Sumu yenye nikotini kali katika mapenzi ni uongo,





Sumu yenye nikotini kali katika mapenzi ni uongo,


 kama wewe ni mzuri wa kupiga porojo katika uhusiano wako, basi mapenzi ni lazima yakutese. Kwanini uwe muongo katika mapenzi? Kuna faida gani ya kuwa na wapenzi wengi? Kwanini mapenzi yanakuumiza?

Leo uko na huyu, kesho uko na yule, maisha hayo hadi lini rafiki yangu? Utaishia kuwadanganya wanawake hadi lini ndugu yangu na wewe mwanamke, utawapanga hao wanaume hadi lini? Unadhani kuwachuna hao mabwana ndiyo maisha yanaishia hapo? Tuachane na maisha ya kutangatanga na mapenzi, badala yake tuhangaikie maisha yetu.

Je, bado mapenzi yanakutesa? Umechelewa, kwani muda unaoupoteza katika kuhangaikia mapenzi, unatakiwa kuutumia kuwaza mambo ya muhimu ili mwisho upate maendeleo.

Kama una mpenzi au bado hujampata, basi vuta subira atakuja. Jambo moja la muhimu kuamini ni kuwa kila mmoja ana mwenza wake maishani, tatizo linakuja pale tunapoishiwa na uvumilivu na badala yake tunageuka watu wa kudandia na kubadilisha wapenzi kama nguo kila kukicha.

Kusema ukweli hayo siyo  maisha. Vuta subira, msubiri wako yuko njiani anakuja, na kama umeshampata, basi tulia naye huku mkipanga mikakati ya mafanikio kwenye ulimwengu huu uliojaa ushindani. Hivi sasa maisha ni magumu, inakuwaje unakubali mapenzi yakutese?






No comments: