Riwaya: CHOZI LISILOSAHAULIKA SEHEMU YA 04
¶Ilipoishia sehemu ya 03¶
.....Mzee mwaya alimalizia shughuli zake huku akiwa anawaza jinsi gani hawa wazee wawili walivyokuwa na matatizo yao. Muda ulipofika taarifa ilitolewa rasmi kuwa wanatakiwa kukutana mahali ili waweze kupewa majukumu na maelekezo ili wakachukue hiyo fimbo ya mfalme kabali katika pango la Mla nyama. Wahusika walikuwa wengi wakiwemo Nyamizi,Chepi, Mzee mwaya aliweza kiwaeleza nini wafanye ila jambo ambalo lilitakiwa wao ni kuleta fimbo ya Mfalme kabali, waliachiwa na kila mmoja akenda njia yake.....
₱ Endelea ₱
Nyamizi kama mtoto wa kike alikuwa ni muoga sana kufanya kazi hiyo akijiangalia mwanamkr ni yeye peke yake, anashindana na wanaume wenye nguvu zao. Mama yake kabla hajaondoka aloweza kumpa moyo kabisa na kumuambia kuwa asijidharau kwani hata mwnamke anaweza na asijisikie huzuni kiwa peke yake katika safari ile. Ndani ya kijiji cha cha Mwenda pole watu waliongelea vibaya sana la kumuweka mwanamke kama nafasi ya kugombea Nafasi ya uongozi mkubwa kama ule. Wengine walidiriki na kusema kwamba 'yani endapo nyamizi akifanikiwa kuchukua nafasi haki ya nani mimi naama hapa kijijini, hii ni laana ambayo inatukaribia na tutaadhibiwa kwa hili', Baadhi ya wazee na watu wengine walimfuata Mwaya ili kwenda kumpa ushauri juu ya swala lake la kumruhusu Nyamizi aweze kuwania nafasi hiyo ya uongozi.
Mzee Mwaya akiwa nyumbani kwake anashangaa kuona wageni wake ambao walifika wakiwa na nia na bwana Mwaya. 'Haya jamani niwasaifie nini?' Mwaya aliwauliza haraka hata kabla hawajamaliza 'bwana Mwaya ulifikiria nini kumruhusu binti kama yule kuwania sehemu na ya umalkia' Mwaya hakiwa na wasiwasi aliwajibu kwa ufasaha kuwa Atakuwa malkia endapo akiwashinda wanaume pindi atakapowaletea fimbo ya kifalme. Baada ya muda kupita ghafla kijiji cha Mwenda pole kilianza kubadilishwa na hali ya hewa ambayo iliambatana na mvua yenye radi kali na mingurumo. Muda mchache mvua iliteremka tena kubwa sana. Mama yake Nyamizi au mke marehemu Mzee Kabali. 'Mwanangu Nyamizi atafanikiwa kweli hali hii' Alijiongelesha yeye peke yake kutokana na mwanae kipenzi kwenda maeneo hatari. Baada ya Mvua kuisha kidogo aliinuka na kugunga mlangobwake aliondoka huku nyuma akisindikizwa na mlinzi ambae alikuwa anafanya kazi hiyo tangu kipindi cha nyuma. Safari ya mama huyu alielekea hadi kwa Mzee Nama, alifika alihodika mara ya kwanza,ya pili, hadi ya tatu ndipo akakaribishwa. Mlinzi alibaki nje. 'Haaa haaa haaa malkia wetu kwa nini usingetuma hata taarifa nikaja kwako?' 'Hapana haimaanishi mimi kuwa malkia mstaafu kuwa nifanye kila nitakalo kupata kwa muda ninao taka' Aliongea Mama Nyamizi.
'Haya sasa najua ujio huu una maana kubwa sana Mama bora kuliko wote Ndani ya Mwenda pole nakusikiliza' aliongea mzee Nama, kumbuka mzee Nama ni mzee ambae aliweza kuwatabiria wazee wawili Chepi na Makasi. 'Baba nipo hapa naomba uniangalizie mwanangu Nyamizi yuko wapi na anafanya nini mana kuna ndoto mbaya ambayo inanishitua' Nama kabla hajaendelea aliacha na kumgeukia Mama mfalme Kabali 'Mama ndoto ipi hiyo' aliuliza Mzee Nama. 'Baba nimeota kuwa kijiji cha Mwenda pole kina didimia lakini ikiwa ina maana anatakiwa apatikane kiongozi haraka sana' Nama alitikisa kichwa huku mdomo wake ukiwa wazi kuonyesha jinsi gani kaelewa vyema. 'Basi haina shida, ndoto yako haina utofauti na ya watu fulani waliokuja kuomba niwatafsirie ila kikubwa tuwaamini wale waliokwenda kwamba watarudi wakiwa na fimbo mkononi mmoja wao na kumpata kiongozi mzuri sana' Basi bwana Nama alichukua usinga ili aweze kujua nini kinaendele kwenye pango la Mla nyama. Ghafla sauti yake ilibadilika kabisa ikaongea sauti ya mwanamke 'Malkia unahitaji nini?' Mama Nyamizi akamjibu 'Nisaidieni kujua mwanangu yupo mahali gani salama?' 'Haaaa haaaa! Kuna watu wamevunja magano ya mfalme Kabali....alafu kikubwa kitatokea miongoni mwenu..namuona hapa Nyamizi akiwa hana hamu ya kuwa maeneo haya alipo anahangaika sana' jambo hilo lilimuumiza sana mama yake. Ukweli ulibakia kuwa katika kijiji chaMwenda pole ni laana ambayo wanaichukulia endepo akiongoza mwanamke.
Safari ya wapiganaji ambao wamejitokeza kuhitaji ufalme.kuna baadhi ya watu walikuwa na ulimbukeni kwa kutofahamu vyema kule waendako. Njia ambayo walipita Mzee Chepi na Makasi ilikuwa na makorongo ya moja ya pango hilo la Mla nyama. Pango la mla nyama ni pango ambalo lilipewa na watu wa zamani baada ya kulipa jina hilo kutokana na tabia ya pango hilo kutorudi Salama pindi mtu awezapo kwenda. Basi wazee hao wawili waliweza kujadiliana kwanza kabla hata hawajaana kuingia 'Chepi unaona lilee pango wale vijana walioingia inabidi tuwafuate nyuma kidogokidogo' walifanya hivyo hadi walipokaribia kwenye mdomo wa pango hilo. Walisikilizia kama kuna kiumbe chochote ambacho kipo karibu nao. Mzee Makasi kwa kuwa ni fundi wa mambo ya kiasili aliende pembezoni mwa pango ambapo palikuwa na jiwe akasikilizia jiwe hilo kwa kutega sikio kwa muda fulani. 'Chepi nasikia kama kuna kundi kubwa la kitu likivuma kwa kasi sana alafu nasikia kama kuna kitu kinadundadunda.
Makasi alitoka hapo. Walichukua kizinga cha moto japo ilikuwa ni mchana basi waliwasha wakaanza kuliingia pango ambalo lilionekana kuwa la muda mrefu sana kutotumiwa. Mzee Chepi na makasi waliamua kuachana njia kila mmoja akafuata ile ambayo alihisi yeye ataweza. Mzee chepi alitembea upande wa mashariki na Makasi upande wa kusini. Chepi alitembea kwa wasiwasi huku akitazama huku na kule kwa kuwa alikuwa na uchu wa kuipata hiyo fimbo. Ghafla alivamia mzoga mbele yake kutokana na kiza kinene.
Mzoga huo ulianza kutoa harufu kali ambayo ni ngumu kuelezea, alijihisi kuishiwa na pumzi ghafla mzee Chepi. Alikimbia ovyo ndani ya pango hilo huku akijaribu kumtafuta rafiki yake Makasi alipiga yowe 'Makasiii, makasii makasiiiiii'. Baada ya muda mchache sauti ilikata kabisa haikusikika. Upande wa pili Alionekana Nyamizi akikurupuka toka kwenye dimbwi la mawazo mazito kabla hajaingia ndani ya pango, alishtuliwa na sauti ya chepi iliyomuita Makasi. 'Alaaah! Kumbe hata hawa wazee wamefika humu mh nisizembee lazima niingie kupata fimbo ya baba niweze kuwa Malkia na nisimuangushe mama' aliyaongea hayo Nyamizi huku akiwa kashikilia mkuki wake. Aliinama na kuuchukua kabla hajainuka alihisi harufu kali iliyomfanya azibe pua yake akainuka taratibu Asalaleeeeee kumbe kulikuwa mnyama hatari sana ambae alionekana ni wa kutisha pia mkali sana akitokea upande mwngine na kuingia ndani ya pango hilo, Nyamizi aliishiwa nguvu kwani dhamira yake kwenda mule pangoni lakini alimuona Mnyama huyo hatar, akashindwa hata kuinuka vizuri kwani mwili wake ulianza kutetemeka pale alipo. Ndani ya pango Mzee Makasi na yeye anapata mwangwi wa sauti ambao uliweza kujirudiarudia akarudi kufuata zile njia ambazo alipita. Alijitahidi hadi alipomfikia kijana Masha na yeye akiwa kwenue harakati. Alishindwa kumuuliza kwa kuwa wapo kwenye mashindano. Lakini kwa hali ambayo anaihisi hakuwa na budi kumuita Masha 'Mashaaa,mashaaaaa ebu njoooo' auti hiyo ya pangoni iliweza kujirudiarudia jambo ambalo lilimfanya Masha ahangaike nani na wapi anakoitwa Akiwa anashangaa Mzee Makasi alimuendea kabla hajamshika kwa mbali alimuona mnyama fulani hivi. Mzee huyo akaona ni vyema kuwa "heri ya lawama kuliko fedhea" alimsukuma Masha hadi karibia kule ambako yuko yule mnyama akiwa kajipumzisha, Masha alishindwa kupiga kelele kwani angemuamsha angegeuzwa kuwa kitoweo. Alipoishia aliweza kuganda hivyo hivyo, ndipo akapiga hatua nyuma kwa mwendo wa polepole, huku akijisemea 'Haki ya nani sijawahi ona mnyama kama huyu haki ya nani kumbe Mzee makasi anataka kunipoteza aaah Uongozi dhamanaa, dada yangu yuko wapi nimuambie aende nyumbani hawa wazee watatuua'.
Alifanikiwa kutoka karibu na yule mnyama huku akishikilia moyo wake uliokuwa ukidunda kana kwamba unataka kutoka mwilini mwake Masha......
Itaendelea.......

No comments: