MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE-24




MREMBO WA WA KIJIJI


           SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE-24

Kundi lile la wanakijiji liliombatana na mtaalamu walijongea kuelekea nyumbani kwa mzee Mligo lakini kabla hajafika mara ghafla mtaalamu akajihisi kuumwa kichwa na punde si punde akasikia sauti  za nyuki masikioni mwake, kitendo ambacho kilimpelekea  kujisjkia kizunguzungu. Hali hiyo limfanya asimame akaachia tunguli alizokuwa ameshika na mara moja kwa mikono yake miwili akashika kichwa chake huku akipiga mayowe ya kuomba msaada. Wanakijiji walishtushwa na hilo jambo wote kwa pamoja wakajikuta wakitazamana wasijue wamsaidieje mtaalamu wao, wakati huo huo mbele ya macho ya mtaalamu wakaonekana wale wachawi watatu waliopewa jukumu la kumuadabisha.

"Ahahahahahah" Waliangua kicheko wale wachawi kisha mmoja akasema "Eti mtaalam..." Alisema mchawi huyo akiongea kwa kejeri na kisha wakatazamana na wote watatu wakarudia kucheka.

"Hapanaaaa.. Hapana.. Hapana" Mtaalamu akiwa chini alipasa sauti akisema maneno hayo. Jambo hilo lilizidi kuwaweka mdomo wazi wanakijiji waliokuwepo pale kwani wao walikuwa hawawaoni wale wachawi zaidi ya mtaalamu peke yake ingawa wale wachawi waliwaona wanakijiji.

"Hapana nini wakati umechagua mwenyewe kuja kwenye uwanja wa vita usiokuhusu? Ngoja tukupe dawa kwanza.." Aliongeza kusema mchawi wa pili na mara baada kusema hayo wote kwa pamoja walishikana mikono punde si punde ukatokea moto katika viganja vyao kisha wakamrushia  mtaalamu kombora hilo la kichawi ambalo nalo hata hivyo mtaalamu alijitahidi akalidhibiti. Kitendo hicho kikawafanya wale wachawi kila mmoja kutumia uwezo wake binafsi, na hapo ndipo waliporusha makombora fululizo kiasi kwamba mtalamu alishindwa kuyadhibiti yote na  baadhi yalimpata.

Mtaalamh akakunguka chini, hakusita kuomba msamaha "Msiniue jamani msiniue tafadhali.."

"Aha hahahah" Waliangua kicheko wale wachawi baada kuona mtaalamu anaweweseka, kisha mmoja wao akasema "Leta nadhili yako"  Mtaalamu alipoambiwa hivyo hakutaka kupingana na amri hiyo kwani aliona tayark maisha yake yapo hatarini, hivyo kwa mikono miwili alivua nadhili yake akawakabidhi wachawi wale watatu, nao kwa pamoja wakashikana mikono kisha wakapotea.

Baada ya dakika kadhaa hali ili ya mtaalamu kusikia sauti za nyuki ilitoweka na hapo aligeuka kulia na kushoto kuwatazama wanakijiji walio mzunguka "Mtaalamu vipi tuendelee..?.." Alisikika mwanakijiji mmoja akimuasa mtaalamu.

Mtaalam akamtazama yule mwanakijiji huyo kisha akajibu "Nina familia jamani inanitegemea.."

"Unamaana gani sasa mtalamu unapotuambia maneno hayo?.." Mwanakijiji wa pili alihoji. Mtaalamu akashusha pumzi ndefu halafu akasema "Nimefanya kazi hii vijiji karibia kumi na vitano tangu nilithishwe kazi hii na marehemu babu yangu lakini kijiji hiki ni komba mwiko, kimenishinda narudi nyumbani tafuteni mwingine.." Alisema Mtaalamu, maneno hayo yaliwashangaza sana wanakijiji ambapo kila mmoja alibaki mdomo wazi.

"Na vipi kuhusu pesa yetu sasa?.." Mnong'ono wa chini ulisikika kwa wanakijiji wawili waliokuwa wakijaribu kujaji suala hilo. Hapo hapo yule aliyeulizwa akapasa sauti kwa uma akisema "Pesa zetu vipi sasa"

"Zipo twendeni mkachukue.." Alijibu mtaalamu na mara moja safari ikaanza kuelekea nyumbani kwa barozi ambako ndiko alikofikia

Saidon akawa ameponea kwenye tundu la sindao kwa maana hiyo alifanikiwa kufanya kile Chaudele alichotaka.
   Baada ya masaa mawili kupita alionekana Chaudele akitoka ndani ya nyumba ya mzee Mligo, akatazama kulia na kushoto hakuona mtu haraka sana akazipiga hatua kurudi nyumbani lakini kabla hajafika mbali aligeuka nyuma akakutana na uso wa kijana Saidon ukiwa umejaa tabasamu bashasha. Chaudele akampungia mkono wa kwaheri Saidon ambavyo ndivyo naye Saidon alivyofanya na kisha Chaudele akatokomea zake. Saidon aliruka kwa furaha ndani ya nafsi yake akajisemea "Daah kumbe ni tamu hivi? Ingawa kanisumbua ila kitu kipya ni kipya tu hata iweje. Sio mjini unakutana na binti kakomaa sehemh ya siri mithili ya nyani halafu anaringa mtaani lakini huku kijijini mambo ni tofauti kabisa, kigori mbichiii hajafunguliwa wala nini halafu haringi.. " Alijisemea maneno hayo Saido kisha akatupia begani fulana yake na kurejea chumbani kuweka mazingira sawa baada kumaliza zoezi nzima la kuchafuana na Chaudele mrembo wa kijiji.
   Upande wa pili Chaudele akiwa njiani akirudi nyumbani ghafla alijihisi maumivu makali sehemu ya siri, alihisi kama mapaja na sehemu yake nyeti panawaka moto na punde si punde mchilizi wa damu ukatiririka mguuni.

"Mmh nitamwambia nini mama akinigundua?.." Alijiuliza Chaudele kwa hofu wakati huo akizipiga hatua za pole pole kwani alijihisi maumivu makali sana. Muda huo huo   akakutana na Chitemo.

Chitemo akiwa kwa mbali alifurahi kumuona  Chaudele, hivyo kwa sauti iliyojaa tabasamu  alisema "Hakika hii ni bahati sana kukutana na mrembo wa kijiji kwa mara nyingine tena. Na kwa jinsi ninayo kupenda Chaudele ukweli nipo tayari hawa ndezi nilonasa leo nikutunuku wewe.." Chaudele hakujibu chochote licha ya kuyasikia maneno hayo ya Chitemo, zaidi aliendelea kusafa na maumivu yake aliyoyapata baada kutolewa usichana wake na kijana Saidon. Mpaka wawili hao wanakaribina Chaudele hakusema neno lolote, hapo Chitemo akashtuka kumuona Chaudele akichechemea.

Kwa taharuki kubwa moyoni akamuuliza "Je,umegongwa na nyoka?.." Chaudele hakujibu alizidi kutembea kwa kuchechemea huku miguu akiwa ameipanua. Na mwishowe Chitemo akajua Chaudele kuna machafu kafanya haraka sana akamsogelea halafu akamuuliza kwa jazba "Chaudele inamaana umefanya mapenzi?.."

Chaudele akasimama akamtazama  kwa jicho la hasira kisha akajibu "Ndio nimefanya na mtu nimpendaye kutoka ndani ya moyo wangu kwani wewe unataka nini? Mimi sikupendi Chitemo nikome acha kunifuatilia katika maisha yangu. Kwani kijiji kizima hujamuona binti mwingine tofauti na mimi?.."

"Aha hahahaha" Alicheka Chitemo huku roho ikiwa inamuuma, na mara baada kukatisha kicheko chake akasema "Chaudele Chaudele Chaudele, mimi ndio mwanaume sahihi kwako. Na utake usitake utakuwa wangu liwake jua inyeshe mvua Chaudele lazima uwe mke wa Chitemo.."

"Mshenzi wewe nani atakubali umuoe mwanaume mwenye chogo kama kiazi? Yupo mwanaume atakaye nioa naye nishamtunuku tunda langu. Si mwingine ni Saidon.." Alijibu Chaudele. Ghafla Chitemo akabadilika uso wake ukawa uso wenye hasira kali tofauti na mwanzo, akajiuliza" Saidon?"  Muda huo huo akaongeza kusema "Huu ni ujinga ulioufanya Chaudele katu siwezi kukubali. Ili nikuthihilishie kuwa sikubaliani na ulicho kifanya ngoja nikuadabishe kwanza halafu nikamalizane na yule mshenzi.."

Alipokwisha kusema hayo  alichukuwa jukumu la kumpiga Chaudele. Chaudele alisafa na maumivu ya kipigo kilichomfanya aangue kilio, Na wakati Chitemo anafanya kitendo hicho  akapita mtoto mdogo wa pata miaka mitano. Mtoto huyo aliweza kushuhudia Chitemo akimpiga Chaudele na ndipo alipotimua mbio kuelekea nyumbani kwa mzee Mligo kwa dhumuni la kupasha habari Saidon.

"Saidon Chaudele anapigwa wahi ukamsaidie.." Alisema bwana mdogo huyo aliyemshuhudia Chitemo akimshushia kipigo Chaudele.

"Anapigwa na nani?.." Aliuliza Saidon kwa mshangao mkubwa.

"Chitemo.." Alijibiwa Saidon, jina hilo halikuwa masikioni mwake. Upesi akatimua mbio kwenda kumtetea mpenzi wake.
  Alipo fika alishuhudia kitendo kile alichokuwa akikifanya Chitemo, lakini wakati anataka kumrushia ngumi ili amalize hasira zake mara ghafla mkono wake ulishikwa, alipogeuka ili amtazame mtu aliyemshika mkono akakutana na uso wa Saidon ukiwa umefura hasira.
"Kumpiga mwanamke huo ni upungufu wa nguvu za kiume kijana. Punguza ushamba, mapenzi hayalazimishwi. Kama una nguvu pigana na mwanaume mwenzako" Alisema Saidon kwa sauti nzito kisha akaushusha mkono Chitemo ulio kunja ngumi.

"Na nilikuwa nakutafuta wewe kwa kipindi kirefu sana.." Aliongea Chitemo. Saidon akacheka kwa dharau kisha akasema "Naam! Na hatimaye umenipata. Sasa basi nataka nikudhirishie kuwa, sio kandanda tu bali hata ngumi naweza, nitakufua"

"Saidon? Naapa endapo ukifanikiwa kupenyeza hata ngumi moja ndani ya mwili wangu, basi mrembo wa kijiji Chaudele atakuwa mali yako" 

   HATA SANA, BAADA YA NDUMBA SASA NI MIKONO DADEKI ✍️
      NANI ATAFUA DAFU? SHEA MARA NYINGI ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA.. MTAALAMU ANASEPA BAADA KUONA MAMBO MAGUMU.. BADO MTUMISHI NAYE MAMAE NDAULAIKE. SHEA



No comments: