NJIA RAHISI ZA KUIDUMISHA NDOA YAKO





1. Mwambie mwenzako “Nakupenda”. neno lisikosekane katika ndoa yenu.

2. Daima uwe mwenye shukrani kwa mwenza wako.

3. Kuaminiana, kuungana mkono, kusaidiana na kuwa na mtazamo chanya juu ya mwenza wako.

4. Daima mridhie mwenza wako na umfanye ahisi kuwa ni mtu maalum.

5. Kamwe usifukue makaburi ya makosa yenu ya zamani. Fikiria kuhusu leo, usiendelee kulilia yaliyopita.

6. Mhamasishe na umpe matumaini mwenza wako katika jambo alifanyalo kwaali ya familia.

7. Pendeleeni kukaa pamoja kadiri inavyowezekana.
8. Msikilize mwenzako, usimkatishe anapoongea. Heshima bora kabisa kwa mwenzako ni kumsikiliza anapoongea, hata kama jambo analoongea hukubaliani nalo, MSIKILIZE.

9. Epuka mabishano. Sema “kumradhi” hata kama kosa sio lako. Nusu shari ni bora kuliko shari kamili, na usalama wa ndoa yako ni bora kuliko ushindani unaoutaka.

10. Daima iombee ndoa yako iwe imara na uhusiano wenu uwe madhubuti.






No comments: