LADIES LET'S TALK




LADIES

1. Ukiwa Kama mwanamke, pale panapotokea maudhi dhidi ya mpenzi wako, nyamaza kimya, ukimya wa mwanamke humsumbua akili mwanaume. Atahisi kuna jambo fulani kichwani mwako na kama anabusara atatafuta njia ya kusuruhisha. Usiwe mtu wa tit-for-tat.

2. Kama atakutumia ujumbe wa maudhi katika simu, usimjibu kwa maneno ya kuudhi pia. Muandikie "Samahani" au "Asante sana.". 3. Hakuna mwanaume anapenda mwanamke anayemrudishia maneno, kama wewe ni mke uliye na busara, funga mdomo wako. Pale atakapokuwa ametulia ongea nae mmalize mgogoro.

4. Usiringie uzuri wako. Hujawaona wanawake wazuri wengi tu bado wako single, huvaa nguo za kuacha miili yao wazi, ziwa linaonekana wazi bila kujua wanaume hawapendi hivyo nao wanaishia kuwa wezi wa waume za watu na uzuri wao kama wameshushwa toka mbinguni? Tabia yako itakuhifadhi katika moyo wake.

5. Kamwe usimfananishe na EX wako au mwanaume mwingine, huwezi jua huyo mwanaume nae ana mapungufu gani katika mahusiano yake. Binadamu hatuko 'perfect' na hatufanani.

6. Usiwe wa kupokea tu, mnunulie chochote, haijalishi kama anavyo vingi au ni kidogo sana, ila kilichotoka kwako siku zote kina umuhimu mkubwa kwake.

7. Kuwa mwanamke mwenye mawazo 'mtambuka' usifikirie jambo moja tu, mshauri masuala ya maendeleo, miradi, kununua vip-longa na mengineyo. Usiwaze habari za kucha, nywele, mapochi na shopping, nguo za kuacha miili wazi, hayo mambo kwa mwanaume yamepita kushoto. Na ni ya ziada tu.

8. Mheshimu yeye pamoja na familia yake, usidharau wadogo zake, dada zake na kaka zake, hana namna hao ndio ndugu zake na kimbilio alilo nalo, hata kama hawana hali nzuri.

9. Mambo madogo ila yana maana kubwa, mpigie simu, kamwe usisubiri yeye ndio akutafute. Mapenzi ni 'two way traffic'. 10. Jithamini wewe kwanza na yeye atakuthamini.

11. Kwa kuwa hana ukwasi leo, haimfanyi kuonekana ndio atakuwa na ukata milele, tizama sana ni nini kinamuendesha kichwani mwake. Tizama sana mawazo yake chanya na njaa ya kutafuta mafanikio. Ila kama yeye awaza ngono na pombe tu, hilo ni jipu uchungu.






No comments: