USIRUHUSU MAPENZI YAKUTESE






Kwa nini mapenzi yakuumize? Unakosea wapi, kwanini ukataliwe kila mara? Kwa nini umekuwa mtu wa kubadilisha wapenzi bila faida yoyote? Haya ni baadhi ya maswali ya kujiuliza kuhusu mateso ya mapenzi unayopitia.

Kamwe katika maisha yako usiruhusu mapenzi yakutese kiasi cha kukata tamaa katika maisha yako, najua yawezekana kila mpenzi unayempata haudumu naye, wewe ni mtu wa kulia kila siku, hujawahi kufurahia maisha hataa siku moja, jipange upya bado unanafasi.

Thamini na jali zaidi maisha yako kwanza, kwakuwa maisha yako ni bora kuliko mapenzi unayolilia, fikiria kipi ni bora kati ya mapenzi na maisha yako, ni kipi kilitangulia? Kama maisha ndiyo yalitangulia  kwa nini usijijenge kwanza kimaisha ndipo mengine yafuate?

Hata kama unateswa na mtu unayempenda kwa dhati, hata kama ni mzuri kushinda malaika, kwani bila yeye maisha hayaendi? Si kweli na kama unaweza kuishi bila yeye kwa nini akutese namna hiyo ikiwa alikukuta ukiwa unapumua kama kawaida? kwani bilal yeye hupati punzi?

Jiamini, wewe ni wathamini sana, wewe ni mtu muhimu wa watu wanaotambu umuhimu wako, kama yeye hakuona thamani yako yupo mtu anatambua umuhimu wako na bila shaka kuna siku atakuja na utafurahia maisha yako.

Ndugu yangu, hakuna kitu kinachouma kama mapenzi endapo utakosea kanauni zake, ukaruhusu moyo wote kuelekea huko, hakika yatakutesa.






No comments: