MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
"Ndio yupo na nimemuita sasa hivi" Alijibu mama Chaudele. Mzee Nhomo akaongeza kusema "Unajua mke wangu huyu mzee J ananitafutia matatizo"
"Kwa nini mume wangu?.." Alihoji mama Chaudele kwa hamaki kubwa huku akimtazama mumewe. Mzee Nhomo hakusema jambo alikaa kimya wakati huo Chaudele alitoka ndani kwa unyonge. "Abee mama.." Aliitikia kwa mara nyingine wakati huo akikunja kunja vidole vyake ilihali mboni za macho yake zikionyesha hofu fulani. Pole pole mama yake akamtazama usoni akashusha macho yake mpaka kwenye miguu ambapo aliweza kuona mchirizi wa damu, alishtuka mama Chaudele ilihali muda huo mzee Nhomo nae akamgeukia kisha akamuuliza "Ni kitu gani kilichomfanya Chitemo akupige?.."
Chaudele akashtuka akawaza amjibu nini baba yake, na mwishowe akaitumia nafasi ambayo Chitemo hutamba nayo kijijini akisema ya kwamba yeye ndio mwanaume pekee atakaye muoa Chaudele mrembo wa kijiji. "Baba Chitemo nilishamkataa lakini hanielewi, leo alipokutana na mimi njiani akachukuwa uamuzi wa kunipiga.." Alijibu Chaudele kwa sauti ya hofu.
"Ulikuwa umetoka wapi?.." Mzee Nhomo akarudia kumuuliza swali. Swali ambalo lilionekana kumtatiza Chaudele kwani alionekana kukodoa macho tu pasipo kusema neno lolote. Mzee Nhomo akarudia tena kuhoji "Si nimekuuliza? Ulikuwa umetoka wapi?.."
"Yani hata kusema nilikutuma dukani unashindwa? Ama ulienda kumtukana nyumbani kwao?.." Sauti ya mama yake ilisikika wakati huo akimfuata Chaudele na kuingia naye ndani ambapo walipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani. Kitendo hicho kilimkera sana mzee Nhomo, kwa jazba alisema "Sio bure nyie mnanitafuta, na inawezekana kuna jambo limejificha nyuma ya pazia. Maana haiwezekani mimi namuuliza mtoto halafu wewe mama mtu unajichukulia uamuzi wa kumshika mkono unaingia ndani. Hamjui kama suala hili ni tatizo? Leo kampiga mwanao kesho utakuja kupigwa wewe urudi nyumbani huna meno ya mbele kisa kufunikia makosa ya kipuuzi. Siku akuletee mimba uanze kusema, oooh.. Baba fulani sasa tunafanyaje, shenzi namgeuza mtu kaka kuona, badala ya kuitwa kaka kuona utaitwa Dada kuona wajinga nyinyi" Aliwaka mzee Nhomo akionekana kukerwa na kile kitendo cha mama Chaudele kumvuta ndani binti yake baada kuona anatoka damu sehemu nyeti, mama huyo alifanya vile kabla mumewe hajagundua kwani laiti kama mzee Nhomo angegundua basi pasingetosha hapo nyumbani.
"Achana na maneno ya baba yako. Chaudele wangu naomba uniambie umeipoteza bikira yako?.." Mama Chaudele kwa sauti ya chini kabisa iliyojaa upole alimuuliza binti yake wakati huo wakiwa wawili tu chumbani. Chaudele akashusha pumzi ndeefu kisha akajibu kwa ishara ya kichwa akikubali kuwa ni Kweli kapoteza usichana wake.
" Eeeeh Chaudele mwanangu mbona umeaibisha mama yako? Kwanini lakini. Looh sikutegemea kama ni wewe Chaudele wangu binti mzuri mpole leo hii unakuja kuniambia bikira huna?.." Mama huyo alilaani kitendo hicho.
" Kwahiyo Chitemo ndio kakuvua usichana?.. ", Swali hilo Chaudele hakujibu kwa haraka kwani tayaru muda huo alikuwa akiangua kilio cha chini chini. Mara baada kuyafuta machozi yake akasema
"Samahani sana mama najua sana nimekukosea naomba unisamehe "
"Mwangu Siku zote muungwana akivuliwa nguo huchutama, kwahiyo nimeshakusamehe ila naomba uniambie ni nani aliyehusika na kitendo hiki.. "
"Saidon, ndio aliyenifanya.. "Alijibu Chaudele. Mama huyo akashtuka baada kuisikia jina hilo, ukweli sio jina geni masikioni mwake mbali na hilo anamfahamu fika kwa sura. Hapo ndipo kwa mara nyingine tena aliposhusha pumzi kisha akasimama akatoka ndani huku nyuma akimuacha Chaudele akiwa kitandani akitokwa na machozi.
Moja kwa moja akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa mzee Mligo kwania njema ya kumueleza kilicho tokea ili wafikie muafaka. Lakini kabla hajafika katika mapanda njia alikutana na mzee huyo akiwa ametoka kuwinda. Siku hiyo mzee Mligo alibahatika kumkamata sungura vile vile kwenye mitego yake aliwanasa ndezi kadhaa. "Mmh kulikoni mama Chaudele mbona pirika hivyo?.." Aliuliza mzee Mligo mara baada kumuona mama Chaudele akikazana mwendo.
"Afadhali tumekutana bwana Mligo, maana mguu huu ni wako.." Alijibu mama Chaudele.
"Enhe ronga nakusikiliza ama tunaweza kuongea huku tunatembea?.." Mzee Mligo aliuliza kwa mara nyingine. Mama Chaudele akakataa, na hapo ndipo alipoanza kuongea hatua ya kwanza mpaka ya mwisho pale Chaudele alivyomtaja kubwa Saidon ndio kamvua usichana. Mzee Mligo alisikitishwa na jambo hilo, kabla hajasema neno lolote mama Chaudele akamuuliza "Kwahiyo sijui unafikiriaje jambo hili,na ukae ukijua kuwa mwanangu sio wa kuchezewa na kisha kuachwa.."
Mzee Mligo alikaa kimya akifikiria jibu la kumpatia mama Chaudele ili alizike nalo wakati huo huo moyoni akijisemea "Tayari Saidon kaharibu, daah huyu mtoto huyu bora angebaki mjini tu. Ila nilijua tu kama mambo haya yangetokea.."
Na kabla hajapata jawabu la kumpa mama Chaudele mara ghafla kijana mmoja wa makomo aliwapita njia panda kwa kasi ya ajabu iliyowashtua mama Chaudele na mzee Mligo. Kijana yule aliposimama hatua kadhaa mbele aligeuka nyuma na kisha akasema "Mzee Mligo upo tu hapa hujui kubwa nyumbani kwako kuna balaa linaendelea?.."
"Balaa? Balaa gani tena hilo?.." Aliuliza mzee Mligo kwa taharuki ya hali ya juu.
"Wakati natoka shamba narudi nyumbani nilikutana na Chitemo akiwa ameshika upanga huku akiongea njia nzima kwamba anakwenda kumfyeka kichwa Saidon. Kwahiyo muda huu naelekea huko kutazama yanayojili.." Alijibu kijana huyo, mzee Mligo alishtushwa na maneno hayo. Akamgeukia mama Chaudele kisha akamwambia " Mama tutaongea ngoja kwanza nikamalize tatizo hili, doh huyu Saidon huyu sasa ananivuruga kiukweli.. " Aliondoka mzee Mligo akiambatana na yule kijana.
*****
Kwingineko nyumbani kwa bibi Pili walitua wale wachawi watatu waliopewa jukumu la kufuatilia mstakabali wa bibi huyo baada kuonekana tayati kapoteza matumaini ya nguvu za giza. Wachawi wale walibisha hodi wakimtaka bibi Pili atoke ndani ili awakabidhi badhi ya vitu mbali mbali vihusio uchawi na kisha baada ya hapo ndipo ageuzwe chakula cha msikule kama sera na masharti yao yasemavyo. Bibi huyo hakuwepo muda huo alikuwa shamba, lakini jambo hilo halikuweza kuwazuia wale wachawi kushindwa kufanya dhamira yao. Ndipo mchawi mmoja aliposugua kiganja chake kwa muda wa dakika kadhaa kisha akakitazama akamuona bibi Pili akiwajibika shambani.
"Nisikilizeni nyinyi.." Alisema moja ya wachawi wale watatu akiwa yeye kama kiongozi wa kundi hilo. "Ndio mkuu" waliitikia wachawi wale.
"Bibi Pili yupo shambani kwake, hivyo basi kinachotakiwa ni kumfuata kule kule, mpaka kieleweke. Sawa sawa?" Aliongeza mkuu wa msafara huo wa wachawi wawili.
"Sawa mkuuuu"
"Haya poteeni hapa" Amri hiyo ilipotoka wote kwa pamoja wakapotea pale nyumbani kwa bibi Pili ikasalia vumbi ambayo haikuchukua muda mrefu nayo ikatoweka, wananzengo hao waliamuwa kula sahani moja na bibi Pili ikiwa upande wa pili nyumbani kwa mzee Mligo ghafla simanzi ilitawala hali ya kuwa kwa mbali vikisikika vilio...
KIPI KILITOKEA? Kwanini MAJONZI?
USIKOSE SHEHEM IJAYO.
Shea mara nyingi ili upate sehemu ijayo.

No comments: