MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA YA ISHIRINI NA TANO-25
MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA YA ISHIRINI NA TANO-25
"Nitakunyoosha goigoi wese" Aliongeza kusema Chitemo wakati huo akikunja vizuri shati yake ambayo ilikuwa ya mikono mirefu. Baada kumaliza zoezi hilo akamsukuma Saidon ambapo Saidon alirudi nyuma hatua kadhaa kisha akasimama ilihali muda huo huo Chitemo aliruka teke ambalo lilipompata Saidon alianguka chini.
Saidon alisafa na maumivu makali pale chini huku akiwa amegusa tumbo lake, kitendo hicho kikamfanya Chaudele kumsogelea ili amuamshe lakini kabla hajamfikia mara ghafla Chitemo aliruka teke lingine kwa mara ya pili, teke hilo lilimpelekea Saidon kutapika damu.
"Saidon unakwenda kijijini, tafadhali sana chonde chonde kuwa muangalifu. Sitaki babu yako apate tabu kwa kesi za kijinga kijinga, utulivu unahitajika sana ili uweze kuishi vizuri na wanakijiji wa Ndaulaike.." Alisema baba Saidon akimuasa kijana wake.
Saidon alitabasamu kidogo kisha akajibu" Sawa baba nimekuelewa, unajua mimi tayari mtu mzima kwahiyo naelewa kipi na kifanya"
" Labda la kuongezea tu baba Saidon " Alidakia mama Saidon akimwambia mumewe. "
Enhee?" Baba Saidon aliitikia na kisha akaonyesha utulivu kumsikiliza mkewe. Ndipo mama Saidon aliposema "Kuhusu michezo yake ya ngumi.. "
" Kweli kabisa nilikuwa nimesahau, Saidon kwanza nilisha kukanya sana kucheza cheza ndondi kwani kuna faida gani unaipata mwanangu?" Baba Saidon alimgeukia kijana wake na kumuuliza swali hilo. Hapo Saidon akakosa jibu la kumpa mzee wake zaidi alijikuta akijiinamia.
Baba yake akaongeza kusema "Sasa basi nataka michezo wako huo ubaki huku kamwe usiupeleke kijijini, watakutoa nyongo nakwambia. Yani mtu akikuchokoza we muuache ikiwezekana mpishe ili kuepusha shari. Natumai umenielewa "
"Ndio baba nimekuelewa na naahidi sitowaangusha wazazi wangu "
Yote hayo Saidon aliyakumbuka akiwa chini amelala asijiweze kwa kipigo ailicho pokea kutoka kwa Chitemo.
"Ndio baba nimekuelewa na naahidi sitowaangusha wazazi wangu "
Maneno hayo ya mwisho Saidon aliyowaahidi wazazi wake yalijirudia kichwani mwake, lakini ghafla akajikuta akivunja ahadi baada kuona Chitemo anamfanyia kitendo kibaya Chaudele. Chitemo alionekana akimlazimisha kupeleka mdomo wake kwenye kinywa cha Chaudele kitu ambacho Chaudele alikuwa hakubaliani nacho ndipo alipopiga mayowe. Punde si punde jopo la vijana lilikusanyika eneo la tukio, wote waliona jinsi Chitemo anavyolazimisha denda kwa Chaudele ila hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza kumsadia Chaudele ajabu baadhi ya vijana walimuunga mkono Chitemo ihali wengine wakimsikitikia.
Timu zikawa mbili tofauti. Baada ya dakika chache Maige naye alifika eneo lile, ghafla akistaajabu kumuona swahiba wake wakuitwa Saidon yupo chini huku hali yake ikiwa dhofu lihali.
"Saidon" Maige alipasa sauti kumuita rafiki yake wakati huo huo Saidon akanyanyuka akamfuata Chitemo kwa hasira huku akiwa amefura hasira. Alipomkarbia alimrushia ngumi nzito iliyomfanya Chitemo kuweweseka, muda huo huo Saidon akaruka juu samasot style ambayo iliwashangaza vijana wa kijiji waliojikusanya kwenye tukio "Waoooh.." Alisema kijana mmoja aliyeonekana kufurahishwa na kitendo kile alichokifanya Saidon, kumbe mbali na soka vile vile Saidon alikuwa ni mcheza ngumi mzuri tu ila hakutaka kujionyesha kuwa anayaweza masuala hayo. Shangwe zilizuka eneo hilo Saidon alimpiga Chitemo kwa jinsi atakavyo lakini mwishowe alijitokeza mzee mmoja wa makamo akaingilia kati, hapo ndio ukawa mwisho wa ungomvi wa vijana hao wawili ambao wote kwa pamoja walikuwa wakitunishiana misuri kisa mrembo wa kijiji wa kuitwa Chaudele.
Muda huo alipelekwa nyumbani na baadhi ya mabinti wa kijiji kwani hali yake ilikuwa sio nzuri ukiachilia mbali maumivu ya kuvuliwa usichana wake, kingine kilichomuumiza zaidi ni kipigo alichopokea kutoka kwa Chitemo.
"Wewe mjinga tu, tena nakwambia hivi hii vita haitoishia hapa. Popote nitakapo kuona ama zako ama zangu mwanaharamu wewe" Alisema Chitemo akiongea kwa sauti ya juu akimtishia Saidon.
Saidon akiwa na jopo la vijana waliokubali uwezo wake aligeuka nyuma akamtazama Chitemo kisha akamuonyesha dole gumba akiashiria kuwa haogopi kelele za chura kwani siku zote hazimtishi tembo kunywa maji.
Upande wa pili mzee Bidobido na kaka yake hali zao zilianza kuimarika, mzee J alishangaa sana kwani alijihisi yupo tofauti kabisa na hapo awali. "Mke wangu kaniletee maji ninywe.." Alisema mzee J. Mama Chitemo alimtazama mtumishi kisha akaachia tabasamu pana na mwishowe akaingia ndani kumchotea mumewe maji. Punde alitoka ndani na kikombe kilichojaa maji alipofika akampa mumewe, mzee J alikunywa haraka sana halafu akataka mengine. Hapo mtumishi akamtaka mama Chitemo alete kabisa ndoo ya maji nje, jambo hilo liliweza kuwa jema sana kwa sababu ndoo ile ndogo ya maji yenye lita kumi waliimaliza watu wa wili kila mmoja ikinywa maji lita tano. Mzee J alikunywa maji lita tano, pia mzee Bidobido naye akanywa maji lita tano. Baada ya dakika tano hali ikawa Shwari kabisa.
Wzee hao walipiga magoti kwa mara nyingine na kuomba kwa hisia huku wakidondosha machozi yao mbele ya mtumishi wa Mungu,kila mmoja akijutia kwa mambo aliyoyafanya katika ulimwngu wa giza. Baada ya toba hiyo mtumishi alisema "Mungu kawasamehe, nyinyi sasa ni watu wapya nafikiri huu ni wakati wa kumtukuza Mungu kwa sifa zote na kushukuru kule alikowatoa kwa sababu tayari mlikuwa wafu mnaotembea.."
"Ni kweli kabisa mtumishi, eeh Mungu sujui nikupe nini Mungu wangu nakushukuru sana baba" Alisema mzee J huku uso wake ukitazama juu. Furaha ilitamaraki nyumbani hapo kwa mzee J lakini ghafla furaha hiyo ikaingia dosari baada Chitemo kufika nyumbani huku akifoka " Baba mbona dharau zinazidi kuongeza hapa kijijini? A mwanao nilivyoumizwa. Sasa naona wewe unawachekea sana kwahiyo acha niingie mwenyewe uwanjani ili hata siku nyingine waiogope familia hii. Haiwezekani mtu mmoja aishushe hadhi familia yetu istoshe mtu mwenyewe mgeni, huu si upuuzi. Nasema haiwezekani.. "Alisema Chitemo maneno hayo kwa hasira na kisha akaingia ndani akachukuwa panga akatoka nalo nje. Akasimama kidete akaongeza kusema "Panga hili linaenda kuchinja mtu "
Mzee J na mkewe pamoja na mzee Bidobido walishangazwa na uamuzi wa Chitemo. Mtumishi akasema "Kijana tafadhali njoo uketi hapa tuliondoe pepo hilo linalo kusumbua, pepo chafu hilo"
"Achana na mimi, kaa chini na utumishi wako kabla sija kutoa kichwa chako. Kaaa chini bwana" Alijibu Chitemo kisha akaambaa na njia kuelekea nyumbani kwa mzee Mligo kwa dhumuni la kumjeruhi Saidon.
Kwingeneko Chaudele alipofikishwa nyumbani aliingia ndani lakini kabla hajaelekea chumbani kwake mama yake alimuita. Alishtuka baada kusikia wito wa mama yake, akajiuliza "Nitamjibu nini mama?.. Nikimwambia nimepigwa na Chitemo, ataniuliza nini chanzo! Na itakuaje atakapoiona damu hii inayonitoka ukeni? Nidanganye Chitemo amenibaka! Ama nimtaje Saidon ndio kahusika na hiki kitendo? Na atanichukuliaje mama wakati nilisha fundwa kuwa bikira ni zawadi kwa mwanaume atakaye nioa?" Alijiuliza mrembo Chaudele bila kupata majibu sahihi. wakati bado anawaza jibu la kumpa mama yake punde alisikia baba yake nje akimuuliza mama yake kwa sauti kali "Hivi Chaudele nimemkuta?.."
HATARI SANA.. KULE CHITEMO ANAENDA KUMCHANJA MTU, WAKATI HUO CHAUDELE NAYE ANAWAZA ATAJIELEZA VIPI ILI AELEWEKE.. Mzee #Nhomo 😂😂
SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA SEHEMU IJAYO.

No comments: