RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA TANO 05
ENDELEA.....................
................Baada ya kuamka nilijihisi kama kaufuraha fulani hivi kwa kuwa ile hali ya kuona nyavu yangu imejaa samaki wengi nikaona kweli unaweza kuota ndoto kuwa umejenga ghorofa kubwa sana lakini ikawa ni tofauti kabisa na uhalisia.
Niliamka toka pale kitandani, kisha baada ya hapo nikajiuliza nifanye nini ambacho kitaniwezesha na maisha yale magumu. Nilinyanyuka nikaelekea kwa Familia ya bwana Kibona niliwakuta wakila chakula na mimi nikaungana nao mpaka pale nilipohakikisha maua ya sahani yanaonekana. Nilipata wazo kuwa nitembelee ufukweni tena. Nilipofika nikaona bahari asubuhi ile mapema imechafuka kweli hata kuingia na mtumbwi kama unajitakia matatizo. Nilijishangaa napatwa na hamu ya kuchukua mtumbwi na kutaka kuingia hata hivyo walikuwepo vijana ambao walikuwa wananishangaa na wengine wakawa wananisihi kuwa nisijaribu kwenda kwani ni hatari.
"Kijanaaah!. Acha kabisa hayo mambo unaona maji mengi hayoo...!"
Mzee mmoja aliongea huku akinikaribia, lakini hata hivyo moyo wangu pia ulinisukuma kuingia ndipo nikausukuma ule mtumbwi hadi karibu na maji mengi nikaingia ndani yake na kuanza kupiga kasia ili kufika katikati. Nikiwa naelekea kule huku nchi kavu watu wananishangilia na wengine wakinisikitikia sana lakini hata mimi mwenyewe nilijishtukia lakini ikawa kama kuna nguvu inanisukuma hivi, na ikinipa hamasa ya kuendelea. Nilijikuta niko mbali kidogo na nchi kavu moyo ukanituma nitoa nyavu mpya ambayo ilikuwemo mule na kuitupa.
Baada ya kuitupa nikawa naangalia, ndipo kwa mbali kidogo nikaona maji kama yanapanda alafu yanashuka..yanapanda kisha yanashuka..yanapanda kisha yanashuka mithlo ya mawimbi makubwa lakini ilikuwa kama kitu ambacho kimejikusanya alafu kikawa kinakuja upande wangu kwa mwendo mdogomdogo. Nilijipa moyo kwa kusema mungu yupo. Hatimae mtumbwi wangu ulianza kusumbua nilianza kupata hofu kwani maji mengi alafu hayajatulia nikajisemea moyoni 'kipi kimenileta na sikusikiliza ya watu?'.
Kwenye ile sehemu niliona kama nyavu ambayo inaonekana. Niliifuata kisha nikaahuhudia kuwa ni ile nyavu yangu ya jana. Nilichukua fimbo ambazo tunatumia kuvutia Nyavu nikaikamatia vyema kisha nikaiweka kwenye moja ya tundu ya ile nyavu kisha nikaanza kuivuta.
Aaah! Hakika ilikuwa ni nzito sana. Niliiweka hivohivo nikafunga nyuma ya mtumbwi ndipo nikaanza kupiga kasia baada ya kuitoa ile ambayo niliiweka muda mchache. Nilipiga kasia kwa nguvu zote baada ya kuhisi labda ile ndoto itakuwa inafanana kweli na jinsi nilivyoiona net yangu. Mawimbi yalinipiga sana lakini nilijikaza niliona nchi kavu watu wakiwa wamejipanga kuniangalia nadhani watu walijua nitapotea na nitakufa hukohuko kama ndugu yangu Kibona.
Niliona watu wakifurahi mimi nikiwa sijui kipi wanakishangilia.
"Eeeh! Jamaniii wengiiii alafu wakubwa kweli...eeeeh ndioooo!".
Nilishangaa kusikia wanasema vile ndipo nikaangalia nyuma na kushuhudia lundo la samaki wakubwa hakika furaha ya ajabu sana ikinijia nilishuka wachche walinisaidia kuwatoa kuna samaki ambao walikaa ndoo kubwa akiwa peke yake.
Watu palepale walijaa wakiulizia bei. Ndani ya masaa kadhaa pesa nyingi nilipata kwa makdilio mauzo yalikuwa ela nyingi. Japo wengi waliniibia kwa kuwa nilishikwa na bumbuwazi kuona maajabu kama yale. Ilifika majira ya saa saba mifuko ilituna ndipo nikaondoka nyumbani huku nyuma nikiwa nimewaachia mshangao mkubwa sana.
Baada ya kufika nyumbani ndipo nikajifungia ndani na kuanza kuhesabu mapato yangu ya maajabu. Kweli mnyonge riziki yake bado ipo muda na saa yeyote ile kikubwa ni uvumilivu wake tu. Nilipanga kiasi cha laki moja na nusu nikaenda kumpatia Mke wa Kibona kwani bila yeye nisingepata mavuno haya. Furaha yake naamini kuwa itaniwezesha mimi kupata vikubwa zaidi ya hivi.
Baada ya wiki nilifanikiwa kununua mashine za kusukumia mtumbwi. Niliona maisha yangu sasa yakiwa mazuri ndipo nikaamua kumtafuta mtoto wangu Asante, maana mtoto mwingine alikuwa wa kumkuta alizaa na mwanaume mwingine. Malengo yangu ni kutaka kulea damu yangu. Nilipata bahati ya kujua wapi anaishi yule mwanamke ambae kwa sasa si mke wangu tena. Nilifanya juhudi zote na kufika hadi mahali ambapo anaishi kiukweli ni pazuri sana. Niliamua kuachana na kazi ya uvuvi mpaka pale nitakapohakikisha mwanangu anakiwa kwenye himaya yangu. Nyumba kubwa ya kifahari iliyopo mbele yangu geti likiwa limefunguliwa na gari nzuri sana inatoka.
Kwa kuwa nilikuwa na uhakika kuwa ndio pale anapoishi Asante na mama yake niliwahi haraka na kulifikia lile gari.
Uzuri lilisimama na kufungua kioo!. Daah! Sikuamini macho yangu.....
TUKUTANE TOLEO LIJALO

No comments: