MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA-27




MREMBO WA WA KIJIJI

      SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA-27
     
"Mbona vilio?.." alijiuliza mzee Mligo mara baada kusikia sauti za vilio nyumbani kwake ilihali umati wa watu nao ukiwa umekusanyika. Mzee Mligo alijongea kuukaribia umati ule, na ndipo alipogundua kuwa mjukuu wake amepigwa panga na muda huo yupo chini akitokwa na damu nyingi.

"Mungu wangu..." aliongeza kusema mzee Mligo, safari hiyo alitupa chini wanyama aliowanasa akamkimbilia mjukuu wake ili ajue kipi kimemkuta. Alipomfikia alichuchuma, chozi likimtoka alimnyanyua na kisha kumtwaa kwenye mapaja yake wakati huo Saidon hapumui wala hapepesi macho. "Mshikeni hivyo hivyo..." sauti ilisikika ikisema hivyo, sauti ambayo iliongea kwa msisitizo ikiwaasa wale watu waliomkamta Chitemo wasimuachie ili endapo kama atakuwa amemuua Saidon basi nao wajue cha kumfanya.

Muda huo Chitemo alilalama na kujaribu kujing'atua kwenye mikono ya wale watu lakini hakufanikiwa. Ilihali mzee Mligo naye alipasa sauti ya kumuita Saidon, sauti ambayo alitoa iliambatana na kilio. Saidon hakuitika bado alikuwa ameyafumba macho yake, baadhi ya wanakijiji waliojikusanya mahali hapo walijua Saidon kafariki wakati wengine nao wakishindwa kuelewa kipi kitaendelra juu ya Saidon kipenzi cha wanakijiji kitendo ambacho kilipelekea simanzi na vilio kuendelea kutanda.

 Mzee Mligo hakukata tamaa alizidi kumuita Saidon kwa kumtikisa ila bado mambo yalikuwa ni yale Saidon hakuitika wala kuyakumbua macho yake. Ndipo kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni  akasema "Saidon mjukuu wangu usitake kuniaminisha kuwa umefariki, nitawajibu nini wanangu hali ya kuwa wewe tu ndio mtoto wao pekee? Amka bwana amka Saidon.." Machozi yalizidi kumtoka mzee Mligo mara baada kunena maneno hayo, moyo wake ulijawa na hofu akifikiria ni kipi atawajibu wazazi wake.  Punde vijana baadhi wasio pungu sita walijiengua wakakaa falagha kisha mmoja akasema

"Jamani hivi mnajua woga ukizidi mwishowe huwa ufala?.. "

"Unamaana gani?.. "Aliuliza kijana wa pili. Yule kijana wa kwanza akajibu. "Nina maana kwamba hatutakiwi kuogopa. Huu ni wakati wa kuonyesha ushirikiano wetu. Mmsahau kuwa asingekuwa Saidon tusingebeba ubingwa na kujishindia Ngo'mbe mnyama?.. "

"Ndio ndio kabisa wala hujakosea, Enhe kwahiyo?.. "kijana wa tatu aliongeza kuhiji. Yule kijana wa kwanza akamjibu "Basi kinacho takiwa ni sisi kushirikiana, mguu kwa mguu mpaka nyumbani kwa mzee J wakati huo kila mmoja wetu akiwa na siraha. Ukichukuwa rungu freshi tu ukichukuwa jembe poa tu ukichukuwa sururu bomba tu, halafu mimi sasa nachukuwa kitu kidogo sana tu. Kitu chenyewe kinafichwa mfukoni ila balaa lake sio mchezo.. "

" Mmmh! Kitu gani hicho " Alihoji moja ya wale vijana walioko falagha.

" Kibiriti. Wakati nyinyi mnawajeruhi mzee J na mkewe, mimi nitamaliza kwa kuchoma nyumba. Kiungo mkata umeme.. " alisema huyo kijana kisha akaa kimya akitupia macho kutazama kule kwenye umati wa wanakijiji waliokusanyika kutazama ugomvi uliomalizika muda mchache uliopita ambapo ugomvi huo haukudumu muda mrefu baada Chitemo kumpiga panga kichwani Saidon kitendo kilichompelekea Saidon kupasa sauti mara moja ya kuhisi maumivu kisha akaanguka chini, hakurusha wala kutikisa kiungo chochote cha mwili wake, Chitemo aliogopa akijua ameua na hivyo akataka kukimbia ila jitihada zake zilishindikana baada kujikuta akikamatwa na wanakijiji.

"Kuna mwenye swali?.." yule kijana aliuliza punde tu alipourejesha uso wake kuwatazama vijana wenzake.  Kijana mmoja akajitokeza akahoji "Ndio, vipi pindi itakapo gundulika sisi kuhusika na vitendo hivyo?..." swali hilo liliwafanya vijana wengine kutazama kisha mmoja akasema "Huyu mjinga, kwahiyo umependa Saidon alichofanyiwa?.. Je, unajua kama kafa ama la!? Ndio maana jamaa akaanza kwa kusema woga ukizidi ni ufala. Kwahiyo wewe ni fala na kuanzia muda huu toweka.."

"Sawa naondoka ila mtanikumbuka.." aliongeza kusema kijana yule aliyeonekana kwenda kinyume na matakwa ya wenzake kisha akaondoka zake.

"Sasa tumebaki vidume hakuna kuogopa" kwa pamoja wakagongeana mikono na kisha Kuanza kupanga mkakati wa kuvamia nyumbani kwa mzee J ambaye tayari ni mrokole.
       ********
Wakati vijana hao wakifanya mipango yao hali ya kuwa sintofahamu nayo ikiwa imetanda juu ya uhai wa Saidon kipenzi cha wanakijiji. Upande mwingine nako bibi Pili alikuwa katika wakati mgumu sana, Wachawi wale watatu walimtokea na kumtaka awape hazina za uchawi alizo salia nazo. Jambo hilo lilimuogopesha sana bibi Pili kwani alijua fika kuwa tayari  yeye ni mtu wa kufa muda wowote, ndipo alipopiga magoti kuomba msamaha.

"Ahahahaha!.."  Wachawi wale walicheka baada kumuona bibi Pili akijishusha chini na kuomba radhi. Na mara baada ya kuhitimisha hicho kicheko, mchawi mmoja alisema "Bibi Pili umekosa umakini wa kulinda hamana yako ya kazi, tazama sasa huna tena uwezo wa kujua kinachoendelea ulimwengu wa giza. Wewe ni mtu wa kufa tu, haraka sana tupe hazina yetu tuondoke.." 

"Mnisamehe jamani naombeni mnisamehe tafadhali msiniue, nani atabaki na mjukuu wangu? Hapa duniani mimi ndio mama yake mimi ndio baba yake, leo hii mkiniua ataishije Pili wangu?.." alisema bibi Pili huku akiangua kilio.

 "Hahahahahhah.." wale wachawi wakarudia wote kucheka kisha mmoja akaongeza kusema kwa msisitizo "Hiyo sisi haituhusu.." baada kusema hivyo alimnyooshea kidole bibi Pili ambapo  punde si punde wakapotea wakaibukia nyumbani kwake.

 "Ingia ndani utupe hazina yetu.." alisema mchawi yule ambaye alijiteua kama kiongozi wa msafara, ndipo bibi Pili kwa shingo upande akazipiga hatua kuingia ndani muda mchache baadaye akatoka na chungu kikuuu lililojaa mazagazaga ya kichawi hali ya kuwa bui bui nao  walikuwa wameshaweka makazi yao. Wale wachawi wakatazamana pindi walipomuona bibi Pili katoka ndani na hazina waliyoihitaji, wakatabasamu kisha mmoja akamsogelea akampokea na kumkabidhi mkuu wake wa msafara "Ahahahaha" alicheka mkuu huyo halafu akasema "Bibi Pili, pole sana ila ndio imeshatokea..". Bibi alitetemeka wakati huo huo alinyooshewa vidole na wale wachawi ambapo vidole vyao vilitoa moto mwembamba kama radi ukampiga bibi Pili kwenye paji la uso wake kitendo kilichompelekea kuanguka chini  akipiga makelele ambayo nayo hayakuchukuwa muda mrefu yalitoweka baada kupoteza fahamu.

 Wale wachawi walipomaliza kufanya kitendo hicho walicheka kisha wakapotea muda huo huo Pili naye alifika akiwa ametokea kisiamani, ghafla  akidondosha ndoo chini baada kumkuta bibi yake yupo chini.

"Bibi.. Bibi. BIbiiii..." Pili alipasa sauti kumuita bibi yake lakini  hakuitikia kwani alikuwa amepoteza fahamu pindi alipo pokea kipigo kikali. Muda mchache baadaye alizinduka ila cha kushangaza alikuwa hawezi kuongea wala kutembea mwili ulidhoofu, hali ambayo ilimfanya Pili kuangua kilio kwa uchungu akidhania kuwa huwenda siku yoyote bibi yake akaaga dunia.

Naam! Kwingineko alioneakana mrembo Chaudele akiwa ametoka bafuni akizipiga hatua kurudi ndani lakini kabla hajaingia ndani mara ghafla akasikia sauti ya swahiba wake "Chaudele upo tu nyumbani unahabari kuhusu Saidon?..." Alisema rafiki yake.

"Saidon?..kafanyaje?.." Kwa hofu na mashaka Chaudele alihoji. Chausiku akashusha pumzi ndefu kisha akajibu kwa sauti iliyoambatana na kilio...

KIPI KILITOKEA? .
    JE, MCHIZI WETU KAKATA KAMBA!?
        Hayo na mengine mengi tukutane sehemu ijayo ijayo..
  SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA.. Mambo yamekuwa makubwa aisee 😢



No comments: