KAMA MUMEO NI DEREVA WA PIKIPIKI (BODA BODA) HII INAKUHUSU




KAMA MUMEO NI DEREVA WA PIKIPIKI (BODA BODA) HII INAKUHUSU

Dear Ladies
Hivi huwa mnakawaida ya kuwaandaa waume zenu kabla hajawasha bodaboda zao na kuelekea kijiweni au wanajiandaa wenyewe? Kama huwa hifanyi hivyo anza sasa.

Hawezekani abiria anapanda bodaboda ya mumeo anakutana na harafu mbaya kutoka kwa mumeo, wewe kama mke unajisikiaje mumeo kuwa katika mazingira hayo? Mbaya zaidi  ukute kavaa koti sasa au ndio ananyeshewa na mvua hadi linakaukia mwilini, hilo vundo... Ile ni ofisi kama ofisi nyengine, jitahidi umfulie mumeo, mpigie pasi vizuri awahi kijiweni. Na kama ana koti moja jitahidi kutumia nyama ya ulimi vizuri mwambie hubby hili koti moja halitoshi, ongeza lingine angalau uwe nayo mawili na hizi mvua zinazoemdelea itakuwa vizuri akiwa nayo mawili au matatu, sio mbaya hata wewe ukajibanabana ukamnunulia, ataona ni kwa namna gani unathamini kazi yake. Akivaa mojo, akiloa anajua mengine yapo nyumbani anaenda kubadili kisha unamfulia vizuri unaliandaa kuvaliwa wakati mwengime.

Sio vyema kumuacha mumeo avae nguo moja wiki nzima eti kwakuwa ni dereva wa bodaboda, mjali na kumpenda mumeo, onesha sapoti na mchango wako katika kazi anayofanya. Jitahidini kuwaweka smart waume zenu. Kumbuka, vile ambavyo wewe mkewe unamchukulia poa mumeo kuna mwenzako anatamani aletwe kwake na upepo wa kisulisuli ili ambadilishe awe smart.





No comments: