Riway::: CHOZI LISILOSAHAULIKA SEHEMU YA 08
¶Ilipoishia sehemi ya 07¶
Nyamizi aliondoka kuelekea porini ili akachukue kuni ambazo zitasaidia katika swala zima la upishi. Bila kufahamu kuwa huko aendeko kuna nini ambacho kinamsubiria kimkute, alitembea harakaharaka kutokana na muda uliopo ni mchache. Mzee Chepi na Makasi walikuwa tayari baada ya kuficha sura zao ambazo hazikuweza kuonekana. Nyamizi alipofika akakuta kuna kundi la kuni ambazo zimekatwa tayari lakini hapajlkuonekana mtu yeyote ambae yupo karibu. Alianza kuweka kamba yake huku akizipanga taratibu zile kuni, ghafla alishtukia akikamatwa na mtu asiyemfahamu akitahamaki tayari kacjomwa kisu mkononi na damu yake akishuhudia ikiwa inakingwa. Maumivu aliyoyapata aliyajua yeye mwenyewe. Maamuzi aliyoyachukua akaweka kamba juu ya mti na kutaka kujinyonga baada ya kuandamwa sana, ghafla sauti ilitokea ambayo ilimsihi kutofanya swala hilo...
¶ Endelea ¶
Nyamizi alisita kuendelea na swala lake la kutaka kujitundika kwenye Kamba hiyo akabaki kuduwaa huku chozi likimtoka kwa huzuni kubwa sana, 'Nyamiziiiiii, Nyamiziiiii hapana usikate tamaaa klbado muda wa kukata tamaa kumbuka maisha ya watu wengi umeyabeba wewe kwenye mikono yako usichukue maamuzi hayo....' Sauti hiyo ilipotea masikioni mwa Nyamizi, alijitoa kwenye kamba ilealiangalia huku na kule ili aweze kuona ni nani ambae anamuona au kama ataweza kuona yule mtu ambae alimueleza jambo lile 'Naniiii kama kweli upo jitokeze kutetea haki zetu, tunanyanyaswa kisa ni sisi ni wanawake kuna faida gani mimi kuishi kunafaida ganiiiii' Nyamizi aliongea kwa jazba kubwa sana kiasi kwamba ile sauti ilirejea kwa hali nyingine. Ghafla radi na wingu ziyo liliotanda kijiji kizima radi za hatari zilirindima kila mahali, Nyamizi ilimfanya aendelee kuogopa kabisa pale alipo Sauti hiyo ilirejea kwa mara ya pili 'Nyamiziiiiii, Nyamiziiiiii haupaswi kukata tamaaa inapaswa upambane uonyeshe kuwa si kama wanavyokudhania nafasi yako iko palepale pambana uipate'. Kutokana na hali ya hewa hiyo Nyamizi ilimbidi aanze kukimbia kuelekea nyumbani huku akitokwa na jasho jingi lililoambatana na Machozi mengi sana. Kwenye mwilo wake.
Kutokana na mbio ambazb alikuwa nazo alisahau kama mkono wake kama aliumia baada ya maumivu yake kuondoka kabisa, alifika nyumbani na hali ya hewa ikarudi kama kawaida, 'Mama mama kuna mtu kuna mtu kuleee' Nyamizi alianza kuweweseka ovyo baada ya kupatwa na tatizo lile mama yake alimtuliza kwanza aweze kumueleza vyema kuhusu swala hilo 'Nyamizi, Nyamizi mama ebu tulia kwanza haya nieleze kuni ziko wapi na nini mbona kama ulikuwa unafukuzwa mama eeeh!' Mama nyamizi aliweza kumtuliza Mwanae wa pekee aliyempenda sana. 'Mama nimefika polini nikakamatwa na watu nisiowajua wakanikata kwa kunichoma kisu hapa..' Alipinda nguo ya mkono wake kweli kulikuwa na damu zimezunguka mkono huo lakini hapakuwa na hata jeraha kabisa. Nyamizi alihangaika kutafuta kidonda kipo wapi hatimae baada ya kufurahi kupona anaanza kusikitika kwa kuhoji wapi kidonda kimekwenda ' Mama mamaaa kidonda changu wapi haaaa' 'Nyamizi siku hizi mwanangu baada ya kufanyiwa yale na kaka yako unaanza kuchanganyikiwa damu tunaziona sasa hiko kidonda wapi?'. Hapakupatikana jawabu zaidi ya Nyamizi kulia huku akimkumbatia mama yake
Mzee Chepi na Makasi baada ya kufanikiwa Kupata damu ya Nyamizi, walifurahi sana kwani tayari watakuwa wamemaliza nyodo zake. Katika tembea yao mbele yao aliweza kutokea Masha akiongozana na vijana mashujaa wawili, Ndipo Chepi akamsimamisha Makasi na kuanza kumueleza jambo ' Eheee! Makasi unamuona yule kijana?' 'Yupo huyo' Aliuliza Makasi 'Yule ni Masha aliyefanikiwa kumnyang'anya dada yake fimbo ya ufalme na leo ana tawazwa baadae katika mto wa Mwenda pole' Aliongea Chepi. 'Ahaaa! Kwa hiyo tunafanyaje?' Chepi alikuna kichwa kwanza ' Nimekumbuka huyu kagombana na dada yake na mama yake kamfukuza kwao, Sasa tukifanikisha tunamharibia kwa kumsingizia kesi ya kutaka kumuua dada yake'. Hiyo ilikuwa ni mipango ambayo ilipangwa vyema na wawili hao. Walitembea hatimae wanakutana 'Salam mueshimiwa Mfalmeeeeee' walimsalimu kwa adabu zote, Masha akaitikia kisha wakainuka 'Yani masha wewe ni kijana hodari sana na makini katika kufanya uongozi wako' Aliongea Chepi. ''Yani mwaya hajakosea kabisa kukutabiria wewe kuliko mama yako anamtabiria mwanamke tangu lini Sikio likaongoza kichwa?' Walicheka sana na ndipo Masha akajiona mtu mwema sana muda huo.
Waliachana huku wakimpaka Masha mafuta kwa mgongo wa chupa. Walimueleza maneno ya unafiki kabisa yasiyo na ukweli wowote ule ndani yake. Walichapa mwendo qa haraka hatimae walifika kwa mzee Njimbi, walitulia kidogo baada ya kumuona mzee huyo akiwa anamalizia kazi fulani. Wakiwa wametulia pale walianza kujadilo juu ya swala lao linalowakabili 'Chepi hivi baada ya kutoka pale ujue kulikuwa na wingu kubwa sana, yani lilitishia kijiji chote wewe si uliona kabisa pale.' ' Ndio ila ile ni kawaida tu bwana hakuna dalili yeyote pale.' Muda mchache waliombwa kuingia ndani na mzee Njimbi. 'Haya nadhani mtakuwa mmebeba Damu ya Nyamizi naombeni' walitoa kifaa wlichohifadhia na kumpatia Mzee Njimbi. Aliitazama damu hiyo kisha akavuta kumbukumbu baada ya kuinusa. Akachukua dawa kisha ikawa tayari kwenye hatua ya mwisho ' haya jamani, hapa nikichanganya hii dawa hapa namaliza kila kitu mko tayari?' Waliangaliana kisha wakaulizana. ' Njimbi hatujaelewa hapo unamaliza kila kitu kivipi' Alicheka sana Njimbi ' Yaani Nammaliza kabisa Nyamizi anakata kabisa tamaa ya kuishi na anaitoa kauli yake mbaya na hatari kwa kijiji, baada ya hapo kazi ya kumnyamazisha Masha ni ndogo tu' Walikubaliana. Mzee Njimbi akamalizia kazi vyema, aliwaambia kuwa sasa mambo safi itabidi wao waoge maji yaliyochanganywa damu hiyo ili waondoe mikosi lakini sharti waoge nja panda.
Upande wa Mzee Mwaya tayari akiwa anajivunia kusubiri jioni sana amtawaze rasmi kuwa Mfalme wa Mwenda pole. Akiwa kajipumzisha mkewe alimjia pale alipo. 'Mume wangu hivi kwa nini mnatuonea sisi wanawake?' Swali hilo lilimtoa kwenye dimbi la usingizi Mzee Mwaya. 'Pumbavuu yani wewe mwanamke unathubutu kutoa nyayo zako kule jikoni kuja kuniuliza kwa nini tunawaonea? Hivi unaweza kunieleza yapi tunawaonea?' Mwanamke huyo alihisi kuwa kakosea alimuomba msamaha mumewe 'pumbavu wewe ni mwanamke basi sisi ndio tunapaswa kufanya mambo yote nyinyi ni kuambiwa. Hakuishia hapo alimpiga vya kutosha kisha akamkanya tabia ya kuhoji mambo yasiyomhusu kabisa. Alikaa tena na hatimae usingizi ulimkuta kabisa. Akiwa katika usingizi alihisi kama yuko kwenye kifungo cha Maswali mengi sana asiyoweza kuyajibu "Mwaya kwa nini unatenda unyama kwa mwanamke? Kwa nini hautumii madaraka yako kumlinda Mwanamke? Kwa nini unatetea nafsi isiyo yakweli ukalazimisha na kuacha nafsi halali ikiteseka? Kumbuka CHOZI MNALOLIANDAA HALITOSAHAULIKA maishani mwenu". Mwaya alikurupuka toka usingizini 'Eeeeheeeehhhhhh Ehhhh Aaaah'. Alihema kwa hofu kubwa sana. Mkewe alikuwepo karibu alishindwa kumuendea baada ya kuadhibiwa makofi na Mwaya. Akabaki kumuangalia.
Mwaya alitoka na kuchukua mkongojo wake, bila kusahau Tumbaku yake ' Mh hizi ni ndoto gani za ajabuajabu hivi. Mh kweli mwanamke atawale inawezekana wapi mambo kama hayo' Safari yake iliishia kwa Mzee Nama rafiki yake. Alifika pale akiwa anahema juu juu kutokana na presha aliyoipata. Kwa bahati nzuri Alimkuta na kuanza kuongea nae. 'Namaa hivi unazungumziaje juu ya kumpa Mwanamke uongozi?' Nama alifurahi kuulizwa swala hilo kwanza ' Mh Mwaya unajua nyakati hizi kila mmoja ana kipawa chake cha ufanyaji kazi, kila mtu anao uwezo wa kuongoza tena yaweza kuwa mwanamke akaongoza vyema kuliko huyo Mwanaume' Nama alimfafanulia Mwaya. 'Haaaaa hapana hiyo haiwezi kutokea kabisa, ila rafiki yangu kuna muda uliopita Ilitokea kama mvua fulani radi kubwa ni nini kile. 'Haaaa ni kweli yani niliangalia ilikuwa ni hasira ambazo sikujua wapi zimetoka lakini tusipokuwa makini tutaangamia kabisa hapa ndugu yangu.
Majira ya kuapisha imewadia Watu walipika mapombe mengi na vyakula vingi sana, vya kila aina. Wakati huo sasa Mzee Chepi na makasi wakiwa na maji yao walitafuta pacha ambayo itaweza kutumia kwa kuoga. Maji yalishawekwa katikati ya pacha. Bila aibu walianza kuvua nguo zao kwa kuwa ilikuwa ni usiku walihisi hapakuwa na mtu atakaewaona. Upande wa pili Masha kawekwa kwenye eneo maalum ambalo litatumika kwa Kumwagia maji ya baraka ya ufalme. Chepi na Makasi waliyaoga maji hayo hadi mwisho. Ajabu walianza kujikuna mwili mzima huku wakitapatapa kwa mamivu wanayoyapata. Walikimbizana na kila mmoja akakimbilia kwake. Mwaya anafanikiwa kumtawaza Masha kuwa kiongozi rasmi ambaye ataanza muda huo kuongoza. Baada ya mambo kukamilika, watu walifurahi sana walicheza ngoma, walikunywa pombe. Taarifa ya Masha kutawazwa iliwafikia kijiji kizima cha Mwenda pole. Kila mmoja alionyesha furaha yake. Japo wengine hawakumtaka Masha.
Siku ya pili Masha aliita wanakijiji wote na kuanza kuongea nao. 'Wanakijiji wa Mwenda pole mpoooooo! ' Masha aliwasalimia kwa Bashasha. 'Tupooooooooo' 'Sawa sasa natoa shukrani za dhati kwenu pia natoa tangazo kuanzia sasa wanawake ambao ni wajawazito na wale wanaotaka kuzaa, ukizaa mtoto wa kike utamlea mwenyewe yani mali ya mama. Ukimzaa mwanaume huyo sio wako ni wa baba na atakuja kubarikiwa hapa kwangu. Wanawake wakaona sasa uongozi umeingiliwa, wakaona afadhali wasingekuwa na uongozi. Upande wa mama Nyamizi na Nyamizi wanaonekana kufunga virago vyao na kutaka kuondoka, tukio hilo Mzee Nama alishuhudia hivyo aliona vyema kuuliza kulikoni. 'Mama mfalme mbona haraka hivyo?' ' Mzee Nama sisi tunaondoka Masha ni mwanangu, nimemuweka tumboni miezi mingi, thamani ya mwanamke haioni na kudiriki kutamka kauli zile za ajabu? Tunaenda kijiji cha NYANYENI. Tunaomba usiwape taarifa hii, kwa heri..."
Nama ilibidi awatakie safari njema huko waendako.
Nini baina ya Chepi,Makasi na Masha?
Itaendelea...........

No comments: