Riwaya:: NDOA NDOANO SEHEMU YA 15
Riwaya:: NDOA NDOANO
SEHEMU YA 15
Endelea.......
.....Majira yale ya usiku wanajikuta wako peke yao porini familia yote wakiwa hawafahamu nini wakifanye cha kuweza kiwasaidia muda huo. Hali ya Mumwa haikuwa nzuri kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa sana. Pia Mwamvita na yeye mkono wake ulizidi kuharibika lakini alizoea ile hali kutokana na kutokuwa na msaada wa dawa. Mzee Mashauri aliweza kumuona Mwamvita akiwa kwenye hali ile, alimshika na kumtazama mkono ule alisikitika sana "Ahaa mwanagu haya majeraha yote haya sababu nini jamani ila usijali utapona"
Alimpa matumaini hiku wakiendelea kuangalia wale watu wa maposo wanavyozungusha vizinga vya moto maeneo yale ambayo walikuwapo mwanzo. Mwisho wakaonekana wanagawana njia za kupita. Mumwa aliona ndio nafasi ya pekee kwao kujinasua isije ikafika asubuhi na bado wako eneo lile wakakamatwa. Mumwa na mzee Mashauri walikutana na kuunda mitego japo ni usiku. Walifanikiwa kutengeneza mitego kadhaa usiku huo kisha wakapumzika.
Asubuhi jogoo linawikaa " kukulukuuuuuuu koooooo"" Lilisikika jogoo la kijiji ambacho wao wanahitajika kufika huko hatimae, wakaanza kutafuta njia za kuelekea huko. Upande wa Maposo usiku wa jana aliweza kuwapanga watu wake mahali tofauti tofauti, kutokana na uchovu basi walijikuta wakilala kwa kila aliyepewa sehemu ya kukaa. Hali hiyo ndio iliwasaidia Mumwa pamoja na wale wengine kupita kirahisi bila kipingamizi chochote kile.
Walisikia kilio cha mwanadamu kikisikika nyuma yao. "Safii wapuuzi kama hao lazima mitego iwaadhibu" Aliongea Mzee Mashauli "Baba una maana mtego wako ndio umemkamata mtu" Mumwa alihoji kwa tabasamu " Haswaaaa". Hatimae wanavuka vizingiti vyote na wanafanikiwa kuibukia ndani ya bonde la Kijiji cha Mumwa. Wakati wanafurahia walishituka wanawekwa kwenye ulinzi mkali sana na wanaolinda mipaka ya kijiji hiko.
Walikubaliana na wao hivyo wakaanza kusindikizwa wakipelekwa mbele ya kiongozi wao. Ni kitambo kidogo toka hapo walipoweka kambi ya ulinzi na ndani ya kijiji. Iliwachukua muda wa kutosha, ukizingatia na uchovu wa safari walionao pamoja na purukushani, waliona ni vyema kuwa chini ya ulinzi wa eneo ambalo mmoja wao anafahamika kidogo. Msafara wao uliweza kuishia kwa Mzee mmoja mkongwe sana aliyezungukwa na watu kadhaa nyuma yake, pembeni yake. Mmoja wa ulinzi akatamka.
"...Baba CHIJUNI sisi ni vijana wako tumewakamata hawa watu wakipitia nyuma ya kijiji hivyo tukawa na shaka nao tumewaleta mbele yako mkuu tunasubiri kauli yako..." Mzee huyo aliwaangalia sana hatimae macho yake yakanasa kwa Mwamvita binti mrembo zaidi. Akamuita kijakazi mmoja wa kike kisha akamnong'oneza jambo. Alionekaana yule kijakazi akimfuata Mwamvita na kumshika mkono akaimvutia mahali tofauti na pale. Kisha akasema.
".....Huyu mama na huyo mtoto utawaweka sehemu tofauti na hawa wanaume utafungie pale...." Mumwa alijitahidi kuomba msaada sana pia na kumueleza kuwa yeye anafahamika pale. Yeye sio mgeni pale lakini mzee alionyesha sura ya kutohitaji maneno yoyote zaidi ya lile alilolisema. Kwa kuwa Mumwa alisumbua sana kupiga kelele basi akapigwa kitu kizito mgongoni kikamzimisha palepale. Mzee Mashauri akaguna.
Walifungwa kamba moja kwenye mti wakiwa wamekalizwa chini ya mti huo. Mzee huyo aliingia kwenye kibanda alichofungiwa Mama Mwamvita na Sikitu. "...Mama huyu binti ni wa kwako?" Akiwa anamaanisha Mwamvita. "...Baba ndio ni mwanangu choonde naomba umuache kama alivyo anaumwa mwanangu jamani baba tuonee huruma tuna matatizo". Kelele za mama huyo hazikusaidia kitu.
Alitoka na kwenda kibanda alichowekwa Mwamvita. Alitolewa nje na wanawake wa pale, kisha akatangaza rasmi kuwa Sasa binti huyo ndie atakuwa Malkia wake kuanzia muda huo. Walielezwa usalama wake ni kukubali tofauti na hapo basi hapatatosha hapo. Mzee CHIJUNI alitangaza uwepo wa kumtawadhisha Malkia huyo mpya, watu walifurika siku ya kumtawadhisha Mwamvita. Kabla ya siku hiyo Mwamvita alimuendea Mumwa na kumwambia " Mumwa mume wangu, najua jinsi gani unaumia mimi sipendi kuidhi na huyu mzee wakati wewe upo, nimevumilia kipindi nimeambiwa umekufa lakini leo mzima kwa nini nisivumilie wakati nakuona"
"Mke wangu hii ndio ndoa kumbuka kuwa nfoa ndoano, itabidi tuvumilie sasa wewe kubali lakini kesho siku ya sherehe, nitafanya jambo usijali lengo atuachie kwanza hapa najua mama akisikia atakuja kututoa msijali tunaondoka wote" walikubaliana kuwa Mwamvita akubali kutawadhishwa kuwa Malkia wa pale. Siku ya sherehe ilitimia ndipo maandalizi yakaanza. Ajabu mambo ambayo walitarajia kama yatakaa vyema hayakuwa kama walivyopanga kwani Mzee Mashauri alipatwa na ugonjwa mbaya sana ambao ulisababisha kutofanya ile mipango waliyoifanya.
Mwamvita hatimae anatawazqa kuwa Malkia kwa Mapenzi ya Mzee Chijuni, kama mke wake mwingine katika idadi ya wanawake alionao. Mambo yanakuwa mambo sasa. Hali ya Mwamvita iko salama lakini ugomvi haukuisha na Mzee katika swala la mke na mume ndani ya ndoa yao ya dharura. Kutokana na purukushani zilizoendelea basi mzee alidonfoka chini na kuaga dunia palepale.
Baada ya wiki kadhaa walifanya mazishi na kijiji kikawa chini ya Mwamvita. Alimshirikisha Mumwa ili ampe ufalme lakini Mumwa alikataa. Maisha ya Mwamvita akiwa anaanza uongozi ambao hakutegemea ndipo ulipoanza kuwa na changamoto...
Itaendelea.........

No comments: