RiwYa:: CHOZI LISILOSAHAULIKA SEHEMU YA 05




¶Ilipoishia Sehemu ya 04¶
...Mzee Makasi alimsukuma Masha hadi karibu pale alipo yule mnyama, hakika kwa kuwa ilikuwa ni jambo la kushtukiza Masha aliogopa sana baada ya kumtambua kuwa yule aliyepo pale ni mnyama mkai sana na hajawahi kumuona kabisa katika maisha yake. Masha aliogopa ndipo alipojitahidi kujizuia ili asiwezr kupiga kelele ambazo zingeweza kumshtua mnyama huyo aliyeonekana kulala, 'haki ya
Nani sijawahi kumuona mnyama mkali kama huyu,alafu kumbe hawa wazee ni wabaya hivi jamani aaah nimtafute dada nyamizi niweze kuondoka nae nyumbani.' Alishikilia moyo wake ulionekana kama unahitaji kutoka mwilini mwake.

                    ₱Endelea₱
Upande wa Mzee Chepi hali yake ilionekana kuwa nafuu baada ya kupata nafuu ndani ya pango hilo, alijiweka sawa akaegemea kwenye moja ya ukuta wa pngo hilo lililojengwa kwa Mawe. Alikaa takribani dakika kadhaa huku akifikiria nini afanye 'Mh! Hii ni shauli ya uongozi na nisipopigana sasa hivi nitakufa hali ya kuwa kwenye ukoo wetu hatuna hata ufalme jambo ambalo siwezi kukubali' Wakati akiendelea kukaa pale ili aweze kuvuta taswira ya lile pango alisikia upande wa pili ambapo kuna mtu akinong'ona kwa sauti ya chini, ilionyesha kuwa kuna mtu alikuwa akiongea nae. Alinyanyuka kutaka kufuata njia ambayo inaelekea upande ambao kasikia ile minong'ono.
Bahati mbaya alijikwaa Moja ya jiwe ambalo liliteremka haraka sana hadi karibu ya ukuta ambao kumbe haukua imara ulipogonga ukatoboa na kuangusha baadhi ya mawe dhaifu yaliyopo na kuonyesha kwa upande wa pili. 'Weee! Hapa kumbe nimefanikiwa yani inaonyesha dhahili kuwa huku haikufichwa fimbo pekee bali na dhahabu pmoja na vito vya tahamani. Alianza kusogelea taratibu kuelekea pale, Sauti ya yule mnyama ilianza kunguruma mule ndani mzee Chepi tumbo joto, alishaona kuwa mqisho wa maisha yake yametimia kuwa ni tamati kabisa. Mnyama huyo alisogelea huku Mzee Chepi akihisi harufu kali tena mbaya.

Upande wa nje Nyamizi japo ni mtoto wa kike alishikilia upinde wake na mshale vyema ipasavyo kushikwa. Japo alikuwa akitetemeka aliufuata mlango wa pango huku akitembea kwa kuhesabu hatua kadhaa, hatimae aliufikia alisimama kwa muda wa dakika kadhaa huku akifikilia 'Mh! Kulikuwa na harufu mbaya sasa hapa imepotea tayari au huyu mnyama katoka' Maswali ambayo alikuwa anajiuliza hapakuwa na mtu ambae alikuwa anafahamu bali yeye mwenyewe. Aliongoza mguu moja mbele huku akisikilizia, akaweka wa pili kisha akasikilizia akajihakikishia kuwa hakuna kiumbe chochote kipo maeneo hayo. Aliingia na kuanza kutafuta kitu ambacho ametumwa. Katika tembea yake alibahatika kumuona kaka yake akiwa hoi chini hajitambui na damu xinamvuja mguuni.
Alimkimbilia haraka, 'Mashaa kaka masha amka twende nyumbani' Masha alifumbua macho na kuona kabisa aliyepo mbele yake ni dada yake basi alifurahi sana, baada ya kujua kuwa usalama upo kuwepo kwa mwanamke mbele yake na akamini kabisa anaweza kumsaidia. Muda mfupi huo kelele zilisikika za mihemo Makasi akiwa kambeba chepi wake nae chepi kwa upande wake alikuwa taabani. Makasi alifanikiwa kutoka nje na kuongoza njia ya nyumbani. Muda huohuo Nyamizi alimuinua Kaka yake na kuondoka nae. Baada ya kufanikiwa kutoka salama ndani ya pango la Mla nyama, Nyamizi aliangalia nyuma akamuona yule mnyama akiwa kabeba mwili wa mwanadamu ilionyesha fika kuwa moja ya wale vijana tayari wameshaliwa.

Ndani ya kijiji cha Mwenda pole Maneno ya chinichini ambayo yalizidi kutawala ni juu ya swala la Nyamizi kuutaka uongozi. Basi katika familia moja palionekana watu kadhaa wakipiga soga 'Haya Nyoni unajua mjuu wangu kipindi sisi tunaishi na babu zenu hatukiwahi kusikia laana hii ambayo inataka kufanyika hapa Mwenda pole' Bibi huyo aliongea kumueleza mjukuu wake Aliyefahamika kwa jina la Nyoni. 'Sasa bibi mimi sioni kama kuna sababu ya nyinyi kutomsaidia nyamizi wakati huyu ni mwanamke mwenzetu hauoni kama atatusaidia au haujui kama hapa kijijini tunaonewa sana alafu wanawake tunanyanyaswa sana' Nyoni aliweza kumueleza bibi yake. 'Mh! Ndio lakini mwanamke hawezi kuongoza kundi kubwa la watu hapa kijijini sisi tumezoeshwa kupika vyakula na kufanya shughuli ndogo ndogo pamoja na kuzaa tu mjukuu wangu' Nyoni hakuweza kuafiki kabisa maelezo ya bibi yake
'Sasa na huko kwenye pango walikokwena watapona kweli?' 'Kupona watapona lakini Nyamizi kwa kuwa ni mwanamke hatoweza kurudi akiwa mzima.'

Walionekana wazee na mabibi wakijaa kwa Mzee mwaya kumshinikiza amuondoe Nyamizi katika orodha ya Kupata uongozi kwani Wanakijiji wanaogopa laana ya mizimu isije kuwafikia. ' Mwaya tangu wafalme wamepita wewe mwenyewe shahidi hatukuwahi kusikia Mwanamke akiwa kiongozi sasa hizi habari wewe unazitoa wapi?, uongozi wako unataka kuupeleka pabaya' kauli hiyo ya mzee aliyejitokeza na kutoa dukuduku lake, lakini kauli yake iliweza kusababisha wengine wote kuungana nao 'Ndioooo... ndiooooo hatumtaki na hatutaki laana ya kijiji' Mwaya alisikiliza akawa ahidi wakirudi atafanya vile watakavyo wanakijiji.
Nyoni alisikia wale wanakijiji wakiyasema ndipo akaenda kumpa taarifa Mama Nyamizi kwa kile alichokisikia kutoka kwa Wale wanakijiji waliokusanyika kwa Mwaya. Mama huyo alibaki kusikitika na Kuomba watoto wake warudi salama.

Upande wa Nyamizi alifanikiwa kukaa mbali kidogo na pango akamuweka kaka yake pembeni. Akarudi kule pangoni, wakati huo Yule mnyama alijitokeza mbele yake ndipo Nyamizi akapatwa na hofu pamoja na mwili wote kutetemeka bila kujifahamu Nyamizi alitokwa na haja ndogo yani "Kujikojolea" kutokana na hofu kutafunwa kama Muogo mbichi. Ajabu yule mnyama alimpisha kisha akakimbia zake mbali na pale. Nyamizi aliangalia huku na kule hakuona mtu akaingia ndani ya pango. Wakati huo Mzee Makasi aliona yale yanayotokea akabaki kuangalia tu ' Haya chepi yule binti kajitoa sadaka kaingia mwenyewe, kwa niliyoyaona mule sitothubutu kuingia basi turudi kijijini' wao walianza kwenda nyumbani.
Nyamizi alifanikiwa kupata ile fimbo akaonekana amembeba kaka yake Masha wakirudi na wao kijijini huku akiwa kashikilia fimbo. Wanakijiji walisubiri kwani muda ambao walijua kuwa watakuwa wanarejea umewadia. Wanakijiji walifahamu kuwa Masha ndie atafanikiwa kwa kuwa ni kijana shujaa wa mfalme Kabali........

Itaendelea...........



No comments: