Riwaya: CHOZI LISILOSAHAULIKA Sehemu: 02




                  ₱Ilipoishia₱
Mzee CHEPI na MAKSI walikaa na kutafakari kuhusu utabiri uliotokea kuwa NYAMIZI anatabiriwa kuwa Malkia na si mmoja kati yao. Walivyotoka pale kwa yule mzee ambae anatabiri walifika mahali na kujiuliza nini na wafanye nini. Mzee MAKSI alimueleza Mwenzake ambae waliamua kuungana baada ya kuambiwa na MWAYA kuwa katika orodha ya kuwa Wafalme hawapo kabisa ndipo Mzee MAKASI alipata ufumbuzi....

                   ₱Endelea₱
Kumbuka kuwa hawa wazee wawili ni wale ambao wanafanya jitihada za kutaka kusimamisha ufalme kati yao na waliopania kuupata kwa njia yeyote ile...."Chepi hivi unadhani kuwa hii ni halali kabisa ambacho Mwaya anataka kutufanyia?"....Makasi alimuuliza rafiki yake Chepi...."Mhh!! Kwa upande mwingine naweza sema hajatenda haki kabisa lakini sio mbaya kumuweka MASHA lakini si kwa yule binti NYAMIZI ni udhalilishaji"....Lakini haikutosha hawakuamini majibu ambayo waliyapata kutoka kwa yule Mtabiri ambae aliwapa majibu mazuri ya kuwaambia kuwa ni Nyamizi pekee ndie anayetabiriwa kuwa Kiongozi wa pale MWENDA POLE na si yeyote kati yao. ..."Chepi hapana hebu jiandae tuende kwa mtabiri ambae alikuwa anamtabiria Mfalme KABALI labda tutapata majibu mazuri yani tunavyokubalika sisi iweje iwe tofauti?"..."Haswaa tena Mwaya naanza kumchukia kabisaaa"...waliondoka na kuelekea mbali kidogo na Kijiji cha Mwenda pole kwani wahenga wanasema  Mtaka cha uvunguni sharti ainame na wengime wakaongezea kwa kusema 'Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga' ndicho ambacho kwa hawa wazee kilichofanyika.
             Walifika huku Mzee Chepi akiwa anaangalia nyuma kama kuna mtu anawaangalia wapi wanaelekea. Wakati huo Masha mtoto wa kwanza wa mfalme Kabali ambae ni Marehemu aliwashuhudia wale wazee wakielekea nje ya kijiji lakini hakutambua wapi wanaelekea. Alifanya haraka sana kwenda kwa mama yake na kumkuta akiwa anaandaa moja ya mapambo ya mwanae....."Mama hivi hilo pambo unaloliandaa si la Kimalkia hilo una maana kuwa Mzew Mwaya kasema kuwa Nyamizi ndie atakuwa kiongozi??"....Alimuuliza mama yake baada ya kumuona akiandaa mapambo ya Kimalkia...."Hapana mwanangu haya ni ya zamani ambayo baba yenu alimuandaliaga Nyamizi sasa nayaweka vizuri tu sawa mwanangu"...."alafu hivi wale wazee wanaelekea wapi? Huyu Chepi na Makasi mbona jioni hii nimewaona wanaelekea kulee kwa Babu NJIMBI?".....Mama yake alistaajabu baada ya kusikia kuwa wazee hao wanaenda kwa Mzee Njimbi...."Haaaa wanahatali hawa watu kuna nini kikubwa kilichofanyika hapa kijijini? Haya hebu nenda kwa Mwaya kamueleze habali hii".... Masha aliondoka na kufika kwa mzee Mwaya alimueleza yote ambayo aliyaona...."sawa nashukuru kweli wewe utakuwa kiongozi ambae anatakiwa kuwa na ujasiri kama huu mimi nitahakikisha nalifanyia kazi muda si mrefu"....
                Haikutambulika kwa nini wawekee wasiwasi mkubwa kwa watu wale ambao wanaelekea kwa mzee Njimbi na kuna jambo gani baya ambalo litazua baada ya wao kwenda huko. Tukiwa upande wa wale wazee wawili Bwana Chepi na Makasi walipofika ilikuwa giza ndio inaingia hivyo ilikuwa rahisi kwao kumkuta mzee Njimbi. Walikaa kwenye mkao na kumueleza shida yao...."Njimbi pamoja na Mizimu yako sisi ni vijana wawili watoto wako ambao tupo mbele yako kuomba ufalme huu uangukie mikononi mwetu lakini tuna shaka na kauli ya Mwaya ya kumtaka mtoto wa mfalme....Masha awe Mfalme lakini ajabu tunashangaa zaidi utabili wa NAMA baada ya kusema kuwa...Nyamili ndie aweze kuwa Malkia sasa tumekuja kwako tusaidieeee"......Mzee Makasi aliongea kwa hisia zake zote ili kuonyesha kama kweli wao wanashida na ufalme...."Haaaa Haaaa Nimewaelewa hapa naona kuwa kweli Nyamizi ni binti aliyechaguliwa na Mfalme Kabali pamoja na Mizimu inayomlinda kabali lakini haina shida kama mnahitaji kazi hii iwe rahisi kwenu mtakuwa tayari kufanya yafuatayo?"..."Aaah kumbe ni kweli Kuwa nyamizi atakuwa Malkia lakini itawezekana vipi?"...."Haaaa haaaa hujui kuwa mfalme akimchagua mtu awe kiongozi anapelekwa na Mizimu imchague yule ambae ataongoza vizuri lakini tutatoa picha mbaya kwa wana Mwenda pole tena ni aibu sana sasa kama mtakuwa tayari mufanye haya yafuatayo"....
                 Waliangaliana wawili hao ili watoe jibu ambalo litakuwa sawa kwa wote. Wakiangalia muda unasonga sana hivyo iliwabidi wamjibu mzee Njimbi haraka....."Bwana lolote liwe hatutaki aibu hii itukute Mzee Njimbi tuko tayari kufanya kazi hiyo"....walikubali na kumsubiri atawaeleza nini....."Aaagryaaaa aaagryaaa Haaa!! haaa!!! haaaa!!! Sasa mizimu inahitaji mfanye yafuatayo mnapewa siku tatu muwe mmefanikisha kuleta hapa Mayai Matatu ya Bundi ambae katagia maeneo ya makaburi pia muyachukue mayai hayo nyakati za usiku kisha mkifanikisha leteni hapa siku ya nne na mtakuwa mmefanikisha".....Chepi na Makasi walinyanyuka na kuanza kurudi nyumbani kwao. Walipita kujadili wapi ambapo watayapata hayo mayai. Walitembea kwa wasiwasi kwani walivyotoka hawakutaka kujulikana wapi wameelekea na wanavyorudi hawataki kujulikana wanatokea wapi. Hivyo walifanikiwa kufika mpaka kwao kwa kila mmoja bila kuonekana. Asubuhi na mapema kilitangazwa kikao cha dharura na Mwaya ambacho kilitakiwa watu wote wafike pale walipo ili kuelezwa mambo muhimu ya maendeleo ya kijiji cha Mwenda pole.
                Watu walifika kwa wingi sana kuja kushuhudia hayo yanayohitajika kuzungumzwa kwa muda huo. Mzee Chepi na Makasi wakiwa njiani wanaelekea kwenye hiko kikao..."chepi mchana wa leo baada ya kikao tutembelee makaburi tukague tujue tunayapata wapi kisha baada ya hapo usiku tunakuja kuyafuata"...."sawa haina shida alafu najua Mwaya anatuchukia sana kwani sisi tuna sela nzuri pia mmoja akiwa mfalme mwingine anakuwa baada ya mfalme mambo yatakuwa vizuri sisi wazee ndio wakuongoza haya mambo lakini si wale watoto"....walifika pale kwenye kikao na kumkuta Mzee Mwaya akiwa anaongea na kuwaweka sawa kabla nini ajasema...."Haya sasa wanakijiji wa Mwenda pole mpooooooo"....
Aliuliza kwa bashasha sana....."tupoooooooooo"......"Nataka kuwapa taarifa kuwa siku zijazo tunatangaza uongozi na nani atakuwa kiongozi lakini bila kusubiri namtanguliza kwenu mtoto wa mfalme kijana Masha kuwa atakuwa mmoja wa watu ambao wataweza kuwania kiti cha baba yake akiwemo na wazee wawili Chepi na Makasi"...watu walifurahi sana.
            Lakini aliwatuliza na kuwaambia kuwa kesho kutwa watatakiwa kufanya mtihani mmoja...."lakini Kutakuwa na mtihani atakae shinda ndie anachukua kiti...Mnajua mfalme KABALI aliacha fimbo yake kwenye pango la MLA NYAMA. Sasa mtatakiwa kesho kuja pale nyumbani ili Mpewe maelekezo...lakini Mtatakiwa kuichukua fimbo hiyo na kuileta hapa atakaekuja nae ndie mshindi hili litamhusu Masha,chepi makasi na yeyote yule anayehitaji".....watu waliitaji kusubiri siku hiyo.
                  Kikao kilifungwa na wazee hao wawili Chepi na Makasi walielekea makaburini. Katika tafuta yao wakabahatika kukuta mayai ya kutosha na Bundi akiwa kakalia...."eheee hapa hatuchelewi usiku tunakuja hapa"....walirudi huku wakipeana ushauri wa kuipata fimbo hiyo..."Makasi kama Nyamizi katabiliwa kuwa Malkia Basi jua kuwa hata hiyo fimbo ataipata Nyamizi"....."Haswaaa ndio maana tukipeleka yale mayai kwa Njimbi yatabadilishwa hayo yote na kuwa upande wetu. Waliongozana na kufika kijijini. Majira ya usiku hawakufanya ajizi walienda kuyachukua alafu wakasubiria majira ya asubuhi ili waende kwa Mwaya wakapate maelezo kuhusu uchukuaji wa hiyo fimbo. Ajabu iliyoje kijiji cha Mwenda pole walijaa Bundi kila mahali na kelele zao wakiendelea kulia. Makasi na chepi walijawa na wasiwasi sana baada ya kuona hali ile na kila mwanakijiji alijiuliza ni nini ambacho kimejili mpaka ndege hawa ambao wanatafsirika vibaya wakajaa maeneo hayo.  Baada ya maelezo kupewa kwa wale wote waliohitaji kupata uongozi huo. Wazee hao walienda kwa Mzee Njimbi kumalizia kazi yao.......

Itaendelea



No comments: