PETE YA KIKE Sehemu Ya 1
MWANAUME MSAFI
Simulizi yetu inaanza rasmi katika mji ambao bado hatuja utambua vyema,.. Lakini ni katika mkoa wa tanga,... Ikiwa ninkatika bustani nzuri sana tena sana,.. Kwa namna moja ama nyingine, ni kwamba bustani hio imetunzwa vyema mpaka kufikia katika hali hio ya kupendeza,.. Alikuwapo malikia mmoja mdogo sana, ila cheo chake ni kikubwa kuliko wote walioweza kumfuata nyuma,.
Malikia huyo ni mzuri hakuna mfano, lakini sasa kumbe malikia huyo ana wafuasi wake ambao ni wasichana na wana uzuri kama wakwake, yaani kuanzia umri wako pamoja na sura hawakupishana kabisa, ispokua kwa cheo ni yeye peke yake,... Sasa kama kuna malikia basi hata mfalme wao yupo,...
Malikia alikaa katika kiti chake cha umalikia, nyuma ya kiti kumezungukwa na njiwa wengi sana haswa weupe peee,.. Kwani hata hawa viumbe waishio hapa, hakuna mweusi, bali wote ni weupe mithili ya wazungu lakini hawa hawakuwa wazungu,...
"nadhani mmekamilika"
Aliongea malikia huyo ambaye bado hatujajua jina lake na wafuasi wake..
"Yeeeeeeeee Murati Sabaha (ndio mkuu Sabaha)"
Waliitikia wale wasichana wapatao wanne kwa idadi ya uwingi wao, hivyo pamoja na malkia wao wanatimiza idadi ya viumbe watano
"shaimati (shamimu) na maimati (maimuna)... Nime waiteni hapa nina shida moja nanyi"
Aliongea malkia huyo huku wawili hao wakiitika
"yeeeeeee Murati sabaha"
"katika himaya yetu, tunahitaji KIJAKAZI kwa ajili ya kutunza mazingira yetu"
Sabaha aliongea hiyo lakini wengine walishtuka kwasababu kwa kawaida mazingira yao hujitunza wenyewe, sasa kwanini kuhitajike kiumbe kingine kwa ajili ya utunzaji?
"yeeeeeee Murati sabaha"
"shaimati na maimati, nawatumeni duniani mkaniletee kijakazi huyo"
Aliongea malikia huyo, akimaanisha anawatuma wawili hao kwenda duniani,.. Kwahio inavyo onekana hapo walipo sii dunia... Sasa haijulikani ni wapi hapo walipo...
"yeeeeeee Murati sabaha (ndio mkuu wetu sabaha)"
"ila, nahitaji kijakazi msafi"
Sasa sabaha alipo ongea hivyo, wale wasichana wote wakashtuka... Waliposikia anahitajika kijakazi msafi,
"Queen sabaha? Huyo kijakazi anahitajika wa kiume ama wa kike"
Aliuliza msichana mmoja kati ya wale wanaotumwa na mkuu wao
"nahitaji KIJAKAZI WA KIUME kwa niaba ya mazingira yetu"
"Queen sabaha, dunia ya sasa sii ya zamani... Kwa sasa kupata kijana msafi ni mtihani kwetu,... Sasa hakuna wasafi duniani"
Aliongea shaimati ambaye ni mmoja kati ya anaetumwa wakati huo maimati kakaa kimya,...
"wapo vijana wasafi wengi duniani... Nawapa siku saba, nahitaji kijana mmoja tu, na hio ni kazi nawatumeni mkaifanye"
Alimaliza malkia sabaha kisha akanyanyuka katika kiti chake, kisha akaingia katika jumba la kifahari ambalo ndilo limezungukwa na bustani nzuri iliopo katika eneo hilo..
Wasichana hao wanne wakiwa ndani wakiendelea kujadiliana kuhusu swala la Murati (mkuu) Sabaha kwenda duniani kutafuta kijana msafi
"shaimati, dunia ya sasa imekuwa chafu sana... Tutapata wapi kijana msafi kwa ajili ya mazingira ya himaya yetu"
Aliongea maimati huku shaimati akimjibu kuwa...
"hatuna budi kukubali agizo lake, ni vyema kutekeleza.... Hivyo usiku wa saa nane, tuianze safari yetu"
Aliongea shaimati, wakati huo Saudati na Suariti wapo kimya mana wao hawapo katika safari hio,...
Sababu ya Saudati na Suariti kuto jumuishwa na safari ya kwenda duniani, wao ni majini ambao hawana asili ya kibinadamu, hivyo wakienda duniani wao wanakua Invisible (hawaonekani)... Lakini hawa wawili Shaimati na maimati wao wana asili mbili, asili ya jini na ubinadamu na hawa wana familia zao huku huku waishio wao, na wazazi wao pia wana asili mbili... Sasa hawa saudati na Suariti wazazi wao ni asili moja tu ya ujini... Hivyo duniani hawato onekana, hususan kwa kazi hio inatakiwa waonekane...
Shaimati na maimati kwa majina ya upande wa kibinadamu wanaitwa MAIMUNA NA SHAMIMU (maimati na shaimati) haya majina ya Maimati na shaimati wamepewa wakiwa huku kwenye himaya yao japo wamezaliwa huku huku lakini bado wazazi wao wana asili mbili,... Na kila mmoja wao ana wazazi wake.... Ispokuwa sio wote kuwa wazazi wao wana asili mbili... Na hata Sabaha pia yeye hana asili mbili, na ndio maana akawatuma wale wenye asili mbili, mana yeye akienda hato onekana kama wengine, bali atakuwa upepo tu
SASA TUACHANE NA HUKO KWA MAJINI... TUJE HUKU DUNIANI
Alikuwepo msichana mmoja mzuri sana alieumbika, yaani mwili wake umegawanyika vizuri,.. Hii ni mkoani tanga katika mtaa uitwao UZUNGUNI, na hapo ni katika duka moja la nguo za Kiislamu alizokua akiuza msichana huyo mwenye umbo na uzuri wa kipekee,.. Mambo ya tanga hayo....
Kama unavyojua wasichana wengi wa tanga ni wao na mahijabu,.. Ukimkuta ndani na hicho kipande cha kanga, utafurahi mpaka upasuke, mlioishi tanga nadhani sio mageni kwenu,... Sasa wakati msichana huyo anapanga nguo, ghafla kuna gari ilisimama katika duka hilo... Alikuwa ni mwana mama mmoja ambaye ndio boss wa duka hilo...
"Faima Asalam Aleykh"
Alisalimia mwanamama huyo kan kwamba huyo msichana muuza nguo anaitwa faima au ukipenda muite (Fei)..
"waaleykh msalam mama karibu"
"ahsante, nimekuja kuangalia mzigo ulio isha"
"ok.. Hapa naona kanzu zimekwisha ipo pisi moja tu"
"ooohhh, aah mzigo umeenda enda kiasi"
"ndio mama, sasa kidogo biashara sio mbaya"
"ni kweli, sasa wacha kesho nielekee dubai kuleta mzigo"
"ni vyema, mana sio mpaka ziishe kabisa"
"sawa, wacha nikafanye utaratibu wa safari mapeema mno"
Aliongea mama huyo huku akipanda gari yake na kuondoka,... Huyo ndio boss wa faima au fei,...
Sasa tukija huku katika mtaa mwingine uitwao PONGWE, alionekana ostadhi mmoja aliovalia vyema kabisa kwa mavazi yalio mjulisha kuwa yeye ni ostadhi ama shekhe... Aliingia katika nyumba moja ya kizamani sana kana kwamba ndipo wanapo ishi katika jengo hilo,.. Tena linaonekana ni yale majengo ya kiserikali... Yale majengo ya mkoloni
"Asalam Aleykh baba"
Kijana huyo alimsalimu baba yake
"waaleykh msalam mwanangu hali yako"
"aahh swalama tu"
"mbona wasema Aah, kunani tena"
"baba? Tuyaache hayo mana ni masala ya kazi tu... Mama yuwapi"
"mamayo kaenda teka maji kisimani huko"
"wacha nikamsaidie basi"
Aliamka kijana huyo na kuvua kanzu yake kisha akachukua baadhi ya ndoo ambazo zipo tupu, kisha akaelekea kisimani ambako mama yake naye kaelekea huko... Alikua ni kijana mwenye kujielewa na kuijua thamani ya wazazi wake,... Inashangaza sana kuwa wapo vijana wasiojua thamani ya wazazi....
"suria? Haya nini kukuru kukuru na ndoo za maji"
Alikua ni mama yake suria, kana kwamba kijana huyu anaitwa suria...
"Asalam Aleykh mama"
"Waleykh msalam,.. Haya kwani wabeba ndoo kwenda kisimani"
"mama, kwani mimi sipaswi kukusaidia? Tena hio iwe ndoo ya mwisho wewe enda na ukae usirudi, kama ni mapima nitajaza mie"
Aliongea suria, ila kwa rafudhi ya tanga, mchanganyiko na Pemba hivi
"ni sawa lakini umeshachoka weye,.. Haya vipi kazi uliofuata huko yapo mafanikio"
Mama yake suria alimuuliza mtoto wake mana kwa sasa suria hana kazi kabisa toka amalize alimu yake ya chuo...
"mama we Enda tu takuja ongea nyumbani, lakini hali ya kazi bado mbaya mamy"
Suria aliposema hivyo mama alinyong'onyea sana, mana furaha yake ni mtoto wake apate kazi...... Basi mama aliendelea na safari yake ya kurudi nyumbani toka kisimani...
Ilipofika usiku mida ya saa mbili,.. Suria akiwa na baba yake toka msikiti kuswali,..
"baba, kuna mahali nilikwenda mchana, walinambia hawawezi kunilipa mshahara kutokana na elimu yangu"
Aliongea suria, huku baba yake akisikitika sana kwa taarifa hizo, mana suria ana elimu kubwa sana, kaomba kazi serikalini lakini bado hapati kwasababu ya elimu yake imebezi sana katika upande wa dini,.. Ila serikali humfanyia fitina kwasababu ana elimu ya juu, yaani suria amepiga kitabu vibaya mno,.. Elimu ya dunia humwambii kitu... Sasa hio elimu ya dini ndio kabisa usiseme,... Quran imejaa kichwani mpaka basi... Vyeti vyote anavyo lakini ana mwezi wa sita sasa hapati kazi...
"lakini suria mwanangu... Kwanini usiachane na taasisi za serikali... Hebu angalia kwenye makampuni binafsi"
"baba, huko ndio kabisa wanasema hawawezi nilipa kutokana na elimu yangu... Wanasema kutokana na elimu yangu napaswa kulipwa milioni nane mpaka kumi... Lakini wao hawana uwezo"
Aliongea suria na wakati huo walishafika nyumbani kwao... Wakiwa mezani wakivuta subra ya chakula cha usiku
"kwanini usingekubali tu kwa huo mshahara wao"
"niliwaambia kuwa nipo tayari kwa mshahara wao.. Lakini wakasema, siku serikali ya haki za kazi ikija kukagua mishahara ya wafanyakazi ikakuta wangu ni mdogo.. Watafunguliwa mashtaka... Hivyo hawawezi kunipa kazi"
"aahhhh, lakini Usijali baba, utapata kazi.. Muamini mwenyezi Mungu kwa kila jambo.. Na hakika hata ukikosa sema alhamdulilah"
Aliongea mzee huyo ambae yeye alikua akifanya kazi katika vituo vya reli hapo tanga,.. Na inasemekana ya kwamba mzee huyo alitakiwa kuwa tajiri mkubwa lakini pesa zake zote alimsomesha suria, sasa suria ana elimu ya juu lakini hapati kazi kutokana na figisu figisu za hapa na pale... Mama aliandaa chakula kisha akawa anatoka nje kwenda kumwaga maji machafu.... Lakini ghafla alimuona mtoto wake wa kike aitwaye ASHA
"heee asha mwanangu, ulikuwa wapi mpaka saa hizi weye"
"mama nilikua kwa rafiki zangu"
Aliongea asha huku akitaka kuingia ndani, lakini vazi aliovaa ni fupi mno kana kwamba hawezi kupita mbele ya baba na mdogo wake wa kiume
"hebu subiri kwanza... Hii nguo ni sahihi kuivaa asha... Mbona unantia aibu mwanangu, hebu muone mdogo wako alivyo.. Mbona havaagi suruali za ajabu"
Aliongea mama huyo wakati huo huku ndani baba na mtoto wanakula
"nyie si mmemsomesha suria,.. Sasa tutaona mtu aliosoma na ambae hajasoma nani wa muhimu... Yeye kasoma sana ndio mana hana tabia mbaya, mimi nimeishia kidato cha nne, ndio mana nina tabia mbaya"
Aliongea asha huku akitaka kuingia ndani,... Sasa hapo kuna vita kali kati ya asha na wazazi wake... Kana kwamba wazazi walizidi kumsomesha mtoto wa kiume sana tena kwa kumpenda mno huku wakiamini ya kwamba mtoto wa kike ni wa kuolewa tu...
"asha, hebu vaa hii kanga.. Baba yako yupo hapo ndani"
Mama alimvalisha mtoto wake kanga ili aweze kupita mbele ya baba yake
"Shikamoo baba"
Asha alimsalimia baba yake huku akipita
"marahaba mama.. Haya saa hizi saa tatu kasoro hii ulikua wapi"
"nilikua kwa rafiki zangu"
"saa hizi.. Rafiki zako wametulia kwao wewe umewafuata"
"ndio, sasa nitakaa na nani"
Aliongea asha huku suria akidakia
"dada asha, hayo sii majibu ya kumjibu baba... Hebu kuwa na heshima kwa nyakati zingine dada"
"we nawe sijaongea na wewe.... Siongei na watu wa vuo vikuu mimi"
Aliongea asha kitu kilichomfanya suria kukaa kimya mana hawezi kubishana na dada yake....
"basi mama nenda ndani tu"
Aliongea baba lakini ni kishingo upande tu...
Ilipofika usiku wa saa nane, kandokando ya bahari walionekana wasichana wawili warembo sana wakiwa na mikia ya samaki, yaani mithili ya nguva,.. Lakini walipopigwa na hewa ya duniani, ile hali ya unguva iliwatoka na kuwa na miguu ya kawaida,.. Kwa kawaida majini hutoka saa saba za mchana lakini sio wote wenye uwezo huo... Wale wanaotoka mchana ni wale wenye asili moja tu,... Ila hawa wenye asili mbili wao hutoka muda wowote, iwe mchana au usiku... Ni maamuzi yao wenyewe... Ila kwa hawa wameamua kutoka usiku... Ni sekunde chache kutoka baharini mpaka barabarani wakiwa wamevalia nguo nyeupe mithili ya malaika, ila hawa ni majini wema, mana kuna majini wabaya na wazuri, sasa hawa ni wale wazuri..
"shaimati, naskia sauti za miziki usiku huu... Kweli kutakua na wasafi kweli??"
Aliongea maimati ambaye ni maimuna, (muna)...
"Afadhali waliopo katika muziki... Ona wale wasichana... Wamevalia mavazi ya aina gani... Ile si nguo ya ndani kabisa ile"
"haaaaaaa Kiukweli haifai hata kuangalia... Shaimati, mimi naona turudi tulipotoka... Wacha tukamweleze Murati sabaha kuwa katika dunia ya sasa hakuna wasafi"
Itaendelea...............
No comments: