Riwaya: NDOA NDOANO Sehemu: 11





             ★  LINDI-RUANGWA★

                         ★Endelea★
Asubuhi na mapema sana Makame na Mwamvita walitoka na kutokomea maporini kwa lengo la kujificha kutokana na kuwakwepa watu wa Mbei na Maposo.
Mzee Mashauri alikuwa wa kwanza katika kuwasaidia na kuwatafutia mahali pazuri ambapo wataweza kukaa kwa muda kipindi wanamtafuta Mumwa. Haikuwa rahisi sana kwani sehemu ambayo walikuwa wanakaa huko porini palikuwa sehemu ya hatari

Asubuhi hiyo Maposo alishituka baada ya kuona mlinzi wake akiwa kajeruhiwa vibaya mno hapo nje baada ya ile vita ya muda. Alijua kama mlinzi kafa basi itakuwa hata Mwamvita hayuko salama. Alihangaika na akatoa amri kiwa mke wake kadhurika na hajui wapi katokomea. Walianza kumtafuta kwa udi na uvumba walifika kwa Mzee Mashauri lakini hawakukuta kitu....."Mnasema mwanagu kapotea?"....Aliuliza mzee Mashauri kana kwamba hajui nini kinachoendelea.

Hawakumjibu chochote zaidi qalichofanya ni kuzunguka nyumba lakini hawakufanikiwa na lolote. Walirudi na kutoa taarifa ya kutomkuta Mwamvita. Taarifa ya kutoonekana Mwamvita ilisikika pia walinzi wote walionekana akiwa mmoja ndie alifariki lakini Makame na Mwamvita hawaonekani. Maposo aliumia sana...."haya najua Makame kakimbia na mke wangu sasa nendeni mkakamate wazazi wake mlete hapa nadhani akisikia mmoja wao kafa atakuja na atatueleza wapi kampeleka Mwamvita".....walitoka hadi kwa wazazi wa Makame mchana huo walichofanya ni kuwakamata familia hiyo huku watu wakishuhudiwa wanavyokusanywa kwa kudhalilishwa....."nyinyi wanakijiji kama hamtaki kuwatoa Mwamvita na Sumae hawa wanakufa huku mkiwaona semeni wapi Mwamvita yupo???....Maposo hakuwa na huruma kabisa Alimshika kijana mmoja kwenye familia hiyo ambae ni ndugu wa Makame alitaka kumchinja mbele yao. Watu waliomba radhi na kwamba watamtafuta ndani ya muda mchache watampata.

Maposo aliwakamata na kuwapeleka kwenye himaya yao mpaka pale atakapopatikana Mwamvita baada ya hapo nyumba yao iliweza kuchomwa moto.
Wakati moto unaendelea kuwaka. Maeneo ya jangwani alionekana kijana mmoja ambae hakufahamika ni nani aliyesimama Kwenye moja ya jiwe kubwa akiangalia uelekeo wa Moshi ambao ulitokea kule kijijini.
Alitembea umbali mrefu kwa kuzunguka ili aweze kutokezea sehemu aliyohitaji.

Mzee Mshauri alikimbia na kwenda kumpa taarifa Makame kuwa mama yake na familia imekamatwa na nyumba yao ilikuwa inawaka moto. Mzee mashauri bila kujua kuwa alikuwa anafuatiliwa na Mmoja wa kijana toka Kwa Maposo aliyepewa dhamana ya Kuchunguza.
Alihakikisha kuwa baada ya kuwaona wapi wamefichwa alijitokeza akiwa na mshale wake na kutoa kauli....."Mzee Mashauli umemficha mwanao huku na watu wanakufa kwa ajili ya Mwamvita binti mzuri aliyependwa na Kijana mtukufu Maposo"...Mzew Mashauli hakujiuliza kutokana na kuwa yeye ndie mwenye mwana isitoshe makame hawezi kupambana na kijana huyo kwani alikuwa hana hali baada ya kusikia wzazi wamekamatwa.

   Alijitoa kimasomaso mzee huyo huku Mwamvita akimhitaji baba yake asifanye mzaha mbele ya silaha hiyo...."Baba acha usifanye hivo baba"...Kijana huyo aliachia mshale uliokwenda kwa kasi lakini Makame alijitokeza na kumkinga Mzee Mashauri na ukamkita yeye kifuani hakika ilikuwa pigo kubwa kwani Alikuwa kijana aliyejitokeza kumsaidia Mwamvita.
 
Makame aliomba kumuambia jambo Mwamvita...."Shemeji hakika jua kuwa nakufa kwa ajili ya kutete amaisha yako na ndoa yako pia naomba mnitunzie familia yangu pia jua kuwa Mumwa yuko hai na yale yote na vifo vyote vilivyofanyika kwa Mbei yeye ndie alikuwa anavifanya."....kijana baada ya kuona kaua alitaka kukimbia lakini alikutana na mtu asiyemfahamu alimkita mshale palepale na yeye akaanguka chini.
Mzee Mashauri aliogopa baada ya kumuona yule kijana tayari kafa na nani aliyemuua hawakumuona. Walijua kuwa wamevamiwa. Walifanya juhudi ya kumsitili kisha mzee Mashauri aliondoka kwenda kuwaita watu ambao watasaidia kumbeba na kwenda kumzika Makame shujaa.

Alikuja na vijana kadhaa ambao ni rafiki wa Makame walikwenda hadi maeneo ambayo alimuacha Mwamvita akiwa na makame. Hawakumkuta walianza kuita lakini hakuna aliyeweza kuitika. Mzee sasa aliweza kuhangaika na kutofahamu wapi mwanae na yule Makame wamekwenda.  ......"kuna hatari niliwaacha hapa sasa siwaoni wapi wamekwenda".....walirudi wakiwa na mawazo ya kupotelewa na Mwamvita na Makame.

Usiku kama kawaida Mbei na Maposi wakiwa eneo ambalo hutumia kama maongezi yao ya kawaida.
Maposo alisema....."baba inabidi tumtafute yule kijana aliyesaidia ile aiku usiku kwenye vita mana nimependa sana ni mwenye nguvu sana"...."Maposo kila kitu nimekuachia wewe fanya utakavyo"....lakini sasa itabidi tuwakamate vijana wote na kuwaweka hapa alafu tuwachunguze kwa kuwapiganisha tukimyona mana najua aina gani ya mapigo anaitumia tukifanya hivyo tutafaidika"...haya na huyu Mwamvita??....Baba kuhusu mwamvita sijachoka nimetoa zawadi kwa yeyote ambae atamuona anapata pia baada ya kumshika na kumuona huyo kijana basi atatusaidia kumkamata Mwamvita"......

Muda mchache walinzi walisikika kupiga yowe la kusisitiza kuwa kuna hatari. Alikuja kijana mmoja mbele ya Maposo na kusema....."Mkuu yule kijana yuko getini anataka kuonana na nyinyi"....aaah mruhusu msimfanye chochote".....kijana aliruhusiwa akiwa na maguo na harufu yake mbaya alitembea hadi pale walipo Maposo na Mbei
Maposo alianza kusonoa maneno...."Haya kijana tunashukuru kwa msaada wako na kuja kwako nadhani unajambo zuri sana unatokea wapi"...."Maposo unamfahamu???...."baba huyu ndio yule kijana niliyekusimulia muda mfupi uliopita"...
Walikaa kimya na kumsikiliza nini atakuja kusema. Alionekana kupiga hatua moja nyuma ya pili na ya tatu akasimama......."Maposo na Mbei nimerudi tena kumbukeni mmefanya dhulma gani kwa Familia ya Mzee MOSHI haikutosha Mkamchukua Mke wangu na kumfanya vile mtakavyo sasa nimerudi hii ni ahadi ya ndoa yangu kila siku utapoteza mtu mmoja hapa kwako"... alipomaliza aliruka kwa umaridadi uzio wa nyumba hiyo na kutupa mshale uliompata mmoja wa mlinzi ambae anawalinda Mzee Mbei na mwanae kisha hakuonekana tena.

Waliduwaa baada ya kutambua kuwa ni MUMWA karudi tenaaaaaaa......

Itaendelea......



No comments: