Riwaya: CHOZI LISILO SAHAULIKA Sehemu: 01





                    ₱ Anza nayo ₱

Kikao kiliendeshwa vyema lakini Bwana MAKASI alionekana kuvutia ngoma kwa upande wake. Lakini vilevile Bwana CHEPI hakuwa legelege katika kutetea hoja yake ambayo aliweza kuitoa mbele ya wazee wenzao ambao walikuwa kama waamuzi na washauri wa swala walilonalo kwa nyakati hizo.
             Kikao kilikuwa nani ambae ataongoza kijiji cha MWENDA POLE baada ya Kiongozi wao aliyeongoza kwa miaka mingi sana aliyejulikana kwa jina la KABALI. Huyu mzee aliongoza kijiji hiki cha Mwenda pole takribani kwa Miaka tisini mpaka kifo chake ambacho kilimkuta baada ya kuugua kutokana na uzee wake. Wazee ambao waliona kuwa si busara kwao kukaa bila kuwa na kiongozi waliweza kuitana na kuwaita watu ambao walihisi kuwa wanaweza kutoa hata hisia jinsi ya kuongoza. Mzee MWAYA alisimama na kutoa amri ambayo ilitekelezwa mara moja....."Sasa tuanaomba kwamba tumeshindwa kumtambua mtu ambae anaweza kuongoza kutokana na ushauri uliotoka muda huu kwanza hatuwezi kuchagua uongozi wakati Mzee KABALI ana familia pia ana watoto aliowaacha sasa tukaamua tuwaangalie kwanza watoto hao nani atatawazwa kuwa kiongozi"......Mzee huyo alitoa kauli hiyo na kufunga kikao ambacho kilichukua muda kadhaa.
                   Watu walitawanyika lakini kumbuka kuwa bwana MAKASI na CHEPI walibishana kwa kugombea nani ambae ataweza kuchukua kiti ambacho kiliachwa kwa muda mwingi. Mzee MAKASI tayari alipita mitaani wakati anaelekea nyumbani kwake alijitahidi kuwapa imani kuwa CHEPI hawezi kuchukua kiti cha Kiongozi KABALI. Kila mtu alitokea kumuamini kwa kuwa ni Mzee Mcheshi sana ambae alikuwa ana uwezo wa kushawishi watu na wakamkubali. Wakati huo familia ya Marehemu KABALI iliishi katika nyumba ambayo waliachiwa na mzee huyo. Pia Mzee aliacha watoto wengi sana lakini walikuwa ni wanawake kasoro mtoto wanaume lakini mmoja ndie wa mwisho kuzaliwa na alikuwa ni mwanamke. Mama yao aliyejulikana kwa jina la Bi' KABALI aliishi nao hao watoto wote katika eneo moja hilo ambao alikuwa anaishi Mzee KABAli  kwa kipindi chote cha uongozi wake.
                Siku moja Bi Kabali aliweza kumuita Mwanae wa kike ambae alimpenda sana. Mama anavyozaa watoto kadhaa basi hutokea mmoja ambae atampenda kuliko wengine japo haishauriwi kwani unajenga matabaka ambayo yatakuja kusababisha maumivu mbele ya safari......"Mwnangu NYAMIZI..."  Mama alimuita mwanae ...."Abee mama".... "kumbuka yale ninayokuambia kuwa baba yako anakutegemea wewe uwe Malkia wa MWENDA POLE lakini alijua kuwa utakutana na Vikwazo katika utwala wako mwanangu sawa...."......sawa mama nimekuelewa.lakini kwa nini sasa asimchague hata kaka pale mmoja mbona wataweza tu...." Mama yake Nyamizi alimuangalia Mwanae kisha akamshika uso wake na akamfuta kana kwamba anamfuta maji. ....."Mwanangu neno la marehemu halipingiki pindi likitamkwa kama la kutekelezwa kwani tukikeuka hatujui madhara tutakayoyapata.....". Nyamizi almkubalia mama yake kisha alinyanyuka na kuelekea ndani.
          Moja wa kijana wa Mfalme KABALI alitokea porini akiwa na kitoweo chake kwani ni muda mrefu sana tangu kifo cha Baba yao waliishi maisha ya kawaida sana sawa na wengine. Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la MASHA alifika kwa kumshitua mama yake kwa kumtupia kichwa cha Mnyama aliyefanikiwa kumnasa na kumchinja aina ya Swala. Mama yake alishtuka sana ndipo MASHA alicheka sana na kumkamata mama yake....."Aaah mama inaonekana ni muoga sana etii......" aliongea MASHA ......"Aaah Masha mwanangu mbona unataka kuniua mpema hivi?"....."Mama usijali upo na Mfalme hapa kwani mimi ndio mrithi wa baba hata hunioni Nimerudi na nyama nikiwa peke yangu huyu nimemkamata mimi mwenyewe na nikamchinja na leo dada NYAMIZI atapika na tutakula"....Mama yake alishusha pumzi kwani mtihani alionao wa kumkabidhi Kiti cha baba kati ya watoto wake hao. Lakini Masha alikaa kwa muda kisha akauliza kitu..."Hivi mama lini nitakuwa kiongozi wa hiki kijiji??...."Mh mwanangu Mbona mapema sana bado Mzee MWAYA na wenzake wakiwa tayari watatangaza kwa hiyo tutajua nani atakuwa kiongozi"...Kwa kweli Masha alisikitika lakini alijiaminisha kuwa yeye kwa kuwa alikuwa ni mtoto wa kwanza pia ni mwanaume basi atakuwa ni kiongozi wa hapo.
                 Siku kadhaa kupita bwana MWAYA alitembelea familia ya bwana KABALI. Alimkuta Bi kabali na  NYAMIZI wakiwa wanaongea. Nyamizi alitoka baada ya kumuona mwaya. ......"aaah mama malkia wa Mwenda pole".... "karibu mshauri wa kuna habari mpya gani huko utokako"...." Sasa hapa nina habari unafahamu kuwa kuna hawa wazee  wawili nakumbuka juzi tulikaa kikao ambacho kilihusisha hawa watu wanataka kuwa wafalme baada ya kufariki mumeo lakini nikaona sio vizuri lazima nije kupata ushauri kwako kuhusu huyu MASHA anaweza kuwa kiongozi mana hawa watu sijapendezwa nao".....Mzee mwaya alieleza jinsi gani kuwa hajaridhika na mambo ya watu ambao wanataka kuwa wafalme.
Mama nyamizi alifuta chozi ambalo lilikuwa linamtoka ....."Mwaya nakutegemea katika kutetea kauli ya Mume wangu alimtabiria kuwa Nyamizi aweze kuwa kiongozi japo ni mwanamke pia alisisitiza kuwa nyamizi aweze kuwa Malkia lakini sasa hawa wazee MAKASI na CHEPI wataharibu ndoto hiyo ya Baba yao".... Mwaya alikaa kimya sana kwani aliyoambiwa yalikuwa ni mageni. ....."sasa kumbe Mfalme alimtabiria mtoto wa kike awe Malkia yani kiongozi wa MWENDA POLE lakini inawezekana vipi kiongozi awe Mwanamke haujui kuwa ni kuzalilisha kijiji au unavyodhani nikimsimamisha Nyamizi kumtangaza kuwa kiongozi unadhani nitaangaliwaje na watu wa hapa ni bora hata kidogo huyo Masha ndie nilimfikilia mimi lakini si nyamizi"..... Aligoma kwa kukataa sana swala la Nyamizi aweze kuwa malkia wa pale. Kumbuka kuwa Nyamizi alikuwa ndani hivyo aliweza kusikia yale yote yaliyokuwa yanayongelewa. Mama Nyamizi aliinama tu chini hakuwa na la kujibu lakini aliamua kuomba msamaha..."Mh samahani naomba sana radhi lakini sasa hiyo ai kauli yangu ni kauli...." kabla hajamaliza Alikatishwa kauli ya kutoendelea kwani alimnyooshea kidole cha kumuambia akae kimya....."nyamaza wewe mwanamke yani huna la kuongea mbele ya wanaume mimi nilipewa dhamana ya kuongelea na kuendesha uongozi huu?? Hujui hilo sasa Atakae wekwa hapa ni Masha basi na si mwingine"...
              Mzee Mwaya aliondoka akiwa na hasira zake ndipo Nyamizi alienda kwa mama yake na kumfuta machozi. ...."Mama nimekuambia mwache tu kaka awe kiongozi kuliko wewe kuwa hivi"..."Mwanangu si kama nalazimisha nahofia yatakayokuja kutokea baada ya kipindi hiko kijacho"....Mzee Mwaya alifika nyumbani kwake na kumkuta Bwana chepi ambae alikuja kwa nia ya kuongea na Mwaya. Alimkaribisha ndipo Chepi akajieleza kwa kina kuhusu yeye kuwa kiongozi yapi atakayoyafanya. ......"Ngoja chepi nikuambie Kati yenu hakuna ambae anataka kuwa Kiongozi isipokuwa ni mtoto wa kiume wa Marahemu mfalme. Yani Masha ndie mfalme nenda kamwambie na huyo mwenzako MAKASI"...."Ebooo bwana Mwaya haya yapi tena umetugeuka mara hii na inawezekana vipi kijana mdogo kuwa kiongozi hataaa hiyo haipo nahisi utakuwa umechanganyikiwa kabisa unadhani utaonwaje na watu ukieleza habari hiyo eti"....."Nimetoa kauli mimi ndie naona nani anafaa yani Mama Masha Anataka mtoto wake wa kike eti Nyamizi ndio awe Malkia nyinyi mnataka muwe nyinyi. Nimeamua kumchagua mimi mwenyewe basi"....Chepi aliondoka kwa hasira na kuelekea moja kwa moja kwa bwana Makasi alibisha hodi alikaribishwa cha kwanza alimpa habari kutoka kwa Mwaya...."Makasi mwaya hatumuelewi anasema katutoa kwenye kuchaguliwa uongozi"...."katutoa alafu kamuweka nani?"...."yani huwezi amini kamchagua mtoto wa Mfalme yule kijana wa kwanza Masha ndie atakae shikilia"..... "haaaa haiwezekani Mwaya atufanyie hivi sisi wazee wenzake lafiki zake atufanyie hayo hapana"...."tena haitoshi kumbe mama yake Masha yani mke wa Mfalme alihitaji Nyamizi ndie awe malkia"...."haaa haaa haaa hapo sasa hakuna kitu yani tuongozwe na mwanamke hawaoni ni kukalibisha laana hiyo hebu ngoja twende kwa mzee NAMA akatabilie haya yanayosemwa."....
           Walifika kwa mzee NAMA na kukaa mkaoni na mzee kutabiria....."haya ni mawe manne  hili la mashariki NYAMIZI hili la Magharibi MASHA hili Kusini CHEPI na hili Kaskazini MAKASI sasa natupa hiki kidunguli kitakapokwenda kulalia ndie anatakiwa kuwa Kiongozi sawa?"....
"Sawaaa".... waliitikia. Kazi ya kuzungusha ilianza ilipoachwa ililala upande wa Mashariki ambae ni Nyamizi. Alijaribu mara kadhaa lakini ililala hukohuko walibadili upande lakini haikufaaa....."jamani kama mnavyoona hapa Nyamizi japo wa kike anatabiriwa kuwa MALKIA."....
Walihuzunika sana wazee hao walitoka huku wakitafakari njia ya kufanya. Mzew makasi alitambua njia ya kufanya......

Je? Ni njia gani

Itaendelea...



No comments: