Riwaya:: CHOZI LISILOSAHAULIKA SEHEMU YA 07
¶ilipoishia Sehemu ya 06¶
..Wazee hao kama kawaida yao pindi tatizo linapowakuta basi hukimbilia kwa Mzee Njimbi. Walifika na kumueleza matatizo ambayo yamewafika kwa nyakati zile ambazo walikuwa katika mtihani wa kupata fimbo ya Mzee Kabali. Ilionyesha kuwa Mzee huyo kuwaeleza kuwa waitafute damu ya Nyamizi kwa hali yeyote ile ambayo wataifanya ili aweze kuwasaidia tatizo lao. Wazee hao hawakuwa na jinsi zaidi walikubali na kutoka hapo na kuelekea kijijini ili kupanga jinsi gani watampata Nyamizi.....
¶ Endelea ¶
Upande wa bwana Nama, alifanikiwa kumuweka hali nzuri Nyamizi kutokana na akili yake kutokuwa sawa baada ya kuchanganyikiwa kutokana na Kaka yake kumfanyia hujuma. Basi alimruhusu aende nyumbani pamoja na mama yake. Waliondoka kurudi hadi nyumbani, Mama yake Nyamizi alisikitika sana baada ya kujua kuwa Masha kamfanyia mambo mabaya ndugu yake ' Masha yani sikudhania kama kweli umemgeuka dada yako mh ama kweli Mzee Kabali kanena kama ni haki yako mwanangu utaipata'. Muda ulipita kidogo ndipo Masha alijitokeza huku akiwa na furaha kubwa sana. 'Mama, mamaa, onaaa furaha imerudi ndani ya familia ya mzee kabali..hatimae nimeshinda katika shindano la kupata ufalme mamaa na kesho natangazwa rasmi'.
Hakika mama yake Nyamizi hakuwa na furaha kabisa alimsubiri afike karibu alafu amueleze yote. Masha alifika hadi pale alipo mama yake kisha akaanza kucheza ngoma ya kiasili kuonyesha furaha yake. ' Masha inaonekana unafuraha sana si ndioo' Aliuliza Bi kabali 'Ndio mama au wewe haufurahi mimi kuwa mfalme' Mama alitulia kimya huku hasira zikimjaa kifuani. 'Sikutarajia kama nitazaa mtoto wa ajabu kama wewe mtoto huna huruma kabisa unadiriki kutaka kumuua ndugu yako kisa ufalme haya Unadhani ndugu yako utamueleza nini'. Mama alifoka sana huku akilia.
'Mama nini sasa unasema,Mamaa hakika mimi niliipata ile fimbo sasa sijajua kwa nini unahisi kuwa nimemdhulumu...huyu mwanamke tuu mama hana nguvu mimi ndio napaswa kuwa kiongozi'. Masha alizungumza kwa huzuni. 'Masha nadhani sasa unanikosea adabu hata mimi mama yako kumbuka kuwa baada ya baba yenu kufa miaka yote nani kakuleeni alafu leo kuwa wanawake hatuna thamani pumbavu mkubwa wewee tokaaa hapa nyumbani tokaaaaa' mama alimfukuza Masha pale nyumbani kwake. 'Haina shida ila jua kuwa Nyamizi hana faida kabisa kwenye swala la uongozi mwanamke atabaki kuwa chini hata wazee ukiwauliza hata leo baba angekuwepo angesema kuwa mimi ndie napaswa kuw kiongozi' Masha aliondoka pale nyumbani.
Mama Nyamizi alilia sana baada kusikia kauli kali kutoka kwa Mwanae. Wakati huo Mzee Chepi na Makasi walikutana na kuongea mambo kadhaa 'Mzee chepi hapa inatakiwa tuwe karibu sana na ile familia ili wasitujue sawa?' 'Pia tukajifanye tunampenda sana nyamizi na tunamkubali awe kiongozi wa hapa Mwenda pole, tukifanya hivyo tutampata kiurahisi sana Nyamizi na hawatotufahamu'.
Walikubaliana katika hatua ya njama ambazo wameziweka muda huo ili wamkamate vyema Nyamizi. Masha tembea yake alifika kwa Mzee Mwaya na kumueleza yale yote ambayo mama yake kayasema. 'Kha!! Yani mimi ndio kujua kwangu ndio huko huyu mwanamke hana uwezo wa kufikilia tangu lini masikio yakazidi kichwa?, sasa usiwe na shaka utalala hapa kesho ukitawazwa utaamia kwenye nyumba yako ya ufalme.
Kweli aliweza kupumzika pale. Bwana chepi alikuwa wa kwanza kwenda kwa Mama yake Nyamizi, alipofika kule alianza kuwa mpole sana ili aweze kupata kile akitakacho kwa muda ule. 'Mama Nyamizi habari yako' Chepi alitoa salamu 'Salama baba karibu' Alisogeza kiti akakaa 'Mama bwana tumekuja kuomba msamaha sana mimi na kwa niaba na rafiki yangu maksi, tulifanya makosa sana kulazimisha Uongozi wakati Aliyestahili ni Mtoto wa mfalme ambae ni Nyamizi..na nimekuja kutoa msaada kuwa tutakuwa bega kwa bega pamoaja na Nyamizi mpaka apate uongozi' Chepi aliongea maneno ya ustaarabu huku akipiga magoti na kuomba msamaha wa hali ya juu. Mwanamke siku zote kaumbwa na roho ya huruma basi aliweza kumsamehe Mzee huyo.
'Mzee chepi ahsante lakini, kaka yake Masha kumbe kampokonya Fimbo dada yake ili yeye ndio awe mfalme kaniuzi sana na nimemtiamua hapa' mzee chepi alifanya kama kushangaa kwa taarifa hiyo aliyoipata. 'Haaa ina maana Masha kataka kumdhurumu dada yake, wakati sisi tulimuona Nyamizi akipambana na mnyama ili achukue fimbo na akambeba kaka yake aliyedhindwa kabida kuendelea! Hapana tutapambana kwa hili'. Mzee huyo alitoka pale kwa hasira kubwa, alipofika mbali na pale akaanza kushusha pumzi kisha akacheka sana 'Hapaa sasa tumemmaliza Nyamizi. Kumbe Masha na Mama yake na Nyamizi wana ugomvi ahaaa hapa ndipo pakutokea. Inatubidi tufanye jambo. Alienda kupeleka taarifa kwa Makasi, hakika alfurahi sana kwa kazi aliyoifanya chepi.
Siku ya pili ambayo ilisemekana kuwa Masha anatawazwa kuwa mfalme rasmi, ndio siku ambayo Makasi na Chepi waliitaji kuitumia kwa makini sana. 'Makasi itabidi wewe ukakae kule porini kabisa njiani ambako Nyamizi anapita kwenda kuchukua kuni nadhani leo nitaenda kuiba zile kuni ambazo zipo kwao ili aje huko kuchukua zingine' Aliongea chepi 'Haaa yani una akili za ziada kama zangu sasa fanya haraka kabla Masha haja apishwa. Kweli chepi alitembea akiwa na mti wake akipita mitaa ambayo imepambwa kwa viyo vya kuvutia. Alipofika kwa Mama Nyamizi aliwasikia wakiwa wanazungumza ndani wawili, mzew huyo alinyanyua kuni zote na kuondoka nazo. Hatua hiyo alifanikiwa kuimaliza, chepi alikwenda hadi kule ambako yupo mkasi ili wasubiri hatua inayofuata ya kumsubiri Nyamizi. 'Chepi una uhakika kuwa atafika huyu?' Makasi aliuliza 'Ndio atakuja' basi walisubiti zaidi.
Nymbani kwa Mama Nyamizi. 'Mwanangu hii ndio dunia ya sasa na ambayo itakuwa inakuja zaidi baada ya sisi kutoweka duniani, kuna baadhi ya vitu sisi kama wanawake tunahisiwa kuwa hatuwezi wakati tukivifanya tunawashinda mpaka wao, kikubwa Nyamizi mwanangu kuvumilia' Nyamizi aliitikia. Wakati huo akitoka nje 'Mama kuni hakuna hata moja ngoja niende nikachukue kule porini narudi nije kupika ugali tule' 'usichelewe mwanangu' ' hayaaa mama nachukua kuni'. Nyamizi bila kufahamu kama anaingia kwenye hatari. Nyamizi alitembea ili akachukue kuni na aweze kurudi nyumbani kwa haraka sana.
Akiwa anakaribia aliziona kuni ambazo ni nzuri sana, Aliinama na kuanza kukusanya, alikusanya zote wakati anataka kuzibeba ziliangushwa chini na kufanya kichwa cha nyamizi kugeuka na kumuona Mtu aliyejifunga kitambaa. Aliinua kisu juu na kumtundika mkononi, ghafla mzew Chepi alikuja na chombo kukinga damu huku Makasi akimshikilia. Nyamizi alilia sana tena sana baada ya wazee hao wawili. Nyamizi alipiga kelele ambazo hazikiwa na faida kwa muda ule. Nyamizi aliona hana haja ya kuishi duniani tena. Aliinuka huku mkono ukimtoka damu. Alichukua kamba ambayo alihitaji kufungia kuni akaiweka juu ya mti mithli ya kitanzi anataka kujiua..
Alianza kuingiza kichwa ghafla bin vuup Sauti ambayo haikujulikana inatoka wapi ikimpa onyo kwa jambo alifanyalo........
Je? Ni sauti ya nani
Je? Atafanikiwa dada Nyamizi kujikwamua kwa changamoto hizo zote?
Itaendelea......

No comments: