MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE-28
"Saidon kaumizwa mpaka sasa bado haijajulikana kama ni mzima ama amefariki.." Alisema Chausiku, ghafla Chaudele akadondosha ndoo chini huku akiangua kilio alizama ndani punde si punde akatoka na nguo ambazo ziliustili mwili wake. Baada ya hapo walielekea nyumbani kwa mzee Mligo, walipofika walikuta umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika mahali hapo ilihali majonzi na vilio vikisikika kutoka kwa wana kijiji baadhi. Mrembo Chaudele akiwa na shauku ya kutaka kujua kilichomkuta Saidon alijipenyeza mpaka akafika sehemu ile aliyoangukia Saidon ambapo alimkuta yupo katika mikono ya babu yake, ila kitendo hicho Katu hakikumzuia Chaudele kushindwa kumsogela zaidi Saidon. Alitokwa na machozi alichuchumaa chini na kisha kuanza kumuamsha "Saidon.. Saidon.. Saidon, amka Saidon wangu. Amka mpenzi wangu." alisema Chaudele wakati huo akibubujikwa na machozi.
Maneno hayo baadhi aliyoongea yalizua gumzo, hata mzee Mligo naye alishtuka na kujiuliza maswali mengi ambayo aliyakosa majibu yake. Kila mmoja alishangaa kwa aina yake juu ya neno (mpenzi)alilozungumza Chaudele pindi alipoanza kumuamsha Saidon.
Chaudele alipoona Saidon haamki wala kutikisa japo kidole aliendelea kulia mara dufu huku akiwa akimtaja kwa jina na kumtikisa. Mwishowe Saidon alifumbua macho,wanakijiji walishangaa sana punde zile nyuso zilizokuwa na huzuni hapo awali ghafla zikaonyesha furaha wakati huo mrembo Chaudele aliendelea kumtaja Saidon na kumuhakikishia kuwa anampenda sana. Saidon hakujibu chochote alimtazama tu mrembo wake na mwishowe akarudia kufumba macho.
"Mzee Mligo njoo mara moja.." mzee mmoja wa makamo alimuita kando Mligo. Mligo alipotii wito mzee yule akamwambia "Tayari tumepata uhakika kuwa kijana yupo hai, lakini endapo kama tutafanya uzembe nakwambia tutampoteza. Sababu hapo alipo yupo hoi kwahiyo ni bora tufanye jitihada za kumuwahisha zahanati kabla hayajatokea mambo mkubwa"
"Ndio sawa sawa nimekuelewa.." Alijibu mzee Mligo akiunga mkono ushauri aliopewa. Baada ya hapo aliwaita vijana wanne wenye nguvu, waliambiwa hali harisi nao hawakuweka pingamizi lolote ndipo mzee Mligo alipotoa nje baiskeli yake, ikafanyika jitihada nzuri ya kumkalisha Saidon kwenye baiskeli na safari ikaanza kuelekea kijiji cha pili ambacho ndicho kilibahatika kupata zahanati.
Kijiji cha Ndaulaike maendeleo yake yalikuwa ni duni sana, usafiri mkubwa walioutegemea ni wakutimia baiskeli na punda. Ndaulaike haikuwa na maji ya mabomba, wanakijiji wake walitumia maji ya visima na mto. Kijiji hicho walau walicho bahatika kupata ni barabara, hata nayo ilitengenezwa na wachina waliokuwa wakisaka kokoto za kujengea lami mjini lakini mradi huo uliota mbawa baada kubughudhiwa na masuala ya kishirikina.
Safari ile ya Saidon kupelekwa hospital ilifanikiwa, salama salimini walifika kijiji hicho chenye maendeleo, haraka sana matibabu yakaanza ikiwa Saidon bado hajafumbua macho kwa mara nyingine.
"Looh Mungu nisaidie.." alisema mzee Mligo wakati alipokuwa njiani akielekea hospital kumuuguza mjukuu wake,nyuma kijiji cha Ndaulaike mrembo Chaudele alioneakana akibubujikwa na machozi akimlilia Saidon, mama yake alipomshuhudia akakubali kuwa Chaudele hana ujanja kwa Saidon Kijana kutoka mjini Kipenzi cha wanakijiji wa Ndaulaike.
"Basi mwanangu atapona wala usijali. Nyamanza usilie" alisema mama Chaudele baada kumuona binti yake akilia kwa uchungu.
Ilihali upande wa pili wale vijana waliokubaliana kwenda kuchoma moto na kufanya fujo nyumbani kwa mzee J, waliahilisha zoezi hilo baada kusikia Saidon kafumbua macho lakini kapelekwa Zahanati. Vile vile walitimua mbio kwenda kumtazama ili wahakikushe kama ni kweli walicho ambiwa, muda huo huo Chitemo aliachiwa akaondoka zake kichwa chini mikono nyuma, moyo ulimuuma hasa baada kuyasikia maneno aliyoyaongea Chaudele mbele ya uma pindi alipokuwa akimuamsha Saidon. "Saidon.. Saidon.. Saidon, amka Saidon wangu.. Amka mpenzi wangu." maneno hayo aliyoyasema Chaudele yalijirudia ndani ya kichwa cha Chitemo, kajana huyo akijikuta akidindosha chozi akiamini kuwa Chaudele sio wake tena.
Lakini mwishowe akajipa matumaini kwamba kwa vyovyote atajua cha kufanya ilimradi amtwae mrembo huyo wa kijiji ama la sivyo bora wamkose wote na kama sio kumkosa wote basi atafanya juu chini muhusika asimchukue Chaudele. "sikubali.." alijisemea Chitemo huku akizipiga hatua akiambaa na njia kurudi nyumbani kwao.
*********
Kwingineko Pili alikuwa akimlilia bibi yake juu ya maswahibu yaliyomkuta,na hapo akaona hakuna haja ya kupoteza muda. Aliyafuta machozi yake kisha akatimua mbio kuelekea kwa mzee Nhomo akiamini kuwa mzee huyo ataweza kumpatia msaada, istoshe alijua fika kuwa mzee Nhomo na bibi yake hawana uhasama wowote.
Lakini wakati Pili yupo katika heka heka ya kuwahi nyumbani kwa mzee Nhomo mara ghafla njiani akakutana na mtumishi wa Mungu akiwa ameambatana na mzee J. Pili aliogopa sana alipomuona mzee J akajikuta akianguka chini huku akipiga mayowe kitendo ambacho kilimfanya mtumishi wa Mungu kumshangaa, muda huo huo akapasa sauti kumuita lakini Pili hakuitika alizidi kukimbia kwa mara nyingine tena akaangua, akanguka tena..
"Binti njoo usiniogope njoo, acha uoga tafadhali.." Alisema mtumishi yule wa Mungu bwana Steve. Pili safari hiyo hakukimbia ingawa aliogopa kumsogezea Steve ambapo alirudi nyuma huku Steve nae akimfuata. Alipomkaribia akamsalimia kwa sauti ya upole "Hujambo binti?.." Pili akaitikia kwa kichwa hali ya kuwa akimkodolea macho mzee J asijue kuwa J wa zamani sio wa sasa. "Usiniogope tafadhali, Haya niambie huku ulikuwa unaelekea wapi?.." Aliuliza mtumishi bwana Steve huku akionyesha kwa kidole kule alikokuwa akikimbilia Pili. Ndipo Pili kwa sauti ya woga iliyojaa wasiwasi akajibu "Kwa baba Chaudele,.."
"Anhaa kuna shida gani? Maana unaonekana kule ilipotoka sio salama.." alirudia kuhoji mtumishi.
Pili alitulia kimya wakati huo akivunja vunja vidole vyake huku akimtazama mzee J kwa jicho la kuibia ilihali J nae akionekana kujawa na furaha full amani akiwa ndani ya damu ya yesu." Niambie basi kuna shida gani? Huwenda nikawa msaada tosha.." aliendelea kusema mtumishi, na ndipo Pili alipoeleza namna hali ya bibi yake ilivyo. Mtumishi Steve aliposikia maelezo ya Pili haraka sana akamtaka warudi ili akafanye maombi.
Zoezi hilo lilifanyika kwa nguvu za Mungu, bibi Pili aliombewa kwa imani ya hali ya juu. Kitu ambacho kiliweza kusababisha kupiga kelele wakati hapo awali alikuwa hawezi hata kuongea, bado mtumishi wa Mungu Steve alizidi kuomba kwa imani huku akikemea nguvu za giza katika kijiji cha Ndaulaike. Hali hiyo ilimfanya nae Pili kuanguka chini, kumbe tayali alikuwa ameshalishwa baadhi ya vyakula vya kichawi. Hivyo maombi hayo yalimfanya kuzua balaa ambapo mwishowe mara baada maombi kumalizika alianza kutapika. Ajabu alitapika mifupa ya vyakula vya ajabu ajabu. Hivyo basi baada ya masaa kadhaa bibi Pili alirudi katika hali yake,.. "Mungu mkubwa.." alisema mzee J, mtumishi wa Mungu Steve akaitikia "Naaam..."kisha akaongeza kusema" bibi pole sana ila kwa sasa upo huru lakini mbali na hilo unatakiwa kutubu makosa yako ili Mungu akusamehe.. "
" Hilo tu baba? Wala hakuna shida.. "alijibu bibi Pili. Jambo hilo mara moja likatendeka, kwa kilio na majonzi bibi Pili alitubu makosa yake. Nae akajiamini sasa kuwa tayali yupo katika mikono salama, kwani laiti kama asingelikuwa Mungu kufanya miujiza yake kupitia mtumishi wake basi usiku wa siku hiyo mwili wa bibi Pili ungekuwa kitoweo cha wachawi na misukule.
Usiku sasa ulipoingia, kijiji cha Ndaulaike ilipofika mnamo saa sita angani walionekana wachawi wakiwa ndani nyungo zao wakipishana kwa kasi ya ajabu huku mikononi mwao wakiwa wameshika vijinga vya moto, ishara hiyo ilidhihirisha kuwa kuna jambo tata limezuka. Jambo ambalo linaweza kughalimu uhai wao..
Jambo gani hilo!?
USIKOSE SHEHEM IJAYO.. Wanahaha kudadeki, sipati picha mzee bifu la CHITEMO na mzee MLIGO 😂

No comments: