Riwaya: CHOZI LISILO SAHAULIKA Sehemu: 03





                  ₱Ilipoishia₱

Mzee CHEPI na MAKASI baada ya asubuhi kudamka ili wapate kuelekea kwa Mzee MWAYA kwa ajili ya kupewa maelekezo ya shughuli ambayo wanatakiwa kuifanya ya kuingia katika pango la Mla nyama ili kwenda kuchukua Fimbo ya mfalme KABALI, walishangaa sana baada ya kuona bundi wengi sana maeneo hayo. Pia wanakijiji wa MWENDA POLE walishtuka na kustaajabu kulikoni ndege hao ambao walijulikana kuwa na sifa mbaya. Walielekezwa na wale wote ambao walihitaji kuwania nafasi ya ufalme kisha wazee hawa wawili walijianda kwenda kwa mzee NJIMBI kwenda kumalizia kazi yao....

                    ₱Endelea₱

Wazee hawa wawili walifanya kila njia ya kufanya haraka ya kuelekea kwa Mzee Njimbi bila mtu yeyote kufahamu kuwa wanaelekea wapi kwa nyakati zile za asubuhi. Kumbuka kuwa katika kikao ambacho walishakaa na Mzee Mwaya kwa lengo la kueleza kuwa ni nani anayepaswa kuwania kiti cha Mfalme Kabali baada ya umauti wake, mzee mwaya alimpendekeza kijana wa kwanza kuzaliwa wa mfalme ambae ni MASHA lakini mama yake Masha alimpendekeza Mtoto wake wa kike NYAMIZI na ulikuwa kama ujumbe wa mfalme Kabali kabla ya kufariki pia Mzew Chepi na makasi walihitaji ufalme utoke kwenye ukoo huo wa Kabali na uingie katika koo hizi mbili za chepi na Makasi ndio maana wanafanya kila jitihada za kuweza kufanikiwa
                    Walifanikiwa kufika hadi kwa mzee Njimbi ambapo walimkuta na wao wakiwa na yale mayai walioagizwa....."Njimbi Babaaaa natumaini utakuwa umetidhika baada ya kuja na mzigo wako ambao ulituagiza sasa baba tupo mbele yako kukukabidhi".....Makasi alimkabidhi kwa kupiga magoti na kumshikisha yale mayai ya bundi. Mzee Njimbi aliyapokea na kuyaweka mahali kisha akawauliza...."Baada ya kuchukua hamkufuatwa na bundi asubuhi maeneo yenu??".....waliangaliana kwanza kisha wakatamka wote kwa pamoja...."tuliwaona bundi asubuhi walikuja ila hatukujua maana yake nini"......Mzee Njimbi alicheka sana kisha akawaambia...."yani hapo tumemaliza kazi kabisa sasa mko tayari kuvunja maagano ya Kabali kwa Nyamizi yaje kwenu???"....Aliuliza kuwauliza wazee hao wawili...."Tupo tayari kuvunja maagano ya Kabali kwa Nyamizi kuja Kwetu".....Alichokifanya mzee Njimbi ni kuyashika yale mayai na kuchukua moja na kutumbukiza mdomoni kwake na kulivunjia humo na kulila kisha kutema maganda. Kiliwashangaza sana baada ya Mzee njimbi kula yai la bundi....."Ukila yai la bundi utakuwa umejilinda kotekote kwani utakuwa makini kama yeye pia kila mmoja achukue moja alile kama nilivyokula mimi"....Haikuchukua muda sana kama unavyojua mtu mwenye shida ni mwenye shida tu.
                Walikula yote yalivyokwisha wakasubiri nini kitafuata. Mzee Njimbi aliinuka na kupiga usinga wake pande zote mbili kisha akachukua moja ya kibuyu na kutoa unga ambao aliweza kuchanganya na nyingine kisha akawapa wanywe. Walikunywa wazee hao. Baada ya hapo akachukua mawe manne na kutandika chini kisha akawambia jiwe hili la mashariki ni MASHA magharibi NYAMIZI kusini MAKASI kaskazini CHEPI ...."Nafanya utabiri tuone ni wapi ambapo litaangukia baada ya kufanya dawa ".... walisubiri ili waone  mabadiliko kama yatatokea. Ilizungushwa kidunguli kisha akakiachia kidunguli hiko kilizunguka kisha kilisuasua kwenda kwa Nyamizi lakini kiliangukia kwa Chepi. Ilifanywa tena  kilirudia kusuasua kwa nyamizi lakini kikaangukia kwa Makasi. Zaidi walivyofanya ndivyo kilizidi kupotea kwa Nyamizi na kuangukia kwa wawili hao. Walifurahi baada ya kufanikisha kazi ya kupoteza ndoto ya Mfalme kabali ya kumtaka Mwanae Nyamizi binti wa kike aweze kuwa kiongozi. Wazee hao walirudi wakiwa na furaha baada ya hapo majira ya mchana walienda kwenye kilabu cha pombe yaKienyeji. Pombe hiyo inayoitwa Ulaka ilikuwa maarufu sana kwao. Lakini ni pombe ambayo Mzee Chepi akinywa na kulewa huwa anakuwa wazi katika mambo yake kuanika kila kitu ambacho kinamhusu.
              Majira ya usiku Mzee Makasi akiwa kalala alishtuka usiku kisha akakaa kitandani. Alisikia sauti ya bundi ikilia juu ya paa ya nyumba yake. Alishtuka sana aliinuka kisha akafungua mlango taratibu akashuhudia bundi kadhaa wakiwa uwanjani. Alifunga mlango kisha akalala tena huku akitafakari nini maana yake. Usiku akiwa amelala alishtuka kwa mara ya pili kisha akajisemea mwenyewe....."Mhhhh hapana inawezekana vipi hiki kijiji cha Mwenda pole kididimie kwenye ardhi hii ndoto ina maana"....Asubuhi na mapema hakuangalia chochote ambacho kilimhusu hapo kwake aliwaachia watoto na mke wake wafanye kila kitu yeye bila kujali alidamka na kuelekea kwa Chepi kwa bahati nzuri chepi na yete akiwa anakuja kwa Mzee Makalani walikutana katikati wote wakiwa wanahema...."chepi huu mguu ni wako"...."khaaa basi hata huu ulikuwa wako kulikoni"...."Mh chepi kuna jambo usiku nimeliota tena linaonyesha la hatari"...." Makasi haina haja ya kusema sana hata mimi nafahamu ndio maana nikataka kuja hapa sasa twende kwa Njimbi au nama sasa hivi"....waliongozana kwa Mzee Nama ambae kama utakumbuka kuwa ndie yule ambae walimuendea kwa swala la utabiri na akawatabiria kuwa Nyamizi ndie anayehitajika kuwa kiongozi. Walifika asubuhi hiyo walimkuta akijiandaa kwena shambani. Walimuomba awatafsirie ndoto ambayo waliota usiku huoo.
                Mzee huyo alidikitika sana kisha akawaambia kuwa ......"yani wazee wangu kumbukeni hayo mliyoyafanya ni hatari kwa kijiji hiki na msipoangalia mtakiweka sehemu mbaya ninachokiona hapa nyinyi mmefanya mambo mabaya sana na pia kijiji kitakuja kulia siku moja sasa cha umuhimu apatikane kiongozi ambae ataweza kulidhibiti hilo mapema"......."Sawa mzee Nama lakini ebuu nenda kadodose nani ambae anahusika kuwa kiongozi hapo baadae".... Mzee Nama aliacha vifaa vya shambani na kukaa kwenye mkao. Walitikisa kidunguli kikaangukia kwa Chepi mara ya pili kwa Makasi. Nama alishuku na anachokiona. Alichoshauli kana ni wao basi itabidi wamueleze Mwaya mapema awaidhinishe ili tatizo linaloonekana mbele ya safari lisije kuwakuta. Walirudi huku wakijipongeza baada ya kuharibu mipango ya kijiji. Mzee Nama aliacha hata kwenda shambani aliona ni vyema kwenda Kwa Mzee Mwaya akamueleze kinachojili. Alimkuta akiwa nyumbani kwake akisubiri cha asubuhi....."ooooh nama habari tena muda muafaka sana huu"..."Ahsante mtukuka wangu uliepewa dhamana ya kuchagua uongozi uliobora hapa Mwendapole ila naomba nina jambo muhimu nahitaji kukueleza wakati unaendelea na swala la kutafuta kiongozi bora"..... Mzee mwaya alitoka pembeni na kuanza mazungumzo....."Niambie ndugu"..."Mwaya unawafahamu Chepi na Makasi??"...."Aaaah hao tena nini walichokifanya tena"..... "Walikuja nyumbani mara ya kwanza kutabiri nani atakuwa kiongozi lakini nikuulize mwaya unadhani nai alipaswa kuwa kiongozi hapa"...."Aaah mimi ninaemuona ni Masha mtoto wa kiume wa Kabali basi"...."Sawa mwaya lakini mbona hata hukunishirikisha maana walipokuja hao wazee Nilifanya akaonekana Nyamizi mara zote"......"Weeee Nama ina maanaa kuwa Nyamizi kaonekana hadi kwako"....."Ndiooo ila cha ajabu leo wamekuja tena wamenihadithia ndoto mbaya sana ambayo kama hatukumpata kiongozi mapema basi itatughalimu san"......"Eheee ikawaje"....."Basi tukakaa mkaoni kupiga tena utabiri wanaonekana waoo mara zote na si Nyamizi tena hiko ndio kimenileta hapa"...."Aah sawa ila kama kweli ni wao tutakutana nao kesho kwenye kuchukua Fimbo ya ufalme atakae shinda si ndio atakuwa mfalme haina shida japo nina shaka na hawa wazee"....."Basi ifanyike haraka pia mimi nikuache kwanza nimeacha mlango wazi".....
                 Waliachana pale huku mzee Mwaya akitafakari taarifa aliyopewa akaanda mambo tayari kwa ajili ya mtu kutangaza taarifa aliyoiandaaa. Siku ya pili yake tangazo lilipita kuwa tayari wale wote waliohitaji kuwania kiti cha mfalme muda wa kwenda kutafuta Fimbo yake imefika sasa wanahitajika wote wawepo maeneo ya tukio. Muda mchache walikusanyika. Waliitwa wale wote ambao waliweza kuhitaji fimbo hiyo ya mfalme. Orodha ilikuwa kubwa wakiwemo Nyamizi,,,Masha,,,Makasi,,,Chepi na vijana wengine waliojitokeza. Mwaya aliwapa maelezo ya kutosha sana na wakaambiwa sasa ruksa kwenda kuchukua fimbo hiyo kwenye pango la Mlanyama na kurudi nayo.

Itaendelea.............



No comments: