PETE YA KIKE Sehemu Ya 2
Kwa kawaida majini hutoka saa saba za mchana lakini sio wote wenye uwezo huo... Wale wanaotoka mchana ni wale wenye asili moja tu,... Ila hawa wenye asili mbili wao hutoka muda wowote, iwe mchana au usiku... Ni maamuzi yao wenyewe... Ila kwa hawa wameamua kutoka usiku... Ni sekunde chache kutoka baharini mpaka barabarani wakiwa wamevalia nguo nyeupe mithili ya malaika, ila hawa ni majini wema, mana kuna majini wabaya na wazuri, sasa hawa ni wale wazuri..
"shaimati, naskia sauti za miziki usiku huu... Kweli kutakua na wasafi kweli??"
Aliongea maimati ambaye ni maimuna, (muna)...
"Afadhali waliopo katika muziki... Ona wale wasichana... Wamevalia mavazi ya aina gani... Ile si nguo ya ndani kabisa ile"
"haaaaaaa Kiukweli haifai hata kuangalia... Shaimati, mimi naona turudi tulipotoka... Wacha tukamweleze Murati sabaha kuwa katika dunia ya sasa hakuna wasafi"
ENDELEA.........
Katika dunia hii kuna viumbe wengi sana ambao wengine hawana asili ya binadamu,.. Lakini katika simulizi hii inaelezea viumbe aina ya majini, lakini wanaoelezewa hapa ni wale majini wa baharini, sio majini wote wa baharini ni wazuri, ila hapa tutaelezea wale wazuri, mana wabaya ndio hao mashetani.. Hivyo hapa hatuelezei mashetani... Mana simulizi ilio elezea mashetani tayari ilishatoka inaitwa THE MEAT OF MY MOTHER, hivyo hapa tunaelezea wale majini wema, wazuri, wanaopenda kusaidia watu...
Murati sabaha ni jini mkuu katika himaya yake, sio kuwa bahari nzima ni yeye mwenyewe, lahasha, bali zipo himaya nyingi ndani ya bahari.. Mfano ni kama tukisema Jiji la Dar es Salaam ndio kama mfano wa bahari nzima,... Sasa himaya zipo nyingi mfano wa Majimbo au kata vitongoji vya jiji hilo au bahari hio...
Sasa katika himaya nyingine ndani ya bahari, wanamiliki binadamu ambao wameamua kuwasaidia kwa kuwapa kazi za kutunza bustani, Sasa Murati sabaha na yeye anataka KIJAKAZI WA KIUME kwa ajili ya kutunza bustani iliopo kwenye himaya yake au jimbo lake... Wanaotakiwa kuja huku Haijalishi jinsia, awe wa kike au wa kiume, kikubwa awe msafi,
Je unajua usafi huo ni upi??.. Haimaanishi msafi wa nguo, au msafi wa roho... Au msafi wa kuoga kila mara.. Bali anahitajika msafi ambaye toka kuzaliwa kwake hajawahi kufanya mapenzi,.. Na hahitajiki mtoto, bali ni kuanzia umri wa miaka 20 kwenda mbele, ilihali ule umri wa balehe umeshapita bila ya mhusika kutamani mapenzi... Hivyo wakisema neno msafi.. Yaani ambaye hajawahi kufanya mapenzi, huyo ndio msafi....
Murati sabaha baada ya kupata wazo la kuhitaji kijana wa kazi,.. Aliwatuma wafuasi wake ambao wana asili mbili katika mili yao,... Shaimati na maimati, hayo ni majina yao ya upande wa baharini, ila huku dunia wanaitwa Shamimu na Maimuna,... Wao wana uwezo wa kuonekana au wasionekane, ila Murati sabaha na wale wengine waliobaki, wakija duniani hawaonekani kwasababu asili yao ni moja.... Hivyo kawatuma maimuna na shamimu wamtafutie mfanyakazi wa kutunza bustani yao..
Saa nane za usiku shaimati na maimati wanafika katikati ya mkoa wa tanga,... Kitu cha kwanza walisikia sauti za muziki ukilindima katima katika tundu za masikio yao
"Afadhali waliopo katika muziki... Ona wale wasichana... Wamevalia mavazi ya aina gani... Ile si nguo ya ndani kabisa ile"
"haaaaaaa Kiukweli haifai hata kuangalia... Shaimati, mimi naona turudi tulipotoka... Wacha tukamweleze Murati sabaha kuwa katika dunia ya sasa hakuna wasafi"
Aliongea maimuna au maimati kuwa ni bora warudi kule walipotoka, kwasababu hali walio ikuta hawawezi kupata binadamu alie msafi,...
"hapana muna,... Ukumbuke kuwa Murati sabaha tulimweleza ya kuwa, kwa dunia ya sasa hatuwezi kupata binadamu msafi tofauti na watoto chini ya miaka kumi... Lakini alikataa na kudai kuwa wapo wengi sana.. Hivyo kwa mimi kurudi ni ngumu maimati"
Aliongea shaimati kumsihi maimati asirudi walipo toka,.. Kwani watagombezwa na mkuu wao ambae kawatuma kuja kutafuta kijana msafi
"lakini shaimati, wewe unaonaje hii hali? Na ukumbuke tumepewa siku saba tu ndani ya dunia hii"
"ni vyema tumalize siku saba turudi tukiwa hatuna, kuliko leo leo turudi"
"sawa, nimekuelewa... Sasa haya mavazi meupe vipi"
"ni lazima tupate nguo za kibinadamu"
Majini hao walishauriana juu ya upatikanaji wa nguo na kupata muafaka juu ya hilo...
*************************************
Tukija huku kwa akina surian au suria akiwa na mpenzi wake... Sasa hapa inashangaza kisogo kwani hapa yupo na mpenzi wake tena walikuwa wakilifaidi tunda la msimu wa siku hio... Ila usiku wa jana kabla ya kulala kwake alikuwa kwao na familia yake, lakini usiku anaonekana yeye na mpenzi wake,... Ila sauti ilikuwa ni ya suria pekee...
Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, mzee Rashidi ambaye ni baba yake suria ama sua, alifika katika chumba alicholala suria kwa niaba ya kumwamsha ili waelekee msikiti kufanya ibada ya Subuh...
"suriaaa"
Aliita mzee Rashidi huku akigonga mlango
"naam baba"
"swalaaa swalaaa swalaaa"
Mzee Rashidi alimwamsha kwa maneno hayo ambayo hutaamkwa kwa nyakati za swala ya asubuhi... Basi suria aliweza kukurupuka, lakini ghafla anaanza kukasirika bila sababu... Aliusogelea mlango na kuufungua bila wasiwasi wa mzee kumwona mwanamke aliekuwa naye usiku wa leo....
"haya twende basi... Mana unatakiwa uka adhini wewe"
Aliongea mzee Rashidi akiwa na maana ya kuwa, suria ndio mpiga adhana wa siku hio.... Lakini suria hakutaka kumficha baba yake....
"Assalam Aleykh baba?"
"waalekh msalam,.. Vipi kheri?"
"aahhh baba, sii kheri sana"
Suria alijibu kuwa hakuna usalama sana....
"nini tena"
"jana nilipitiwa na usingizi hadi kusahau kusoma dua ya kulalia"
Aliongea suria huku mzee wake akiwa kasimama nje ya mlango wa chumba cha suria...
Sasa baba yake kuskia hivyo tu, akajua suria kuna jambo limemkuta usiku wa leo
"basi we kakoge utanikuta nje hapa"
"kwanini usitangulie baba.. Mana nataka zifua nguo hizi.. Mana dada aisha akijua atancheka kweli yule"
"sawa pia.. Mimi nitakusubiri baba.. Wewe enda kakoge kisha nikute nje"
Aliongea mzee Rashidi, huku akitoka nje,... Hawa wanaongea rafudhi ya pemba hivi.. Hivyo hio Enda kakoge ni rafudhi yao... Basi mzee Rashidi alitoka nje na kuanza kushika udhu (kujisafisha ili aweze kuswali)... Wakati huo suria aliingia bafuni na kuvua nguo zile ambazo alilalia leo..
"daahh uyu mwehu leo kaniweza kweli huyu... Yapata mwezi wa sita sasa hajaja.. Kaona nimejisahau tu usiku kaja..."
Aliongea suria huku akifua nguo hizo ambazo amezichafua baada ya ndoto ya usiku akiwa na mpenzi wake,... Na hio ni mbinu ya jini mahaba ambaye tabia yake ni kuchafulia watu bila sababu....
Jini mahaba ni mmoja wa majini ambao ndio mashetani, wao hawana jema nawe binadamu... Na jini mahaba hua anawafuata wale wanaume ambao hawana wapenzi, au wana muda mrefu bila kufanya mapenzi, na hata hawa jini mahaba wao pia hawataki mwanamume mchafu ambae ana zini kila wakati.. Na hua hawataki zile mbegu zinazo mtoka mwanaume... Mana kwao ni uchafu, hivyo anamfuata mwanaume na kuanza kufanya nae tendo la ngono, sasa pale mwanaume anapokaribia kufika mshindo, huyu jini mahaba yeye hujitoa ili zile mbegu za kiume zisimguse... Hivyo shida yake ni kukuchafua wewe na sio yeye.. Na ndio maana hataki uchafu wako,... Uchafu ubaki nao mwenyewe, kama ni raha keshapata sasa wewe jichafue mwenyewe.... Ndio asubuhi unajikuta tayari umeshaloa... Na pia wapo majini mahaba wa kiume ambao huwafuata wanawake,.. Ila kwa wanawake sio sana... Ila majini mahaba wa kike, hupenda kuwafuata wanaume wasio na wapenzi au wenye muda mrefu bila kufanya mapenzi....
Saa moja za asubuhi, suria na baba yake wana tabia ya kufanya mazoezi baada ya ibada ya asubuhi... Hukimbia kilometa kadhaa kwa ajili ya kuilinda miili yao, na hio ni faida moja wapo ya kidunia kwa wale wanaoswali swala za asubuhi... Wakati huo wanaingia nyumbani ili waweze kuoga....
Ilipofika saa tatu wakiwa mezani wanapata chai,... Wakati huo suria kaweka vyeti vyake mbalimbali katika meza... Mzee Rashidi akiangalia hivyo vyeti, anajua hio ndio pesa yake iliipotea miaka yote hip... Unaambiwa mzee huyo alimuwekezea sana mtoto huyo aweze kusoma kwa bidii kwani ndie mwokozi wao,... Na kweli kamsomesha suria vizuri sana, ila ukubwa wa elimu yake unamkosesha kazi katika baadhi ya kampuni binafsi, kwani akienda serikalini anaambiwa aambatanishe vyeti vyake na karatasi inayo muonyesha uzoefu wa kufanya kazi kwa miaka mitatu... Sasa mwanafunzi katoka shule mwaka huu, je huo uzoefu wa miaka mitatu kautolea wapi... Hicho ni kikwazo ambacho anakutana nacho suria katika ngazi za serikali.... Na huko binafsi wanamwambia, kwa ukubwa wa elimu yake hawawezi kumlipa...
"sasa mwanangu... Mimi nikushauri jambo moja kama utalikubali"
Aliongea mzee Rashidi, mana suria akimaliza kunywa chai anaondoka zake kwenda kutafuta kazi...
"ushauri gani baba..."
"kwanini usitafute kazi ya ualimu tu..."
Aliongea baba yake suria,
"baba,... Yaani elimu nilio nayo, kila sekta hawaitaki... Nilikwenda katika shule moka kubwa hapa mkoani Tanga,... Tena ni shule ya sekondari ya mtu binafsi,.. Shule kubwa sana katika mkoa huu... Lakini mkuu wa shule hio alipo ona vyeti vyangu.. Alinuna hapo hapo... Nilipotoka ofisini kwake, nikakutana na head master... Akaniuliza kama nimefanikiwa... Mana yeye ndie alienielekeza kwa mkuu wa shule hio.. Nikamwambia kuwa mkuu nimemwonyesha vyeti vyangu lakini hakunijibu zaidi ya kuniambia hakuna nafasi.... Yule head master akaniambia, nafasi zipo lakini elimu yangu ni kubwa kumzidi yeye.. Hivyo naweza kumpindua katika kiti chake"
Aliongea suria kama kumpa stori baba yake aliotaka akaombe kazi ya ualimu,...
"daaaahh pole sana mwanangu... Ila mimi nilikua na maana uende kufundisha shule za dini"
Aliongea mzee huyo akimaanisha kua suria akaombe kazi ya ualimu wa shule za Kiislamu, akafundishe somo la ISLAMIC KNOWLEDGE, na hilo ni somo la kiislamu na ni shule ya sekondari inayofundisha masomo yote lakini ni shule ya Kiislamu... Ila hata za kawaida zipo ila mpaka uongozi uamue kuweka somo hilo..
"labda nijaribu huko kama nitapata"
"ah ah, usiseme kama... Sema kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu nitapata"
"sawa baba"
"ila, kama unakwenda huko... Punguza hivi vyeti.. Nenda na vyeti husika.. Hivyo vingine acha"
Aliongea mzew Rashidi, mana suria ana vyeti vingi... Yaani kasoma vyuo vingi sana na kila chuo ana cheti chake alicho somea jambo fulani,..
"sawa baba"
Sasa ikiwa ni nyakati za saa nne asubuhi, katika duka la nguo za jinsia zote.. Waliingia wale wasichana wawili ambao wametokea katika dunia nyingine ya chini ya maji.. Na duka walilo ingia ni duka ambalo anauza Faima...
"karibuni, karibuni"
Faima alikuwa mkarimu kwa wateja wake, japo walikuwa wamevalia mavazi meupe peee...
"nipatie hijabu lile pale"
"lile jeusi"
"ndio"
Aliongea maimati huku faima akitungua hijabu hilo na kumkabidhi maimati... Papo hapo na shaimati nae akaagiza hijabu lake lenye rangi ya ugoro ugoro hivi...
Walielekezwa mahali pa kubadilisha nguo mana wamedai kuzivaa kwa nyakati hizo... Faima hana wazo lolote kuwa wasichana hao ni majini,.. Shaimati na maimati walilipa bidhaa zile kisha wakaondoka... Faima alishangaa sana pesa zao kuwa mpya kuliko mpya za benki... Ila aliona ni wateja tu....
"maimati..."
"yeeeeeee"
"toka jana usiku tuingie duniani,.. Kwa mara ya kwanza nimeona msichana msafi"
Aliongea shaimati kuwa leo kaona msichana msafi....
"shaimati... Nadhani sisi tumetumwa mvulana, sasa wasichana wanini? ... Najua yule msichana alietuuzia hizi nguo ni msafi.. Lakini sifuatilii hilo"
Aliongea maimati huku wakiendelea kutembea kwa hatua kubwa kubwa,..
"sawa, lakini niliongelea tu"
Shaimati alikubali huku maimati akisema kuwa
"sasa hapa mimi naona tujibague... Kila mmoja apite njia yake"
Aliongea maimati huku wakilifanya jambo hilo, yaani majini wakijadili jambo, ni wakati huo huo linafanyika..
Shaimati na maimati kila mmoja na njia yake,... Na wao hawana uwezo wa kugundua moja kwa moja kuwa mtu huyu ni msafi,... Ila ugunduzi wao wana uwezo wa kuongea na kiumbe kiitwacho QARENA, kiumbe hiki huzaliwa na kila binadamu... Na kiumbe hiki sio salama sana katika maisha ya binadamu... Na hakuna binadamu anaweza kuongea naye, ispokuwa viumbe ndivyo vinaweza kuongea na QARENA, ambaye ni pacha wa binadamu.... Huyu kiumbe kazi yake ni kitoa taarifa za binadamu kwa viumbe wengine au wanadamu wenye upeo wa kweli kama vile waganga wa kienyeji wale wa kweli,.. Watu wenye majini marohani pale majini yanapo wapanda watu.. Ndipo mtu huyo ana uwezo wa kuongea na QARENA,... Sasa majini hawa wanapata taarifa za mtu kupitia QARENA, na QARENA ndio kazi yake kitoa umbea wa binadamu, ila kama binadamu hajui kitu, basi hata QARENA pia hajui, hivyo wewe ukijua tu unakwenda kukojoa basi hata QARENA anajua unakwenda kukojoa....
Wakati huo suria yupo mbio mbio kwenda katika shule moja ya Kiislamu ambayo baba yake kamwelekeza akajaribu hapo kama ataweza kupata kazi,.. Hivyo alikuwa ana haraka mno,...
Sasa huku kwa shaimati, ukumbuke wamegawana njia, kila mmoja apite njia yake ili kuweza kupata kile walicho tumwa... Mana majini ndio wanatumwa ila binadamu huagizwa..
Shaimati alikutana na dada yake suria akiwa kavalia vazi la kanga moja, sasa shaimati yeye anajali sana wasichana wenzake... Vazi hilo la kanga moja lilimfanya aisha awatoe wanaume udenda, kwani vazi hilo lilikuwa likionyesha dhahiri vazi la ndani (chupi)... Hivyo vidume macho kwa aisha ambaye ni dada yake na suria,... Na nyakati hizo alikuwa akitoka sokoni... Shaimati alikuwa hana kitenge lakini ghafla tu kaonekana kashika kitenge na kumvisha aisha... Lakini aisha hakujua kama kavishwa kitenge, ila akijiangalia anahisi kuwa na ile ile kanga moja.... Shaimati hio kazi yake, anapenda sana kujali wanawake wenzie... Hivyo aliendelea na kazi iliomleta duniani.... Unajua mwanamke anafanyaga makusudi kuvaa nguo fulani,.. Na anajua lazima wanaume wampigie mbinja na wengine kumuita wengine kumsifia kutokana na muonekano wake.. Sasa alifika mahali alishangaa mbona sifa alizokuwa akipewa awali sasa hazipo.. Na alikuwa kila kipishana na mwanaume lazima ageuke, lakini sasa hivi hakuna anaemuangalia... Chezea kitenge wewe... Sasa alipofika nyumbani alishangaa kupewa sifa na mama yake...
"heeeee, aisha mwanangu... Kweli mungu mkubwa, siamini ulivyotoka na jinsi unavyorudi"
"una maana gani mama"
"kile kikanga ulicho toka nacho.. Kiukweli sikukipenda kabisa... Lakini nimefurahi umevalia kitenge kwa juu"
Aliongea mama yake aisha lakini aisha akijiangalia, anajiona ana kile kikanga ila watu wanaomuangalia wanaona bonge la kitenge tena kipyaa... Aisha hajaelewa kabisa mama yake ana maanisha nini, hivyo walikua ni watu wasio elewana
Sasa huku dukani kwa faima,.. Kumbe shaimati karudi huku dukani tena, yaani hana mzuka wa kutafuta KIJAKAZI WA KIUME, bali kafurahi sana kwa kuona msichana ambaye hajawahi kuguswa kwa namna yeyote ya kimapenzi,..
"ooohh karubu tena"
Faima alimkaribisha shaimati kana kwamba labda kapenda kuja kuongeza nguo nyingine, kumbe yeye ndio kapendwa kwa usafi wake...
"usijali,... Kiukweli wewe ni mrembo sana"
Aliongea shaimati huku faima akisema
"ni kweli ila sijakuzidi wewe"
"mmmhh urembo wangu ukiujua, hutokula siku nzima"
Aliongea shaimati akimaanisha kuwa akimweleza jinsi alivyo uhalisia wake, basi hatokula siku nzima...
"kwanini nisile siku nzima"
"ah tuachane na hayo.. Vipi umeolewa wewe"
Shaimati alimuuliza swali hilo ilihali anajua faima ni bikra...
"ndio, nimeolewa na nina mtoto mmoja"
alijibu faima, huku shaimati akicheka na kusema kuwa
"inaonekana unapenda kuolewa sana"
"nimekwambia nimesha olewa na nina mtoto"
"ila uaijli, hivyo vyote vina wakati wake... Utaolewa na utapata mtoto"
Aliongea shaimati, lakini faima alishtuka mana anamdanganya mtu, wakati mtu mwenyewe anajua ukweli wake....
"sawa Nashukuru kwa ushauri wako dada"
faima alishukuru kwa kupewa ushauri
"ila nimependa kwa jinsi ulivyo jitunza... Hebu niambie, umewezaje hadi kufikia miaka 21 bila kujichafua"
Aliongea shaimati na kumfanya faima azidi kushtuka... Yaani mpaka miaka yake kaitaja...
"umejuaje kuwa nina miaka 21 na nani kakwambia mimi nina bikra"
"usijali faima... Sisi ni sote ni wanawake hujuana sana jinsi tulivyo"
"na jina langu nani kakuambia ingali ndio mara ya kwanza nakuona"
Aliuliza faima ila hapo hofu ilianza kumjia... Mana mtu anajua siri zake zote
"alafu kumbe una mchumba, mbona sioni pete ya uchumba"
Yaani shaimati yeye hapendi kujibu maswali, wewe ukiuliza na yeye anauliza, hio ndio tabia ya majini, wao kutoa majibu ni ngumu ila wao wanataka majibu pale wanapo uliza
"ndio, ninae... Na huyo ndio atanioa"
"na yeye pia hajawahi kama wewe"
"ndio,.. Tuko sawa na yeye pia hawajawahi kufanya mapenzi"
Sasa shaimati kuskia hivyo, alishtuka na kumuuliza faima kuwa
"yuko wapi huyo mwanaume msafi... Anaishi wapi na anaitwa nani"
Sasa tukija huku kwa suria, akiwa katika harakati zake za kwenda shuleni tena kwa kutumia usafiri baiskeli aina ya sehewa,... Mbele ya kitenga cha baiskeli kaweka vyeti vyake... Alikuwa na haraka mno... Sasa alifika kwenye kona fulani almanusura amgonge dada mmoja kwa haraka zake...
"ooohhh samahani dada yangu... Kwanza Assalam Aleykhum"
Suria alimsalimia mdada huyo ambaye kavaa baibui au hijabu, wengine huita nikabu.. Japo kilabu ni kile kininja...
"waaleykh msalam, haya mbona wataka nigonga na usafiri wako"
Aliongea dada huyo huku suria akiomba radhi
"niwie radhi dada yangu... Nipo katika upesi kuwahi mambo yangu"
Aliongea suria, kisha dada huyo akasema kuwa
"sawa kaka... Unaweza kwenda"
Aliongea dada huyo, lakini suria alisisimkwa na nywele zake, ikiwa na maana kuwa aliopishana nae sio binadamu wa kawaida....
lakini sasa kumbe huyu dada ndio maimati mwenyewe, mmoja wa wale majini waliokuja duniani kutafuta MWANAUME MSAFI
Itaendelea...............
No comments: