Riwaya:: NDOA NDOANO SEHEMU YA 12::




Riwaya:: NDOA NDOANO
SEHEMU YA 12::

Endelea....
Mzee Mbei na mwanae Maposo waliona ni vyema sana endapo wakipanga mipango ya kumtafuta Mumwa, Ila wanamtafuta kwa njia gani na ilhali si mtu wa kawaida, basi asubuhi ilipofika Maposo aliweza kutoa taarifa kwa watu kuwa Mumwa karejea na ndie ambae aliweza kuua watu pale kwa Mzee Mbei.

Mashauri alivyopata taarifa ya kuwa Mumwa yuko mzima na ndie ambae aliweza kufanya mauaji ya siri ambayo hayakujulikana kwa muda mrefu.'Mke wangu umepata taarifa kuwa Mumwa kumbe ni mzima?' Aliongea Mashauri kumueleza Mkewe Monalisa. 'Aah ina maana pale kwenye moto aliweza kupona kabisa bila kuungua eti!'.

Muda mfupi alishangaa kuona kundi la watu na si wengine walikuwa ni watu wa mbei ambao walikuja hapo kwa Mzee Mashauli, mashauli hakufahamu japo alipata mshituko.' Hawa nadhani wanakuja hapa nyumbani lakini..' aliongea Mashauli 'Mh! Yani hapa tunaishi kwa wasiwasi sasa wakimhitaji Mwamvita itakuwaje?' Aliuliza Monalisa.
'Sasa hivi mke wangu sio kuwadekeza hawa watu watatuonea sana'.

Vijana hao walifika hapo wakionekana kuwa na hasira, pia walichokifanya ni kuingia ndani kwa baadhi yao. Lakini wengine walibaki nje ndipo mzee Mashauli aliweza kusimama huku akichungulia dirishani huku akiwaangalia wanachokifanya ndani humo. Lakini hawakubahatika kupata chochote ambacho walikhitaji ndipo walitoka na kusimama mbele ya Mashauli na Monalisa. 'Mzee tunakupa siku tatu uwe umeshamleta Mwamvita Maposo hawezi kuishi bila yeye' Aliongea mmoja wa watu hao, ' sasa mwamvita hapa kaja kuchukuliwa na Mumwa sasa ni bora mukaenda kumchukua huko.nisipopajua'. Vijana waliondoka huku wakiwaacha Monalisa na Mashauli wakishangaa.

Maeneo ya Pori moja alionekana Mwanamke mmoja akiwa anaonekana akiwa anaamka, Binti huyo kwa mbali alionekana kuwa na mshangao ambao hakufahamu wapi alipo kwani alikuwa anashangaa huku na kule. Pembeni yake alionekana kijana mwingine ambae na yeye alikuwa bado yuko kwenye usingizi mzito wa aina yake.
Kumbe hakuwa mwingine bali ni Mwamvita ndie ambae alikuwa hapo pembeni yake alikuwa ni Makame ambae hali yake ilikuwa ni mbaya sana 'Makame makame ebuu amkaaa!' Makame nae aliamka taratibu hadi akili yake ilivyokaa vyema. 'Mwamvita tupo wapi hapa?' Aliuliza Makame huku akigugumia kifua kwa maumivu. 'Mh! Hata mimi bado sijapafahamu na wala sijui tumefikaje hapa vipi upoje asa hivi'.

Muda mchache kwa mbali alionekana Kijana ambae hakutambulika na Macho ya Mwamvita na Makame mapema. Hasa mwamvita alijikuta akijipeleka kwa makame ambae na yeye hakuwa vyema kwa hali mbaya aliyonayo kwa kumhofu kijana huyo anayewajia mbele yake. Makame nae alimuogopa kwani hakumtambua pia. Kijana huyo alikaribia hapo karibu yao akaacha mkungu wa ndizi ambao alikuja nao huku akiwa kabeba majibkwenye moja ya kibuyu kikubwa cha kuhifadhia maji.

Baada ya kuacha yeye aliweza kuondoka mahali hapo. Makame alimkataza Mwamvita kutumia vile vitu kwani hawamjui vyema huyu mtu.'sasa mimi nina njaa tutakula nini?' 'Sawa ila unamjua vyema huyu mtu?' 'Hata kama kama kufa mimi nilishakufa haina shida'. Mwamvita alichukua ndizi moja akamenya kisha akaila,akachukua ya pili akaila ya tatu akaila ndipo akachukua maji akanywea. Makame akaona ni ajabu kwake kwa nini hajadhurika japo na hali yake alijitahidi sana kuchukua moja lakini alishindwa kwani alitokwa na damu nyingi kifuani kwani ule mkuki ulikita barabara ungempotezea maisha yake. Mwamvita alimchukulia kisha akaanza kumlisha.

Upande wa Maposo na Mbei. Walijianda vyema huku wakijiridhisha kwa lengo la kupita mitaani kumtafuta Mwamvita kwa hali yoyote ile. Waliingia mitaani huku wakipiga watu ovyo na kuwasababishia maumivu makali sana kwa kuwalazimisha kusema wapi alipowekwa Mwamvita.
Wengi walijuta sana kwa nini yupo pale kijijini kutokana na hali ya manyanyaso anayoyapata.

Mpaka jioni wengi walikuwa hoi na wengine waliweza kukimbia kijiji na kuelekea porini. Lakini yote kwa kuhofia maisha yao. Waliokuwa wanathirika sana ni vijana. Hawakuishia hapo walitangaza kuwa atakaemkamata Mumwa basi kijiji kitakuwa salama kwa mateso. Lklakini kama hakuna atakaejua wapi yupo basi kijiji kila siku kitashuhudia mauaji ya kila aina.
Watu waliondokwa na roho ya huruma walianza kumsaka kama paka mwizi.

Katika msako wao wa wanakijiji kumtafuta Mumwa hatimae walimkuta akiwa anamlilia Makame aliyekuwa akilalama kuwa na hali mbaya. Alipowaona wale wanakijiji wakija na silaha zao huku wakiwa na hasira walisikiasauti ya wale wanakijiji wakisema 'waleeee palee twendeni'. Walifika karibu yao kisha wakawazunguka 'Mwamvita una uzuri gani ambao una hangaisha maisha ya wanakijiji hapa' aliongea mmoja wa watu hao 'Kwani jamani hamfahamu kuwa nimeolewa mbona mnanifanya kunilazimisha kuwa na mtu nisiyempenda..' 'hata kama binti itakubidi uachane na huyo Mumwa kunusuru maisha ya wengine ona huyu kijana Makame atakufa kwa ajili yako'. ..'Haaah nilidhani kuwa nyinyi hizi nguvu mkazitumia kumdhibiti Maposo mnakuja kutukamata sisi hivi mnafahamu mateso gani ninayapata kule'.

Walimkamata lajini Makame alijitutumua na kusimama lakini alipigwa lubega yani kiwiko kifuani ikawa moja kwa moja hadi chini kufariki..hali hiyo Mwamvita anayoshuhudia kuwa Makame anakufa mara yapili ya kwanza alihisi kafa lakini aliokolewa hii ya pili ni mazima.

Alilia sana huku akiwa kakamatiwa na Wanakijiji wenye hasira kali. Mwamvita alipiga yowee la msaada..'Mamaaaaaaa, mumwaaa weeee kama kidume kweli ulieniahidi kuwa utanipenda na kunilinda ona ninavyoonewa hapa njoo mwanaume uniokoe' maneno aliyokiwa anaongea yaliwachekesha sana wale wanakijiji hivyo haikuwafanya wabadili msimamo.
Ghafla mbele yo alijitokeza kijana akiwa kategesha mishale mitatu kwenye mkuki mmoja. Walitulia lakini walitumia udhaifu wa Mwamvita kumkamata Mumwa. 'Kijana ukileta kujua sisi ni wawindaji hodari tuliochoka kuumia kwa ajili yenu. Asa njoo jisalimishe ili huyu tumuache'. Mumwa alijifikilia akaona ni vyema ajitoe kwenda pale kwani hakuweza kubishana na kundi la watu wote wale. Aliacha mkuki akizipiga hatua kwenda pale walipo.

Waliweza kumshika na Mwamvita na kuwapeleka mbele ya Maposo. Hakika maposo alifurahi mno.
Akawa ahidi kuwa hawatoumizwa tena. Mzee mashauli aliumia sana. Alijitoa kimasomaso mtaani huku akiongea maneno yaliyowafungua akili watu.
'...Wanakijiji hamna huruma wala ushirikiano..mume mpeleka mwanangu kwa kuwa hamfahamu anayofanyiwa kule kwa nini sisi tusiungane kumtokomeza huyu mpuuzi. Ila munaungana kuumizana sisi kwa sisi. Mnaifanya ndoa ya mwangu iwe anajutia au kwa kuwa ni mwanamke mbona nyinyi wanenu hamkuwapeleka jamani sawa mimi nitajitahidi kumsaidia mwanangu'.
Aliondoka huku akiwa na hasira.

Itaendelea



No comments: