RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA NNE 04
ENDELEA..................
................Baada ya Miezi kadhaa kupita hali yangu iliweza kutulia kabisa na kuwa na unafuu, nilijikuta nikiwa peke yangu ndani ya nyumba yangu japo nilizoea kuonana na wanangu pamoja na mke wangu. Siku hiyo nilitoka zangu nikaelekea nyumbani kwa bwana Kibona ambako nilifanikiwa kumkuta mkewe ambae yupo akiwa kwenye hali ya majonzi kama mjane. Nilijitahidi kumtuliza na kumueleza kuwa ni mapito tu ambayo kila mmoja anatakiwa kuyapitia.
Ili kumpa matumaini zaidi nilimueleza jinsi mke wangu alivyonikimbia kutokana na hali ya maisha yangu. Kadai taraka na niandike kuwa taraka tatu si mke wangu tena. Hapo ndipo alianza kujishangaa yeye na akaacha kulia. Mipango tuliyoipanga ni kuwa nitajitahidi kuishikilia ile familia na kuihudumia kama alivyokuwa akihudumia marehemu kibona. Hapo ndipo alinipatia kila kitu ambacho bwana kibona alikuwa anatumia katika harakati zake za uvuvi.
Nilijipa moyo kuwa nitafanikiwa na kupata samaki wengi tena wakubwa sana nilichukua zile nyavu tena zingine zilikuwa ni mpya kabisa hivo sikupata tabu ya kutaka kununua nyavu zingine hali ya kuwa mpya zipo pale. Sikuwa mzoefu sana katika harakati za uvuvi japo nilikuwa na uelewa nao kidogo nilioupata kwa muda mfupi ambao tulikaa na bwana kibona. Maisha yangu sasa yalibaki kuwa ya uvuvi kwani hakuna jambo ambalo nilikuwa nalitegemea tofauti na swala hilo.
Siku iliyofuata nilidamka asubuhi kwanza kisha nikatembelea baharini, lengo kuu lilikuwa ni kuangalia mazingira ya pale baharini. Ilikuwa kama majira ya asubuhi sana na kipindi kile ambacho mvua zimeacha kunyesha karibuni. Kipindi hiko kilikuwa cha Bamvua la kushitukiza yaani kipindi cha Majikujaa ambayo yalikuwa yanashitukiza. Sikuwa nafahamu nilichoelewa ni kuwa maji yatulie. Kwa mbali nilishuhudia samaki mkubwa akiruka juu na kuingia tena ndani ya maji. Nilishtuka na nikajua kitu tofauti na samaki kimemdhuru kumbe ilikuwa ni kawaida pale aliporejea ule mchezo kama mara mbili hivi.
Vijana wengine nilipata kuwasikia kuwa ni Papa lakini mimi sikuwa namfahamu anafananaje huyo papa. Kidogo majonzi yalipungua lakini nilifahamu kuwa bado mke wangu ataendelea kuwa kichwani mwangu lakini ndio basi siwezi kuishi nae tena kwa kuwa yeye si mke wangu kabisa. Nilikuja kushtuka muda umekwenda mfukoni nina senti chache nahitajika hata ninunue samaki kwa ajili ya familia ya Kibona pamoja na mimi mwenyewe. Kiasi cha pesa nilichonacho hakiwezi kununua mahitaji ya pande mbili yani hata kwangu mwenyewe hazitoshelezi. Ndipo nilipomuendea jamaa mmoja alikuwa anauza samaki pembezoni mwa beach.
"Habari yako...samaki hawa naweza pata kiasi gani?". Niliweza kumuuliza ili ninunue. "Hao wote elfu mbili" Fedha niliyonayo shilingi miatano "basi naomba unisaidie Samaki hawa nina shida ya mboga kesho nitakupitishia hapa mimi pia ni mvuvi nitakupatia pesa yako kesho asubuhi kwa sasa nina kiasi hiki cha miatano". Nilimshangaa akiwa ananicheka sana huku akinisikitikia. "Weee mvuvi wa wapi wewe acha kuingilia kazi za watu sema una shida usaidiwe lakini usijitie mvuvi....".
Japo na zile dharau aliweza kunipatia wale samaki ndipo nikaenda kumpatia mke wa marehemu Kibona na mimi nikawachukua wachache nikarejea nyumbani. Nikiwa nawaanda nilimkumbuka mama Asante, mpaka napika nilikuwa namkumbuka yeye, hakika alinikaa kweli akilini.
Majira ya jioni nilifika baharini nikaelekea pale ambapo mtumbwi wangu ulikuwa unakaa kutokana na Kibona alipapenda. Niliuchunguza ndipo nikaingia na kuanza kupiga kasia zangu kuelekea kwenye kina kirefu cha bahari ili nitundike nyavu humo.
Uoga ulinitoka kwa kuwa mimi pekee ndie nategemewa na familia ya Kibona. Nilifika katikati, nikafanikiwa kuiweka Nyavu ile kisha nikawa nimetulia kusoma mazingira na muda wa kuitoa.
Chemli yangu ilikuwa na mafutaa mengi ya kutosha ghafla nilihisi kama kichwa kinaniuma hivi, kwa mbali niliona taa za wavuvi wenzangu wakiwa wansogea karibu kwa kuwa ni kawaida. Nilijikuta nalala ndani ya mtumbwi wangu usingizi mzito kweli. Ghafla pumzi nahisi kama zinaniishia ndipo najikuta mtumbwi maji yamejaa unataka kuzama. Nilipata hofu isiyo na mchezo. Nilipata ujasiri nikayatoa kwa kutumia kikombe kilichopo ndani yake.
Ajabu zaidi pale nilipojikuta niko peke yangu bahari nzima. Niliyapakua mpaka kuchoka huku nikipiga kasia kurejea nchi kavu bila kujua kama wavu upo au laa! Nilipofika karibu na nchi kavu nikasikia kicheko kama mtu ananicheka mimi. Nilipaniki sana ndipo nikajikuta najitupa ndani ya maji na kuanza kutapatapa mpaka nje, nilikunywa maji ya kutosha ambayo yalinisumbua sana mwilini nilichojua ni kuutoa mtumbwi wakati huo chemli imedondokea ndani ya maji.
Sikutamani hata kujua chochote kile tu kiliniogopesha. Nilirejea nyumbani kabisa usiku huo huku nikiwa nakumbuka maneno ya Kibona kuwa baharini kuna mambo mengi kikubwa vumilia. Nilifika nyumbani nikalala bila kujua ni saa ngapi.
Nilijikuta naingia kwenye ndoto kubwa inayonielezea mazingira ya bahari na ile net niliyoiacha nikiwaona samaki wakubwa sana wakiwa wanaingia ndani yake. Nilizidi kushangaa mpaka pale nilipowaona wamejaa mpaka net inataka kuchanika na wanashindwa kutoka. Nilishtuka toka kwenye ndoto hiyo na kujikuta niko Asubuhi na kichwa kinaniuma kutokana na yale maji chumvi.........
TUKUTANE TOLEO LIJALO

No comments: