MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA YA ISHIRINI NA TATU-23
MREMBO WA WA KIJIJI
SEHEMU YA YA ISHIRINI NA TATU-23
"Naam huu ndio wakati muafaka wa kumrudia Mungu wenu, kwa kuwa na wewe umejitokeza basi ni jambo la heri" Alisema mtumishi wa Mungu huku akiinamana kuchukuwa Biblia yake, maneno hayo ya yalimfanya mzee Bidobido kujiuliza "Anajiamini nini huyu mtu?.." wakati huo mzee J kwa sauti kali akamwambia mdogo wake "Bwana mdogo usipoteze muda, ukiachilia mbali yule anayejiita mtalamu na huyu ni moja ya watu wa kupigwa vita. Haraka sana muadabishe"
Lakini licha ya mzee J kumuamuru mdogo wake ili amshambulie mtumishi yule wa Mungu, ajabu mzee Bidobido aligoma, hasira zake zikayeyuka upesi kitendo ambacho kilimshangaza sana mzee J kwa jazba akahoji "Mbona utaki kufanya kile ninacho kwambia? Unamuogopa"
Mzee Bidobido kwa sauti ya upole akajibu "Ndio bwana mkubwa, kweli nimeamini hii ni kazi isiyo kuwa na faida hapa duniani. Nafikiri unafahamu nina miaka gedegede nikiutumikia ulimwngu wa giza lakini leo hii malipo yangu yanakuwa umauti kisa kosa moja ambalo ningeliweza kusamehewa"
"Umauti!!?.." Mzee J alishangazwa na maneno hayo ya mdogo wake asielewe kamanisha nini kusema hivyo. Mama Chitemo na mtumishi wa Mungu bwana Steven walitulia huku wakimtazama mzee Bidobido nao pia wakishangazwa na maneno aliyozungumza. "Bado sijakuelewa bwana mdogo, tafadhali nifafanulie vizuri ili nipate kukuelewa" Aliongeza kusema mzee J, ndipo mzee Bidobido alipokisugua kiganja chake cha mkono wa kulia kwa kutumia vidole vya mkono wa kushoto, zoezi hilo lilichukuwa muda wa dakika kadhaa kisha akakunjua kiganja akamwambia kaka yake atazame.
Katika kiganja cha mzee Bidobido ilioneakana senema. Mzee Bidobido alikuwa na wachawi wenzake kwenye kilinge, mkuu wake mzee Bidobido akasimama na kisha kusema "Wandugu, tu fahamu kuwa hapa tulipo tayari kuna mmoja wetu ametusaliti. Kwa siku nyingi alikuwa akijihusisha na vitu visivyo muhusu kitendo kilicho pelekea kutohudhulia baadhi ya vikao na mkutano yetu. Kugundua hilo sisi kama wa kubwa wa kundi hili tumeamuwa mwanachama huyu tuachane naye kwani kama mwanachama hewa yaani hana faida kwetu, lakini licha ya kuchukuwa uamuzi huu bado tumeona huyu mtu hastahili kuishi matokeo yake ni kumfanya kitoweo cha misukule yetu. Sababu endapo kama tutamuacha basi tujue muda wowote tutakuwa hatarini, katu tusitegemee kwamba mtu huyu ataweza kukaa kimya.. " Alisema mkuu huyo, maneno hayo yaliwafanya wachawi wote waliokuwa wamekusanyika mahala pale kuwa na hofu kubwa mioyoni mwao kila mmoja alimtazama mwenzie wakati huo mkuu yule alikuwa amekaa kimya huku akitazama kule na huku kitendo kilichozua ukimya fulani kilingeni hapo. Baadaye kidogo kimya hicho kilipotea baada mkuu yule kumtaka mzee Bidobido asimame, mzee Bidobido alishtuka aliposikia jina lake lakini hakuwa na namna alisimama ili amsikilize mkuu wake atamwambia nini.
"Bidobido, wewe mzee ni msaliti. Haiwezekani uondoke kufanya mambo yako bila kuomba ruhusa sehemu husika. Je, ilani ya chama chetu huijui? Hapo awali tulijua labda ni safari ya dharura lakini baada kuona jambo hili ni endelevu tukajua ni makusudi yako tu, hivyo basi mimi na washauri wangu tumeona tukuengue kwani yawezekana hufurahishwi na maisha yetu. Kwahiyo kuanzia sasa tumekuvua uanachma na usiku wa kesho utakuwa kitoweo cha misukule yetu mjinga mkubwa wewe.. " Mzee Bidobido alionekana kushtushwa na maneno hayo ya mkuuu wake, ghafla machozi yakamtoka huku akiomba msamaha, lakini kiongozi wake hakutaka kusikiliza msamaha wake cha zaidi alifunga kikao na kisha kuwaamuru kila mmoja arudi nyumbani kwake.
Wachawi wote waliokuwepo pale kilingeni walitoweka akabakia mzee Bidobido ambaye alikuwa akiwaza na kujiuliza juu ya adhabu aliyoipata. "Ni miaka mingi Bidobido nautumikia ulimwngu wa giza, leo hii malipo yangu yanakuwa umauti kwa kosa ambalo naweza kusamehewa. Miaka ya nyuma nilisikia habari kuhusu Mungu, watu wakawa wanasema Mungu husamehe hatakama umekosea vipi na ukweli kama kwa jambo hili inapaswa nimtafute Mungu ambaye ataweza kunirudisha njia sahihi. Bidobido leo hii sio wa kulipwa umauti..." Alijiuliza na kuwaza pia mzee Bidobido asiamini kile ailicho ambiwa, na yote hayo yalikuwa yakijili katika kiganja chake namna ilivyotokea usiku uliopita. Ikimbukwe mzee Bidobido siku zote alikuwa bega kwa bega na kaka yake akimsaidia kumpata mrembo Chaudele binti aliyetakiwa kuolewa na mtoto wa kaka yake wa kuitwa Chitemo. Kumbe yote hayo mzee Bidobido aliyafanay pasipo kuomba ruhusa kwenye kundi lake kitendo kilicho pelekea kuonekana msaliti na huwenda akagawa siri za kuhusu kundi alilomo, kuamini hilo mkuu wake akaamuwa kumbwaga huku adhabu pekee anayo stahili msaliti ni kifo na mwili wake kuwa chakula cha misukule.
"Ooonh pole sana bwana mdogo lakini ondoa shaka mimi kaka yako nitakusaidia katika hili" Alisema mzee J mara baada kutazama kwenye kiganja yote yaliyojili. Mzee Bidobido baada kusikia maneno hayo ya kaka yake akajibu "Kaka utanisaidiaje wakati wewe mwenyewe unahitaj msaada?.."
J alishangazwa na maneno ya mdogo wake, na kabla hajaongeza neno lolote, mtumishi yule wa Mungu akasema "Mzee ondoa shaka kwa sasa upo katika mikono salama kabisa, yupo Mungu asiyefananishwa na kiumbe chochote hajazaa wala hajazaliwa kupitia mwili wangu na roho mtakatifu basi amini utapona na hao wabaya wako watakuogopa. Biblia inasema njooni kwangu nyote muelemao na mizigo nami nitawapumzisha. Kwahiyo wewe mzee ulikuwa umeelemewa na mizigo mizito, hivyo basi njoo kwa Mungu aliyehai ili akupumzishe. Huu ni wakati wa kukivua kiatu ulichokuwa umekivaa kwa miaka mingi sasa unakivua, Mungu alimwambia musa. Musa hicho kiatu kivue maana hapa ni mahala patakatifu. Ailicho maanisha Mungu sio saganyoka hiyo uliyovaa wewe mzee bali ni dhambi ulizo nazo, hirizi unazo miliki hicho ni kiatu kivue katika Jina la yesu. Kutembea na mke wa mtu hicho nacho ni kiatu, kuamini uchawi hicho nacho pia ni kiatu. Sasa leo hii ndio siku ya kukivua kiatu hicho ulicho nacho.. Naomba upige magoti, usiogope mzee wangu piga magoti ili nikuombee " Alisema mtumishi wa Mungu akimtaka mzee Bidobido apige magoti ili apate kukombolewa, na hata pale Bidobido alipoogopa mtumishi alimtoa hofu na mwishowe mzee Bidobido akapiga magoti chini haraka sana mtumishi akamuombea. Anga lika ng'aa, zile radi na Ngurumo zikatoweka upesi.
Wakati maombi yamekolea, mama Chitemo naye aliungana na mzee Bidobido kuombewa na mwishowe mzee J naye alikubali akapiga magoti maombi yakawakumba wote kwa pamoja.
"Amen.. Mungu akubariki sana mama. Aamh unaweza kutoa mkeka nje ili tuwalaze hawa watu waweze kupumzika" Alisema mtumishi yule wa Mungu baada maombi kumalizika na kuonekana mzee J na mdogo wake kuanguka chini huku viongo vyao vikiwa vimelegea wakishindwa hata kuongea. Mama Chitemo akaingia ndani punde si punde akatoka na kilago akatandika pembezoni mwa nyumba na kisha akasadiana na mtumishi kuwabeba wazee wale na kuwalaza kwenye kilago, zoezi hilo lilipo malizika mtumishi yule wa Mungu akamwambia mama Chitemo "Mama muda huu tunangojea watu hawa warudi katika hali yao, ngoja nikusomee vifungu mbali mbali vya Biblia ili ujue kuwa Mungu yupo.."
*****
Wakati hayo yakijili nyumbani kwa mzee J, upande wa pili mtalamu nae alianza kazi yake, aliambatana na jopo la wanakijiji nyumba mpaka nyumba kuwaumbua wachawi. Na kila nyumba iliyobainika kuwa inawachawi ilichomwa moto, ndilo waliloamuwa wanakijiji licha ya kwamba mtaalamu hakupendezwa nalo suala hilo ila wanakijiji walionyesha kuchoshwa na mambo hayo ya kichawi.
Kwa muda wa nusu saa kijiji cha Ndaulaike kilichafukwa na moshi mzito wa nyumba na matunguli yaliyokuwa yakiungua, mchana kweupe wachawi waliumbuka kitendo kilicho washangaza wanakijiji wale ambao hawakudhaniwa kama fulani angelikuwa mchawi. Kipindi hayo yanaendelea kutokea, upande mwingine kwa mara nyingine alionekana mrembo Chaudele akizipiga hatua za haraka haraka kuelekea nyumbani kwa mzee Mligo kwa dhumuni la kumfuata Saidon. Alipofika alimkuta Saidon akimalizia kuanika nguo alizo fua. Saidon tayari hamj ya kuendelea kuishi kijijini ilikatika baada kuona maisha yake yapo rehani kwa sababu ya matukio ya kichawi, na sasa alifikiria kurudi jijini Dar es Salaam.
"Saidon.." Chaudele alipasa sauti kumuita Saidon, Saidon aliposikia sauti ya mrembo huyo akageuka, mara ghafla akatabasamu huku kimoyomoyo akijisemea "Afadhali umekuja Chaudele punde tu nilikuwa nakuwaza, leo hii nitaandika historia kwako kwa kuwa mwanaume wa kwanza kukuingilia kimwil ili hata nikiondoka unikumbuke na pia siku nikirejea kijijini Ndaulaike nisianze upya kukubembeleza kama naomba kazi.. Hahahahah " Alijisemea Saidon ndani moyo wake wakati huo Chaudele aking'ata kidole akiinamana kwa haibu, na mwisho wa yote akaingia ndani "Hapa ni kujiongeza kudadeki mbuzi kafia kwa muuza supu, kesho narudi mjini labda mloge gari ipinduke ila leo huyu mtu simuachi" Aliongeza kujisemea kijana Saidon na kisha naye akaingia ndani kupata vitu adimu kwa karne ya leo.
Lakini Saidon alipofunga mlango tu mara ghafla kundi lile la wanakijiji walioambatana na mtaalamu kwa dhumuni la kuwaumbua wachawi wa kijiji, lilionekana likija nyumbani kwa mzee Mligo.
KIPI KILITOKEA HAPO? JE SAIDON ALIFANIKIWA DHAMIRA YAKE? NA VIPI SAIDON AKIGUNDUA KUWA BABU YAKE NAYE NI MSHIRIKINA IKIWA WAKATI MZEE MLIGO HATAKI MJUKUU WAKE AJUE?
HAYO NA MENGINE MENGI TUKUTANE SEHEMU IJAYO..

No comments: