Riwaya:: CHOZI LISILOSAHAULIKA SEHEMU YA 06
¶ ilipoishia Sehemu ya 05 ¶
...Nyamizi alirudi pangoni baada ya kumuacha Kaka yake Masha ambae hakuwa na hali nzuri, Alielekea kwenye lile pango ambalo walitoka muda mchache uliopita. Ghafla wakati analikaribia basi akatokea yule mnyama hatari sana Nyamizi hakuamini kwani Alianza kutetemeka, hofu ilimtanda moyoni na haja ndogo ilianza kumtoka "kujikojolea". Ajabu yule mnyama alipisha na akatokomea mbali na pale. Wakati huo mzee Makasi alimuona binti huyo akamueleza rafiki yake 'chepi yule binti anathubutu tena kuingia mule hakiamungu siwezi kwenda tenda ebu turudi nyumbani' wao walitangulia. Nyamizi alifanikiwa kuchukua ile fimbo na kurejea nyumbani huku akiwa kambeba kaka yake. Wanakijiji walisubiri kwa kudhani kuwa atakaekuja na fimbo ni masha mtoto shujaa wa mfalme kabali....
¶ Endelea ¶
Bashasha ya watu ni kumuona Masha mtoto shujaa ambae walitabiri wengi kama Mzee Masha aliyeweza kusema tangu mwanzo kuwa masha ndie chaguo la kijiji cha Mwenda pole. Muda uliyoyoma kwelikweli ndipo wakatokea Makasi na Chepi, walivyoonekana kwa mbali Mzee Mwaya akaamuru wakae kimya wasikilize Taarifa kutoka kwa Wazee hao. Hatimae wamekaribia na wakapokelewa japo hawapendwi sana kutokana na tabia ambayo waliipata kipindi cha nyuma hiko kilichpita zamani
'Haya Tupatieni fimbo au tupatieni habari kipi kinaendelea huko mlikokawa' kauli hiyo pia iliwafanya kukaa kimya ili wapate kusikiliza kipi ambacho atakisema. Makasi alianza kwa kukohoa kidogo "koh koh kohhh" baada ya hapo akatazama watu waliozunguka pale. Akasogea kisha akaanza kusema, 'kwanza wanakijiji wa Mwenda pole tukio mnaloliona mbele yenu ni kweli tumerudi, kusema ukweli kwenye lile pango kuna mnyama mkali sana oneni kamtafuna Chepi mguu kidogo hapa, Alafu ajabu sasa yule mnyama wakati tumeishika fimbo akaja kutuvamia akaikamata na meno yake makali ile fimbo na kutoroka nayo ndio maana tukarudi mikono mitupu.'
Watu walishangilia kwa kupiga makofi mengi sana. Mzee makasi akajiona mshindi mkubwa sana. Baada ya kuona anashangiliwa, alizidi kuwahamasisha waendelee kupiga makofi lakini walimcheka tu! ' kweli mimi shujaa kabisa haya piga makofi kabisa wanawake kwa wanaume na watoto na wazee wenzangu pigeni makofiiii'. Aaaah ! Masikini kumbe hakuwa anapigiwa yeye alionekana kwa mbali Nyamizi akiwa kambeba kaka yake Mgongoni.huku akiwa kaishikilia ile fimbo ya ufalme wa pale.
Makasi aibu ilimkuta baada ya kuona wenye fimbo wamewadia. Nyamizi alimshusha Kaka yake ndipo fimbo akaiweka chini ili amuweke vizuri. "USIYEMDHANIAE SIE KUMBE NDIE". Nyamizi hakuamini macho yake, kaka yake Masha akainuka ghafla akaishikilia ile fimbo na kusimama nayo kisha akainyoosha juu kuashiria kuwa yeye ndie shujaa ambae kaikamata fimbo kwa macho yake.
Watu walimiminika kwa kupiga vigelegele vingi, wakati huo Nyamizi haamini kitu ambacho kaka yake kakifanya mbele yake. Kamsaidia kumbeba tangu mahali pa hatari sana na yeye ndie kaitafuta fimbo kwa mikono yake na siku ya mwisho kaka yake anamgeuka. Alilia sana tena sana, uchungu alioupata hauelezeki, Macho yalikuwa mekundu muda mchache tu. Kaka yake Masha akamjia na kumuambia 'Wewe ni mwanamke na mimi ni mwanaume Mwanamke ni mwanamke tuu haijalishi kuwa wewe ni dada yangu uongozi lazima uje kwangu haaaaa haaaaa dada karibu siku natawazwa kuwa mfalme wa Mwenda pole ahsante' Ni maneno ambayo Masha aliweza kuyaongea. Nyamizi alijitahidi kusimama huku miguu yake ikiwa imeloa damu alijikokota kuitafuta njia ya nyumbani kwake binti huyo.
Njiani walimsema vibaya sana kwa kumueleza maneno yasiyo na maana. 'Khaaah! Yaaani umeshindwa kukaa nyumbani unajifanya kutaka umalikia na hauweziii ona unacholia nini' Nyamizi alibaki kuumia tu na kweli alijihisi ni mjinga sana. Njiani aljiuliza maswali ''Nyamizi mimi, kipi nimemkosea kaka yangu, baba kwa nini ulimuachia maagizo mama kuwa mimi niwe Malkia wa hapa baba ona kaka anachonifanyia..kama kweli baba uliahidi hivyo onyesha chuki zako juu ya wanaume wanaotudharau sisi wanawake'' Aliongea maneno makali sana ambayo laiti yangekuwa kisu ni kikali sana.
Alifika nyumbani akamkuta mama yake akiwa analia na yeye kumbe aliona vile vitendo vyote. Alisimama akamkimbilia Nyamizi aliyeonekana kuishiwa nguvu, hatimae nyamizi anadondoka chini kabla hata mama yake hajamfikia. 'Mwananguu nyamiziii amka mamaaa nyamiziiii jamani msaadaaa'. Katika hali hiyo mama huyo aliomba msaada ndipo binti mmoja aitwae Nyoni alikuwa katika matembezi akabahatika kuona hali ile. Alikimbia moja kwa moja hadi maeneo ya kwa mzee Mwaya ambae anaendeleza taratibu za furaha za bwana Masha kushinda dhindano, alimtafuta mzee mmoja hatimae akamuona kumbe alikuwa mzee Nama. 'Babuuu twendee Kule nyamiziii nyamiziii babuuuu' Mzee Nama hakuweza kuelewa 'Nyamizii nini binti haya eleza Nyamizi kafanyaje?' 'Kaanguka babu'. Ndipo walipokimbia kuelekea huko Mzee Nama japo mzee wa makamo lakini hakuwa haba kwenye mbio. Walifika hadi pale ambapo mama huyo alizidi kumlilia Mwanae Nyamizi. 'Oooh Nyamiziii haya hebu ngoja nimbebe chukueni vitu vyake muvilete kule nyumbani haraka sana.
Walifanya hivyo. Baada ya siku kupita hali ya Nyamizi ilikaa sawa. Mzee Nama alimhoji maswali lakini Nyamizi hakuweza kusema lolote. Mzee huyo alichukua dawa zake za utabiri alizungusha kisha alivyoachia akashika mdomo wake huku akitumbua macho. Alinyanyuka kumfuata mzee Mwaya. 'Mzee kuna hatari mbele yetu inaonyesha hatari kubwa mno iko karibu pindi tusipofanikisha basi tutaangamia' Nama alimueleza Mwaya lakini mwaya hakutaka kuelewa ndipo mzee Nama akarudi huku akitikisika kwa kichwa.
Mzee chepi na Maksi kama kawaida walirudi kwa fundi wao mzee Njimbi, walimueleza kila kitu 'Sasa kuna hatari ambayo ninaiona hapa ' Mzee Njimbi alisema 'hatari gani tena mzee?' Chepi aliuliza 'kosa lililofanyika hapa yule aliyekuwa na fimbo kanyang'anywa kachukua mwingine. Sasa huyu aliyenyang'anywa kuna maneno ya hatari sana japo ni madogo sasa hapa kuna kazi nzito'. Walichanganyikiwa kabisa. 'Sasa unatusaidiaje kwa hilo mzee mana uongozi unatuondoka hivyo' Mzee huyo Aliyejulikana kwa Njimbi alitikisa kichwa mara nyingi kisha akasema 'Njia rahisi ni kupata damu ya Nyamizi,' walishtuka 'yani una maana tumuue binti huyo?' 'Hapana namaanisha kuwa Mupate damu yake tu mukija nayo hapa tunavunja ahadi yake aliyoiweka ambayo ni hatari sana hata kwa kijiji...
Wazee walihemwa sana ndipo wakaondoka kurudi kijijini huku wakipanga njia ya kumkamata nyamizi na kumtoa damu.....
Je? Watafanikiwa kumtoa damu dada yetu Nyamizi!
Kujua hayo tukutane sehemu ijayo.
Itendelea........?

No comments: