MWANAMKE: NI JUKUMU LAKO KUJIPA MUONEKANO WA KUMVUTIA MUMEO BAADA YA KUJIFUNGUA






MWANAMKE: NI JUKUMU LAKO KUJIPA MUONEKANO WA KUMVUTIA MUMEO BAADA YA KUJIFUNGUA

Kwa mwanamke ni jambo la faraja kupata mtoto baada ya kuolewa, lakini kupata mtoto kunaambatana na mabadiliko ya mwili kwa mwanamke. Ni wanawake wachache sana wanaobaki na miili yao mara baada ya kujifungua, lakini wengi wao hupoteza muonekano wa awali na kuongezeka mwili au tumbo na hivyo kupoteza muonekanao wake wa awali.

Ingawa pia tatizo la baadhi ya wanawake kuhamisha mapenzi kwa watoto wao badala ya baba zao linasumbua ndoa nyingi, lakini hili la kupoteza muonekano na kuwa tipwatipwa limeonekana kuchangia wanaume wengi kupunguza mapenzi kwa wenza wao na hata kuwasaliti.

Jambo hilo kwa baadhi ya wanaume ambao mapenzi kwa wenza wao ni muonekano wa nje wa mwanamke, jambo hilo huzua kero na kupoteza hamu ya kukutana kimwili na mwenza wake kama awali. Hapo ndipo tatizo la kuchepuka linapoanza. Najua umeshakutana na sentensi kama hizi baada ya mwanamke kupata mtoto, “Nilipojifungua mtoto wa kwanza tu mume wangu akaanza tabia ya kuchepuka”. Mabadiliko na muonekano huo baada ya kujifungua unaweza ukawa sababu.

Kwa ushauri tu ni kwamba, wanawake wanapaswa kubadilika na kuanza kufanya mazoezi na kuzingatia mlo wao wa siku kwa kuacha kula hovyo hovyo ili kuepuka kupoteza muonekano wao wa awali. Si lazima kwenda kwenye nyumba za mazoezi kwa sababu kunahitaji gharama ambazo wengine si rahisi kuzimudu, lakini kwa mazoezi ya kutembea kwa umbali wa maili mbili kwa siku asubuhi au jioni kila siku na kufanya mazoezi ya kucheza mziki (Aerobics) kunaweza kusaidia kuweka mwili katika muonekano mzuri.






No comments: