RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA SABA 07





LIKE , SHARE NA COMENT USISAHAU KUSAMBAZA CHAPISHO HILI

ENDELEA.....
................Nilibaki kucheki mchezo unaendeleaje kati ya wale wawili na yule mzee ambae alikuja kunipa lile dili. Niliwaona wakiongea kwa mbali hivi ndipo nikamuona yule mzee akinionyeshea mkono kama anawaonyeshea mimi pale nilipo. Nikaona mambo sasa yanaenda mwake mungu anaanza kunionyesha njia.
Ndipo aliponiita na mimi sikufanya ajizi maana haya mambo ni kuwahi ukicheza tu kuna vijana wengi sana ambao wapo pale wanatafuta hata nafasi ndogo ya kupata miambili. Nilitembea haraka hadi pale walipo.
"Ehe! Sasa huyu kijana anaitwa Mnali, ndie kati ya wale vijana ambao wataifanya ile kazi". Nilimeza mate kwanza kujiweka safi koo langu ili nipate kujibu kama nitapata swali.
"Sawa nimemuona sasa mbona kama mdhoofu sana ataiweza kweli". Alinitazama yule mzee kisha akaniminyia jicho.
"Hapana yani huyu kijana hapa ufukweni anajulikana kama unakumbuka juzi nilikuambia kuwa kashika samaki wengi sana tena wakubwa ndio maana nikakuletea". "Haya twende ndani ya gari alafuuuu wale wengine nitakuja kesho kuwaona acha huyu nikaongee nae". "Sawa bosi wangu ila kuwa makini mtunze kijana wangu huyo". Niliombwa kuingia kwenye lile prado, niliingia kisha tukaondoka pale hadi kwenye hoteli moja hivi kubwa tena nzuri ya kifahari. Nilikuwa mshamba sana ndani ya gari kwani sikuwahi kupanda gari hilo maana maisha yangu baiskeli mpaka tunafika kwenye hoteli siamini kabisa.

Nikiwa pale hotelini nilishindwa hata kukaa maana vitu vilivyomo mule ni adimu sana tofauti na nilivyozoea mimi mwenyewe. Nguo zangu hazikuwa na hadhi ya kukalia kochi safi za bei kama zile niliona nachafua.
Yule Jamaa alikuwa mnene sana alinikaribisha mezani ili tuanze mazungumzo. "Hapana bosi nguo zangu chafu ona nitachafua hapa samahani sana nitasimama". "Haaa! Haahaaaa!" Alicheka sana " kijana usinifurahishe ni kawaida kabisa wewe kaa tuongee mambo hayo wahusika wapo,". Nilikaa kisha nikawa namsikiliza. "Kijana nahitaji kufanya kazi na wewe naitwa Mr. Paul hii ni hoteli yangu ndio ambapo hao samaki wanahitajika, sasa je? Unataka nikulipe kwa kiasi gani na kwa muda gani?". Daah! Ilikuwa mtihani sana kwangu kutaja bei mpaka alinigundua kuwa nashindwa kutaja bei ambayo itakuwa nafuu kwangu. "Ok! Usijali nitakulipa kwa mwezi laki tatu pamoja na kila siku elfu kumi na nitakulipa kubwa zaidi ukiniletea mzigo mzuri na mkubwa sawa". Nilimshukuru sana mpaka nikamsogelea pale kutaka kuzidi kushukuru. "Hapana kijana fanya kazi nione kwa sasa utashika hii laki moja utaenda kutumia ila kesho njoo nimeagiza boti toka nje likija nitakukabidhi uanze kazi haraka sana." " nakushukur pia nakuahidi kuwa nitaifanya kazi yako vizuri sana bila hata uwoga wowote.". Hakika alifurahi sana. Basi nilirejea hadi kule ufukweni nikiwa na amani tele maana mfuko umetuna japo nilitoka kula vipigo kwa Mama Asante.
Baada ya kufika ufukweni nilijitahidi kumtafuta yule mzee kwanza nilifanikiwa kumpata ndipo nilianza kumueleza kile ambacho nilikipata kutoka kwa Mr Paul. "Babu kwanza nashukuru sana maana niliyoyapata kule ni makubwa na ambayo sikutarajia kabisa kuyapata", "yapi hayo?" Aliniuliza. "Mh! Kwanza nimefika tu tukapandisha juu ghorofani mule ndani mnanukia sijui harufu gani ile nimeipenda sana kama ni mafuta basi mazuri zaidi ya maelezo, Kingine nilipewa kinywaji kizuri sana pia niliwaona wazungu pale". Wakati naendelea kuongea ndipo akanisimamisha kwanza "Ebu eleza mliongea nini maana unazunguka sana mpaka nashindwa kukuelewa".
"Daaah! Babu kanipa kazi kuwa kwa mwezi atanipa laki tatu alafu kila siku elfu kumi na nikimpelekea samaki wengi ataniongezea hela na pia kesho boti la kutumia mashine linakuja atanikabidhi na kazi kuanza". Nilimuona mzee kama kasizi hivi kisha akanipa mkono akataka kuondoka, ndipo nikaingia mfukoni nikachukua elfu thelathini na kumpatia nilivunja mzizi wa fitina kabisa pale.
Ile siku niliimaliza na furaha ndipo nikaelekea nyumbani kwa mke wa Kibona na kumuangali. Napo niliwaachia kiasi cha fedha na mimi kuelekea nyumbani. Usiku wa manane nakumbuka niliota ndoto mbaya sana nilipoamka nikajishangaa mwili wangu unatokwa na jasho jingi ambalo ni tofauti kwangu likanifanya nitoke kwenda kuoga huku nikiwaza kipi kinajiri. Wakati huo nafahamu niamke nielekee kwa yule mzee kukabidhiwa kazi rasmi. Kama kawaida yangu asubuhi lazima nipitie kwa Mke wa Kibona ndipo nielekee ufukweni kuangalia mazongira halisi. Nilipofika ufukweni sikuamini pale nilipokuta Nyavu zangu pamoja na mtumbwi wangu umechomwa moto nilihuzunika sana, kila mtu niliekuwa namuuliza hakunijibu sawasawa ilionekana kama ni dili la wale vijana kuniharibia. Yule mzee alitukutanisha vijana watatu ambao tunahitajika na yule tajiri. Tulikaa mimi nikiwa nafikilia nani kafanya ule ushenzi wenzangu wanafurahia tu.
Ndipo lile gari likaja na wote tukaingia kwenye lile gari hadi sehemu ya kazi ambayo tunatakiwa kufika. Walipewa mikataba wale wengine ndipo na mimi nikapewa sehemu ya kuthibitisha kuwa pindi ninapopoteza maisha mrithi wa pesa zangu ni nani nilimuandika Asante pamoja na ndugu yangu mmoja. Sikuwa na uhakika kama kweli Asante kafa.
"Sasa, vijana Hoteli yangu kuna wageni wengi wanakuja sasa leteni mzigo mkubwa pia mkifanya vyema zaidi naweza kuwagawa kuna tajiri mwingine na yeye anatafuta vijana kama nyinyi sawa".
Tuliitikia kwa pamoja. Ndipo tukatolewa kuelekea bandarini huko tuliikuta Boti moja Kubwa ambayo tutaweza kuitumia. Hapohapo tuliingia na dereva wa lile alielekezwa maeneo gani ambayo akaiweke, tulifika hadi kule na tukakaa kupata maelekezo zaidi ya kazi.

TUKUTANE TOLEO LIJALO



No comments: