HESHIMU MUDA ANAOTENGA MWENZIO KWA AJILI YAKO







HESHIMU MUDA ANAOTENGA MWENZIO KWA AJILI YAKO

Nomophobia ni moja ya magonjwa ya akili ambayo yanasumbua watu wengi sana, matumizi ya simu yaliyopita kiasi na ambayo yamewaathiri watu wengi hadi kupata hofu ya kuwa mbali na simu zao za mkononi umekua ugonjwa mkubwa sana. Mahusiano mengi na ndoa nyingi zimevurugika, na nyingine hata kuvunjika kutokana na kukosekana muda wa kutosha wa kuwa faragha.

Simu za mkononi zimechukua nafasi kubwa sana na hata kupewa thamani kubwa sana zaidi ya hata binadamu anayekupikia na kukufanya ujisikie wewe ni binadamu. Hali hii imekua ikiwatesa watu wengi sana hasa ndani ya mahusiano na kuwafanya wajisikie vibaya na wengine hata kuwa depressed kwa kukosa bond ya kutosha na mwenzie na badala yake bond yote imehamia kwenye simu ya mkononi.

Kwa ufupi huo ni ukatili ambao unapelekea baadhi ya watendwa kutafuta mbinu za ziada za namna gani ya kukabiliana na ukatili huu, je wewe kwako unaichukuliaje hii??! Ushairikiana nae katika muda anaotenga kwa ajili yako?






No comments: