RIWAYA:: KAZI YANGU YA UVUVI SEHEMU YA TATU 03
ENDELEA........
..................Ilikuwa ni pigo kubwa sana baada ya kupata taarifa ya Kibona kupotea Ndani ya Bahari. Sikuwa na raha kutokana na hali ya mwili wangu haukuwa vyema kabisa. Baada ya miezi kadhaa nilipata nafuu lakini matatizo mengi pale nyumbani.
Nilianza kutafuta sasa jinsi gani naweza kujitatua na matatizo yangu niliyonayo. Kutokana na hali ya kukosa pesa ya kuihudumia familia yangu ndipo chokochoko kwa mke wangu.
Hapo ndipo alipoanza kubadilika, sikudhani kama anaweza kubadilika kwa kiasi kama hiki, kwanza maongezi yalianza kukata kati ya mimi na mke wangu, alianza kugoma sana hata kuongea na mimi hapendi kabisa.
Nikitoka nyumbani basi na yeye anatoka kurudi alianza kurudi usiku lakini anarudi akiwa na mboga pamoja na Mchele. Nilikuwa sina nguvu ya kufanya kazi ngumu ambazo zingeniwezesha kupata kipato cha kuhifadhi familia yangu.
Nilizidi kuumia sana zaidi ya maelezo majibu ya mke wangu yalinionyesha dhahiri kuwa sasa kanichoka kabisa. Hata nikihitaji haki ya ndoa lakini nilinyimwa huku akisema kuwa kachoka sana.
Nilijaribu kupata hata ushauri wa Marafiki zangu nipate hata ushauri. Mwili wangu ulikosa nguvu kutokana na maradhi niliyokapata. Niliamua kumfuata Dada mmoja alikuwa rafiki wa Mke wangu Mama Asante.
"Monika, samahani nahitaji kujua kwa nini mke wangu anakuwa vile?, siku hizi kabadilika kabisa nakuomba hata umueleze kama kuna jambo nimemkosea basi aweze kuniambia labda naweza kujirekebisha".
Nilimuambia kila kitu ili niweze kupata msaada. Monika alinionyesha hali ya kutaka kunisaidia baada ya kunionea huruma kutokana na hali niliyonayo.
Niliondoka na kwenda nyumbani huku nikiwa hoi kabisa, homa au ugonjwa nilionao sikuufahamu kabisa kwa sababu sikuwa na pesa baada ya bwana Kibona kupotelea baharini. Ilipita siku kama mbili mke wangu hajarudi kabisa nyumbani wanangu walikuwa wananiuliza sana kuhusiana na mama yao kutoonekana.
Siku ambayo alirudi alikuwa na hasira sana na kiburi kikubwa sana baada ya kuona kuwa namtegemea yeye.
"Mke wangu, haya kulikoni huko utokako siku ya tatu hii hujarudi watoto wanakuulizia"
Niliweza kumuuliza lakini hakunijibu kitu.
Nilimfuata hadi chumbani ndipo nikamshuhudia akipanga nguo zake kwenye begi.
"Mke wangu bado hujanieleza kulikoni".
Sikuamini kama Mama Asante atanisukuma na kuangukia sufuria yenye maji machafu ikafanya suruali yangu kuchafuka lakini sikuwa na nguvu ya kusimama kutokana na mwili kutetemeka.
Nilibaki kuumia moyoni huku nikiwa nimechutama pale chini. Nilijikongoja kidogo kisha nikainuka na kumsogelea mke wangu. Sikuadhania kabisa kwani alinikunja shati langu shingoni huku akinisukuma hadi ukutani nilijigonga na kichwa Tiii!, kama mti ulioanguka chini, chozi lilinidondoka nashindwa kumzuia nguvu sikuwa nazo.
"Nakuomba unielewe wewe mwanaume usiejitambua, siwezi kukulisha hapa kila siku. Nataka utambue kuwa, nimempata mwanaume ambae anaweza kunihudumia! Pia usinisumbue na sasa nakutaka uniandikie Taraka haraka sana laaa! Sivyooo! Nitakuharibu sasa hivi."
Alipoanza kuongea hadi anapomaliza, sikuwa naamini kama kweli anaweza kunifanyia haya anayonifanyia.
"Mke wangu nikuache kwa sababu gani maalumu ambayo inasababisha wewe kutamka hivo mke wangu".
Alinipiga kama mtoto vile mpaka nikaanguka chini. Nilipandwa na jazba nikajikakamua kuinuka kisha nikataka hata kupambana nae lakini niliishia kufinywa kipigo alichonipiga hakika sikufahamu maana maumivu yalinizidi hadi nikatamani kulia.
"Mke wangu Unaniuaaaaaaaah!"
Nililalamika sana. Lakini hakutaka kunielewa ndipo alipochukua karatasi na penina kunijia pale nilipo. Alinilazimisha nimuandikie Taraka ili nimuache.
"Andika nitakunyonga...pumbavu wewe".
Basi niliandika Taraka tatu si mke wangu lengo ili nilinde maisha yangu.
Aliwachukua watoto kisha akaondoka nao.
Sikufahamu wapi kaelekea mimi nilibaki kulala pale kitandani. Nilizidi kuugulia kutokana na hali niliyonayo, rafiki yangu Kibona sitomuona tena, maisha yangu nilitarajia Uvuvi sasa hakuna chochote ambacho naweza kujitetea ili kupata fedha yeyote ile. Basi niliamua kukalisha hata uji ili nipate nguvu, niliyafanya hivyo ili nipate nafasi ya kwenda kutafuta chochote.
TUKUTANE TOLEO LIJALO

No comments: