Riwaya:: NDOA NDOANO SEHEMU YA 16
Riwaya:: NDOA NDOANO
SEHEMU YA 16
Endelea.........
....Uongozi wa Mwamvita ulianza kuwa na changamoto kubwa sana, kwa kuwa ilimuia vigumu kuzoea yale mazingira pia hata kuwafahamu watu wake ambao kavamia kuwaongoza. Alikubali ili aweze kuwa na nguvu ya kuepukana na kikundi cha Maposo na baba yake. Mumwa alimtafuta mama yake ndani ya kijiji hiko lakini hakubahatika kumpata kabisa. Alirudi kwa Mke wake Mwamvita ambae kwa muda huo hakujulikana kama Malkia ana Mwanaume ambae ni wa ndoa kabisa.
Wanakijiji wa hapo walizoea kila kipindi cha muda fulani kwa upande wa wanaume kuwa na ngoma ambayo inahusisha kucheza, kulewa ilikuwa inaitwa Sikukuu ya Kujifariji. Sikukuu hii ilianzishwa na Mzee Chijuni mfalme ambae ni marehemu kwa nyakati hizo. Mdhauri alikiwa ni mwanaume sasa Mwamvita akambadilisha akamkabidhi Baba yake Mzee Mashauri kuwa ndie atakuwa Mshauri mkuu pamoja na Mzee wa hapo ambae ni mzoefu wa muda mrefu.
Basi skku zilipokaribia Mzee yule ambae alikuwa mzoefu wa pale alimshauri Mzee Mashauri 'Mzee vipi sikukuu ya kujifariji itakuwepo maana sioni maandalizi' Hapo ndipo Mashauri akapata kuuliza swali ' Ndugu unafahamu kuwa huyu malkia mpya hivi hiyo sikukuu inahusu nini?' Kwanza alianza kucheka sana ndipo akaelekeza vyema ' bwana hiyo sikukuu tunakunywa,tunalewa,wanawake watakaa uchi ndicho ambacho tunapenda na kila ambae hajagusa ni ruksa kumshika mwanamke umtakae kumgusa' Mashauri akaona kumbe ni skkukuu ya kipumbavu kabisa isiyo na faida.
'Khaa yani nifurahie huo upuuzi hapa hakuna hiyo sherehe'. Baada ya siku kufika watu walihaha sana hasa wanaume ambao huwa wanafurahi sana pindi inapofika kipinfi hiki, lakkni ilionekana ajabu sana kwa nini safari hii hakuna. Malkia alihitajika kujibu mashitaka ambayo anatuhumiwa. Wanakkjiji walifurika kwa wingi kuuliza nini?. 'Malkia tangu ukae madarakani hatujaona sikukuu ya kujifariji kabisa mbona hatuelewi' Mwamvita alishindwa ajibu nini ndipo baba yake aliyeonekana kama mshauri akasimama na akasema ' Malkia kasema hakuna hiyo sikukuu kwani mnawaonea sana wanawake na yeyote atakaebisha basi atavhukuliwa hatua' Haikutosha basi Mumwa akakazia kabisa. Ndipo akasimama mmoja.
'Wewe kijanaa wewe...' Alimuonyeshea Mumwa. 'Mama yako kapatikana kwa njia hiyo faida yake kuna wanaume hawana uwezo wa kuzalisha tunapoweka hii sikukuu basi tunasaidiana baada ya kujua fulani hana uwezo huo' Iliwapanikisha sana vijana wa kiume ghafla ukazuka ugomvi baada ya Wanawake kufurahi mno baada ya tatizo lao kupatiwa ufumbuzi wengine walimpenda dana Mwamvita.
Baada ya muda kupita Mwamvita alipatiwa dawa ya Mkono ambao ulikuwa unamsumbua. Inafika mwaka na kitu Mwamvita na Mumwa hawajawahi kukutana kama mke na mume kwani kutokana na pirikapirika za hapa na pale na mambo mengi iliwafanya washindwe kukutana. Vijana wa hapo hawakupenda ule mfumo.
Siku moja kuna kijana ambae anakaa kule ambako Anaishi Maposo na Mbei baba yake. Alimuona Mwamvita katika moja ya shughuli zake. Mwamvita na yeye alifanikiwa kumuona na akahisi jambo baya litatokea mbele yake. Mwamvita aliomba jeshi lake likae sawa kwa chochote kitakachotokea kwa siku za usoni.
Kutokana na wasiwasi.
Kumbe mumwa anakuja kutambua kuwa mama yake alishauliwa na kundi linalokuja kuvamia hapo ambao ni kundi la Maposo. Basi yule kijana alienda kutoa taarifa kwa Maposo kuwa kumbe Mwamvita kamuona kijiji cha pili. Maposo hakutaka kuchelewa tena alituma jeshi lake mapema kwenda kumchukua Mwamvita. Kwa bahati mbaya ndani ya mipaka hiyo wanakutana na kikwazo cha walinzi ambao walielekezwa kutii amri ya Mwamvita.
Basi mmoja alifanikiwa kurudi salama ila wengine walibadilishwa majina na kuitwa Marehemu. Maposo aliumia sana. Wakati huo haikutambulika kama Mwamvita anaongoza kijiji Mzee Mbei alipanga safari kwani mzee Chijuni anamfahamu sana anweza kuongea nae na akampata kiurahisi sana Mwamvita. Walinzi walimkamata jambo ambalo aliishangaa sana.
Hatimae Mzee Mbei anawekwa chini ya ulinzi. Mwamvita alihitaji kulipiza kisasi ambacho Maposo kamfanyia ukatili mkubwa.
Alimtoa nje ya mji na akamchinja kwa mikono yake, hakika Mumwa hakuamini kabisa. Kisha akatumwa mjumbe apeleke zawadi kutoka kwa Chijuni imfikie Maposo. Kichwa cha Mzee Mbei kikiwa Kimevirigiwa kama furushi la zawadi. Kweli kijana alipeleka kisha yeye akarejea alikotokea.
Maposo alikuwa na hamu kubwa ya kuangalia zawadi gani kutoka kwa Mzee Chijuni......
Itaendelea.......

No comments: